Saturday, 14 October 2017

Rais wa TFF kufungua mkutano wa Uchaguzi wa bodi ya ligi Kesho

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ndiye atafungua Mkutano wa Uchaguzi wa Kamati ya Uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) utakaofanyika kesho Jumapili, Oktoba 15 mwaka huu, kuanzia Saa 2.00 asubuhi hadi Saa 7.15 mchana.
Kwa mujibu wa ratiba, Saa 2.00 asubuhi, Wajumbe na viongozi wengine watawasili Ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kabla ya mkutano huo kufunguliwa saa 3.00 asubuhi na Rais wa TFF, Wallace Karia atayekuwa Mgeni Rasmi.
Taarifa ya TFF imesema kwamba kutakuwa na mkutano na wanahabari saa 7.15 mchana mara baada ya mkutano wa Baraza hilo.
Jumla ya wajumbe 44 watashiriki Mkutano huo wa uchaguzi wa Baraza Kuu la TPLB. Wajumbe hao ni klabu 16 za Ligi Kuu, klabu 24 za Ligi Daraja la Kwanza na wawakilishi wanne wa klabu za Ligi Daraja la Pili.
Nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa kuwakilisha klabu za Ligi Kuu zitapigiwa kura na klabu 16 pekee za Ligi Kuu.
Wagombea saba wamepitishwa kuwania uongozi wa TPLB baada ya Kamati ya sasa kumaliza muda wote. Kamati mpya ya Uongozi itakayochaguliwa katika uchaguzi huo unaosimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF utakaa madaraka kwa kipindi cha miaka minne.
Waliopitishwa kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya orodha ya mwisho iliyotolewa Oktoba 9, mwaka huu ni Clement Andrew Sanga kutoka Yanga na Hamad Yahya Juma wa Mtibwa Sugar wanaowania uenyekiti wa TPLB.
Wengine ni Shani Christoms Mligo wa Azam FC ambaye ni mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti. Nafasi tatu za kuwakilisha klabu za Ligi Kuu kwenye Kamati ya Uongozi zimevutia wagombea wawili; Hamisi Mshuda Madaki (Kagera Sugar) na Ramadhani Marco Mahano (Lipuli).
Almasi Jumapili Kasongo kutoka Ashanti United FC ni mgombea pekee aliyejitokeza kuwania nafasi ya uwakilishi wa klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Klabu za Daraja la Kwanza zina nafasi mbili.
Klabu za Ligi Daraja la Pili zina nafasi moja kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB, na mgombea pekee aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo Edgar William Chibura kutoka Abajalo FC.

Yanga yaishusha chini Simba na Azam baada ya kuifunga kagera sugar mabao 2-1,,,,,,,

Klabu ya soka ya Yanga imeendeleza ubabe mbele ya Kagera Sugar baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu wamefanikiwa kuchukua alama tatu mbele ya wenyeji wao kupitia mabao ya Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu wakati bao pekee la Kagera limefunga na Jafari Kibaya.
Yanga sasa imesogea hadi kileleni ikifikisha alama 12 baada ya michezo sita sawa na Azam FC ambayo imelazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya Mwadui FC kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Mwadui Complex.
Matokeo mengine kwenye mechi za leo ni sare ya 0-0 kati ya Njombe Mji na Lipuli FC, wakati Ruvu Shooting nayo imetoka sare ya 0-0 na Singida United. Ndanda FC wametoshana nguvu na Majimaji baada ya kufungana 1-1.

Michezo: Klopp amsifu lukaku,,,,,,

London, England. Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amekiri kuwa wakati wote alikuwa anajua Romelu Lukaku atakuwa mshambuliaji bora dunia wakati timu yake ikijiandaa kumkabili nyota huyo wa Manchester United leo.
Lukaku amekuwa na mwanzo mzuri ndani ya Manchester United akiwa amefunga mabao 11 katika mechi 10 alizocheza za mashindano yote.
Klopp ambaye kikosi chake cha Liverpool kinawakaribisha vijana wa Jose Mourinho kwenye Uwanja wa Anfield, alisema alijua ubora wa Lukaku kabla ya kusajili kwa pauni 75milioni na Man United.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari, Mjerumani huyo alisema: "Amekuwa bora zaidi, na pia bado ni kijana mdogo.
"Nafikiri hakuna shaka yoyote kuwa ni mshambuliaji bora duniani na alishakuwa hivyo tangu akiwa Everton.
"Na sasa yupo katika kikosi cha wachezaji bora wa Man United wanamsaidia kukua zaidi."
Man United inaingia katika mchezo huo ikiwa na lengo la kuweka rekodi mpya baada ya mechi nane inataka kuvuka idadi ya pointi 20 ilizowahi kupata katika msimu wa 2011/12 na 1999/00.
Lakini wakiwa na pengo kubwa katika safu yao ya kiungo kutokana na kuwakosa nyota wake majeruhi Michael Carrick, Paul Pogba na Marouane Fellaini.
Liverpool wenyewe wanabidi kujitazama upya katika safu yao ya ulinzi kutokana na kufanya makosa mengi katika mechi zilizopita.
Pia, watamkosa Sadio Mane aliyeumia akiwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Senegal wiki hii, hivyo Klopp atalazimika kujifikiria upya.

News: Mugabe Kumpa nafasi kubwa mkewe

Harare, Zimbabwe. Rais Robert Mugabe amekubali kugeuza kongamano la mwaka la Zanu PFlililopangwa kufanyika Desemba kuwa mkutano mkuu wa congress unaotarajiwa kutumika kumshusha Makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa na kumpaisha mkewe Grace kuwania urais katika chama.
Kamisaa wa Taifa wa Zanu PF Saviour Kasukuwere ndiye aliyependekeza suala la mkutano wa congress alipokuwa anawasilisha ripoti yake kwenye kamati kuu ya chama Jumatano lakini ilibainika kuwa kinara huyo wa kundi la G40 alikuwa amepata ushauri kutoka majimbo matatu tu.
"Mugabe alisema utakuwa ukiukwaji wa taratibu hivyo akaagiza kamati ya maandalizi kuhakikisha ushauri umepatikana kutoka majimbo yote. Kutakuwa na vikao vya uratibu wa majimbo kutafakari suala hilo kuanzia mwishoni mwa wiki hii.
"Mkutano mkuu wa chama umepangwa ili kufanya mabadiliko ya katiba ili kuingiza kifungu cha kuwa na makamu wa rais mwanamke au kuanzisha makamu wa tatu wa rais,” mtu wa ndani alidokeza.
"Suala la urais limekamilika lakini misuguano ya ndani kuhusu kuwania mamlaka na umri wa Mugabe vimelazimisha kutafakari na Nyanja mbalimbali. Kumbuka kuwa Grace anataka madaraka na amekuwa akiomba awe makamu wa rais sambamba na Mnangagwa".
Msemaji wa Zanu PF, Simon Khaya Moyo amekataa kuzungumzia suala hilo.
Miezi miwili iliyopita Mugabe aliwataka wajumbe wa Zanu PF kufikiria kuingiza katika katiba nafasi ya makamu wa tatu wa rais. Hii ilikuwa baada ya mkewe kumtaka kiongozi huyo mkongwe wa Zanu PF kumtangaza mrithi anayempendelea katika mkutano mkuu wa wanawake.

Sifuti Mwenge - Magufuri,,,,,,,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema hatafuta Mwenge wa Uhuru katika kipindi chake cha uongozi kwasababu una faida mbalimbali kwa taifa.
Hayo ameyasema leo kwenye hotuba yake wakati akihitimisha mbio za Mwenge mwaka huu sambamba na kuazimisha miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa kwenye sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
Rais Magufuli amesema kwenye awamu yake kamwe hatafuta mbio hizo kwani zina saidia kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo nchini pamoja na kumuenzi Baba wa taifa Hayati Mwalimu Nyerere ambaye ndiye muasisi wa Mwenge wa Uhuru.
“Nafahamu kuna watu wanataka mbio za Mwenge zifutwe kwa kisingizio cha gharama lakini wanasahau kuwa Mwenge huo unasaidia kuanzishwa na kukamilika kwa Miradi ya maendeleo nchini. Nataka niwahakikishie kuwa kwenye uongozi wangu na Dkt. Shein hatutafuta Mwenge wa Uhuru”, amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa mbio za Mwenge zimekuwa zikisaidia kubaini madudu mbalimbali yanayofanyika kwenye Halmashauri nchini ikiwemo Miradi hewa. Rais ameahidi kuipitia ripoti nzima ya mbio hizo na kuyafanyia kazi mapendekezo yote yaliyoainisha.

Rais Mgufuli afunguka kuhusu Kufuta Mbio za Mwenge,,,,,,

“Nafahamu kuna watu wanataka mbio za Mwenge zifutwe kwa kisingizio cha gharama lakini wanasahau kuwa Mwenge huo unasaidia kuanzishwa na kukamilika kwa Miradi ya maendeleo nchini. Nataka niwahakikishie kuwa kwenye uongozi wangu na Dkt. Shein hatutafuta Mwenge wa Uhuru”, amesema Rais Magufuli.
Hayo ameyasema leo kwenye hotuba yake wakati akihitimisha mbio za Mwenge mwaka huu sambamba na kuazimisha miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa kwenye sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
Rais Magufuli amesema kwenye awamu yake kamwe hatafuta mbio hizo kwani zina saidia kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo nchini pamoja na kumuenzi Baba wa taifa Hayati Mwalimu Nyerere ambaye ndiye muasisi wa Mwenge wa Uhuru.
Mara baada ya kukabidhi Mwenge wa uhuru kwa Rais John Magufuli, kiongozi wa mbio hizo Amour Ahmad Amour amemueleza salamu za Watanzania kuwa wamempongeza kwa jitahada anazofanya kuikomboa Tanzania kiuchumi, hata hivyo aliongeza kuwa mbio hizo hazikuridhishwa na utekelazaji wa miradi katika baadhi ya halmashauri nchini.
Hata hivyo Waziri Wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Na Wenye Ulemavu Jenista Muhagama amewataka Watanzania wote kulinda tunu ya amani ambayo imekuwa ikihamasishwa na Mwenge huo, na kwamba katika mbio hizo miradi yenye thamani ya shilingi trilioni 2.1 ilizinduliwa na kati yake miradi 151 ni ya viwanda, Aidaha ameongeza kuwa jumla ya miradi 21 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.1 ilikataliwa kuzinduliwa na kuwekwa jiwe la msingi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mahamoud amemueleza Rais kuwa mwenge huo ulikimbizwa katika wilaya zote 3 za mkoa huo ambazo ni sawa na kilimeta za mraba 65 na kushuhudiwa na wananchi takribani laki moja na elfu ishirini, hata hivyo aliongeza kuwa kupita kwa mwenge huo umesaidia kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya.
Mbio hizo zilianza 2017 April 2, 2017 katika mkoa wa Katavi na kukimbizwa katika mikoa yote 31 Tanzania bara na visiwani umezimwa kitaifa katika Mkoa wa Mjini magharibi Visiwani Zanzibari ilikiwa na kauli mbiu ya Shiriki kukuza uchumi wa Viwanda kwa maendeleo ya Nchi yetu
Mbali na Rais Magufuli maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa na Makamu wa Rais wa pili Zanzibar Balozi Seif Iddi, Makamo wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, Viongozi waandamizi serikalini, Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, wakuu wa mikoa, Wawakilishi wa vyama na mabalozi wa nchi wa mbalimbali.
Kwa mwaka 2018 uzinduzi wa mbio za mwenge utafanyika mkoani Geita na mbio hizo zitamalizikia mkoani Tanga. Rais Mgufuli afunguka kuhusu Kufuta Mbio za Mwenge
 

Audio | Msaga Sumu_Watu Wasiojulikana | Mp3 Download

Bovya hapa  kudownload,,,,
https://my.notjustok.com/track/download/id/280296/by/_nBVZ4WU1n

Gambo: Madiwani wanakunwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kusema kuwa madiwani ambao wamehama kutoka CHADEMA na kuhamia CCM si kama wamenunuliwa au kuhongwa rushwa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu bali wanakunwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli.
Mrisho Gambo amesema hayo leo jijini Arusha na kusema kuwa kama CHADEMA wanajiamini wanakubalika na wananchi hivyo wasubiri uchaguzi ndiyo utawapa majibu kwani anaamini kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiyo kitashinda nafasi hizo kutokana na kukubalika kwa wananchi.
"Wale madiwani wamekunwa na utendaji uliotukuka wa Rais John Pombe Magufuli na siyo Arusha pekee yake, kule Arumeru madiwani wametoka, Monduli wametoka na kule Ngorongoro wametoka, wao kama wanajiamini wanakubalika na wanajiamini kuwa wale watu wao wamenunuliwa lakini wao kwenye maeneo hayo wanakubalika si wasubiri si tunakwenda kwenye uchaguzi, huko hakuna uteuzi na wanaokwenda kupiga kura ni wananchi hivyo wajipange waende kusomesha watu kule" alisema Mrisho Gambo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ni kati ya wateule wa Rais ambao CHADEMA kupitia kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki wanawatuhumu kuhusika na kutumia nafasi zao kununua baadhi ya madiwani wa CHADEMA kwa kigezo cha kuwa madiwani hao wanakubali kazi anazofanya Rais John Pombe Magufuli.

Yanga kamili kuivaa kagera sugar ,,,,

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, George Lwandamina amethibitisha kuwa kikosi chake kipo tayari kuivaa Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara VPL leo jioni kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Akizungumza katika mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo, Lwandamina amesema wachezaji wake wote wapo vizuri kuivaa Kagera ambayo itakuwa nyumbani.
Pamoja na kuwakosa wachezaji wake watatu, kiungo Thabani Kamusoko, mshambuliaji Donald Ngoma na mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe lakini bado Lwandamina ana imani na wachezaji wengine waliopo kwenye kikosi chake.
“Timu yetu inawakosa Tambwe, Ngoma na Kamusoko, lakini bado timu yetu ina kikosi cha kutosha na nina imani na wachezaji wote wanaweza kufanya vizuri,”amesema Lwandamina.
Ukiacha mchezo wa Yanga, Ligi Kuu itaendelea leo kwa mechi zingine nne ambapo Mwadui FC wataikaribisha Azam FC Uwanja wa Mwadui Complex, Ndanda watawakaribisha Maji Maji ya Songea, wakati Singida United itacheza na wenyeji Ruvu Shooting ya Pwani.
Njombe Mji na Lipuli ya Iringa watacheza kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe

Breaking News: Marekani yasikitishwa na Hatua ya Odinga

Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imesema inaheshimu lakini inajutia uamuzi wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, kujiondoa kwenye Uchaguzi mpya wa urais tarehe 26 mwezi huu.
Hata hivyo, Marekani imeendelea kusisitiza kuwa, itaendelea kushinikiza kuwepo kwa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki.
Afisa wa juu katika Wizara hiyo ameliambia Gazeti la Daily Nation kuwa, pamoja na hilo Odinga anakaribishwa nchini Marekani.
Taarifa hii imekuja baada ya kuwepo kwa madai kuwa Odinga amenyimwa Visa ya kwenda Marekani.
Marekani imesema hakuna kinachomzuia Odinga kuja nchini Marekani wakati wowote anaotaka.
Kwa sasa Odinga yupo jijini London nchini Uingereza, anakotoa midhahara ya kisiasa na kukutana na viongozi mbalimbali

Video : Diamond Platnumz Alivyokinukisha Uganda,,,,,,


Kocha Lwandamina: Vijana wapo tayari kwa kuipigania Yanga kesho

KOCHA wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amesema kwamba wachezaji wake wako vizuri kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Akizungumza baada ya mazoezi ya jioni Uwanja wa Kaitaba, Lwandamina amesema wachezaji wake wote wapo vizuri kuelekea mchezo huo kesho jioni.
Lwandamina amesema japokuwa atawakosa wachezaji wake watatu tegemeo, Wazimbabwe kiungo Thabani Kamusoko, mshambuliaji Donald Ngoma na mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe - lakini hana shaka vijana waliopo watafanya vizuri.
“Tutawakosa Kamusoko, Ngoma na Tambwe, lakini nina imani na wachezaji niliokuja nao hapa wanaweza kufanya vizuri,”amesema.
Kwa ujumla, Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho na mbali na mabingwa hao watetezi, Yanga kuwa wageni wa Kagera Sugar, Mwadui FC wataikaribisha Azam FC Uwanja wa Mwadui Complex,
Shinyanga na Ndanda watawakaribisha jirani zao, Maji Maji ya Songea Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati Singida United itasafiri hadi Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi kucheza na wenyeji Ruvu Shooting ya Pwani.
Majirani wengine, Njombe Mji na Lipuli ya Iringa watacheza kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe ilihali michezo mingine ya Ligi hiyo ikifanyika Jumapili Oktoba 15, ambako Simba itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Tanzania Prisons itacheza na Stand United kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.