Thursday, 16 November 2017

Breaking: Hatimaye Mhasibu mkuu wa Takukuru afikishwa mahakamani

Breaking: Hatimaye Mhasibu mkuu wa Takukuru afikishwa mahakamani



MHASIBU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai,  anayedaiwa kumiliki mali nyingi kuliko kipato chake, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma zinazomkabili.

Gugai amefikishwa katika mahakama hiyo baada ya taarifa iliyotolewa siku chache zilizopita na Naibu Kamishna wa Takukuru, Brigedia John Mbungo,  kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa ametoroka.  Mtuhumiwa huyo anatajwa kumiliki majumba na viwanja karibu kila mkoa nchini.

Mchoro ya Yesu wauzwa dola milioni 450 Marekani

Mchoro ya Yesu wauzwa dola milioni 450 Marekani



Mchoro ya Yesu Salvator Mundi au (Mkombozi wa Dunia) umeuzwa dola milioni 450 Marekani
Mchoro wa miaka 500 wa Yesu unaoaminiwa kuchorwa na Leonardo da Vinci, umeuzwa mjini New York kwa kima cha dola milioni 450.

Mchoro huo unajulikana kama Salvator Mundi (Mkombozi wa Dunia).

Ndio mchoro wa bei ya juu zaidi kuwai kuuzwa kwa mnada.

Leonardo da Vinci alifarika mwaka 1519 na kuna chini ya 20 ya michoro yake iliyobaki.

Ni huo mmoja tu unaoaminiwa kuwa mikononi mwa mtu ambao unaamimiwa kuwa ulichorwa baada ya mwaka 1505.

Picha hiyo inamuonyesh Yesu akiwa ameunua mkono mmoja huku mwingine ukishika kioo.

Mwaka 1958 mchoro huo uliuzwa kwenye soko la mnada mjini London kwa Dola 60. Wakati huo mchoro huo uliaminiwa kuwa kazi ya mfuasi wa Leonardo na wala haukuwa wa Leonardo mwenyewe.

Miaka minne iliyopita mchoro huo ulinunuliwa na raia wa Urusi kwa dola milion 127.5 lakini wakati huo hakuuzwa katika mnada

TRA yapiga stop mabasi ya Kilimanjaro

TRA yapiga stop mabasi ya Kilimanjaro


Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesitisha utoaji huduma za usafiri kwa Kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express Ltd baada ya kushindwa kulipa kodi ya Sh500 milioni.

Akizungumza na gazeti hili jana, mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema wamefikia uamuzi huo baada ya majadiliano ya muda mrefu na uongozi wa kampuni hiyo kutokuzaa matunda.

Kayombo alisema kwa kipindi cha hivi karibuni biashara haikuwa nzuri kwa kuwa mabasi yake 26 yalipungua hadi 12, lakini si kigezo cha kutolipa kwa kodi ya Serikali.

“Ni kweli Kilimanjaro Express inadaiwa Sh500 milioni, jambo ambalo lilitufanya kusimamisha shughuli zake tangu Jumatatu (Novemba 13) hadi atakapolipa kodi anayodaiwa,” alisema.

Naye mmiliki wa kampuni hiyo, Roland Sawaya alisema wamezuia mabasi yake ambayo yalikuwa yameegeshwa katika ghala mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, huku akieleza kuwa amekuwa akilipa deni hilo kwa awamu.

Sawaya alisema hivi karubuni alilipa Sh50 milioni na mwezi huu walitaka kulipa Sh35 milioni, lakini TRA walikataa na kuwataka kulipa kiwango chote huku akieleza kuwa mazungumzo yanayoendelea ana imani yatafikia mwafaka.

Kilimanjaro ambayo imekuwa ikifanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Moshi na Arusha kwa zaidi ya miaka 20 ni kampuni tanzu ya Kilimanjaro Cargo Truck


Kukataliwa kwa ripoti wazua mjadala

Kukataliwa kwa ripoti wazua mjadala



Dar es Salaam. Licha ya maofisa wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kuzuia kuzinduliwa kwa ripoti inayoelezea unyanyasaji wa watumishi wa ndani wa Kitanzania wanaofanya kazi nchini Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), hatua hiyo imezua sintofahamu baada ripoti hiyo kupatikana mitandaoni na kuanza kujadiliwa.

Ripoti hiyo inayoitwa ‘Kufanya kazi mithili ya Roboti’ inatokana na utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Utetezi wa Haki za Binadamu (Human Rights Watch), ilikuwa izinduliwe juzi lakini ilishindikana baada ya kuzuiwa.

Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena alisema hatua ya kuzuia kuzinduliwa kwa ripoti hiyo wakati tayari wanahabari walishafika kwa ajili ya shughuli hiyo ni kunyima uhuru wa habari.

Hata hivyo, Meena alisema Serikali inapaswa kuipokea na kusoma uhalisia wa maisha ya watumishi wa ndani kwenye nchi hizo, ili kutumia mapendekezo yaliyoainishwa kutatua tatizo hilo.

“Serikali wamekuwa wakali bila sababu. Hata hivyo, hakuna kipya kilichozuiliwa kwa sababu ripoti ipo na imeshasambaa,” alisema.

Naye ofisa mawasiliano wa Shirika la Human Rights Watch, Audrey Wabwire alisema hata kabla ya uzinduzi wa ripoti hiyo ilikuwa tayari imewekwa mtandaoni.

Akizungumza kwa simu, mmoja na wanawake waliohojiwa kwenye ripoti hiyo anayeishi Bagamoyo, alisema alitoa ushirikiano alipohojiwa na watafiti wa shirika hilo.

“Nilisharudi na nafanya kazi nyingine siku hizi, lakini walikuja kunihoji na niliwapa ushirikiano mzuri nikieleza nilivyofanyiwa,” alisema.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu ch Dar es Salaam (UDSM), Profesa Benson Bana alisema hakubaliani na hatua ya kuzuia ripoti hiyo wakati inatetea maslahi na utu wa Mtanzania.

“Naona kuna mkono wa mtu hapo ambaye pengine ana maslahi binafsi amezuia ripoti isiwafikie watu. Utazuiaje wakati watu wameshafanya utafiti, unategea hadi wakati wa kuizindua ndipo uzuie?” Alihoji Profesa Bana.

Ofisa mtafiti wa Costech, Dk Willium Kindeketa alisema ripoti hiyo imezuiliwa na tume hiyo kwa kuwa ndiyo yenye mamlaka na kwamba, watafiti hawakufuata taratibu zinazotakiwa ikiwamo kupeleka wasifu wa watafiti husik

Hatua ya jeshi la Zimbabwe ni kama mapinduzi: AU

Hatua ya jeshi la Zimbabwe ni kama mapinduzi: AU


Mkuu wa AU Alpha Conde

Hatua ya jeshi la Zimbabwe ya kuchukua madaraka na kumzuilia Rais Robert Mugabe, inaonekana kama mapinduzi wa kijeshi, Muungano wa Afrika AU umesema.

Mkuu wake, Alpha Conde, alisema kuwa AU inataka kurejea mara moja hali ya kawaida.

Jeshi linakana kufanya mapinduzi ya kijeshi, na kusema kuwa Mugabe yuko salama, na kuwa hatua zao ni dhidi ya waalifu wanaomzunguka.

Hatua ya jeshi inafuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi Bw. Mugabe.

Makamu wa rais, Emmerson Mnangagwa alifutwa kazi wiki iliyopita, na kuchangia mke wa rais Grace kuwa na fursa wa kumrithi Mugabe, hali iliyosababisha maafisa wa vyeo vya juu jeshini kuhisi kutengwa.

Bwana Mugabe 93, ametawala siasa za nchi tangu ipate uhuru kutoka Uinghereza mwaka 1980.

Akijibu yale yaliyotokea Bw. Conde ambaye pia ni rais wa Guinea, alisema kuwa wanajeshi wa Zimbabwe walikuwa wamejaribu kuchukua madaraka.

Mwandishi wa BBC aliye nchini Zimbabwe anasema kuwa Misri ilifukuzwa kutoka AU wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2013, kwa hivyo jeshi la Zimbabwe linaweza kuwa linajaribu kuzuia hali kama hiyo kw kutaja hatua yao kuw isiyo mapinduzi ya kijeshi



Viboko 12 vyamngoja ‘bilionea’ nyumba za Lugumi


Busega. Siku moja baada ya Jeshi la Polisi kumwachia kwa dhamana, Dk Loius Shika ambaye alikuwa ameshikiliwa kwa siku sita kwa madai ya kuharibu mnada wa nyumba za Said Lugumi, familia ya daktari huyo imesema lazima achapwe viboko 12 kama anataka kusamehewa.

Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwake katika kitongoji cha Misheni katika Kijiji cha Chamugasa juzi, kaka mkubwa wa Dk Shika, Pelanya Lunyalula alieleza kuwa mila na tamaduni za kabila la Wasukuma hazitoi msahama hivihivi hadi pale kikao cha baraza la ndugu kitakapoketi na kumpa adhabu ya viboko.

“Mpaga ibanza lya badugu (hadi kwenye kikao cha baraza la ndugu wa ukoo) wakiketi kumjadili na yeye akiwepo ndipo uamuzi hufanyika wa kumuonya kwa tabia za kudharau ukoo na huchapwa viboko zaidi ya 12 na kutakiwa kujirekebisha vingine atafutwa kabisa,” alisema.

Lunyalula alisema uamuzi huo hufanywa endapo mtu kama huyo ameamua kutengana na ndugu zake kama anavyodaiwa kufanya Dk Shika kwa madai misiba mingi imetokea na yeye kupatiwa taarifa lakini hakufika kuhani.

“Hii ni dhahiri kwamba ameona ndugu zake hawaendani na elimu yake kitendo ambacho kila mmoja alishakichukia, hivyo hata hilo suala lililomkuta huenda ni malipo ya matendo yake aliyoyafanya,” alisema Pelanya mwenye umri wa miaka 84.

Kauli hiyo iliungwa mkono na mpwa wa Dk Shika ambaye pia ni mwenyekiti wa Kitongoji cha Misheni, Emmanuel Komanya ambaye alitumia nafasi hiyo kuwaonya watu wengine wasiige tabia kama hiyo.

Ndugu hao ambao kwa pamoja walionekana kuwa na huzuni wakati wakizungumza na Mwananchi baada ya kupata taarifa za kushikiliwa kwake, walisema hawataweza kwenda kuonana naye.

“Kwanza familia yetu ni masikini hatuna uwezo wa kutafuta fedha za kwenda huko, lakini pia hata kama tungekuwa na uwezo tusingeweza kwenda (Dar es Salaam),” alisema.

Hata hivyo, Dk Shika mwenyewe alipozungumzia kuhusu familia yake hiyo alisema hawasiliani nayo kwa kuwa huenda wenzake hawana simu na hadhani kama atakwenda huko kwa kuwa wazazi wake wote wameshakufa hivyo hata akienda haitasaidia.

Juzi Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilifikia uamuzi wa kumwachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kujidhamini mwenyewe kutokana na kukosa mtu wa kumwekea dhamana.

Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema, “uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyefika kutaka kumwekea dhamana, yaani anaishi kama mtu wa nyikani.


Ndikumana azikwa

Ndikumana azikwa



 Mwili wa nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda, Hamadi  Ndikumana Katauti na mume wa muigizaji wa filamu Bongo, Irene Uwoya, umezikwa jana katika makaburi yaliyopo kwenye mji wa Nyamirambo nchini Rwanda.

Ndikumana ambaye pia ni baba wa  watoto waili huku mmoja akiwa amezaa na Irene Uwoya, amezikwa na mamia ya wadau wa soka nchini humo wakiwemo mashabiki wa klabu ya Rayon Sport, ambayo alikuwa akifanyia kazi kama kocha msaidizi.

Taarifa zaidi zinasema kwamba Irene Uwoya hakuwahi kuhudhuria mazishi hayo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Ndikumana alifariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake nchini Rwanda, na kuacha majonzi makubwa kwa wapenzi wa soka na watu wake wa karibu, kutokana na kifo chake kilichotokea ghafla bila kuumwa.

Tazama hapa watu walivyojazana msibani



Msekwa anena kilichotokea kwa Mugabe

Msekwa anena kilichotokea kwa Mugabe


Dar es Salaam. Sintofahamu iliyotokea Zimbabwe baada ya jeshi la nchi hiyo kutanda jijini Harare na kumuweka chini ya uangalizi Rais Robert Mugabe imeelezwa ni jambo jipya ambalo halijawahi kutokea.

Baada ya taarifa kusambaa kuwa jeshi linaidhibiti nchi hiyo baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa hapa nchini mbali ya kueleza kuwa ni jipya, pia wameeleza kuwa ung’ang’anizi wa madaraka ni tatizo.

Akizungumza na Mwananchi jana kuhusu kilichotokea Zimbabwe, makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa alisema ni jambo jipya kuwahi kutokea katika kipindi hiki ambacho nchi nyingi za Afrika zinafuata mfumo wa demokrasia wa kuchagua viongozi kupitia vyama.

Msekwa, ambaye pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge alisema anasita kuita mapinduzi kutokana na kilichotokea Zimbabwe kwa kuwa mapinduzi ya kijeshi huhusisha kuitoa Serikali iliyopo madarakani kisha jeshi kushika hatamu, jambo ambalo kwa nchi hiyo wanajeshi wametangaza kuwa hawako tayari kukamata madaraka.

“Katika kumbukumbu zangu sikumbuki kama hili jambo limewahi kutokea tangu miaka ya 60, kuna tofauti kubwa sana kuita haya ni mapinduzi ya kijeshi. Ni mapinduzi kwa sababu Serikali iliyokuwepo imetolewa lakini jeshi limesema halina nia ya kuchukua madaraka, ni jambo jipya sana kwangu ndiyo maana nasita kuita ni mapinduzi ya kijeshi,” alisema.

Hata hivyo, kada huyo wa chama tawala alisema kila jambo lina mwanzo wake pengine na hilo limekuja kwa makusudi ili watu wajifunze.

Msekwa alilipongeza jeshi hilo kwa kuhakikisha wanafanya mambo hayo kwa amani bila kumwaga damu.

Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Profesa Gaudence Mpangala alisema jambo lililofanyika nchini humo ni matokeo ya ung’ang’anizi wa madaraka, ingawa nyuma Mugabe alisukumwa na chama kilichokuwa kikitaka kiendeee kutawala milele. “Sasa tupo katika utawala wa kijamhuri unaotaka kuwe na uchaguzi huru, ukimuangalia Mugabe alishafika umri wa zaidi ya miaka 90 na bado alikuwa anang’ang’ania madaraka ndiyo maana amepata aibu,” alisema.

Profesa Mpangala alisema Mugabe angejiwekea heshima kubwa kama angekubali kung’atuka mapema na kuandaa vijana ambao wangemrithi na siyo mpaka kusubiri jeshi ‘limpindue’.

Alisema tukio hilo ni funzo kubwa kwa nchi mbalimbali kwa kuwa si kiongozi pekee anayeng’ang’ania madaraka anachokwa, lakini pia chama kiking’ang’ania nacho kinajiweka katika wakati mgumu.

“Ni lazima kuwe na mfumo wa kubadilishana madaraka, hiyo ndiyo demokrasia unayotaka na ni lazima Serikali iweke mazingira ya ushindani sawa kwa vyama vyote vya upinzani,” alisisitiza Profesa Mpangala.

Akizungumzia suala hilo, mratibu wa Mtandao wa Wapigania Haki za Binadamu, Onesmo Ole Ngurumwa alisema Rais Mugabe amejitengenezea mwenyewe mazingira hayo.

“Kilichotokea ni matokeo ya kutoheshimu demokrasia, alikuwa na muda wa kutoka kwa heshima na kuandaa watakaomrithi lakini ameshindwa hilo na matokeo yake akafanya chama ni mali ya familia,” alisema.

Ole Ngurumwa alipongeza hatua hiyo na kusema kuwa ilifika wakati wake na kuwa wananchi walishachoshwa na kiongozi huyo ambaye alianza kuongoza mara tu baada ya uhuru wa nchi hiyo kupatikana kutoka kwa wakoloni wa Uingereza.

Hata hivyo, Ole Ngurumwa alilipongeza jeshi hilo kwa kitendo chake cha kutomwaga damu na kusababisha maafa kwa wananchi.

“Wakati mwingine tunashuhudia damu ikimwagika bila sababu za msingi, tunashukuru jeshi la Zimbabwe limefuata njia bora ya demokrasia ambayo haimwagi damu na kuheshimu watu,” alisisitiza Ole Ngurumwa

TANGAZO: CHUO CHA TUMAINI JIPYA MAFINGA KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO



MKUU WA CHUO CHA AFYA CHA  TUMAINI JIPYA MAFINGA ANA FURAHA KUWATANGAZIA KUWA CHUO KIMEANZA KUPOKEA MAOMBI YA MASOMO KWA MWAKA WA MASOMO 2017/18 KATIKA KOZI ZIFUATAZO.
                                                    
1. CERTIFICATE IN CLINICAL MEDICINE YAANI TABIBU MSAIDIZI KWA MIAKA MIWILI

Sifa za mwombaji: Awe na ufaulu wa kidato cha nne kwa angalau alama D nne yakiwemo masomo ya sayansi yaani Fizikia (Physics), Kemia (Chemistry) na Baolojia (Biology)

2. CERTIFICATE IN COMMUNITY HEALTH (Uhudumu wa afya ngazi ya jamii) MWAKA MMOJA

Sifa za mwombaji: Awe na ufaulu wa kidato cha nne kwa angalau D nne likiwemo somo la Baolojia (Biology)


MUHULA MPYA UTAANZA MWEZI HUU WA SEPTEMBA, 2017.

YOTE HAYO YANAZINGATIA MWONGOZO WA WIZARA YA AFYA NA NACTE.

CHUO KIMESAJILIWA KWA USAJILI WA KUDUMU KWA NAMBA 144.

ADA ZETU NI NAFUU NA ZINALIPWA KWA AWAMU.

FOMU ZINAPATIKANA CHUONI TUMAINI JIPYA MAFINGA – IRINGA AU KWENYE WEBSITE YA CHUO.www.tumainijipya.ac.tz

Kwa maulizo tafadhali wasiliana na chuo kwa namba 0755 535 301 AU 0625 716 530 AU 0754 444 151







Breaking: Hatimaye Mhasibu mkuu wa Takukuru afikishwa mahakamani

Breaking: Hatimaye Mhasibu mkuu wa Takukuru afikishwa mahakamaniMHASIBU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai,  anayedaiwa kumiliki mali nyingi kuliko kipato chake, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma zinazomkabili.


Gugai amefikishwa katika mahakama hiyo baada ya taarifa iliyotolewa siku chache zilizopita na Naibu Kamishna wa Takukuru, Brigedia John Mbungo,  kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa ametoroka.  Mtuhumiwa huyo anatajwa kumiliki majumba na viwanja karibu kila mkoa nchini.

Wednesday, 15 November 2017

Tshishimbi atakiwa na vilabu hivi




Kuna taarifa zinazoeleza kwamba kiungo wa Yanga Pappy Kabamba Tshishimbi anatakiwa na klabu moja ya nchini Afrika Kusini huku pia akitajwa kunyatiwa na klabu ya Azam FC katika kipindi hiki cha dirisha dogo linalofunguliwa leo (Nov 15, 2017).

Taafifa iliyotolewa jana na gazeti moja la michezo nchini imeeleza kuwa, Azam wanataka kutumia upenyo wa Yanga kuyumba kiuchumi ili kumnasa Tshishimbi.

Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema, hadi sasa bado hawajapokea taarifa yoyote mezani kwao kutoka klabu yoyote inayomtaka Tshishimbi.

“Mchezaji kutakiwa na timu ningine si jambo geni, sisi kama klabu hatujapata hiyo taarifa tunasikia kama watu wengine wanavyosikia lakini zitakapofika tutafanyia kazi kwa sababu ni kawaida pia mchezaji kutoka klabu moja kwenda nyingine ni jambo ambalo lipo tangu mpira umeanzishwa duniani kwa hiyo huwezi kumzuia.”

“Hata sisi yupo kwetu kwa sababu alitoka pia timu nyingine kwa hiyo wakati utakapofika tutajua nini kitakwenda kufanyika

Tuesday, 14 November 2017

Takukuru kushuulika na swala la nyalandu

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), imesema kuwa suala la aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu imelisikia na imeanza kulifanyia kazi.
Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbungo amesema kuwa wakimkuta na hatia watamfikisha kunakostahili.
Kauli hiyo ya Mbugo ameitoa leo Jumanne ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala kumlipua Nyalandu akimtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.
Akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/2018 jana Jumatatu Dk Kigwangalla aliiagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu.
Dk Kigwangala alisema Nyalandu aliikosesha Serikali mapato ya Sh32 bilioni kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.
Soma: Waziri Kigwangala amshukia Nyalandu
ziibuliwe sasa zaidi ya miaka miwili tangu aachie uwaziri.