Tanzania\'s leading online News Edition (The National Newspaper). Get access to the most current and latest authoritative news on local issues, politics, events, celebrations, editorial, columnists, features, people and business.
Monday, 27 November 2017
Wabunge nane CUF wazungumzia maamuzi ya mahakama kurejeshwa bungeni
Wabunge nane CUF wazungumzia maamuzi ya mahakama kurejeshwa bungeni
Kikwete akerwa navitendo vya uvunjivu wa amani na migawanyiko
Mbunge wa jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CMM Mh. Ridhiwani Kikwete ameeleza kutofurahishwa na vitendo vya uvunjivu wa amani na migawanyiko, vilivyojitokeza katika uchaguzi mdogo wa madiwani nchini uliofanyika jana.

"Siasa ya uchaguzi haipaswi kuwa mwanzo wa migawanyiko, mbegu tunayopanda leo kama haikukemewa itakuja kutusumbua siku sijazo, niwaombe Watanzania wenzangu, tudumishe upendo na tukatae fujo zisizo na lazima”, amesema Ridhiwani.
Aidha Ridhiwani ametoa ushauri unaolenga kuondoa visingizio na propaganda za kutumia wanachama kama ndio sehemu ya vurugu hizo akidai kuwa wafanya vurugu hao ni wananchi na sio CCM wala CHADEMA kama ambavyo kila upande unadai.
“Wanaopigana ni wananchi, sio CCM wala CHADEMA, maana naona pande zote zinalalamika, tuwe na hukumu sahihi, la msingi tukatae fujo, nchi hii ni muhimu na tuenzi mawazo sahihi ya wazee wetu”, ameongeza Ridhiwani.
Wananchi katika Kata 43 za mikoa 19 nchini kote jana wamepiga kura kuchagua madiwani katika uchaguzi mdogo ambapo vitendo kadhaa vya vurugu viliripotiwa kutokea huku CHADEMA ikijitoa kushiriki uchaguzi huo katika kata 5 za wilaya ya Arumeru.

"Siasa ya uchaguzi haipaswi kuwa mwanzo wa migawanyiko, mbegu tunayopanda leo kama haikukemewa itakuja kutusumbua siku sijazo, niwaombe Watanzania wenzangu, tudumishe upendo na tukatae fujo zisizo na lazima”, amesema Ridhiwani.
Aidha Ridhiwani ametoa ushauri unaolenga kuondoa visingizio na propaganda za kutumia wanachama kama ndio sehemu ya vurugu hizo akidai kuwa wafanya vurugu hao ni wananchi na sio CCM wala CHADEMA kama ambavyo kila upande unadai.
“Wanaopigana ni wananchi, sio CCM wala CHADEMA, maana naona pande zote zinalalamika, tuwe na hukumu sahihi, la msingi tukatae fujo, nchi hii ni muhimu na tuenzi mawazo sahihi ya wazee wetu”, ameongeza Ridhiwani.
Wananchi katika Kata 43 za mikoa 19 nchini kote jana wamepiga kura kuchagua madiwani katika uchaguzi mdogo ambapo vitendo kadhaa vya vurugu viliripotiwa kutokea huku CHADEMA ikijitoa kushiriki uchaguzi huo katika kata 5 za wilaya ya Arumeru.
Waziri Kamwelwe asimamia ubomoaji wa majengo Ofisi za Wizara ya Maji

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ametoka Dodoma kuja Dar es Salaam kusimamia ubomoaji wa majengo ya ofisi za wizara kupisha upanuzi wa barabara.
Kamwelwe amesema leo Jumatatu Novemba 27,2017 kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli na kupisha ujenzi wa barabara pana inayokwenda Chalinze mkoani Pwani.
Amesema atahakikisha majengo yote yaliyo ndani ya hifadhi ya barabara yanabomolewa leo.
Waziri amesema watendaji wake wamejipanga na ofisi yake tayari ilishahamia Dodoma.
"Nimekuja juzi kutoka Dodoma kuja kusimamia ubomoaji wa majengo haya ya Serikali. Jana tumekaa mpaka saa mbili usiku na kukubaliana kwamba leo lazima tubomoe," amesema waziri.
Amesema tayari wananchi wameshabomolewa nyumba kupisha ujenzi wa barabara, hivyo Serikali nayo ni lazima itimize wajibu wake kwa kubomoa majengo yake kama inavyotakiwa.
"Sitaondoka mpaka majengo yote yabomolewe. Ninachotaka leo lazima majengo yawe chini," amesema Kamwelwe.
Guardiola akiri maajabu
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola, amesema timu yake imeonesha ushindani wa ajabu wakati ikihangaika kusawazisha na kuongeza bao la ushindi kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England jana dhidi ya Huddersfield.

Guardiola amekiri kuwa kama timu inataka kushinda ubingwa lazima iwe tayari kuonesha maajabu kama ilivyokuwa jana huku akisisitiza kuwa wachezaji wake wanatakiwa kuzoea hali hiyo.
Manchester City ilitoka nyumba kwa bao 1-0 kabla ya kusawazisha kupitia kwa Sergio Aguero kisha kuongeza bao la ushindi kupitia kwa Raheem Sterling. Baada ya ushindi huo matajiri hao wa jiji la Manchester wamefanikiwa kuendelea kukaa kileleni wakifikisha alama 37 dhidi ya 29 za wapinzani wao Manchester United wanaoshika nafasi ya pili.

Pia vinara hao wa ligi wamefikia rekodi yao ya mwaka 2015 ya kushinda mechi 11 za ligi mfululizo. Man City jana ilipata ushindi kwa mara ya kwanza tangu Aprili 1995 ikitokea nyuma kipindi cha kwanza kisha kushinda kipindi cha pili.

Guardiola amekiri kuwa kama timu inataka kushinda ubingwa lazima iwe tayari kuonesha maajabu kama ilivyokuwa jana huku akisisitiza kuwa wachezaji wake wanatakiwa kuzoea hali hiyo.
Manchester City ilitoka nyumba kwa bao 1-0 kabla ya kusawazisha kupitia kwa Sergio Aguero kisha kuongeza bao la ushindi kupitia kwa Raheem Sterling. Baada ya ushindi huo matajiri hao wa jiji la Manchester wamefanikiwa kuendelea kukaa kileleni wakifikisha alama 37 dhidi ya 29 za wapinzani wao Manchester United wanaoshika nafasi ya pili.

Pia vinara hao wa ligi wamefikia rekodi yao ya mwaka 2015 ya kushinda mechi 11 za ligi mfululizo. Man City jana ilipata ushindi kwa mara ya kwanza tangu Aprili 1995 ikitokea nyuma kipindi cha kwanza kisha kushinda kipindi cha pili.
Meya Jacob aweka wazi Sababu ya Kukamatwa
Meya wa Manispaa ya Ubungo kupitia CHADEMA Jacob Boniface ambaye jana alishikiliwa na polisi, ameweka wazi sababu ambayo jana ilimsababishia kukamatwa na jeshi la Polisi na kulala ndani, huku uchaguzi ukiendelea.


Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Meya Jacob amesema yeye alikuwa ni msimamizi wa vituo vya kupigia kura ambayo ipo kisheria, lakini baada ya muda alishangaa kuona polisi wanakuja kumkamata kwa tuhuma ambazo hazikuwa za kwlei.
“Nilikuwa nasimamia uchaguzi kama msimamizi wa uchaguzi wa chama changu, nikiwa kituoni nashangaa kuona nakuja kukamatwa na polisi, nilipofika kule wakaniambia kuwa wamepata taarifa kwamba nimejipanga kufanya vurugu na wenzangu, kitu ambacho sio kweli”, amesema Jacob Boniface.
Meya huyo ambaye ni miongoni mwa viongozi machachari wa CHADEMA amesema mpaka sasa hajajua hatma yake kama anapelekwa mahakamani au la, kwani aliachiwa huru majira ya saa saba usiku baada ya kulipa dhamana, huku uchaguzi ukiwa umeshakwisha.
Heche amjia juu anayemshauri Nassari
Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche amewachana wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi kwa kuwaambia kwamba wataendelea kuwapata wafuasi wachumia tumbo na kwamba yeye na wengine wameamua kuchagua upande wa ukweli.

Heche amefunguka hayo baada ya kijana anayedhaniwa kuwa mfuasi wa CCM kumshauri Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kama anataka kujiendeleza Kisiasa.
Baada ya ujumbe huo Heche imemlazimu kusema kwamba "Hizi ndio akili za kijinga za ccm kufikiri kila alieamua kuingia kwenye siasa anatafutia tumbo lake au utukufu binafsi wengine tanajua kwamba CCM ipo lakini tumechagua upande wa ukweli pamoja na maumivu tunayoyapata tutavuka na tutafika ng'ambo".

Jibu la Heche kwa aliyekuwa akimshauri Nassari kuhama chama
Ameongeza kwamba "Wachache wachumia tumbo mtawapata. Watu wenye moyo mwepesi ndio mnaamini hivyo jiulize wale waliopambana na wakoloni wangekua na fikra hizo leo tungekua huru?


Heche amefunguka hayo baada ya kijana anayedhaniwa kuwa mfuasi wa CCM kumshauri Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kama anataka kujiendeleza Kisiasa.
Baada ya ujumbe huo Heche imemlazimu kusema kwamba "Hizi ndio akili za kijinga za ccm kufikiri kila alieamua kuingia kwenye siasa anatafutia tumbo lake au utukufu binafsi wengine tanajua kwamba CCM ipo lakini tumechagua upande wa ukweli pamoja na maumivu tunayoyapata tutavuka na tutafika ng'ambo".

Jibu la Heche kwa aliyekuwa akimshauri Nassari kuhama chama
Ameongeza kwamba "Wachache wachumia tumbo mtawapata. Watu wenye moyo mwepesi ndio mnaamini hivyo jiulize wale waliopambana na wakoloni wangekua na fikra hizo leo tungekua huru?

Zitto: Tumekubali kushindwa

Baada ya kukamilika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 nchini, Kiongozi wa ACT –Wazalendo, Zitto Kabwe amesema wamekubali kushindwa.
Zitto katika taarifa aliyoitoa leo Jumatatu Novemba 27,2017 amesema ACT Wazalendo katika uchaguzi wa jana Jumapili Novemba 26,2017 ilisimamisha wagombea katika kata 17.
“Tumepata matokeo ya kata zote na hakuna kata tuliyoshinda. Wapiga kura wameamua na sisi tumekubali. Tunafanya tathmini ya matokeo nchi nzima na tutazungumza na wananchi. Tunawashukuru kwa kura tulizopata. Tutazienzi kwa kuwa ndiyo haki yetu,” amesema Zitto.
Amesema wanajiandaa kwa uchaguzi mdogo ujao ukiwemo wa ubunge kwenye majimbo yaliyo wazi.
Zitto amesema watatumia mafunzo waliyopata kwenye uchaguzi mdogo kujipanga kwa uchaguzi ujao.
“Kwetu sisi chama cha ACT Wazalendo, uchaguzi ulikuwa fursa ya kuzungumza na wananchi na kufikisha ujumbe wetu kwa kuwa kuzuiwa mikutano ya hadhara kunatunyima fursa hiyo. Hatutachoka kuendelea kusambaza sera zetu kwa kuwa tunaamini ni bora zaidi na zinazoweza kuleta unafuu kwa wananchi wetu,” amesema.
Niyonzima: Mavugo hakosi Timu

WAKATI tetesi za kutemwa kwa mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo, kiungo mchezeshaji wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mchezaji huyo hawezi kukosa timu kama akiachwa.
Mavugo ni kati ya wachezaji waliopo kwenye orodha ya wachezaji watakaoachwa kwenye usajili huu wa dirisha dogo la msimu huu wa Ligi Kuu Bara, kwa kile kinachotajwa kiwango chake kushuka.
Mrundi huyo, tayari ameanza kunyatiwa na baadhi ya klabu za nje ya nchi na kati ya hizo ni Gor Mahia ya Kenya.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Niyonzima alisema Mavugo bado ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, lakini vitu vidogo ndiyo vinamfanya ashindwe kutimiza majukumu yake.
Niyonzima alisema, mshambuliaji huyo kinachomfanya ashindwe kucheza ni presha kubwa iliyopo kwenye timu huku akimtabiria kuwa akienda kwingine atacheza vizuri.
“Mavugo siyo mbaya kiasi hicho, binafsi naona ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao katika timu.
“Lakini kitu kikubwa kinachomfanya ashindwe kucheza vizuri ni presha iliyopo katika timu pekee na siyo kitu kingine.
“Ninakuhakikishia akienda timu nyingine tofauti na Simba atakuwa tegemeo, kwani ana uwezo mkubwa,” alisema Niyonzima.
Mrembo wa Afrika Kusini atwaa taji la Miss Universe 2017
Ni furaha kubwa kusikia nchi yenu imefanikiwa kuzibwaga nchi nyingine katika mashindano ya dunia. Shangwe limetawala nchini Afrika Kusini baada ya mrembo wao Demi-Leigh Nel-Peters kufanikiwa kushinda taji la Miss Universe kwa mwaka huu.

Demi ambaye ana umri wa miaka 22, amefanikiwa kutwaa taji hilo Jumapili hii mjini Las Vegas nchini Marekani ambapo shindano hilo lilipokuwa linafanyika.
Mrembo huyo alifanikiwa kuwabwaga washiriki wengine ambao waliingia katika hatua ya tano bora akiwemo mrembo kutoka Colombia, Jamaica, Thailand na Venezuela.

Picha ya washiriki wa Miss Universe ambao walifanikiwa kuingia kwenye tano bora


Demi ambaye ana umri wa miaka 22, amefanikiwa kutwaa taji hilo Jumapili hii mjini Las Vegas nchini Marekani ambapo shindano hilo lilipokuwa linafanyika.
Mrembo huyo alifanikiwa kuwabwaga washiriki wengine ambao waliingia katika hatua ya tano bora akiwemo mrembo kutoka Colombia, Jamaica, Thailand na Venezuela.

Picha ya washiriki wa Miss Universe ambao walifanikiwa kuingia kwenye tano bora

Baiskeli zinavyosaidia wananchi kukabiliana na uhaba wa maji

Kutokana na uhaba wa upati-kanaji wa majisafi na salama katika Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, wananchi wanalazimika kutumia usafiri wa baiskeli kwenda maeneo ya mbali kutafuta huduma hiyo. Asilimia kubwa ya wananchi wa vijiji vya Mwanga hata katika baadhi ya maeneo ya mjini hutu-mia baiskeli kama usafiri wa kubeba maji kutoka eneo moja kwenda lingine.
Katika maeneo yaliyoendeleana yenye maji ya kutosha ni nad-ra kuona mtu amebeba maji kwa baiskeli, lakini wilayani hapa ni jambo la kawaida kwa sasa.Jambo hili huchangiwa na uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo, hivyo baiskeli kubakia kuwa ndio usafiri unaotegemewa kuwasaidia wananchi hasa wan-awake wilayani humo.
Kiwango cha maendeleo ya jamii yoyote kinategemea kuwe-po kwa maji ya kutosha yaliyo safi na salama. Maji ni mojawapo ya huduma muhimu katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Mwaka 2025. Licha ya malengo hayo kusema kila mwananchi anapaswa kutembea umbali wa mita 400 tu ndipo apate majisafi na salama, kwa Wilaya ya Mwanga jambo hilo bado ni kutendawili. Inaendelea uk 24
Ukosefu wa maji katika wilaya hii umekuwa ni tatizo sugu na linalowapa mateso wakazi wa wilaya hiyo.
Tatizo hili limekuwa likiwatesa zaidi akina mama na watoto ambao huwa wakiamka usiku wa manane kwenda kusaka maji kwenye maeneo yanakopatikana.
Licha ya kuwepo kwa miradi mbalimbali ya Serikali na ile iliyojengwa na taasisi mbalimbali za kiraia, bado tatizo hili limekuwa ni kitendawili kisichokuwa na majibu.
Namna baiskeli zinavyotumika
Sikushangaa kuona baiskeli zikitumika kubebea maji, bali nilishangaa kuwa katika nchi inayoelekea kuwa ya viwanda bado wapo watu wengi wanaohangaika kubeba maji kwa kutumia baiskeli kutokana na uhaba mkubwa wa huduma hiyo.
Juma Amini mkazi wa Kata ya Jipe, anasema kuwa usafiri wa baiskeli umekuwa msaada mkubwa kwao kupata maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Amini anasema takribani kila nyumba ina baiskeli ya kubebea maji. Anatahadhalisha kuwa tatizo hilo si la kupuuzwa na Serikali kwakuwa linahatarisha maisha ya watoto na wanawake ambao mara nyingi wao ndio wanategemewa kusaka maji.
Watoto wa kike nao wanatumia usafiri huo kwa kubeba madumu matatu hadi manne ya maji hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa afya zao.
Mkazi wa Kijiji cha Kivisini Kata ya Kivisini, Amina Ally anasema wanawake na watoto wanachangamoto nyingine ya kusubiri maji kwenye foleni kwa muda mrefu.
Anasema baada ya kuyapata huduma hiyo hutumia baiskeli au mkokoteni ili kubeba madumu mengi ya maji kwa wakati mmoja.
Amini anaeleza kuwa matumizi ya baiskeli yanawasaidia wananchi kuokoa muda na kupata maji mengi kwa wakati mmoja.
Anasema wanatoka nyumbani saa 11 alfajiri kwaajili ya kuwahi foleni ya maji.
“Kama unavyoona foleni ya maji haya ni ya mvua yanatiririka kutoka mlimani, wakati wakiangazi tunachota maji kijiji kingine hivyo mtu hawezi kuchota ndoo moja akarudi inambidi aje na baiskeli au mkokoteni,”anasema Amini.
Haruna Msofe, anasema bila kutumia usafiri wa baiskeli wanaume wengi hawawezi kubeba maji kichwani hasa wanapoyafuata maji maeneo ya mbali.
Msofe anasema, baiskeli na mikokoteni hutumika zaidi kipindi cha kiangazi wakati ambao uhaba wa maji huwa mkubwa zaidi.
Anaongeza kuwa wakati wa msimu wa kiangazi ndio matumizi ya baiskeli huongezeka mara dufu kwakuwa maji hupatikana mbali zaidi katika maeneo ambayo kuna kisima.
Kwa upande wake Hawa Amani anasema licha ya kuyafikia maji hayo, wanachota ndoo sita kila mtu kwa siku kutokana na uchache wa maji.
Hata hivyo, matumizi haya yanatumiwa na wahudumu wa Serikali kwakuwa alionekana mhudumu wa afya katika zahanati ya Kivisini akiwa katika foleni ya kuchota maji.
Mhudumu huyo ambaye alikataa kutaja jina lake, alipoulizwa alisema kuwa wanalazimika kutumia mikokoteni kubebea maji ya kufanyia usafi pamoja na shughuli nyingine katika zahanati hiyo.
“Nafanya kazi Zahanati ya Kivisini, nimelazimika kuja hapa kuchota maji kwaajili ya zahanati, natumia mkokoteni kila siku kuja kubebea maji ili yatoshe,” anasema mhudumu huyo.
Katika Kijiji cha Jipe, Kata ya Jipe ambako wanatumia maji ya ziwa, wakihitaji maji kwaajili ya kunywa wanayapata mbali kwa kuyanunua ni lazima waende na usafiri huo.
Wakati nikielekea Kijiji cha Jipe wananchi wamebeba ndoo za maji kwa kutumia baiskeli, mikokoteni na wengine vichwani.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Jipe, Abdalah Hatibu anaeleza shida wanayoipata wananchi wa kijiji hicho ikiwa ni pamoja na hatari ya kukumbwa na magonjwa kutokana na matumizi ya maji ya Ziwa Jipe.
Hatibu anasema kutokana na ukosefu wa majisafi na salama katika eneo hilo, usafiri huo hutumika kufuata maji walau ya kupooza kiu tu.
Anasema: “Katika ziwa hilo, mifugo wanakunywa maji hapo, wavuvi nao wanafanya kila aina ya uchafu huko ziwani halafu hapo hapo tunachota maji tunakunywa na kupikia.”
Hatibu anasema kuwa wakitaka kupata maji mazuri ya kunywa wanalazimika kwenda kununua katika kijiji kingine kwa Sh500 kwa ndoo moja.
“Kwa mtu ambaye ana uwezo mdogo ndiye anaweza kwenda na baiskeli kununua maji hayo walau ya kunywa,” anasema Hatibu.
Watumia Punda
Katika Kijiji cha Pangaro, Kiverenge na mgagao Kata ya Mgagao wanawake wa kabila la Wamasai nao wanakabiliana na adha hii ya maji hivyo hutumia usafiri wa punda.
Pamoja na kwamba wao hutumia maji yaliyo kwenye malambo, lakini lazima usafiri wa punda uwepo.
Wanawake na watoto ndio wahusika wakuu na wanateseka zaidi wanalazimika kutumia maji ya lambo kwa matumizi ya nyumbani.
Agnes Moleli, anasema licha ya maji hayo kuwa mabaya lakini yamekuwa mkombozi kwao na usafiri wa punda unawasaidia kwakuwa bwawa hilo lipo mbali kidogo.
“Hatuna njia nyingine ya kupata majisafi na salama hivyo lazima tutumie haya, tunakuja hapa na punda halafu tunaingia nao kwenye bwawa tunajaza madumu ya maji kisha tunaondoka,” anasema Mollel.
Anasema kuwa kipo kijiji cha jirani ambacho kuna maji ya kisima lakini hata kwa usafiri huo ni mbali zaidi.
Akizungumza kijijini hapo, diwani wa Kata ya Mgagao, Longoviro Kipuyo anasema kuna kisima kimoja ambacho kipo Pangaro lakini kipo mbali na Kijiji cha Kiverenge.
Anaiomba Serikali kuwasaidia kutafuta mashine na mabomba kwaajili ya kusambaza maji katika vijiji hivyo, kwakuwa kipo kisima ambacho kimechimbwa, lakini hakitoi maji kutokanana ukosefu wa vifaa hivyo.
Kauli ya Mkuu wa Wilaya
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Aron Mbogho anasema kuna mradi mkubwa wa maji unaoendelea kwa sasa, unaofadhiliwa na Serikali kwa asilimia 50.18 na asilimia 49.82 ni kutoka Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (Badea) na Shirika la Opec Fund For International Development (OFID).
Anasema, mradi huo utakapokamilika unatarajia kuwahudumia wananchi zaidi ya laki nne wa vijijini 24 vya tambarare wilaya za Same na Mwanga na vitano katika Wilaya ya Korogwe.
Butiku aitaka Serikali Izingatie fidia kwa wanaobomolewa

Mwanasiasa mkongwe nchini, Joseph Butiku amesema wakati Serikali inatekeleza miradi yake mikubwa, kama ujenzi wa miundombinu, izingatie suala la fidia kwa wananchi wanaotakiwa kupisha miradi.
Amesema hayo wakati wakazi wa maeneo kadhaa nchini, hasa Ubungo hadi Kibaha, wakibomolewa nyumba zao kupisha upanuzi wa Barabara ya Morogoro huku wengine wakipisha ujenzi wa reli pana.
Katika maeneo mengi, wananchi hawajalipwa fidia kwa maelezo kuwa wamejenga ndani ya hifadhi ya barabara, wakiwemo wakazi wa Kimara hadi Kiluvya ambao wamebomolewa kwa kuzingatia utashi wa sheria ya kabla ya nchi kupata uhuru.
Akizungumza katika mahojiano na Mwananchi mwishoni mwa wiki, Butiku, ambaye alikuwa msaidizi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisema ni lazima jitihada za Serikali zielekezwe katika kufanya mambo yanayowaridhisha wananchi na yanayowajengea amani.
“Kwa mfano, juzi kuna mtu aliniuliza kuhusu bomobomoa, nikasema itaendelea. Kwa nini, kwa sababu barabara tunataka kupanua, mabwawa ya maji yanataka kuchimbwa, reli tunataka kujenga, maeneo ya kucheza watoto yawepo,” alisema.
“Yote hayo hayapo, katika kuyaweka kutakuwa na maamuzi ya kuvunja nyumba zilizo mahali hapo.”
Alisema wakati hatua hiyo inatekelezwa, kikubwa ni wale ambao walikuwa wamejenga maeneo yanayotakiwa kwa miradi na hawakujua kwamba ni eneo la barabara au mradi mwingine, wafidiwe.
Butiku alisema inabidi siku zote mambo yanayotendeka yafanyike kwa jina la wananchi kama Rais John Magufuli anavyosema mara kwa mara.
Butiku, ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, alitoa mfano wa mpango wa Serikali kupanua barabara ya Morogoro hadi Chalinze, akisema uamuzi huo haukwepeki. “Sijui wanataka kujenga njia saba, kwa sababu magari yameongezeka. Leo kwenda Morogoro inachukua saa tatu mpaka saa nne, zamani ilikuwa ni saa moja na nusu. Hatuwezi kuendelea hivi lazima kupanua ile barabara. Na hivyo zile nyumba zilizopo zitavunjwa,” alisema.
Lakini alisema kuna watu, wakiwamo hata viongozi, hawakujua upana unaotakiwa wa barabara.
“Mara utasikia barabara hizo zilikuwa mita 22 kutoka katikati ya barabara, mara 35 na sasa nasikia mita 120. Hii mia moja na ishirini sijawahi kuisikia,” alisema.
“Mabarabara haya nimeyakuta Uchina huko. Kama ni hivyo, sawa. Lakini inabidi mliowakuta muwalipe fidia.”
Alisema Serikali inabidi iwatendee haki wananchi hao kwa sababu walijua ni upana wa mita 35, leo zimeongezeka hadi mita 120.
“Inawezekana Serikali haina pesa za kutosha, hilo ni tatizo la Serikali, lakini haki ya huyu aliye na nyumba pale inayobomolewa katika eneo ambalo kwa mujibu wa sheria linapanuliwa na hakujua. Hili si jambo la kubishana, ni jambo la haki tu, jamani,” alisema.
“Na haki inazungumzwa. Serikali ina haki ya kusimamia maendeleo na raia wana haki ya kupata haki yao kama katika kupata maendeleo mali zao zinapotea.
“Lakini kusema hamuwezi kubomoa, ohoo ni maskini. Haiwezekani, sasa umaskini tusiwe na barabara?”
Mzee Butiku alisema kwa Taifa lililokomaa kwa miaka mingi, masuala kama hayo yanatakiwa yawe yametungiwa sheria na sheria inayotokana na Katiba ya wananchi.
Hata hivyo, alisema wakati Tanzania inapita kwenye kipindi cha mpito, kuna maeneo mengi ambayo hayajatungiwa sheria na mengine yametungiwa sheria lakini wananchi hawazijui kwa sababu hakuna aliyezieleza kwao.
Alisema kuna sheria zilizotungwa wakati wa uhuru ambazo hata baadhi ya viongozi wa sasa hawazijui.
“Swali, iko sheria, inasemaje? Wananchi wanaifahamu, tusiende ile ya Waingereza kwamba kutojua sheria si kinga ya kuvunja sheria. Hapana, hiyo ipo lakini tuegemee zaidi kwamba watu wetu hawa kwa miaka hii 56 (ya uhuru) sheria hii hawailewi.”
Alihoji, “kwa mfano sheria zetu za ardhi nani anazifahamu, kwa hiyo ni muhimu kuona watu wetu wanaelewa na pale wanapokuwa hawaelewi ni kutoa nafasi kuhakikisha wanazielewa.”
Hata pale zinapotungwa sheria mpya, Butiku alishauri kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kupitia wabunge au vyombo vya Serikali ili kuchukua mawazo yao kwa kuwa sheria inayotungwa ni kwa ajili yao.
Jengo la Tanesco
Akizungumzia uamuzi wa kubomoa sehemu yake kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro, Butiku alisema huo ni ujumbe kuwa hakuna nyumba itakayobaki kwenye eneo hilo.
“Juzi nilifurahi Rais Magufuli amezuia bomoabomoa. Nadhani alizuia ili kuondoa wasiwasi, sijui, sitaki kumsemea lakini baadaye akafanya kitu cha mfano akaenda pale Ubungo akasema lile jengo la Tanesco libomolewe,” alisema. “Sasa ukishabomoa jengo la Serikali la nani litabaki? Nadhani hiyo ndiyo meseji. Kama hili limekwenda ili barabara ipite mengine yote yatatoka,” alisema.
Hata hivyo, katika utekelezaji wa uamuzi huo, alisisitiza fidia iwepo.
Mahakama
Akizungumzia wakazi wa Kimara waliokuwa na kesi mahakamani, Mzee Butiku alihoji walikuwa na lengo gani, walipwe fidia au wazuie barabara isijengwe.
Alisema kama ni suala la fidia mahakama inaweza kusema walipwe lakini barabara ijengwe. Kama hakuna pesa kwa sasa, inaweza kusubiri hata ikalipwa mwakani.
Subscribe to:
Posts (Atom)