Saturday, 14 October 2017

Rais Mgufuli afunguka kuhusu Kufuta Mbio za Mwenge,,,,,,

“Nafahamu kuna watu wanataka mbio za Mwenge zifutwe kwa kisingizio cha gharama lakini wanasahau kuwa Mwenge huo unasaidia kuanzishwa na kukamilika kwa Miradi ya maendeleo nchini. Nataka niwahakikishie kuwa kwenye uongozi wangu na Dkt. Shein hatutafuta Mwenge wa Uhuru”, amesema Rais Magufuli.
Hayo ameyasema leo kwenye hotuba yake wakati akihitimisha mbio za Mwenge mwaka huu sambamba na kuazimisha miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa kwenye sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
Rais Magufuli amesema kwenye awamu yake kamwe hatafuta mbio hizo kwani zina saidia kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo nchini pamoja na kumuenzi Baba wa taifa Hayati Mwalimu Nyerere ambaye ndiye muasisi wa Mwenge wa Uhuru.
Mara baada ya kukabidhi Mwenge wa uhuru kwa Rais John Magufuli, kiongozi wa mbio hizo Amour Ahmad Amour amemueleza salamu za Watanzania kuwa wamempongeza kwa jitahada anazofanya kuikomboa Tanzania kiuchumi, hata hivyo aliongeza kuwa mbio hizo hazikuridhishwa na utekelazaji wa miradi katika baadhi ya halmashauri nchini.
Hata hivyo Waziri Wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Na Wenye Ulemavu Jenista Muhagama amewataka Watanzania wote kulinda tunu ya amani ambayo imekuwa ikihamasishwa na Mwenge huo, na kwamba katika mbio hizo miradi yenye thamani ya shilingi trilioni 2.1 ilizinduliwa na kati yake miradi 151 ni ya viwanda, Aidaha ameongeza kuwa jumla ya miradi 21 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.1 ilikataliwa kuzinduliwa na kuwekwa jiwe la msingi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mahamoud amemueleza Rais kuwa mwenge huo ulikimbizwa katika wilaya zote 3 za mkoa huo ambazo ni sawa na kilimeta za mraba 65 na kushuhudiwa na wananchi takribani laki moja na elfu ishirini, hata hivyo aliongeza kuwa kupita kwa mwenge huo umesaidia kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya.
Mbio hizo zilianza 2017 April 2, 2017 katika mkoa wa Katavi na kukimbizwa katika mikoa yote 31 Tanzania bara na visiwani umezimwa kitaifa katika Mkoa wa Mjini magharibi Visiwani Zanzibari ilikiwa na kauli mbiu ya Shiriki kukuza uchumi wa Viwanda kwa maendeleo ya Nchi yetu
Mbali na Rais Magufuli maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa na Makamu wa Rais wa pili Zanzibar Balozi Seif Iddi, Makamo wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, Viongozi waandamizi serikalini, Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, wakuu wa mikoa, Wawakilishi wa vyama na mabalozi wa nchi wa mbalimbali.
Kwa mwaka 2018 uzinduzi wa mbio za mwenge utafanyika mkoani Geita na mbio hizo zitamalizikia mkoani Tanga. Rais Mgufuli afunguka kuhusu Kufuta Mbio za Mwenge
 

No comments:

Post a Comment