Thursday, 16 November 2017

TRA yapiga stop mabasi ya Kilimanjaro

TRA yapiga stop mabasi ya Kilimanjaro


Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesitisha utoaji huduma za usafiri kwa Kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express Ltd baada ya kushindwa kulipa kodi ya Sh500 milioni.

Akizungumza na gazeti hili jana, mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema wamefikia uamuzi huo baada ya majadiliano ya muda mrefu na uongozi wa kampuni hiyo kutokuzaa matunda.

Kayombo alisema kwa kipindi cha hivi karibuni biashara haikuwa nzuri kwa kuwa mabasi yake 26 yalipungua hadi 12, lakini si kigezo cha kutolipa kwa kodi ya Serikali.

“Ni kweli Kilimanjaro Express inadaiwa Sh500 milioni, jambo ambalo lilitufanya kusimamisha shughuli zake tangu Jumatatu (Novemba 13) hadi atakapolipa kodi anayodaiwa,” alisema.

Naye mmiliki wa kampuni hiyo, Roland Sawaya alisema wamezuia mabasi yake ambayo yalikuwa yameegeshwa katika ghala mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, huku akieleza kuwa amekuwa akilipa deni hilo kwa awamu.

Sawaya alisema hivi karubuni alilipa Sh50 milioni na mwezi huu walitaka kulipa Sh35 milioni, lakini TRA walikataa na kuwataka kulipa kiwango chote huku akieleza kuwa mazungumzo yanayoendelea ana imani yatafikia mwafaka.

Kilimanjaro ambayo imekuwa ikifanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Moshi na Arusha kwa zaidi ya miaka 20 ni kampuni tanzu ya Kilimanjaro Cargo Truck


No comments:

Post a Comment