Wednesday, 25 October 2017

Mawaziri watatu wapigwa STOP

Mfalme wa Morocco Mohammed VI Mfalme wa Morocco Mohammed amewafuta kazi mawaziri wake wa elimu, makaazi na afya kwa kuchelewesha maendeleo ya kiuchumi katika jimbo la Rif lililopo kaskazini.

Eneo hilo lilishuhudia maandamano mwaka jana ambayo yalisababishwa na kifo cha muuza samaki katika makabiliano na polisi - tukio ambalo liliashiria matumizi ya nguvu kupitiliza, rushwa na hali ya kutojali.

Mwezi July, Mfalme Mohammed aliwasamehe watu ambao awali walikamatwa wakati maandamano hayo yakiendelea, huku akiwalaumu maafisa wa serikali kushindwa kupeleka miradi ya maendeleo katika jimbo la Rif.

Eneo hilo lilikuwa kati kati ya vuguvugu ya kisiasa ya mwaka 2011 ambayo ilichochea maandamano nchini Morocco.

No comments:

Post a Comment