Thursday, 23 November 2017

Mnada wa nyumba za Lugumi kufanyika tena kesho



Mjengo wa Lugumi

NYUMBA mbili za Lugumi ambazo hazikufanikiwa kuuzwa katika minada iliyopita, zitauzwa kwenye mnada utakaofanyika kesho jijini Dar es Salaam maeneo ya JKT Mbweni na Upanga.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya udalali ya Yono, Scolastica Kevela, alipozungumza na vyombo vya habari ambapo alitoa onyo pia kwamba watu wasiokuwa na nia ya kununuanyumba hizo wasifike sehemu hizo kwani watachukuliwa hatua.

Alirudia kusisitiza kwamba watu watakaofanikiwa kununua nyumba hizo ni lazima watangulize asilimia 25 ya bei husika na iliyobaki ilipwe ndani ya siku 14 la sivyo fedha iliyotangulizwa haitarudishwa.

Usajili wa Yanga imebaki siku Tatu



IKIWA Dirisha Dogo la Usajili limefunguliwa Novemba 15 mwaka huu na litafungwa Disemba 15, klabu hutumia kipindi hiki kidogo cha usajili kuongeza wachezaji katika kuimarisha vikosi vyao katika kuelekea Raundi ya 11, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema baada ya siku tatu mambo yatakuwa hadharani.

Mkwasa amesema kwa kipindi hiki bado wapo katika mikakati ya kuangalia wapi panahitaji mtu wa kuziba pengo baada ya hapo watatoa taarifa kamili baada ya kukaa na kamati ya usajili na kutangaza rasmi ni mchezaji gani ameongezwa kwa kusikiliza mahesabu ya Kocha Mkuu George Lwandamina.

Tukiangazia klabu mbalimbali, kwa upande wa Klabu ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo, wakifanya hivyo msimu wa 2014-15, 2015-16, 2016-17, lakini pia wakisimama kama mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo kwa mara 27 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1965, inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 20.

Kwa misimu wa mwaka 2017/18, Yanga wamekuwa wakiweka mikakati katika usajili kwa maana ya kuandaa timu nzuri katika mapambano ligi hii, ndiyo maana kwa sehemu kubwa wameweza kupambana ili kupata pointi na kutaka kuongoza ligi ingawa changamoto kubwa ni michuano ya kimataifa.

Zitto Kabwe afungukia Meli ya Wachina



 Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe, amesema kitendo cha watu kujazana kufuata matibabu kwenye meli ya wachina iliyopo bandarini, inadhihirisha ni namna gani wananchi wanashindwa kumudu gaharama za matibabu, na iwe somo kwa Taifa

Zitto Kabwe ameyasema hayo kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wakewa facebook na kusema kwamba taifa lenye hali kama hii haliwezi kupiga hatua kimaendeleo, hata kama wakijenga miundombinu ya kisasa, na kuitaka serikali kuweka misingi imara kwenye jamii yake.

"Nimepita kituo cha reli ya kati Dar na kuona msururu wa watu. Nimeambiwa wanakwenda kwenye meli ya madaktari wa wachina. Hii ni ishara kuwa watu wetu wanaumwa na hawana uwezo wa kuhudumia afya zao. Taifa lenye hali hii haliwezi kamwe kusonga mbele hata lijenge fly overs kila kona. Maendeleo ni watu, hili liwe somo. Tujenge Hifadhi ya Jamii ya Taifa ili tuwe na Taifa lenye afya bora na Uchumi shirikishi", ameandika Zitto Kabwe.

Hivi karibuni meli kutoka china yenye madktari bingwa imetia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam, na kutoa huduma ya matibabu kwa wakazi wa jiji hilo bila gharama zozote.

Wasanii 2O wakatwa kwenye Fiesta Dar

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, Alhamisi hii katika kipindi cha Clouds360, amesema amepunguza wasanii 20 katika list ya wasanii ambao walipanga kuwepo kwenye show ya tamasha hilo linalotarajiwa kufa
nyika Jumamosi hii katika viwanjwa Leaders Club.




Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba

Ruge alisema miongoni mwa wasanii hao walioondolewa kisa muda ni pamoja na Lulu Diva, Zaiid, pamoja na ChinBeez.

‘’Tulikaa kama kamati jana tunatumia nguvu kubwa mno kwenye suala la muda wakati tuna shoo kubwa iliyokamilika, kwahiyo tumeamua kuachana na suala la muda,tumeamua tukae kwenye muda tulioupanga sisi na kuhakikisha tuna ‘six hours’ za entertainment ambazo zimepangwa na kupangika,” alisema Ruge.

Aliongeza, “Kitakachokosekana ni wale wasanii zaidi ya 20, kama, Bright, Mimi Mars,Lulu Diva, Zaiidyao, ChinBeez,hao bahati mbaya ni lazima tuwaondoe kwa sababu ya ratiba kubana kutokana na muda, tungeweza kuwaingiza lakini hatuna muda’’



Mashinji akanusha taarifa kuhusu kuhamia CCM




Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  Dkt. Vicent Mashinji amekanusha habari za kwamba anahamia Chama cha Mapinduzi na kusema kwamba yeye siyo mtu wa kuamini kwenye zidumu fikra za Mwenyekiti bali nguvu ya mamlaka ya umma.

Mashinji amesema kwamba yeye siyo mjamaa bali ni mlengo wa kipepari hivyo amewataka wananchi wawe na amani kuhusu hizo taarifa za yeye kuhamia CCM si za ukweli.

"Napokea simu nyingi eti nahamia CCM, mi si Mjamaa. Mi ni mlengo wa kibepari. Siamini kwenye “zidumu fikra za mwenyekiti” Ninaamini katika “nguvu na mamlaka ya umma”. Naomba ndugu zangu muwe na amani kabisa" Mashinji.

Dkt Mashinji ameongza kwamba "Nitaendelea kutumikia CHADEMA kwa makini na kutimiza ndoto za watanzania".

Kamikaze na tuhuma za kumzalilisha mpenzi wake

Star wa Bongo Fleva Cyril Kamikaze amefunguka kupitia eNEWZ kuhusu tuhuma zinazomkabili za kumzalilisha mpenzi wake Feza Kessy kwa kuanika picha inayoonyesha matiti yake katika mtandao wake wa instagram.



Kamikaze amesema haoni tatizo lolote la ile picha kwani ni picha  ya kawaida sana na haijaonyesha kiungo chochote cha Feza anachojua ni kwamba picha ile inaonyesha sehemu kidogo ya matiti  ya Feza ambapo ni sawa tu na wanawake wanaovaa brazia kuyabusti maziwa yao ili yaonekane.

Hata hivyo Kamikaze amesema hawezi kumdhalilisha Feza kwani anamuheshimu sana na Feza ndo alipiga ile picha na kumtumia yeye na hata alipoipenda na kuamua kuipost katika mtandao wake wa instagram alimpigia Feza kumuambia kuwa anaipost na Feza alikubali bila wasiwasi

Kamikaze amemalizia kwa kusema kuna wasanii wengi wanapiga picha za utupu zaidi hata ya ile mbona watu hawashangai?anamalizia kwa kusema watu wanapaswa kufahama kwamba Feza ni msanii na anapaswa kupiga picha za aina ile ilimradi hayupo uchi.

Mhasibu feki atiwa mbaroni kwa wizi



Mhasibu wa hospitali ya mkoa mjini Singida aliyeachishwa kazi kwa kosa la kumiliki vyeti feki, Edith Talasi (49) mkazi wa Minga,anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kuvunja milango ya ofisi yake ya zamani na kuiba shilingi 873,000 taslimu, kwa kutumia funguo bandia.

Talasi  ambaye imelelezwa kwamba alifanya kazi hospitalini hapo kwa  muda na baadaye alirejeshwa kwenye kituo chake cha kazi manispaa ya Singida,kwenye wizi huo, alimshirikisha mlinzi wake wa nyumba ya kulala wageni Nandau, Antony Felix (51).Mlinzi huyo naye anashikiliwa na polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, ACP Debora Magiligimba, alisema tukio hilo limetendeka Novemba, 21 saa 6.30 usiku huko katika hospitali ya mkoa mjini hapa.

Alisema siku ya tukio muuguzi wa zamu Shamir Omari (27) akitokea maeneo ya mapokezi akielekea wodini, alimwona mtu akiwa amesimama karibu na ofisi ya mhasibu, alisimama akamsalimia na mtu huyo aliondoka.

“Muuguzi huyo aliamini kuwa mtu aliyemwona,huenda alikuwa  mgonjwa au mtu aliyeleta mgonjwa hospitalini.Lakini aliporudi,alimwona mtu yule yule amerudi eneo lile lile, kitendo kilichopelekea amshuku kuwa sio mtu mzuri,” alisema kamanda huyo.

Alisema muuguzi huyo baada ya kumtilia shaka mtu huyo, alitoa taarifa kwa mlinzi wa zamu wa hospitali hiyo, Abubakari Jumanne,ambaye alimweka chini ya ulinzi mtu huyo.

ACP Magiligimba alisema hata hivyo mtu huyo alijitetea kuwa amefika hospitalini hapo, kwa ajili kuchoma sindano na kuonyesha dawa ya unga na kichanganyio chake.

“Wakati wanaendelea na mahojiano hayo,waliona makufuli  mawili ya mlango wa nje/grili yapo chini na mlango huo wa chuma upo wazi. Mtuhumiwa mlinzi Antony alieleza kuwa bosi wake (mtuhumiwa Edith) kwa wakati huo,alikuwa ndani ya ofisi ya mhasibu amejifungia ndani,” alisema.

 Akifafanua  alisema  jeshi la polisi baada ya kupata taarifa ya wizi huo, liliweza kufika eneo la tukio na kukuta mlango wa ndani ukiwa umefungwa kwa ndani.

“Walipoamuru mhasibu afungue mlango huo kwa kutumia funguo zake,walimkuta mtuhumiwa (Edith) akiwa amejibanza kwenye kona ya mlango na watumishi wa hospitali hiyo, waliweza kumtambua. Alipohojiwa ameingiaje humo ndani,alionyesha funguo saba (07) na zilipojaribiwa ziliweza kufungua milango yote ya ofisi ya mhasibu,” alisema Magiligimba.

Alisema pamoja na wizi huo wa shilingi 873,000,imeelezwa kwamba aprili mwaka huu,wahasibu wa hospitali hiyo,walibaini upotevu wa shilingi 1,800,000.Oktoba mwaka huu,pia walibaini upotevu wa shilingi 3,600,000.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. David Mwasita,amekiri kutokea upotevu huo lakini wahasibu katika wakati huo,waliweza kuziba upotevu huo, kwa fedha zao za mishahara.

Ameeleza kuwa wahasibu hao walilazimika kutoa fedha zao binafsi, na wasingeweza kutoa taarifa ya upotevu huo, kwa vile milango na kasiki, ilikuwa imefungwa kama kawaida.

ACP Magiligimba amesema kwa sasa wanaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na baada ya kumalizika kwa mahojiano hayo,watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.

Umemuona Dk Shika kwenye video ya Kibamia ya Rostam? Aifanya Itrend #1 Bongo


Kuna tatizo Wema Sepetu kum-wish Davido ‘happy birthday’?


Audio | Runtown – Energy.| Mp3 Download

Audio | Runtown – Energy.| Mp3 Download


Audio | Runtown – Energy.| Mp3 Download




https://cloudup.com/files/iEgGb5Uj9CT/download

Sukari ya viwandani yakwama bandarini Dar




Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) limesema sukari ya viwandani ya wanachama wake imekwama katika Bandari ya Dar es Salaam kwa wiki mbili sasa, jambo linaloweza kuathiri uzalishaji.

CTI imesema wanashindwa kuiondoa sukari hiyo baada ya kukosa kibali cha kufanya hivyo kutoka Bodi ya Sukari kwa kile kinachoelezwa kuwa ni agizo la Serikali kuzuia uagizaji wa bidhaa hiyo.

Hata hivyo, mtaalamu wa sera wa CTI, Akida Mnyenyelwa alisema agizo hilo halikulenga sukari hiyo inayotumika viwandani kuzalisha bidhaa za aina tofauti kama vile dawa na vinywaji baridi.

“Jambo kubwa linalosababisha sukari hiyo kukwama ni wahusika kushindwa kutofautisha kati ya sukari ya kawaida na ya viwandani. Kutokana na sukari hiyo kutozalishwa katika nchi zote za Afrika Mashariki (EAC), upo utaratibu wa kuiingiza ndani ya nchi wanachama tena kwa msamaha wa kodi. Nchini, hutozwa ushuru wa asilimia 10 tu,” alisema Mnyenyelwa.

Alisema kutokana na zuio hilo, baadhi ya viwanda vimekosa sukari kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa licha ya taratibu zote muhimu za kuingiza mzigo huo kufuatwa.

Mtalaamu huyo alisema uingizwaji wa sukari hiyo umefuata taratibu zote zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupata vibali vya uagizaji kwa ajili ya matumizi ya viwanda.

Taratibu zilizopo kukamilisha uingizaji wa sukari hiyo, Mnyenyelwa alisema, muombaji anatakiwa kupata ruhusa ya Bodi ya Sukari ambayo itapeleka taarifa zake Mamlaka ya Mapato (TRA) inayopitia orodha ya waombaji wote kabla ya kupeleka majina ya waliokidhi vigezo kwenye Sekretarieti ya EAC.

Alisema majina ya waombaji walioridhiwa na nchi zote wanachama wa EAC yakishapokelewa, huchapwa kwenye gazeti la jumuiya hiyo kisha kupata msamaha wa kodi kwa mujibu wa sheria.

Baada ya hapo, kila muombaji anaweza kuagiza mzigo kwa kadri alivyopendekeza na kukubaliwa kwenye maombi yake. Kwa waagizaji wa nchini, hupaswa kupata kibali cha Bodi ya Sukari kuwaruhusu kuiondoa bandarini.

“Huko ndiko tulikokwama. Bodi haijatoa vibali tangu Rais (John Magufuli) azuie uagizaji wa sukari. Tunaambiwa wameomba ufafanuzi ofisi ya waziri mkuu lakini mpaka sasa hawajajibiwa, hivyo sukari bado ipo bandarini,” alisema.

Miongoni mwa waagizaji ambao sukari yao imekwama, alisema ni Bonite Bottles iliyoagiza tani 650 na Nyanza Bottles yenye tani 1,450. Alisema kwamba kuendelea kubaki bandarini hapo kunaongeza gharama za utunzaji (storage) pamoja na tozo za bandari (demurrage charges).

“Uhakiki matumizi ya sukari hii ikishaingia hufanywa na TRA kujiridhisha kama inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa,” alisema Mnyenyelwa.

Februari mwaka jana, Rais Magufuli alipiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje ili kuvilinda viwanda vya ndani na kuagiza vibali vyote vya kufanya hivyo vitolewe na ama ofisi yake au ya waziri mkuu. Akiwa kwenye ziara wilayani Missenyi hivi karibuni ambako pia alitembelea kiwanda cha Sukari Kagera, alisisitiza kuwalinda wazalishaji hao.

Uongozi wa Bodi ya Sukari ulithibitisha kuwapo kwa changamoto za kutoa vibali vya kuondoa sukari hiyo bandarini lakini ukasema juhudi za makusudi zinaendelea kuhakikisha muafaka unapatikana.

“Jana (juzi) viongozi wa bodi wakiwa na wawakilishi CTI walikutana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Ndani ya siku mbili tatu hizi mambo yatakaa sawa,” alisema ofisa mmoja ambaye si msemaji wa bodi hiyo.

Kwa kutambua kero iliyopo, waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema atawaondoa wafanyakazi wote wanaokwamisha utoaji wa mizigo bandarini hapo kabla hajawajibishwa.

“Nitawafuta mmoja baada ya mwingine na kuna mtu mmoja anaitwa Khalid anashinda sana bandarini. Nitamtoa hata kama aliteuliwa na nani,” alisema Mwijage.

Alisema kwa hali ya Tanzania ilivyo sasa bado inaagiza bidhaa nyingi kutoka nje kuliko inazouza, hivyo ni lazima atengeneze mazingira mazuri yasiyo na vikwazo kutoka kwa watumishi wa idara hiyo nyeti.

Waziri huyo alisema hayo jana alipokuwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa majengo matatu ya usambazaji bidhaa za kampuni ya NBMG kutoka China utakaogharimu Dola 75 milioni za Marekani (zaidi ya Sh165 bilioni).

Mama Ndikumana afunguka waliomuua mwanae




Hamad Ndikumana ‘Ndiku’ enzi za uhai wake.

DAR ES SALAAM: Wakati muigizaji nyota wa filamu nchini, Irene Uwoya akiwa nchini Rwanda kuhani msiba wa aliyekuwa mumewe, Hamad Ndikumana ‘Ndiku’, mama mzazi wa mwanasoka huyo wa zamani wa kimataifa, amewataja watu waliohusika kusababisha kifo cha mwanaye.

TUJIUNGE KWANZA NA UWOYA
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko kutoka Kigali aliko msibani, Uwoya alisema awali alipata taabu ya kufanya mawasiliano na ndugu na jamaa wa mumewe huyo wa zamani na baada ya kuwakosa, akaamua kuwasiliana na Asma, mwanamke ambaye siku chache nyuma, Ndikumana aliposti picha zake katika mtandao wa kijamii, akimnadi kama mpenzi wake.

“Nilipompata huyo, nikajitambulisha na kumwambia juu ya nia yangu ya kutaka kuja huku, katika namna ya kufurahisha, akanikubalia na tangu wakati huo ndiye nilikuwa nawasiliana naye na hata nilipofika hapa, yeye ndiye alinipokea na kunipeleka nyumbani kwa wazazi wa Ndikumana,” alisema muigizaji huyo. APELEKWA KWA

WAZAZI, WAMKUBALI
Uwoya ambaye alizaa na marehemu mtoto mmoja wa kiume aitwaye Krish, alisema baada ya kufikishwa nyumbani kwa wazazi wake, alipokelewa vizuri na ndugu na jamaa ambao walimweleza kuwa hawana kinyongo naye kwa sababu mambo yote yaliyotokea huko nyuma ni mapito ya duniani.

Irene Uwoya akiwa na Ndikumana enzi za uhai wake.
“Yaani huwezi kuamini, walinipokea vizuri sana, tofauti kabisa na huko nyumbani jinsi wanavyonizungumzia. Nimekaa nao na wao ndiyo walioniambia kitu ambacho kilinishangaza sana kuhusu chanzo cha kifo cha Ndikumana,” alisema Uwoya.

SIKU YA TATU MAMA MKWE AMDUWAZA

Uwoya alisema ilipofika siku ya tatu ya msiba, ambayo kwa kawaida ndiyo siku ya kuanua matanga, mama huyo alimweleza wazi juu ya watu ambao wanahusika na kifo cha mtoto wao, ambao familia inawatambua na inajua namna ya kushughulika nao.

“Mama Ndiku alisema anawafahamu waliomuua mtoto wao, alisema ni wachezaji wenzake sijui, wale watu wake wa mpira, wanasema chanzo ni kuwa yeye alikuwa mtu anayependwa na viongozi wa timu, hicho ndicho kilichowafanya wenzake wawe na wivu naye.

“Alinishtua sana, anasema wamegundua kuwa Ndiku aliwekewa sumu na wenzake na suala hilo linashughulikiwa na familia yao, sijajua watachukua hatua gani, lakini hicho ndicho kinachoendelea huku msibani,” alisema.

MANENO HAYO YAMEMFARIJI

Uwoya ambaye baadhi ya wadau wanamtaja kama mtu aliyesababisha msongo wa mawazo kwa mumewe baada ya hivi karibuni msanii Dogo Janja kung’ang’ania amefunga ndoa na muigizaji huyo, alisema kwa maneno hayo, amefarijika, kwani angalau mzigo wa lawama atautua.


“Maneno yalikuwa ni mengi sana kwa kweli huko nyumbani, kila mtu Uwoya Uwoya, afadhali mama amekata mzizi wa fitina, kifo chake wala siyo msongo wa mawazo, ni mchezo aliochezewa na wenzake huko kwenye mambo yao ya mpira,” alisema.

KWA NINI ALITAJWA UWOYA?

Kifo hicho cha ghafla cha Ndikumana, aliyefariki usiku wa Novemba 14 mwaka huu, kilisababisha baadhi ya watu kumtaja Uwoya kuwa huenda akawa chanzo kutokana na mtiririko wa matukio tangu ndoa ya wawili hao ilipovunjika miaka michache iliyopita.

Kwa muda wote ambao wawili hao walikuwa tofauti, Uwoya amekuwa akidai apewe talaka yake ili awe huru kuolewa na mtu mwingine, kitendo ambacho kinadaiwa kumuumiza mchezaji huyo wa zamani wa Stand United ya Shinyanga.

wakazi Dar wailalamikia Bomoabomoa mpya




picha ya mtandao

Wakati wafanyakazi wa Wakala wa Barabara (Tanraods) wakiendelea kuweka alama kwenye nyumba zinazotakiwa kubomolewa kupisha upanuzi wa Barabara ya Morogoro, wakazi wanaoishi kati ya Ubungo na Kimara wamelalamikia kitendo hicho.

Baada ya kutekeleza ubomoaji wa nyumba kati ya Kimara na Kiluvya zilizo ndani ya mita 121.5 kutoka katikati ya barabara hiyo, ubomoaji mwingine utazikumba takriban nyumba 1,200 zilizo ndani ya mita 90, zikiwemo tano za ibada, vituo vya mafuta na majengo ya biashara nyingine kama za starehe.

Ubomoaji huo pia utalikumba moja ya majengo maarufu ya makao makuu ya Shirika la Umeme (Tanesco) lililopo Ubungo.

Eneo hilo na mengine ndiyo yaliyozua utata mwaka 2011 baada ya kutangazwa ilani ya kubomoa nyumba zote zilizo ndani ya hifadhi ya barabara bila ya kulipa fidia na kumsukuma aliyekuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutangaza kusimamisha ubomoaji ili kusubiri uamuzi wa Baraza la Mawaziri.

Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete pia alisema bila ya kutaja eneo kuwa ubomoaji ni lazima uzingatie historia ya eneo husika na haki za binadamu kwa kutoa muda wa kutosha kwa wakazi ikiwa nyumba zao ni lazima zibomolewe kutokana na mipango ya Serikali.

Mpango huo ulisimama na sasa, miaka saba baadaye, ubomoaji huo umefufuliwa na wafanyakazi wa Tanroads wanapita maeneo hayo kuweka alama ya “X”.

Wakizungmza kwa nyakati tofauti, wananchi wa maeneo hayo waliiambia Mwananchi kuwa kitendo cha kubomoa nyumba zao kitawasababishia machungu kwa kuwa hawajui pa kwenda.

“Kubomoa nyumba kutanizidishia msongo wa mawazo. Mume wangu alifariki mwaka juzi na nimebaki na watoto watatu. Nategemea nyumba hii kama njia ya kuniingizia kipato,” alisema mkazi wa Kimara Baruti aliyejitambulisha kwa jina la Furaha Nassoro ambaye ameishi eneo hilo kwa miaka 12.

“Nimeweka wapangaji vyumba sita. Hii ndiyo ajira yangu, sina kazi wala biashara ngingine.”

Alisema wakati Tanroads wanakwenda kuweka alama, walimtaka awe ameondoka ndani ya mwezi mmoja, hali iliyompa wakati mgumu kwa kuwa hautoshi.

“Watoto wangu wote wanasoma kwa uhamisho wa harakaharaka hivi nawezaje kumudu gharama hizi? Mwezi ujao kama watakuja kubomoa, itabidi wanangu wasiende shule hadi hapo nitakapopata pesa kwa ajili ya kuhama,” alisema.

Alisema kinachofanyika ni kwa ajili ya maendeleo, lakini alidai kuwa maendeleo hayawezi kuja wakati wananchi wana machungu ya kubomolewa nyumba na badala yake kulala nje. Mkazi mwingine wa Ubungo, James Haule alisema alipokea kwa huzuni taarifa ya nyumba yake kuwekwa alama ya kutakiwa kubomolewa kwa kuwa alimaliza ujenzi wa nyumba hiyo mwishoni mwa mwaka jana.

Haule aliiomba Serikali kuongeza miezi mingine miwili.

“Mwezi mmoja dada hautoshi. Tuna watoto, tunasomesha, maisha yenyewe ya sasa kama unavyoyaona. Mwezi huu mmoja napata wapi pesa ya kupanga au Serikali inataka tuaibike?”alihoji.

Katika eneo jingine, Mwananchi ilimkuta mzee aliyejitambulisha kwa jina la Onesmo Mwinuka akiwa nje ya nyumba yake huku akitazama alama ya “X”, usoni akionekana kupoteza matumaini.

“Hivi si walishabomoa Kimara? Huku tena wanataka nini? Kwani eneo lote la Kimara halitakiwi kuishi mtu? Sisi ni wanyonge, Rais atuonee huruma,” alisema Mwinuka.

Alisema kwa kuwa lengo la Serikali ni kuleta maendeleo ya nchi, lakini pia iangalie namna ya kuwasaidia wazee kwa vile maisha yao yatakuwa hatarini watakapobomolewa.

Diwani wa kata ya Kimara, Pascal Manota alisema alishaongea na wananchi kuwataka wajiandae kulipokea suala hilo kwa kuwa haliwezi kuepukika.

Alisema kwa sasa anawashauri wananchi hasa wapangaji kulipa kodi ya muda mfupi ili kuepuka hasara baadaye kwa kuwa muda wowote huenda Tanroads wataanza kubomoa nyumba hizo.

“Wametoa notisi ya mwezi mmoja, kwa hiyo huenda mwezi ujao zoezi la kubomoa likaanza kwa hiyo nini cha kufanya ni kuwashauri tu wananchi wajipange na kuzoea hii hali,” alisema. Akizungumza na Mwananchi, meya wa Ubungo, Boniface Jacob alisema amewaambia wananchi wapeleke suala hilo mahakamani ili wapewe haki zao na atawatafutia mwanasheria.

Alisema kitendo cha kutoa mwezi mmoja ni kuwanyima haki kwa kuwa ilibidi wananchi wafuatilie kwanza kujua hatima yao.

Meneja wa Tanroads wa mkoa, Julius Ndymukama alisema uwekaji alama utafuatiwa na ubomoaji.

“Tumetoa notisi ya mwezi mmoja na baada ya hapo tutaanza kubomoa,” alisema.