Monday, 23 October 2017

Ajibu, Okwi gumzo kwenye mitandao ya kijamii

 Ibrahim Ajibu
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu na yule wa Simba, Emmanuel Okwi ndiyo wachezaji wa Ligi Kuu Bara wanaozungumzwa zaidi mitandaoni kwa sasa.
Gumzo la Ajibu na Okwi limeshika kasi kubwa kutokana na mambo matatu:
MABAO:
Okwi raia wa Uganda ana mabao 8 wakati Ajibu tayari ametupia matano. Hali ya kasi ya kufukuzana kwao na upinzani wa timu zao umesababisha mjadala mkubwa.
Wako wanaamini Ajibu atamfikia Okwi na wengine wakisema hana nafasi hiyo.
UZURI WA MABAO:
Mjadala wa nani amefunga mabao mazuri zaidi nao umechukua nafasi kubwa, wako wanaosema ni Okwi na wengine Ajibu.
Hali hiyo imekuwa ikisababisha mvutano mkubwa na kila mmoja akiamini tofauti au kuwa kwenye kundi moja.
KUZIBEBA TIMU:
Nani zaidi kaibeba timu, kafunga mabao katika mechi zipi na pointi zilikuwaje nao umekuwa ni mjadala mbadala kutaka kupata uhakika kuwa yupi anaibeba timu zaidi.
Mijadala hiyo haina mwisho kwa kuwa kwa kiasi kikubwa inaonekana kutawaliwa na ushabiki badala ya hali halisi hivyo kuifanya iwe endelevu na hoja mpya kila wakati zikianzishwa.
Okwi

No comments:

Post a Comment