Thursday, 16 November 2017

Kukataliwa kwa ripoti wazua mjadala

Kukataliwa kwa ripoti wazua mjadala



Dar es Salaam. Licha ya maofisa wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kuzuia kuzinduliwa kwa ripoti inayoelezea unyanyasaji wa watumishi wa ndani wa Kitanzania wanaofanya kazi nchini Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), hatua hiyo imezua sintofahamu baada ripoti hiyo kupatikana mitandaoni na kuanza kujadiliwa.

Ripoti hiyo inayoitwa ‘Kufanya kazi mithili ya Roboti’ inatokana na utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Utetezi wa Haki za Binadamu (Human Rights Watch), ilikuwa izinduliwe juzi lakini ilishindikana baada ya kuzuiwa.

Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena alisema hatua ya kuzuia kuzinduliwa kwa ripoti hiyo wakati tayari wanahabari walishafika kwa ajili ya shughuli hiyo ni kunyima uhuru wa habari.

Hata hivyo, Meena alisema Serikali inapaswa kuipokea na kusoma uhalisia wa maisha ya watumishi wa ndani kwenye nchi hizo, ili kutumia mapendekezo yaliyoainishwa kutatua tatizo hilo.

“Serikali wamekuwa wakali bila sababu. Hata hivyo, hakuna kipya kilichozuiliwa kwa sababu ripoti ipo na imeshasambaa,” alisema.

Naye ofisa mawasiliano wa Shirika la Human Rights Watch, Audrey Wabwire alisema hata kabla ya uzinduzi wa ripoti hiyo ilikuwa tayari imewekwa mtandaoni.

Akizungumza kwa simu, mmoja na wanawake waliohojiwa kwenye ripoti hiyo anayeishi Bagamoyo, alisema alitoa ushirikiano alipohojiwa na watafiti wa shirika hilo.

“Nilisharudi na nafanya kazi nyingine siku hizi, lakini walikuja kunihoji na niliwapa ushirikiano mzuri nikieleza nilivyofanyiwa,” alisema.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu ch Dar es Salaam (UDSM), Profesa Benson Bana alisema hakubaliani na hatua ya kuzuia ripoti hiyo wakati inatetea maslahi na utu wa Mtanzania.

“Naona kuna mkono wa mtu hapo ambaye pengine ana maslahi binafsi amezuia ripoti isiwafikie watu. Utazuiaje wakati watu wameshafanya utafiti, unategea hadi wakati wa kuizindua ndipo uzuie?” Alihoji Profesa Bana.

Ofisa mtafiti wa Costech, Dk Willium Kindeketa alisema ripoti hiyo imezuiliwa na tume hiyo kwa kuwa ndiyo yenye mamlaka na kwamba, watafiti hawakufuata taratibu zinazotakiwa ikiwamo kupeleka wasifu wa watafiti husik

No comments:

Post a Comment