Friday, 20 October 2017

UN yatoa Dola160 milioni nchini

Mratibu mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez
Dar es Salaam. Umoja wa Mataifa (UN) umetoa Dola 160 milioni za Marekani kati ya Dola 200 milioni zinazitakiwa kutolewa mwaka huu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwamo kuwahudumia wakimbizi waliopo kambi mbalimbali Kigoma.
Nusu ya fedha hizo zimeelekezwa kwenye mradi wa Kigoma wa kuwahudumia wakimbizi na kiasi kingine kimeelekezwa kwenye miradi mingine ya maendeleo inayofadhiliwa na mashirika mbalimbali ya UN.
Oktoba 24, UN itaadhimisha miaka 72 tangu kuanzishwa kwake na sherehe za maadhimisho hayo kitaifa zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni zaidi ya 500 wakiwamo na mabalozi, wanafunzi na vyombo vya ulinzi na usalama.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ‘Maendeleo ya Viwanda na Utunzaji Mazingira kwa Maendeleo Endelevu.’
Akizungumzia maadhimisho hayo jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kimataifa na kikanda, Dk Susan Kolimba alisema wameamua kuunganisha kauli mbiu ya Serikali ya kuendeleza viwanda na mpango wa UN wa kutekeleza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Mratibu mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez alisema programu ya Kigoma imebuniwa ili kukidhi vipaumbele vya maendeleo ya mkoa huo na hasa kuzilenga jamii katika wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko.

Yanga yaipiga mkwala stand UTD

KOCHA MSAIDIZI WA KLABU YA YANGA, SHADRACK NSAJIGWA.
KOCHA msaidizi wa klabu ya Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema maandalizi waliyoyafanya kuelekea mchezo wao dhidi ya Stand United ni ya kiwango cha juu na wenyeji hao wasitegemee urahisi.
Yanga itashuka kwenye Uwanja wa Kambarage, ulioko Shinyanga keshokutwa ili kusaka pointi nyingine muhimu za kutetea ubingwa wanaoushikilia.
Akizungumza na gazeti hili jana kutoka Tabora walipokuwa wameweka kambi ya muda kujiandaa na mchezo huo, Nsajigwa, alisema kuwa, wamejiandaa vizuri na mchezo wao wa kirafiki waliocheza juzi dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora umewaongezea nguvu.
“Tulijiwekea mikakati katika michezo miwili ule wa Bukoba na huu tunaokwenda kucheza Shinyanga, tuondoke na pointi zote sita, tumefanikiwa mchezo wa kwanza, tunaenda Shinyanga kukamilisha kile tulichokianza Bukoba,” alisema Nsajigwa.
Aliongeza kuwa wanajua watakutana na ushindani kutoka kwa wenyeji wao, ambao watataka kutumia vyema uwanja wa nyumbani, lakini wamejipanga kuondoka na ushindi.
Kuhusu wachezaji watakaoanza kwenye mchezo huo hasa kuepuka wale wenye kadi mbili za njano ambao wanaweza wakapelekea kuukosa mchezo dhidi ya Simba, Nsajigwa alisema suala lipo chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina.
“Tuna siku ya leo (jana) kesho (leo) na Jumamosi kuangalia nani ataanza kwenye mchezo wa Shinyanga, tunafahamu tunatakiwa kuwa na tahadhari, si tu kwa kadi lakini pia kuepuka wachezaji wetu wasiumie kwa sababu ya mchezo wa Oktoba 28, hilo suala linafanyiwa kazi,” alisema Nsajigwa.
Wachezaji wa Yanga ambao wana kadi mbili za njano na wako katika hatari ya kuikosa Simba kama wataonyeshwa kadi yoyote Jumapili ni Kelvin Yondani na Juma Abdul.

Uongozi wa Trump wakosolewa na Marais hawa

Marais wa zamani George Bush na Barrack Obama
Marais wawili wa zamani nchini Marekani wameonyesha wasiwasi wao kuhusu hali ya kisiasa nchini humo bila kumtaja rais Donald Trump kwa jina.
Barrack Obama aliwataka wapiga kura kukataa kile alichokitaja kuwa siasa za kuwagawanya watu mbali na siasa za hofu.
Alikuwa akimfanyia kampeni mgombea wa chama cha Democrat anayewania wadhfa wa gavana wa jimbo la New Jersey.
Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya mtangulizi wake George W. Bush kukosoa unyanyasaji na chuki katika maisha ya kawaida ya raia Marekani.
Katika hotuba, alisema chuki dhidi ya wale wanaokupinga zimeongezwa nguvu huku maadili ya kiraia yakisahaulika.
Bwana Trump ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa mtangulizi wake bado hajatoa tamko lolote.
Marais wa zamani nchini Marekani kwa kawaida huwa nadra kutoa maoni yao kuhusu hali ya kisiasa na ilionekana kuwa makosa makubwa kwa rais aliyetangulia kumkosoa mrithi wake katika ikulu ya Whitehouse.
lakini maadili na viwango vya tabia ambazo awali zilikuwa zikifuatwa sasa zimesahaulika katika mazingira ya kisiasa ya wakati huu.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni za chama cha Democrat , mjini New Jersy, Obama alisema kuwa Wamarekani wanapaswa kutuma ujumbe kwa ulimwengu kwamba tunakataa siasa za kugawanywa na siasa za hofu.
Aliongezea: Kile ambacho hatufai kuendelea nacho ni kuwa na siasa za zamani za kugawanyana ambazo zimekuwepo nyakati za wali.
Siasa tunazoziona sasa tulidhani zimepitwa na wakati, hiyo ni kurudi miaka 50 nyuma.Ni karne ya 21 sio 19. jamani!.

Korea Kaskazini yaionya Australia

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Serikali ya Australia imesema kuwa imepokea stakhabadhi kutoka Korea Kaskazini ikiitaka Canbera kutojihusisha na utawala wa rais Trump.
Barua hiyo imeshutumu onyo la Marekani kwamba itaiangamiza Korea Kaskazini iwapo italazimika kujilinda.
Waziri mkuu wa Australia PM Malcolm Turnbull amesema kuwa barua hiyo pia ilitumwa kwa mataifa mengine.
Amesema inaonyesha kuwa shinikizo za kidiplomasia dhidi ya Korea Kaskzini zimeanza kufanya kazi, licha ya barua hiyo kuwa na ufyozi na malalamishi ya kawaida ya taifa hilo.
Barua hiyo yenye ukurasa mmoja ilitumwa kupitia ubalozi wa Korea Kaskazini nchini Indonesia na inadaiwa kutoka kwa kamati ya maswala ya kigeni ya Korea Kaskazini.
Imezitaka serikali nyengine kujitenga na hatua zisizokuwa na heshima za rais Trump ikisisitiza kuwa Marekani inaweza kusababisha janga kubwa la kinyuklia.
Bwana Turnbull amesema kuwa Korea Kaskazini ndio inayosababisha wasiwasi kwa kutishia kuyashambulia mataifa ya Japan, Korea Kusini na Marekani kwa kutumia silaha za kinyuklia.
''Wametuma barua hizi kwa mataifa mengi , kama barua iliosambazwa'', alisema Bwana Turnbull kwa kituo kimoja cha redio 3AW.
Waziri wa maswala ya kigeni Julie Bishop aliitaja barua hiyo kuwa hatua isiokuwa ya kawaida ya Korea Kaskazini.
Baadaye bwana Turnbull alionekana kutojali umuhimu wake akiifananisha na ufyozi na malalamishi kuhusu Donald Trump unaotolewa na Korea Kaskazini.
Hatahivyo wote wanakubaliana kwamba huenda ni ishara kwamba shinikizo za kimataifa dhidi ya taifa hilo zimeanza kuzaa matunda na kuwa na matumaini kwamba kutakuwa na majadiliana ya kimataifa.
Siku ya Jumamosi Pyonyang iliionya Australia kwamba haitaweza kuzuia janga iwapo itashirikiana na sera za Marekani dhidi ya utawala wa Kim Jong Un.
Korea Kaskazini imekiuka makubaliano ya kimataifa katika miezi ya hivi karibuni kupitia kufanyia majaribio kombora lake la kinyuklia mbali na kurusha makombora mawili juu ya anga ya taifa la Japan.
Marekani imejibu kwa vitisho vya kijeshi , lakini waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson anasisitiza kuwa bwana Trump yuko tayari kuutatua mgogoro huo kupitia diplomasia.

Chris Brown kurudiana na Rihanna?

Mkali wa Muziki wa Pop, Christopher Maurice ‘Chris Brown’ akiwa na Rihanna.
TAARIFA kutoka chini ya kapeti zinaeleza kuwa, miezi michache baada ya kutengeneza filamu fupi ya maisha yake, mkali wa Muziki wa Pop, Christopher Maurice ‘Chris Brown’ huenda akarudiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Rihanna.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Chris, baada ya filamu hiyo kutoka inayoitwa Welcome To My Life, Chris anaamini kwa asilimia kubwa Rihanna ameiona yote na atakuwa tayari kurudiana naye. “Chris anaamini Rihanna ameshamsamehe baada ya kuangalia filamu.
Chris alishawahi kumwambia rafiki yake anataka kuwa anamchukua Rihanna na kwenda naye kwenye filamu,” kilisema chanzo.

Moto wateketeza Hoteli ya Kifahari

Moto mkubwa imeteketeza hoteli kubwa ya kifahari katika mji wa Yangon nchini Myanmar na kumuua mtu mmoja.
Watu wengine walijeruhiwa kwenye moto huo ambao ulianza mwendo wa saa 20:30 GMT siku ya Jumatano katika hoteli ya Kandawgyi Palace.
Iliwachukua mamia ya wazima moto saa kadha kuuzima moto huo. Zaidi ya wageni 140 waliondolewa.
Haijuliana moto huo ulinza kwa njia gani huku ripoti za kukanganya zikisema kuwa kulikuwa na mlipuko wa mtungi wa gesi au hutilafu ya umeme.
"Hakukuwa na king'ora na vurugu zilikuwa ni kama kulikuwa na walevi hotelini," mtalii mmoja alisema, akiongeza kuwa ni mfanyakazi mmoja ambaye alimuelekzea eneo salama.
Wageni wamehamishwa kweda kwa hoteli zingine mjiji Yangon.
Hoteli hiyo ili kando ya ziwa Kandawgyi, ilijengwa miaka ya 1990 lakini huenda uwepo wake uliazia miaka ya 1930 wakati eneo hilo lilikuwa likitumia kama klabu ya wanajeshi wa Uingereza.
Hoteli ya kifahari kabla ya kuteket

AUDIO | Timmy Tdat Ft Dela _ We'll Be Ok | Download

AUDIO | Timmy Tdat Ft Dela – We’ll Be OK | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/282765/by/DM19joF3B~

VIDEO : Harmonize _ Nishachoka | Download

https://cloudup.com/files/iuRG9ODfNAv/download

Thursday, 19 October 2017

Nyalandu Akomalia katiba

Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) amefunguka na kusema katika kikao cha Tisa cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Novemba 7, 2017 Dodoma anakusudia kuwasilisha azma yake ya kupeleka muswada binafsi utakao weka sharti la kurejea mjadala wa Katiba Mpya.
Nyalandu amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii na kusema amekusudia kufikisha jambo hilo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai.
"Nakusudia kuwasilisha kwa spika wa Bunge Mh. Job Ndugai. Azma yangu ya kuleta muswada binafsi wa sheria katika kikao kijacho cha Bunge itakayoweka sharti la kurejea upya mjadala wa Katiba Mpya ya Tanzania, kwa kuzingatia rasimu ya Katiba kama ilivyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba" alisema Lazaro Nyalandu
Suala la Katiba Mpya licha ya kuwa siyo kipaumbele cha Rais John Pombe Magufuli lakini wadau mbalimbali wamekuwa wakilizungumzia wakisema kuna haja kubwa ya mchakato huo wa Katiba mpya kuendelea sasa wakidai kuwa huu ni wakati sahihi zaidi mchakato wa Katiba Mpya kuendele

Chadema yajilipua kuhusu lowassa

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu amefunguka na kusema kwamba wanawaruhusu Chama cha Mapinduzi watumie nafasi ya Lowassa kuwepo Chadema kuwaita wao mafisadi kama jinsi wao walivyofanya kwa miaka mingi.
Salumu amesema kwamba kuwataja watu ambao waliwaita vinara wa ufisadi na leo wapo nao kwenye chama chao ulikuwa ni wajibu wao kama chama cha upinzani kutumia upenyo wa udhaidfu wa chama cha mapinduzi kuonyesha wananchi madhaifu ya serikali.
"Lazima ukubali kwamba ni wajibu wetu kuonyesha madhaifu ya serikali, Kama tulikuwa tunampinga Lowassa kwamba ni fisadi ulikuwa ni wajibu wetu Chadema. Sasa kama leo hii Lowassa yupo kwetu ni wajibu wao CCM kuwaambia watanzania kuwa Chadema kina mafisadi. Kwa sababu Lowassa amekuja Chadema ni yule yule wala hajawa malaika kama jinsi ambavyo kelele zinavyopigwa," Mwalimu amefunguka
Akizungumzia kuhusu chama kupwaya na kumtegemea mtu mmoja kuwa mkosoaji wa serikali iliyopo Madarakani, Mwalimu amesema kupanga ni kuchagua hivyo wao kama Chadema wanauwezo mkubwa wa kukosoa lakini huamua kuchagua nani atoe hoja kwa wakati gani na siyo kwamba wameishiwa.
"Hata kwenye timu ya mpira wapo mastaa wengi wanaofanya vizuri lakini huangaliwa ni nani wa kuibeba timu, ndivyo hata Chadema ilivyo, mnaweza kuwa wengi lakini kupanga ni kuchagua, Tundu ni Mwanasheria Mkuu wa chama hivyo chama kinaanda ajenda lakini atachaguliiwa mmoja wa kuifikisha ajenda hiyo huku wengine tukitoa sapoti, inategemea ajenda hiyo pia inatolewa wakati gani, mbona hapa katikati mengine yametokea kwani tumemuinua Lissu kitandani atusaidie kusema. si tulisema wenyewe. ? hivyo hakuna mtu mmoja anayeibeba Chadema bali tunashirikiana pamoja", Mwalimu ameoneza.
Huu ni utaratibu wetu hata kipindi cha kina Mh. Zitto Kabwe pamoja na Dkt. Slaa wote agenda zilikuwa ikitengenezwa na watu ndani ya chama na wanaozipeleka mbele huwa ni wachache siyo kwamba eti chama kimepwaya.
Katika hatua nyingine Mwalimu amesema lengo la chama cha upinzani ni kushika dola na siyo kusikiliza jinsi ambavyo watu wengine wanavyokosoa na kusisitiza kwamba Chama chao kilianzishwa kwa malengo ya kuja kushika dola.

Wema Sepetu na wasanii wengine wamfaliji Lulu

Dar es Salaam . Msanii wa fani ya uigizaji filamu nchini, Wema Sepetu ni miongoni mwa watu waliomfariji Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia iliyoanza kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Wasanii wametumia mtandao wa Instagram kumfariji mwigizaji Lulu ambaye ni mshindi wa tuzo za filamu za AMVCA.
Jackline Wopler, Katarina Karatu, Nisha, Aunt Ezekiel na wengine wametuma picha za mwigizaji huyo zikiambatana na maneno ya kumfariji wakimweleza kuwa atavuka salama katika mtihani huo.
Kupitia ukura wake wa Instagram, Wema ameweka picha ya Lulu na kuandika, “This Too Shall Pass Baby… God is Great u know… so have faith… ur in my prayers,” akiwa na maana hata hili litapita, Mungu ni mkubwa hivyo anatakiwa kuwa na imani na atamwombea.
Lulu anadaiwa Aprili 7,2012 alimuua bila ya kukusudia mwigizaji mwenzake Steven Kanumba, eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Kesi inasikilizwa na Jaji Sam Rumanyika.

Harmonize afurahia support anayopata toka kwa Wolper

Msanii wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka mambo kadhaa kuhusu aliyekuwa mpenzi wake, Jacqueline Wolper.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Shulala’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa anafurahi kuona anapata support ya Wolper katika muziki wake.
“Nadhani mwanzo ilikuwa hasira tu, nashukuru kuona support ya Wolper, namchukulia kama shabiki yangu tu” amesema Harmonize.
Hiyo juzi katika mtandao wa Instagram Jacqueline Wolper aliposti video mbili zikimuonyesha akifurahia kusikiliza ngoma hiyo ambayo Harmonize amemshirikisha Korede Bello.

Waziri kigwangalla atoa siku 7

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kuwapa siku saba wavamizi ambao wapo kwenye pori tengefu la Loliondo kuondoka mara moja ndani ya siku hizo kwani wasipofanya hivyo baada ya hapo mali zao zitataifishwa na serikali.
Kigwangalla amesema uwepo wa wavamizi hao ambao wana ng'ombe zaidi ya 6,000 na matrekta zaidi ya 200 kutoka nchi ya jirani imekuwa sababu kubwa ya chanzo cha mgogoro wa ardhi baina ya vijiji na hifadhi hiyo.
"Kuna taarifa kwenye eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu la Loliondo, kuna ng'ombe zaidi ya 6,000 na trekta zaidi ya 200 toka nchi jirani, yote kinyume cha sheria! Uwepo wao siyo tu unahatarisha uhai wa mfumo wa ikolojia ya Serengeti-Mara, bali pia unapunguza eneo la kuchungia kwa wenyeji wa Loliondo. Hivyo kuleta kiu ya wananchi wa Loliondo kuingia ndani zaidi ya eneo la hifadhi kutafuta malisho na hatma yake kuhatarisha uhai wa Serengeti. Uvamizi huu wa wenzetu kutoka nchi jirani ni moja ya sababu kubwa (zilizojificha) za mgogoro wa ardhi baina ya vijijj na hifadhi kukolea moto" alisema Waziri Kigwangalla
Aidha Waziri huyo amesema wakati wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu wamewataka wavamizi hao kuondoka katika maeneo hayo
"Wakati tukiendelea kutafuta suluhisho la kudumu, tutaondoa makando kando kama haya haraka. Leo tumetoa siku saba kwa wavamizi wote toka nchi jirani waliopo eneo la Loliondo bila kufuata taratibu za kisheria waondoke na mali zao la sivyo tutazitaifisha" alisisitiza Kigwangalla.