Monday, 23 October 2017

Kichuya awekwa sokoni

UONGOZI wa Klabu ya Simba umemuweka sokoni kiungo mshambuliaji wake, Shiza Kichuya kwa kukaribisha ofa kutoka klabu yoyote.
Hivi karibuni Klabu ya Ismailia ya Misri ilishindwana na Simba juu ya dau la kumuuza kiungo huyo ambalo lilikuwa dogo, hivyo kusababisha uongozi wa klabu hiyo kukataa.
Kichuya ni miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao wanacheza kwa kiwango kizuri na kuisaidia timu yake hiyo, jambo ambalo timu nyingi zimekuwa zikimnyemelea.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amefunguka kuwa, dili lao na Ismailia juu ya kumchukua Kichuya limekufa rasmi, lakini wamemuweka sokoni mchezaji huyo kwa timu yoyote itakayomhitaji.
“Ile dili kati yetu na Ismailia ilishakufa rasmi kwa sasa hakuna ishu ya Kichuya kwenda huko, lakini tupo tayari kupokea ofa yoyote ile, iwapo kuna timu itamhitaji tutakuwa tayari kumuuza mchezaji huyo.
“Simba tumekuwa na desturi ya kuwaachia wachezaji wetu kuwauza pale tunapofanikiwa kupata timu ya kucheza, hivyo mchezaji yeyote yule atakayetakiwa tutakuwa tayari kumuachia,” alisema Manara.

No comments:

Post a Comment