Mbele ya Jaji
Sam Rumanyika leo Oktoba 25, 2017 katika mahakama kuu Kanda ya Dar es
salaam, imemaliza kusikiliza ushahidi wa kesi namba 125/2012 inayomuhusu
Msanii Elizabeth Michael maarufu kama 'Lulu' ya kumuua mpenzi wake
Steven Kanumba bila kukusudia, ambapo kesho Oktoba 26 Mahakama hiyo
itasikiliza maoni ya Baraza la wazee wa mahakama sambamba na kupanga
tarehe ya hukumu.
Kwamujibu wa
maelezo ya shahidi namba 2 na wa mwisho kwa upande wa mshitakiwa,
aliyefahamika kama Josephine Mshumbus yaliyosomwa kwaniaba yake na Staff
Sajenti wa polisi Detective E103 Aitwaye Nyangea, aliyotoa 23/04/2012,
ameeleza kuwa yeye alimfahamu Marehemu Steven Kanumba Kama Mgonjwa wake
katika kituo chake cha tiba mbadala cha Precious Clinic kilichokuwepo
karibu na Jengo la Mawasiliano Jijini Dar es sala.
"Steven Kanumba alikuwa ana matatizo ya sumu mwilini na alikuwa anakuja
kwenye kituo changu cha Kliniki Ambapo alikuwa akifanya vipimo vya
mwili mzima na aligundulika kuwa na tatizo la Mafuta (Cholestrol),
tatizo la Moyo, Upungufu wa Hewa ya Oksijeni kwenye Ubongo ambayo
yalimsababishia maumivu makali.
Hata hivyo niligundua kuwa wakati akiendelea na tiba alikuwa akifanya
mazoezi ya kutanua misuli, nilimkataza mara moja kwakuwa angeweza
kupoteza maisha au Kupooza baadhi ya sehemu za mwili wake.
Kuna siku alikuja kunilalamikia kuhusu maumivu makali anayopata kwenye
Moyo, lakini kulingana na wingi wa wateja sikuweza kumuhudumia lakini
tulipanga kuonana siku nyingine lakini haikuwezekana tena" Maelezo ya
Shahidi yameeleza.
Upande wa Mstakiwa uliongozwa na Wakili msomi Peter Kibatala, Huku Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Faraja George.
Upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi Nne, na Upande wa Mstakiwa uliwasilisha mashahidi Wawili.
No comments:
Post a Comment