Tuesday, 17 October 2017

Wachezaji Wa Yanga waliokuwa wamebaki Dar waongeza nguvu tabora,,,,

Klabu ya soka ya Yanga itaungana na wachezaji wake waliokuwa wamebaki jijini Dar es salaam wakati timu imesafiri kwenda mkoani Kagera kucheza na Kagera Sugar wikiendi iliyopita.
Yanga tayari imeshatoka Kagera na kutua mkoani Tabora ikijiwinda na mchezo wake wa ligi kuu raundi ya 7 dhidi ya Stand United utakaopigwa wikiendi ijayo mjini Shinyanga.
Meneja wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Hafidh Saleh amewataja wachezaji hao kuwa ni Juma Mahadhi, Pato Ngonyani, Ramadhan Kabwili, Abdallah Hajji, Juma Mahadhi na Saidi Mussa.
Aidha meneja Saleh amesema kuwa wachezaji waliokuwa majeruhi ambao ni Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Amisi Tambwe wataendelea na mapumziko hadi timu itakaporejea jijini Dar es salaam.
Kesho Yanga inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora kwenye uwanja wa Al Hassan Mwinyi kabla ya kuelekea mjini Shinyanga kucheza na Stand United

Wakenya wawachangia damu waadhirika Wa mabomu Somalia,,,,

Mamia ya Wakenya pamoja na raia wa Somalia wanaoishi nchini humo walishiriki katika shughuli ya kutoa damu ili kuwasaidi wale waliojeruhiwa katika mlipuko wa bomu nchini Somalia uliowaua takriban watu 276.
Kampeni hiyo ya kutoa damu ilizinduliwa kupitia mitandao ya kijamii katika eneo la Eastleigh mjini Nairobi kufuatia bomu hilo.
Tayari takriban miili 165 isiotambulika imezikwa katika kaburi la pamoja mjini Mogadishu.
Chombo cha habari cha serikali kinasema kuwa ni watu 111 waliotambuliwa.
Baadhi ya waliojeruhiwa walisafirishwa hadi nchini Uturuki kwa matibabu zaidi kulingana na mpiga picha mmoja wa chombo cha habari cha AFP.
Hatua hiyo inajiri kufuatia ombi la serikali ya Somalia kuomba msaada wa damu .
Waziri wa habari nchini Somalia aliambia BBC kwamba idadi ya watu waliofariki huenda ikaongezeka na kwamba usaidizi zaidi ulihitajika.
Alisema kuwa zaidi ya watu 300 walijeruhiwa nchini Somalia kufuatia shambulio hilo ambalo limetajwa kuwa kubwa zaidi katika kipindi cha miaka 10 huku miili kadhaa ikidaiwa kufinikwa chini ya vifusi.
Ndege mbili kutoka Marekani na Qatar zimewasili mji Mogadishu.
Serikali ya Kenya imesema kuwa itatuma tani 31 za dawa mjini Mogadishu mbali na kuwasafarisha baadhi ya waathiriwa wa mlipuko huo hadi Nairobi kwa matibabu zaidi.
Serikali ya Djibout nayo tayari imetuma madaktari 30 nchini Somalia wakiongozwa na waziri wa afya nchini humo ili kutoa msaada wa dharura.
Mlipuko huo wa Jumamosi ulilenga eneo lenye watu wengi na kuwaua raia wakiwemo madaktari na wanafunzi.
Hakuna kundi ambalo limekiri kuhusika lakini serikali ya Somalia inalaumu kundi la wapiganaji wa al-Shabab.
Shghuli ya kuchangisha damu pia inaendelea nchini Somalia ambapo maafisa wa Jeshi la AMISOM wanatoa damu.

Meya wa Kinondoni atoa sababu 3 za kusaini mkataba na CRJE

Meya wa manispaa ya Kinondoni Benjamin Samweli Sita leo amesaini mkataba wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata takataka na kuwa mbolea kitakachojengwa na kampuni ya CRJE ambapo ujenzi huo unatarajia kuanza kesho.
Meya Sita amewaeleza waandishi wa habari kuwa sababu ya kusaini mkaba huo ni kwamba mbolea aina ya mboji itakayozalishwa na kampuni hiyo haitaharibu udongo kwani tofauti na njia ambayo imezoeleka ya Chemical Fertilizer ambayo inaharibu udongo kwa kiasi kikubwa.
Pia amesema kujengwa kwa kiwanda hicho kitaongeza ajira kwa wananchi pia kitawasaidia wakulima kutumia mbolea ambayo ni bora na ya kisasa huku ikiwa haina athari kwa udongo na hata mazao.
Aidha kupitia mkataba huo manispaa ya Kinondoni itakuwa imeunga mkono kiasi kikubwa jitihada za Rais Magufuli katika kuelekea Tanzania ya viwanda, hivyo wananchi watapata ajira mbalimbali za kutoka kiwanda hicho.


Shonza kuanza na wasanii wanaovaa vibaya na kutumia maneno mabaya

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza imetangaza kuanza kushughulika na wasanii ambao wanavaa vibaya na kutumia maneno mabaya kwenye kazi zao za sanaa.
Juliana Shonza amesema hayo leo alipokuwa anapokelewa ofisini na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe na kusema alipoteuliwa tu aliona kuwa kwenye sanaa hususani wasanii wamekuwa wakivaa vibaya kwenye kazi zao na kutumia maneno yasiyo na maadili kwenye kazi zao hizo na kusema kama serikali lazima wahakikishe wanalifanyia kazi ili kulinda utamaduni wa Tanzania.
"Nilipoteuliwa tu ni jambo ambalo nilianza nalo ni mmomonyoka wa maadili kwa kweli imekuwa ni changamoto kubwa sana nimeshuhudia saizi hata ukiangalia kwenye nyimbo na kazi za sanaa lugha ambayo inatumika inakuwa siyo nzuri, lakini kama haitoshi kuna nyimbo ambazo zinaibwa ukifuatilia ndani unakuta maadili siyo mazuri, lakini hata katika suala la mavazi mimi nalisema wazi nitawaambia wasanii wa kike wajitahidi kuvaa vizuri, kwa sababu hatuwezi kuacha hivi vitu vikawa vinaendelea tu kila taifa na misingi yake na tamaduni zake" alisema Juliana Shonza
Mbali na hilo Naibu Waziri wa Habari amesisitiza kuwa ni jukumu la viongozi kuhakikisha utamaduni wetu unaendelezwa na kusimamia misingi ya taifa.

Hii ndio ratiba ya kufuzu kombe la dunia kwa mechi zilizosalia

Shirikisho la soka dunini FIFA leo limetoa ratiba ya mechi za mtoano kuwania nafasi nne za kufuzu Kombe la dunia kwa upande wa bara la Ulaya.
Katika droo ambayo imechezeshwa leo na nyota wa zamani wa Hispania Fernando Hierro jijini Zurich Uswis, Italia ambayo ilishindwa kufuzu mbele ya Hispania kwenye kundi G itacheza na Sweden.
Timu zingine ambazo zilipata sifa ya kucheza mechi za mtoano ni Ireland ya Kaskazini ambayo itacheza na Uswisi wakati Croatia itachuana na Ugiriki.
Mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa Novemba 9 hadi 11 na kurudiana Novemba 12 hadi 14 ili kujua ni timu gani zitaungana na mataifa mengine 27 ambayo tayari yamefuzu kwa fainali za mwakani nchini Urusi.

Wenger Achinguzwa na chama Cha soka England (FA)

London, England. Arsene Wenger anachunguzwa na Chama cha Soka England (FA) kwa kosa la kumtolea lugha ya ukali mwamuzi katika mchezo wao na Watford.
Arsenal ilichapwa mabao 2-1 na Watford katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa ambao Mfaransa huyo aliondoka uwanjani akiwa amechanganyikiwa.
Wenger alimshukia mwamuzi Neil Swarbrick akipinga baadhi ya uamuzi hatua ambayo imetafsiriwa ni utovu wa nidhamu na FA imeanza uchunguzi.
Endapo atakutwa na hatia anaweza kuchukulia hatua ikiwemo kufungiwa katika baadhi ya mechi za Ligi Kuu England.
Kocha huyo amekuwa katika mazingira magumu na mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakimpigia kelele kutaka ang'oke Makao Makuu Emirates.
Mashabiki wa klabu hiyo wanamtaja Wenger ni kocha asiyetaka mabadiliko katika kikosi chake na amekuwa akiigharimu kwa kushindwa kununua wachezaji nyota.
Arsenal inashika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 13, katika mechi nane ilizocheza msimu huu.

Wataka Mugabe Afie Ofisini,,,,

Harare, Zimbabwe. Umoja wa Vijana wa chama cha Zanu PF unataka Rais Robert Mugabe, licha ya umri wake mkubwa, aruhusiwe kufia ofisini hali inayoibua fununu kwamba mzee huyo hana mpango wa kuachia madaraka kwa sasa.
Pendekezo hilo limekuja wakati huu ambao wanachama wengi katika chama hicho tawala kwenye majimbo nchi nzima walikutana mwishoni mwa wiki na kuamua kuitisha mkutano wa dharura Desemba kushughulikia mgawanyiko uliosababishwa na Mugabe kushindwa kumwandaa mrithi wake kwa miaka 37 aliyokaa madarakani.
Mikutano ya kwenye majimbo iliitishwa siku chache baada ya uamuzi toka juu uliofanywa na mkutano mkuu na kamati kuu kutaka uitishwe mkutano mkuu maalumu ili ushughulikie migogoro ya ndani inayotishia kuisambaratisha Zanu PF kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.
Mmoja wa makamu wa Mugabe, Emmerson Mnangagwa anadaiwa kuongoza kundi linaloitwa "Team Lacoste" linalohaha kumpigia kampeni aweze kumrithi Mugabe akiondoka madarakani.
Kundi jingine la vijana zaidi linalojiita "Generation 40" linaloungwa mkono na Memsapu Grace Mugabe limeelekeza mashambulizi dhidi ya Mnangagwa wakati jina la Waziri wa Ulinzi Sydney Sekeramayi limeingizwa kwenye vita ya urais na Waziri wa Elimu ya Juu Jonathan Moyo anayemwona kuwa anafaa.
Katikati ya mnyukano huu wa kuwania kumrithi Mugabe, mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Zanu PF, Mubuso Chinguno amesema chama hakina mgombea mwingine zaidi ya mzee huyo mwenye umri wa miaka 93.
"Rais Mugabe ni rais wetu wa maisha. Hatuna tatizo naye hata akifia ofisini kwa hiyo tunakaribisha mapendekezo haya mapya ya kuwepo Kongamano la Mwaka Desemba ambalo litageuzwa kuwa mkutano mkuu maalumu,” alisema Chinguno.

Nyumba 9 zakubwa na bomoabomoa segerea

Dar es salaam. Kikosi cha bomoabomoa chini ya usimamizi wa mgambo kimevunja nyumba tisa katika mtaa wa Mogo, njia panda ya Segerea jijini Dar es Salaam.
Wakazi katika nyumba hizo wamesema hawakupewa taarifa kwamba leo Jumanne, Oktoba 17, 2017 zingebomolewa.
Baadhi ya wapangaji katika nyumba hizo wamesema wanamtambua mmiliki lakini hawakuwa wameelezwa chochote.
“Wamekuja asubuhi saa 11:00 wakaanza kubomoa watu tumelala ndani, tunawauliza wanasema oda ya kuondoka imetolewa wiki mbili zilizopita kwa mmiliki, lakini sisi hatujui, hakuna tangazo lolote lililotolewa kwa wapangaji," amesema mpangaji aliyejitambulisha kwa jina la mama Aloyce.
Baadhi ya wapangaji wamesema mmiliki wa nyumba hizo anadaiwa na benki.
Nyumba zilizobomolewa ni za makazi ya kuishi, vyumba vya biashara na kituo kinachotumiwa na Kanisa la Moravian Ukonga.
Wakati bomoabomoa hiyo ikiendelea, aliyekuwa akisimamia kazi hiyo alitoweka, huku wengine waliohusika kubomoa hawakutaka kueleza chochote.
Askari wa Jeshi la Polisi waliofika eneo hilo hawakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo wakisema si wasemaji.

BREAKING NEWS : TAKUKURU Yampa onyo Joshua Nassari,,,,

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imeita Waandishi leo Dar es salaam na kutoa onyo kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ambae alipeleka ushahidi wa rushwa kwa taasisi hiyo dhidi ya Mkuu wa Wilaya Arumeru Alexander Mnyeti.
TAKUKURU imesema “Ni kama Mh. Nassari na wenzie wanataka kulifanya hili swala kama la kisiasa badala ya kuwa la kisheria, namuonya Mh. Nassari ameshaleta taarifa yake kwetu, atuachie tufanye kwa mujibu wa sheria na sio kutushinikiza kama kauli aliyoitoa jana….. ‘nitaendelea kutoa series’ “
“Hii Taasisi haishinikizwi na mtu yeyote na hapaswi hata mara moja kutushinikiza…. natoa onyo jingine, endapo ataendelea na utaratibu huu tutachukua hatua za kisheria dhidi ya

Kampuni ya televisheni Uingereza yadukuliwa na Korea kaskazini,,,,

Wadukuzi wa Korea Kaskazini wamelenga kampuni moja ya vipindi televisheni nchini Uingereza ambayo inatengeneza kipindi wa kuigiza kuhusu nchi hiyo.
Kipindi hicho ambacho kilitarajiwa kuandikwa na mwandishi ambaye ashateuliwa kuwania tuzo za Oscar sasa kimesitishwa.
Mwezi Agosti mwaka 2014 Channel 4 ilitangaza kuwa kipindi hicho kitakuwa kipya na cha kuchokoza.
Kipindi hicho kinachojulikana kama Opposite Number, kinahusu mwanasayansi ya nyuklia muingereza ambaye amefungwa nchini Korea Kaskazini.
Mradi huo haujapiga hatua kutokana na kushindwa kupata ufadhili kwa mujibu wa kampuni hiyo.
Maafisa wa Korea Kaskazini walijibu kwa hasira wakati taarifa kuhusu kipindi hicho zilifichuka mara ya kwanza.
Pyongyang ilitoa wito kwa serikali ya Uingereza kuzima kipindi hicho ili kuzuia kuharibu uhusiano.
Korea Kaskazini kisha ikachukua hatua zaidi na kudukua kompiuta za kampuni husika.
Udukuzi huo haukusababisha uharibifu lakini, kuhusika kwa wadukuzi wa Korea Kaskazini mitandaoni kulizua hofu juu ya ni kipi wana uwezo wa kukifanya.
Hofu hiyo ilitokana sababu Sony Pictures ililengwa na udukuzi kama huo mwezi Novemba mwaka 2014.
Marekani ilisema kuwa udukuzi huo uliendeshwa na Korea Kaskazini.
Udukuzi huo nao ulikuwa ni jibu kwa filamu iliyopangwa kutolewa kwa jina The Interview, mchezo ambao kiongozi wa Korea Kaskazini aliuawa.

Malori ya Dangote yaua madereva

WATU watatu kati ya sita waliokuwa wakisafiri na malori yanayomilikiwa na kiwanda cha saruji cha Dangote mkoani Mtwara, wamekufa papo hapo na wengine kulazwa Hospitali ya Sokoine ya mkoa wa Lindi, baada ya magari hayo kugongana uso kwa uso.
Waliofariki ni Issa Rashidi Mbweso (28) ambaye ni dereva wa lori namba T 481 DJZ na mkazi wa mjini Mtwara, Haruni Nazir Mbonde (48) ambaye pia ni dereva wa lori la kiwanda hicho pamoja na utingo wake aliyefahamika kwa jina moja la Rajabu.
Majeruhi ni Ramadhani Nasoro (30) utingo na mkazi wa mjini Mtwara, Sophia Isumaili (35) na dada yake, Mawazo Omari (40) wakazi wa Kata ya Mandawa wilaya ya Kilwa.
Wakizungumza na Nipashe katika hospitali hiyo Lindi, majeruhi hao akiwamo utingo wa lori hilo namba T 481 DJZ lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mtwara, walisema ajali hiyo ilitokea eneo la kitongoji cha Mihambwe, kwenye barabara kuu ya Kibiti-Lindi juzi mchana.
Sophia Isumaili na dada yake Mawazo Omari waliokuwa wameomba lifti kutoka Mandawa kwenda Newala mkoani Mtwara, walisema walipofika kitongojini hapo na kukuta barabara imezibwa na wingu la moshi mzito, alimuomba dereva Issa ambaye ni marehemu asimamishe gari wasubiri kupungua kwa moshi huo, lakini alikaidi na kujitosa.
“Tulipofika eneo lile na kukuta moshi mwingi nilimshauri dereva wetu tusimame ili kupisha moshi, lakini hakuwa tayari na kujibu atapita tu bila shida,” alisema Sophia.
Utingo Ramadhani Omari alisema kutokana na dereva kukaidi ushauri huo, walijikuta wakigongana uso kwa uso na lori lingine lililokuwa limebeba saruji likiwa limesimama kando ya barabara kupisha kupungua kwa moshi huo.
Alisema baada ya malori hayo kugongana, kulijitokeza cheche za moto na kuteketea kwa magari yote hayo wakiwamo madereva na utingo, kabla ya gari la Zimamoto kutoka Manispaa ya Lindi kwenda eneo la tukio Mihambwe kuuzima moto.
Mganga wa zamu katika Hospitali ya Sokoine, Dk. Edgal Mlawa, alithibitisha kupokea miili na majeruhi watatu, lakini hakuwa tayari kutoa maelezo zaidi akisema hadi mkuu wake wa kazi atakapofika.
“Licha ya kuwa nipo zamu muda huu, lakini siwezi kuelezea zaidi kwani mwenye mamlaka ya kuzungumza na vyombo vya habari ni mkuu wangu wa kazi,” alisema Dk. Mlawa.
Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Renatha Mzinga, alipoulizwa kupitia simu yake ya mkononi, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza taarifa kamili ataitoa baada ya kupelekewa na vijana wake waliokuwapo eneo la tukio.

Audio | Mr Nana _ You Know Me | Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/281463/by/wt9QqBDHn_

VIDEO | Benjamin wa Mambo Jambo – Bang | Download

VIDEO | Benjamin wa Mambo Jambo – Bang | Download