Monday, 23 October 2017

Ubunifu wa Makonda waimarisha Jeshi la Polisi Dar es Salaam

Makonda akabidhi magari 18 kwa jeshi la polisi Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhi Magari ya kisasa 18 kati ya 26 yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro yakiwa Mabovu kwa ajili ya kufufuliwa.
Magari hayo yalipelekwa Kilimanjaro yakiwa yamebebwa kutokana na ubovu lakini sasa yanarejea Dar es Salaam yakiwa mazima na mwonekano kama magari ya UN ambapo yatakuwa na uwezo wa kubeba Askari 11 wakiwa wamekaa na silaha zao.
Akikabidhi magari hayo kwa Jeshi la Polisi leo Makonda amesema yataenda kuhudumia wananchi kwa kuimarisha ulinzi na usalama jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa kilichomgusa kuboresha Jeshi la Polisi ni baada ya kuona askari wakifanya kazi katika mazingira magumu na wakati mwingine kuvamiwa na majambazi kisha kuuawa na kuporwa silaha.
Aidha Makonda ameishukuru kampuni ya Rajinder Motors Ltd (RSA) kwa kumuahidi kutengeneza magari 56 ya Polisi Dar es Salaam bila kutumia fedha za serikali. Makonda ametumia makabidhiano hayo kutuma salamu kwa majambazi, vibaka na wale wenye nia ya kuvuruga amani na usalama kuwa kiama chao kimefika.
Amesema alipotangaza mpango wa kufufua Magari yaliyokufa wapo waliombeza lakini sasa wanajionea magari yakiwa mapya. Makabidhiano hayo yameshuhudiwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mngwira, Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar ea Salaam Lazaro Mambosas na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama ambapo wamempongeza Makonda kwa ubunifu mkubwa aliona

Waziri mkuu wa Japan kula sahani moja na Korea Kaskazini

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameahidi kukabiliana vilivyo na Korea Kaskazini baada ya matokeo ya kwanza kuonyesha kuwa alipata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa siku ya Jumapili.
Bw. Abe alikuwa ameitisha uchaguzi wa mapema kwa ahadi ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili Japan, likiwemo tisho kutoka Korea Kaskazini.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muungano wa Bw. Abe umeshinda theluthi mbili ya viti vya bunge.
Hii inampa Bw. Abe nafasi ya kuifanyia mabadiliko katiba ya baada ya vita vya pili vya dunia.
Awali waziri mkuu alikuwa ametoa wito wa kutaka jeshi la nchi lifanyiwe mabadiliko, hatua yenye utata ambayo anasema kuwa inahitajika kuboresha ulinzi wa jeshi la Japan.
Akizungumza baada ya kutolewa matokeo ya kwaza Bw. Abe alisema: "Jinsi nilivyoahidi lengo langu kubwa ni kuikabili Korea Kaskazini.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muungano wa Bw. Abe umeshinda theluthi mbili ya viti vya bune.
Miezi miwili tu iliyopita umaarufu wake ulikuwa ukishuka kufuatia kupatikana kwenye sakata, lakini alipata mwamko mpya baada ya Korea Kaskazini kurusha makombora mawili kupitia anga ya Japan.
Vyombo vya habari viliripoti kuwa muungano wa chama tawala cha Abe cha Liberal Democratic Party (LDP) na chama cha Komeito ulishinda viti 312 kati ya viti 465 katika bunge la chini, ushindi unaoupa muungano huo nguvu za kubadilisha katiba.
Awali Bw. Abe alikuwa ametangaza kuwa alikuwa anataka kukifanyia mabadiliko kipengee cha katiba kinachozuia vita na kupelekea kutambuliwa kwa jeshi la Japan.
Miaka miwili iliyopita Bw Abe alifanikiwa kubadilisha katiba ambayo iliruhusu wanajeshi kupigana vita nje hatua ambayo ilipingwa vikali.

Kichuya awekwa sokoni

UONGOZI wa Klabu ya Simba umemuweka sokoni kiungo mshambuliaji wake, Shiza Kichuya kwa kukaribisha ofa kutoka klabu yoyote.
Hivi karibuni Klabu ya Ismailia ya Misri ilishindwana na Simba juu ya dau la kumuuza kiungo huyo ambalo lilikuwa dogo, hivyo kusababisha uongozi wa klabu hiyo kukataa.
Kichuya ni miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao wanacheza kwa kiwango kizuri na kuisaidia timu yake hiyo, jambo ambalo timu nyingi zimekuwa zikimnyemelea.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amefunguka kuwa, dili lao na Ismailia juu ya kumchukua Kichuya limekufa rasmi, lakini wamemuweka sokoni mchezaji huyo kwa timu yoyote itakayomhitaji.
“Ile dili kati yetu na Ismailia ilishakufa rasmi kwa sasa hakuna ishu ya Kichuya kwenda huko, lakini tupo tayari kupokea ofa yoyote ile, iwapo kuna timu itamhitaji tutakuwa tayari kumuuza mchezaji huyo.
“Simba tumekuwa na desturi ya kuwaachia wachezaji wetu kuwauza pale tunapofanikiwa kupata timu ya kucheza, hivyo mchezaji yeyote yule atakayetakiwa tutakuwa tayari kumuachia,” alisema Manara.

Ajibu, Okwi gumzo kwenye mitandao ya kijamii

 Ibrahim Ajibu
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu na yule wa Simba, Emmanuel Okwi ndiyo wachezaji wa Ligi Kuu Bara wanaozungumzwa zaidi mitandaoni kwa sasa.
Gumzo la Ajibu na Okwi limeshika kasi kubwa kutokana na mambo matatu:
MABAO:
Okwi raia wa Uganda ana mabao 8 wakati Ajibu tayari ametupia matano. Hali ya kasi ya kufukuzana kwao na upinzani wa timu zao umesababisha mjadala mkubwa.
Wako wanaamini Ajibu atamfikia Okwi na wengine wakisema hana nafasi hiyo.
UZURI WA MABAO:
Mjadala wa nani amefunga mabao mazuri zaidi nao umechukua nafasi kubwa, wako wanaosema ni Okwi na wengine Ajibu.
Hali hiyo imekuwa ikisababisha mvutano mkubwa na kila mmoja akiamini tofauti au kuwa kwenye kundi moja.
KUZIBEBA TIMU:
Nani zaidi kaibeba timu, kafunga mabao katika mechi zipi na pointi zilikuwaje nao umekuwa ni mjadala mbadala kutaka kupata uhakika kuwa yupi anaibeba timu zaidi.
Mijadala hiyo haina mwisho kwa kuwa kwa kiasi kikubwa inaonekana kutawaliwa na ushabiki badala ya hali halisi hivyo kuifanya iwe endelevu na hoja mpya kila wakati zikianzishwa.
Okwi

Nafasi za Ajira za Leo October 23

Bonyeza Links zifuatazo Kusoma na Kuapply
Nafasi Zingine ingia Nafasi za kazi leo October 23
6 Job Opportunities at Tanzania-Zambia Railway Authority (TAZARA)
2 Job Opportunities at Mwananchi Communications Limited
Job Opportunity at KP Recruiters, Sales Engineer
Job Opportunity at SET, Head of Road Freight
Golden Tulip Hotel Dar Es Salaam, IT Technician
Job Opportunity at RK Consulting, Business Development Officer
Job Opportunity at UN, Gender Expert

Job Opportunity at Nokia Tanzania

www.ajirayako.co.tz

Barrick Kuunda Kampuni Mpya ya Kusimamia Shughuli za Uchimbaji Madini Tanzania

Barrick Gold Corporation yenye makao yake jijini Toronto, Canada, litaunda kampuni mpya (sio Acacia) kuendesha migodi yake ya Bulyanhuru, Buzwagi na North Mara nchini Tanzania.
Katika taarifa yake juu ya makubaliano na serikali ya Tanzania yaliyofikiwa juzi jijini Dar es salaam, Shirika hilo limesema msimamo wa uwazi ulioafikiwa baina ya washirika (Tanzania na Barrick) ndio utaoainisha namna kampuni hiyo mpya itafanya shughuli zake.
"Kwa mfano Serikali ya Tanzania itashiriki katika maamuzi yahusuyo shughuli, uwekezaji, mipango, manunuzi na masoko (ya kampuni hiyo mpya itapoanzishwa)", sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Barrick Gold anayeshughulikia Shughuli za Uwekezaji na utawala Bw. Daniel Oh na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Barrick anayeshughulikia Mawasiliano Bw. Andy Lloyd.
Taarifa imesema kampuni hiyo mpya itaajili Watanzania, itawajengea uwezo wazawa katika ngazi zote, kuanzia uanachama wa bodi hadi shughuli zote, na kwamba itaongeza ununuzi wa bidhaa na huduma ndani ya Tanzania katika kuhakikisha faida ya dhahabu inaifaidisha nchi.
Taarifa hiyo imethibitisha kwamba faida ya kiuchumi kutoka katika migodi hiyo mitatu itagawanwa nusu-kwa-nusu ama 50-kwa-50 baina ya kampuni hiyo mpya na serikali ya Tanzania, faida yake ya kiuchumi ikitokana na mirahaba na kodi huku asilimia 16 ikibakia pale pale.



http://www.barrick.com/investors/news/news-details/2017/Barrick-Comments-on-Proposed-Framework-for-Acacia-Mining-plc-Operations-in-Tanzania/default.aspx

Waziri kigwangalla afuta vibali vya uwindaji,,,,

Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla amefuta vibali vyote vya uwindaji kwa kampuni kuanzia Oktoba 22,2017 na kutoa siku 60 kwa watendaji ili waratibu mchakato upya utakaowezesha vitalu kugawiwa kwa mnada.
Dk Kigwangalla pia amemwagiza katibu mkuu wa wizara hiyo, ndani ya muda mfupi kuwaandikia Hazina ili kuzichukua hoteli 10 kati ya 17 zilizobinafsishwa ambazo zimeshindwa kutimiza masharti.
Ametoa maagizo hayo jana alipohitimisha mazungumzo na wadau wa sekta ya utalii na maliasili aliokutana nao mjini Dodoma.
“Kwa mamlaka niliyonayo katika sheria, natamka kwamba, nafuta rasmi vibali vyote vya uwindaji kwa kampuni vilivyotolewa na wizara yangu kwa mwaka huu. Pia, naagiza watendaji wote wanaosimamia hili wahakikishe wanaandaa mchakato ndani ya siku 60 ili mnada ufanyike na uwe wa uwazi,” aliagiza Dk Kigwangalla.
Kuhusu vitalu vyenye migogoro vikiwemo vya Loliondo na Natroni, ameagiza visigawiwe hadi migogoro itakapokwisha.
"Kwenye hili la hoteli, nataka katibu uwasiliane na mamlaka husika, ikiwemo Msajili wa Hazina ili ndani ya siku 60 uje na majibu tutangaze kwa wawekezaji watakaokwenda na masharti," amesema

Breaking news : Lulu akutwa na kesi ya kujibu kuhusu kifo cha kanumba.....

Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo Oktoba 23, 2017 imemkuta Msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael Maarufu kama Lulu, anakesi ya Kujibu.
Ni kuhusu tuhuma zinazomkabili za kumuua msanii mwenzake, marehemu Steven Kanumba ambaye pia alikuwa ni mpenzi wake, April 6 mwaka 2012.
Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wao kwa kuita mashahidi wanne.
Kesi imeahirishwa hadi saa tano kamili ambapo Lulu ataanza kujitetea.