Wednesday, 25 October 2017

Audio | Baraka Da Prince _ Sometimes | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/284708/by/A0yGnzN9Zr

AUDIO | RICH MAVOKO FT PATORANKING _ RUDI | MP3 DOWNLOAD

https://my.notjustok.com/track/download/id/284754/by/MtTPFaHxVR

TPA yasema idadi ya meli zinazoingia nchini imeshuka


TPA yasema idadi ya meli zinazoingia nchini imeshuka Muungwana Blog 1 Wednesday, October 25, 2017 Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imesema idadi ya meli zinazoingia nchini imeshuka kutoka 1,200 hadi 1,000 huku mapato yanayotokana na biashara hiyo yakiongezeka. Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Mhandisi Deusdedit Kakoko alisema kwamba hata mizigo inayoingia nchini pia imepungua. Kakoko alilazimika kuyasema hayo wakati akijibu swali liloulizwa na Mbunge wa Kilindi, Omary Kigua ambaye alitaka kupata ufafanuzi wa kuhusu hali ikoje katika biashara ya bandari. “Kuna speculation (minong’ono) kuwa idadi ya meli zinazoingia nchini zimepungua. Nilitaka kufahamu hali biashara ikoje?”alihoji Kigua. Kakoko alisema hatua wanazochukua zinalenga ufanisi , tija, gharama wanazotoza na huduma kwa mteja na kwamba kwa kukamilisha mambo hayo kutawezesha meli nyingi kuingia nchini. “Uchunguzi wetu umejionyesha kuwa unapochukua hatua matokeo yake yanakuwa mbele hizi hatua ambazo tunachukua zinazaa matunda. Alitaja sababu nyingine ya kupungua kwa meli ni uwezo wa kutia nanga kwa meli ambao hutegemea kina cha maji na kwamba kuna meli nyingi ambazo zinasubiri nje ya gati. Alisema kina cha maji kuna mahali ni mita saba wakati kwingine ni mita 10.5 na meli nyingi duniani ni kubwa hivyo nyingine kusababisha meli kutofika nchini. “Kwa hiyo kuna meli zinasubiri siku saba na meli inatengeneza hela ikitembea ikisimama inatumia hela kwasababu ni kama gari, hiyo ndio sababu inayotuathiri lakini sasa tumeanza ujenzi wa kuchimba gati zetu,”alisema. Alisema sababu nyingine za usalama ambapo kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiibiwa hadi betri na kwamba nyingine ni usimamizi wa sera ambapo awali kulikuwa kuna baadhi ya watu wanaleta mizigo hawalipii. Alisema pia kampeni za masoko zilienda chini licha ya miaka 1960 ilikuwa ni bandarini yenye nguvu. Mbunge wa Magomeni, Jamal Kassim alisema hoja nyingi za ukaguzi kwa mamlaka hiyo zinatoka na mfumo mbuvu walionao taasisi hiyo. “Mwenyekiti (Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari Profesa Ignas Rubaratuka) ulituambia kuwa mmevuka malengo kutoka Shilingi 632 bilioni hadi 705 bilioni lakini kutokana na mfumo mbovu Serikali wharfag (fedha za mizigo) zikusanywe na TRA ( Mamlaka ya Mapato Nchini),”alisema. “Mkurugenzi atuambie hizo fedha walizokusanya zinajumuisha pia fedha za wharfag na atumbie pia ukoje huo utaratibu?”alihoji. Akijibu Mhandisi Kakoko alisema wamerejeshewa Sh 112bilioni ambazo ni mapato yanayotokana na mizigo ya kipindi cha Agostihadi Desemba mwaka jana na kwamba walishazitumia. Hata hivyo, alisema wanadai Serikali Sh 183 bilioni ambazohazijarejeshwa katika mamlaka hiyo. “Awali makubaliano kati ya TRA na mamlaka kuwa watakusanya mapato hayo ya mizigo lakini hili lilifutika baada ya sheria ya bandari kufanyiwa marekebisho na kutoa mamlaka kwa TRA kukusanya mapato hayo ya mizigo na kisha kurejeshwa kwa TPA,”alisema. Akisoma maazimio ya kamati hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kaboyoka aliagiza mamlaka kuwasilisha mpango kazi wa kusimika na kuanza kutumika kwa mfumo wa Tehama katika ofisi ya Katibu wa Bunge. “Bodi ikamilishe zoezi la uthaminishaji wa mali katika mwaka wa fedha 2017/18,”alisema. Chanzo Mwananchi.

Daktari ahukumiwa kifo Iran

Daktari ahukumiwa kifo Iran

Mahakama nchini Iran inaaminika kumhukumu kifo daktari mmoja mzaliwa wa Iran aliye na kibali cha kuishi nchini Sweden wakimtuhumu kwa kuifanyia ujasusi Israel.

Mkuu wa mashtaka nchini Iran alisema mtu alipatikana na hatia ya kuwapasha habari majasusi wa Israel anuani 30 za wanasayansi wa nyuklia, wawili kati yao waliouawa kwenye mashambulizi ya mabomu mwaka 2010.

Lakini mke wake daktari Ahmadreza Djalali, alisema kwa mume wake alikuwa amekuhukumiwa kwa mashtaka sawa na hayo.

Shirika la kupigania haki za binadamu la Amnety International, lilisema kwa hukumu hiyo ilitolewa baada ya mateso ya kisaikolojia na hukumu isiyo ya haki.

Mkuu wa mashtaka huko Tehran Abbs Jafari-Dowlatabadi, aliuambia mkutano wa maafisa wa mahakama kuwa mtu ambaye hakutajwa jina aliwapa majasusi wa Isreal anuani za watu 30 muhimu.

Alisema kuwa anuani hizo ni za wanasayansi wa nyuklia Massoud Ali-Mohammadi na Majid Shahriari, ambao waliuawa kwenye milipuko ya mabomu mjini Tehran mwezi Januari na Novemba mwaka 2010.Mkuu wa mashtaka alisema kuwa mtuhumiwa alitoa taarifa hizo kwa Israel ili alipwe pesa na msaada wa kupata kibali cha kuwa mkaazi wa Sweden.

Amnesty international ilisema kuwa Bw. Djalali ambaye ni daktari na muathiri kwenye taasisi ya Karolinska mjini Stockholm, alikuwa kwenye ziara ya kibishara nchini Iran mwezi Aprili mwaka 2016, wakati alikamatwa na maafisa wa ujasusi na kuzuiliwa bila ya kuruhusiwa kukutana na wakili kwa muda wa miezi saba.

Bw. Djalali anasema kuwa wakati akiwa kuzuizini alilazimishwa mara mbili kukiri mbele ya kamera kwa kusoma taarifa zilizokuwa zimeandikwa na wale waliokuwa wakimhoji.

Anasema alikuwa chini ya shinikizo kali kupitia mateso ya kisaskolojia na vitisho vya kumuua na kuwakamata watoto wake ili aweze kukiri kuifanyia ujasusi serikali ya Israel.

Mawaziri watatu wapigwa STOP

Mfalme wa Morocco Mohammed VI Mfalme wa Morocco Mohammed amewafuta kazi mawaziri wake wa elimu, makaazi na afya kwa kuchelewesha maendeleo ya kiuchumi katika jimbo la Rif lililopo kaskazini.

Eneo hilo lilishuhudia maandamano mwaka jana ambayo yalisababishwa na kifo cha muuza samaki katika makabiliano na polisi - tukio ambalo liliashiria matumizi ya nguvu kupitiliza, rushwa na hali ya kutojali.

Mwezi July, Mfalme Mohammed aliwasamehe watu ambao awali walikamatwa wakati maandamano hayo yakiendelea, huku akiwalaumu maafisa wa serikali kushindwa kupeleka miradi ya maendeleo katika jimbo la Rif.

Eneo hilo lilikuwa kati kati ya vuguvugu ya kisiasa ya mwaka 2011 ambayo ilichochea maandamano nchini Morocco.

Mahakama kuu Kenya kutoa uamuzi kesi ya dharura ya kupinga kufanyika uchaguzi kesho

Mahakama ya Juu nchini Kenya, inasikiliza kesi ya dharura iliyowasilishwa siku ya Jumanne na wapiga kura watatu, wakitaka Uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika kesho kuahirishwa kwa siku tisini. Wapiga kura hao wanasema mazingira ya kisiasa nchini Kenya sio rafiki kuwezesha kufanyika kwa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki. Wakili wao Harun Ndumbi amesema ana imani Mahakamani itawapa ushindi. “Uchaguzi huu hauwezi kufanyika na kuwa huru na haki kwa sababu ya mazingira mabaya, tunataka Mahakama ya Juu iahirishe Uchaguzi huu kwa siku tisini,” amesema Harun Ndumbi. Jaji Mkuu David Maraga alikubali kusikiliza kesi hiyo na kuwaagiza Majaji wengine kusikiliza kesi zote kuhusu Uchaguzi hivi leo, pamoja na kwamba, leo ni siku ya mapumziko. Kesi hii imezua wasiwasi nchini humo kuhusu hatima ya Uchaguzi wa kesho. Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga wanasubiri tangazo la kiongozi wao huku wafuasi wa chama cha Jubilee wakisema wako tayari kupiga kura. Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati, amemteua Consolata Maina kuwa Naibu msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa urais, uteuzi ambao umezua hisia mseto. Naye mlinzi na dereva wa Naibu Jaji Mkuu wa Kenya Philomena Mwilu alivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa risasi jijini Nairobi. Tukio hilo lilitokea baada ya mlinzi huyo kumfikisha nyumbani Naibu Jaji Mkuu huyo ambaye pia ni Jaji katika Mahakama ya Juu. Waziri wa Usalama Fred Matiang'i amesema uchunguzi unaendelea kubaini waliotekeleza shambulizi hilo lakini akawahakikishia wafanyikazi wa Mahakama na hasa Majaji kuwa, wako salama.

China yatangaza kuachana na mila za urithi

China yatangaza kuachana na mila za urithi

China imetangaza kamati mpya ya viongozi wakuu na kuachana na mila ya kutomtangaza mrithi wa rais Xi Jinping.

Kutotangazwa mrithi kunaashiria kuongezeka ushawishi wa Xi madarakani katika kipindi cha miaka mitano inayokuja, siku moja baada ya jina lake kujumuishwa katika katiba.

Uteuzi huo ulifanywa kwa kamati ya watu inayojulikana kama Politburo, ambayo ina nguvu zaidi nchini China.

Kamati hiyo mpya ilizinduliwa kwenye ukumbi mashuhuri wa watu wa China.

Kando na Xi mwenye umri wa miaka 64, waziri mkuu Li Keqiang, 62, ndiye mwanachama pekee wa kamati ambaye alidumisha nafasi yake.

Viongozi wa China miongo ya hivi karibuni wamekuwa wakimteua mrithi mmoja ua kadhaa katika kamati kuu, wakati wa kuanza kwa muhula wa mwisho kuonyesha warirhi watakaochukua usukani.
kumekuwa na uvumi kuwa Bw Xi anaweeza kuwainua wanachama Chen Miner na Hu Chunhua, wote ambao wana umri wa miaka ya 50 kuweza kuwa warithi wake.

Kamati kuu ya kijehi nayo ilitangazwa. Itaongozwa na Xu Qiliang ambye anadumisha cheo hicho na Zhanga Youxia mshirika waa karibu wa Bw. Xi.

Wajumbe pia waliteua kamati kuu ya nguvu ya wanachama 200 ambao hukutana mara mbili kwa mwaka.

Mashirika ya habari ya kimataifa likiwemo la BBC yalinyimwa vibali vya kuingia ukumbi wa matangazo.
Hatua ya kutoteuliwa kwa warithi wa kamati kuu inampa nguvu zaidi Bw Xi katika miaka mitano inayokuja na kuashiria kuendelea kuwepo kwake baada ya mwaka 2022.

USHAHIDI: Daktari ataja magonjwa mengine ya Kanumba

Mbele ya Jaji Sam Rumanyika leo Oktoba 25, 2017 katika mahakama kuu Kanda ya Dar es salaam, imemaliza kusikiliza ushahidi wa kesi namba 125/2012 inayomuhusu Msanii Elizabeth Michael maarufu kama 'Lulu' ya kumuua mpenzi wake Steven Kanumba bila kukusudia, ambapo kesho Oktoba 26 Mahakama hiyo itasikiliza maoni ya Baraza la wazee wa mahakama sambamba na kupanga tarehe ya hukumu.
Kwamujibu wa maelezo ya shahidi namba 2  na wa mwisho kwa upande wa mshitakiwa, aliyefahamika kama Josephine Mshumbus yaliyosomwa kwaniaba yake na Staff Sajenti wa polisi Detective E103 Aitwaye Nyangea, aliyotoa 23/04/2012, ameeleza kuwa yeye alimfahamu Marehemu Steven Kanumba Kama Mgonjwa wake katika kituo chake cha tiba mbadala cha Precious Clinic kilichokuwepo karibu na Jengo la Mawasiliano Jijini Dar es sala.
 "Steven Kanumba alikuwa ana matatizo ya sumu mwilini na alikuwa anakuja kwenye kituo changu cha Kliniki Ambapo alikuwa akifanya vipimo vya mwili mzima na aligundulika kuwa na tatizo la Mafuta (Cholestrol), tatizo la Moyo, Upungufu wa Hewa ya Oksijeni kwenye Ubongo ambayo yalimsababishia maumivu makali.
Hata hivyo niligundua kuwa wakati akiendelea na tiba alikuwa akifanya mazoezi ya kutanua misuli, nilimkataza mara moja kwakuwa angeweza kupoteza maisha au Kupooza baadhi ya sehemu za mwili wake.
Kuna siku alikuja kunilalamikia kuhusu maumivu makali anayopata kwenye Moyo, lakini kulingana na wingi wa wateja sikuweza kumuhudumia lakini tulipanga kuonana siku nyingine lakini haikuwezekana tena" Maelezo ya Shahidi yameeleza.
Upande wa Mstakiwa uliongozwa na Wakili msomi Peter Kibatala, Huku Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Faraja George.
Upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi Nne, na Upande wa Mstakiwa uliwasilisha mashahidi Wawili. 

Msajili wa Vyama Nchini Awataka watumishi Kufuata sheria

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi amewataka watumishi kutoka ofisi yake kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuleta weledi katika kazi.
Hayo ameyazungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa kwa ajili ya watumishi watakaoshiriki katika usimamizi wa utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Gharamaza Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa na wagombea yaliyofanyika Jana na Leo katika ukumbi wa Bunge Jijini Dar esa Salaam.
“Chapeni kazi na kuwa vinara wa kusimamia gharama za uchaguzi na maadili ya Vyama vya Siasa ili kubaini wagombea ambao hawafuati matakwa ya sheria ” amesisitiza Jaji Mtungi.
Naye Bi Piencia Kiure, Msajili Msaidizi wakati akitoa mada juu Elimu ya maadili ya Vyama vya Siasa ,amewasisitiza watumishi kuendelea na utamaduni wa kufanya kazi kwa weledi.
Sheria namba 6 ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2015 kupitia Amri ya Gharama ya uchaguzi inaweka wazi viwango vya juu vya matumizi kwa wagombea, kudhibiti matumizi ya fedha zinazotumika wakati wa uchaguzi kuanzia katika mchakato wa uteuzi, kampeni na kupiga kura ili kuweka uwanja sawa wa kisiasa na kudhibiti vitendo vya rushwa.
Sheria hii hubainisha wajibu wa Mgombea na Chama cha Siasa kujaza fomu maalumu za gharama za uchaguzi ili kubainisha bajeti yake ambayo ni mapato na vyanzo vya mapato na kurejesha katika ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ndani ya siku saba baada ya uteuzi wa wagombea unaofanywa na Tume ya uchaguzi .
Fomu maalumu ya kubainisha marejesho ya matumizi ya uchaguzi inayoambatana na kumbukumbu na stakabadhi za malipo hujazwa na mgombea na kurejeshwa kwenye chama chake ndani ya siku sitini baada ya uchaguzi, chama cha siasa kina wajibu wa kuiwasilisha fomu hiyo kwenye ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ndani ya siku 180 baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi
Hata hivyo ukiukwaji wa sheria hii unaambatana na adhabu kali ambayo hutolewa kwa chama ambacho kitashindwa kuwasilisha mapato na matumizi ya kila mgombea ambayo ni pamoja na kufutiwa kushiriki uchaguzi endapo kitashindwa kutoa maelezo ya kuridhisha.
Usimamizi wa Sheria ya gharama za Uchaguzi katika uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika tarehe Novemba 26 mwaka huu ni mwendelezo wa usimamizi wa sheria hii ambao hufanywa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakati wa uchaguzi wa Urais, Wabunge na Madiwani. Kwa mara ya kwanza sheria hii ilianza kutumika katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010