Friday, 26 January 2018

Waziri Lukuvi atangaza uamuzi mzito Mwanza


WANANCHI wanaomiliki nyumba 664 katika mitaa ya Kigoto na Kabuhoro katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza wametakiwa kuwa na subira wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa mgogoro uliopo kati yao na Jeshi la Polisi.

Pia wamezuiwa kujenga nyumba zingine mpya kwenye maeneo ya mitaa yao na badala yake wawe walinzi na kuonya watakaothubutu kujenga hawatalipwa fidia ambapo awali walitakiwa kuondoka na kupisha eneo hilo baada ya kuandikiwa ilani ya siku saba na jeshi la polisi.

Akizungumza na wananchi hao Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema serikali imesikia kilio chao na hivyo amekuja chunguza mgogoro huo ili ifanye uamuzi wa kuutatua.

 Alisema serikali inataka kufahamu mahitaji ya wananchi na polisi na kuonya wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo wasithubutu kujenga (kuongeza) majengo mengine zaidi ya yaliyopo sasa na watakaokaidi hawatalipwa fidia.

“Nimekuja kuangalia mgogoro huu na kuchungumza jambo hili ili serikali ifanye uamuzi. Msidhani nina majibu, majibu yatatolewa ndani ya mwaka mmoja lakini msituhubutu kuongeza nyumba zingine zaidi, kuweni walinzi wa maeneo haya na tunataka muwe maeneo mzuri ili tuwarasimishie,”alisema Lukuvi.

Waziri huyo wa ardhi alisisitiza baada ya uchunguzi atamshauri vizuri Rais John Magufuli namna ya kumaliza mgogoro huo baina ya wananchi na taasisi hiyo ya serikali.

Lukuvi alieleza eneo la Kigoto ambalo Polisi inadai inataka kujenga Chuo cha Polisi wanamaji, nyumba za askari na  gati la boti na meli za doria zinaweza kujengwa popote lakini eneo hilo lazima lipangwe upya hata kama matumizi yakibadilishwa kwa kuwa haiwezekani watu waishi kwenye nyumba za ovyo ovyo.

“Miaka 70 hadi leo kwa nini ujenzi haukuzuiwa,hakuna viongozi hapa na kama mngewashirikisha wangewasaidia kuzuia.Je, upembuzi yakinifu ulifanyika kwenye eneo mnalotaka kujenga mdomo huo wa gati la boti za polisi?

Aidha akizungumza kwa niaba ya wenzao ,Ferdinand Mtundubalo alimweleza Waziri kuwa hawana tatizo na ujenzi wa gati la boti za polisi isipokuwa warasimishiwe makazi yao ili waondokanane na mgogoro huo.

Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi aliwataka wataalamu wa wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waainishe eneo la Uwanja wa Ndege wa Mwanza na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha Ihale ili kila mmoja alinde eneo lake.

Pia alishauri eneo la Nyamwilolelwa litakalobaki baada ya kutengwa la uwanja wa ndege na JWTZ lipimwe wapewe wananchi wa eneo wapatao 1,961 na kuhusu barabara ya Mwanza –Igombe uamuzi wa Rais Magufuli ubaki ulivyo na uheshimiwe.

Kampeni za Ubunge Jimbo la Ubungo kuzinduliwa na Lowassa, Mbowe


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kesho Januari 27, 2018 watakuwepo katika uzinduzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Kinondoni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CHADEMA leo inasema kuwa viongozi hao watakuwepo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni kumtambulisha Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Salum Mwalimu.

Uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika katika viwanja vya Mapilau kuanzia saa nane mchana mpaka saaa kumi na mbili jioni ambapo wageni rasmi watakuwepo Lowassa pamoja na Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA.

Tarehe 17 Februari mwaka huu unatarajiwa kufanyika uchaguzi wa marudio katika majimbo ya Siha na Kinondoni kutokana na wabunge wa majimbo hayo kujiuzulu nafasi zao za Ubunge wakiwa katika vyama vya upinzani na kuingia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa wanagombea nafasi hizo wakiwa chini ya CCM.

New VIDEO: Maleek Berry – Pon My Mind

New VIDEO: Maleek Berry – Pon My Mind

New VIDEO: Maleek Berry – Pon My Mind


Audio | King James – Uri mwiza | Mp3 Download

Audio | King James – Uri mwiza | Mp3 Download

Audio | King James – Uri mwiza | Mp3 Download

New Audio | AKA – Sweet Fire

New Audio | AKA – Sweet Fire
New Audio | AKA – Sweet Fire

New Audio | Professor ft Cassper Nyovest & Mono T – Can’t Get Away

New Audio | Professor ft Cassper Nyovest & Mono T – Can’t Get Away

New Audio | Professor ft Cassper Nyovest & Mono T – Can’t Get Away

Audio | Man Fongo ft Badria – Kimya Kimya |Mp3 Download

Audio | Man Fongo ft Badria – Kimya Kimya |Mp3 Download

Audio | Man Fongo ft Badria – Kimya Kimya |Mp3 Download


  1. DOWNLOAD

MAGAZETI YA LEO 26/1/2018























Wema matatani kwa kudaiwa kuwafuga Mashoga




Mrembo wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amejikuta akiingia matatani kwa kudaiwa ‘kuwafuga’ wanaume wanaodaiwa ‘si riziki’ (mashoga) nyumbani kwake, Salasala.

Kwa mujibu wa chanzo makini, mrembo huyo amekuwa akiishi na wanaume hao tata kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likiwakera majirani wanaomzunguka na kuwafanya wamshitaki serikalini.

“Unajua hii tabia yake si ya leo, ameanza muda mrefu na amekuwa akiwakera majirani zake kwani wanahofia kuharibiwa watoto wao wa kiume kwa kufuata matendo yao,” kilidai chanzo.

Kikizidi kushusha madai hayo chanzo hicho kilienda mbali zaidi kwa kusema mrembo huyo ni sikio la kufa kwani alikuwa akiishi na mashoga hao tangu alipokuwa anaishi maeneo ya Ununio jijini Dar hadi kumsababishia matatizo pia. “Kule Ununio alikuwa nao hawa mashoga, sijui ni marafiki zake au ni watu wa aina gani kwake.

Watu wengi wanajiuliza kwanini anawakumbatia, wanakosa majibu. “Kama mnakumbuka vizuri hata mama yake aliwahi kwenda kuwatimua mashoga hao baada ya kuona wanamharibia lakini sijui Wema anawapendea nini, bado yuko nao tu,” kilizidi kumwaga ubuyu chanzo hicho. Baada ya kunasa ubuyu huo, wanahabari wetu walifika nyumbani kwa Wema alikohamia kwa sasa, Salasala jijini Dar ili kuweza kujionea mashoga hao lakini ilishindikana baada ya kugonga geti muda mrefu bila kufunguliwa.

Hata hivyo, Ijumaa lilifanikiwa kuzungumza na mjumbe wake wa nyumba kumi, Marko Mbaku ambaye alisema taarifa za uwepo wa mashoga amezisikia lakini ameshindwa kupata ushirikiano kutoka kwa Wema.

“Kwanza niseme tu simtambui Wema maana hajaja hata kujitambulisha kwangu tangu amehamia hapa, nimeletewa malalimiko mengi dhidi yake lakini kila nikimpelekea barua hajibu chochote wala haji,” alisema mjumbe huyo na kushauri waandishi waende ofisi za serikali ya mtaa kwani kuna taarifa zaidi.

Ijumaa lilifika Ofisi za Serikali ya Mtaa wa Salasala na kuzungumza na wajumbe wake ambao kwa pamoja walikiri kuwepo kwa mashoga nyumbani kwa Wema na kushauri waandishi wazungumze na mwenyekiti wao kwa  taarifa zaidi.

Alipotafutwa Mwenyekiti Hashim Bakari, alikiri uwepo wa malalamiko hayo ofisini kwake na kwamba wanajipanga kwenda kuzungumza na mrembo huyo ili kama atashindwa kuwatoa, basi wamhamishe mtaa.

“Ni kweli malalamiko hayo yapo, tunajipanga kwenda kumuona Wema Sepetu ili kama wapo hao mashoga awaondoe, akikaidi tutamhamisha hapa mtaani kwetu,” alisema mwenyekiti huyo

. Waandishi wetu katika jitihada za kumpata Wema ili kuzungumzia madai hayo, kwanza walifika nyumbani kwake tena ambapo safari hii walifunguliwa geti na mwanaume ambaye alisema staa huyo hayupo na kwa maelezo zaidi apigiwe simu. Wema alipopigiwa simu mara zote iliita bila kupokelewa. Jitihada za kumpata bado zinaendelea.

Barcelona watinga nusu fainali Kombe la Mfalme



Klabu ya Barcelona usiku wa kuamkia Leo imefanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe  la Mfalme maarufu kama Copa del Rey kwa ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Espanyol .

Magoli ya Barcelona yamefungwa na Lionel Messi na Luis Suarez ambapo kwa matokeo hayo Barca imefuzu kwa jumla ya tofauti ya goli 2-1 baada ya mechi ya kwanza Barcelona kufungwa goli 1-0.

Barcelona imeungana klabu ya Valencia, Sevilla na Leganes ambazo zote zimefuzu juzi

Trump kuinyima msaada Palestina?


Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kusitisha misaada kwa taifa la Palestina iwapo litakataa kushiriki katika mazungumzo ya amani.

Wizara ya maswala ya kigeni imethibitisha kuwa alikuwa akizungumzia msaada wa kiuchumi na usaidizi wa kiusalama.

Bwana Trump aliishutumu Palestina kwa kuivunjia heshima Marekani akisema ''kwa nini tuwafanyie kitu na wao wenyewe hawatufanyii chochote''.

Palestina imeikataa Marekani kuwa mpatanishi asiyependelea upande wowote katika mazungumzo hayo ya amani.

Wamekasirishwa na hatua ya Washington kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Afisa aliyekuwa akiongoza ujumbe wa mazungumzo upande wa Palestina Saeb Erakat alijibu matamshi ya hivi karibuni ya rais Trump: Trump anaweza kununua vitu vingi na fedha lakini hawezi kununua heshima yetu.

Akizungumza katika kongamano la kiuchumi mjini Davos, Switzerland, bwana Trump alisema kuwa Marekani inawapatia Palestina mamia ya mamilioni ya madola kama msaada na usaidizi kila mwaka.

Alilalamikia hatua ya uongozi wa Palestina wa kukataa kukutana na makamu wa rais wa Marekani Mike Pence katika eneo hilo mapema wiki hii.

Amesema kuwa yeye ndio rais wa kwanza kwa kuhusisha msaada na mpango wa amani.

''Hizo pesa ziko katika meza lakini hazitawafikia hadi pale watakapokubali kuketi katika meza ya mazungumzo na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu''.

''Ninaweza kuthibitisha kwamba Israel inataka kuanza mazungumzo ya amani nao, na wao Palestina watalazimika kukubali kuanza mchakato huo ama la sivyo hatutashughulika tena''.


Kigwangala atoa siku saba kwa Kampuni za Uwindaji Nchini


WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala, ametoa siku saba kwa kampuni sita za uwindaji nchini kufika katika ofisi za wizara hiyo Dodoma, kujieleza kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya ujangili.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Dk. Kigwangala alisema kampuni hizo zina leseni halali za uwindaji, lakini ndani yake wamekuwa wakifanya vitendo ambavyo vinaashiria uvunjifu wa sheria na uhalifu dhidi ya wanyama.

Alizitaja kampuni hizo kuwa ni Berlette Safari Corporation Ltd,  Game Frontiers of Tanzania Ltd, Mkwawa Hunting Safaris Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris Ltd, Wengert Windrose Safari Ltd na Geenniles Safaris Ltd.

Alisema wakurugenzi wa kampuni hizo na washirika wao wanatakiwa kufika ofisi za Wizara Dodoma kuhojiwa na kikosi kazi maalum kuhusiana na tuhuma hizo.

“Waje hapa wazungumze na kikosi hiki wajieleze ni kwa nini tusichukue hatua za kisheria dhidi yao, lakini pia wajibu hoja mbalimbali zitakazohusisha makosa mbalimbali. Wakurugenzi wote na washirika wao wafike wao wenyewe bila kutuma uwakilishi na bila kutoa sababu zozote,” alisema.

Alisema baada ya kuwahoji watachukua hatua za kiutawala kulingana na sheria ya uwindaji na baada ya hapo kwa makosa yatakayojulikana ni ya jinai yatapelekwa vyombo vya dola vinavyohusika na makosa hayo ikiwamo ya ujangili kama itabainika kwenye kikosi hicho.

Dk. Kigwangala alitaja tuhuma zingine kuwa ni uwindaji haramu, uhawilishaji wa umiliki wa vitalu vya uwindaji bila kufuata sheria, ikiwamo makosa ya ujangili, kujaza fomu za udanganyifu, rushwa, uhalifu dhidi ya rasilimali za wanyamapori, uhujumu uchumi, ukiukwaji wa kanuni za uwindaji na kutolipa tozo mbalimbali.

Pamoja na kampuni hizo, alimwagiza mmoja wa watumishi wa wizara hiyo, Alex Aguma, afike pia kuhojiwa.

MTANDAO WA MAJANGILI

Waziri huyo alisema katika kipindi cha siku 100 ambazo amekuwa katika nafasi hiyo,  wizara hiyo imekamata watuhumiwa 74 na kubaini mitandao yao yote na hatimaye kubainisha mtandao mzima ambao una washirika 949 wa ujangili.

Alisema kati ya hao nusu wamechukuliwa hatua mbalimbali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani na kwamba wanaendelea na ufuatiliaji wa watuhumiwa wengine ambao wametajwa na washiriki wao, lakini wengine wamekimbia maeneo mbalimbali.

“Lakini pia napenda kutambua kazi kubwa iliyofanywa tangu mwaka 2010 hadi 2013-2014 ambao ilikuwa  mwisho wa operesheni tokomeza ambayo ilikuwa inajibu mashambulizi kutokana na kukithiri kwa ujangili ambao ulikuwepo mwaka 2010-2015.

“Operesheni tokomeza serikali iliweza kubainisha watuhumiwa mbalimbali takribani 2130 ambao walituhumiwa kwa uhujumu uchumi, lakini kukutwa kwa silaha 3715 zilizokamatwa, meno ya tembo ghafi 3789 yenye uzito wa kilo 12,194, vipande 695 vya meno yaliyochakatwa,”alisema.

Jangili adakwa Loliondo

Aidha Dk.Kigwangala alisema usiku wa kuamkia jana amekamatwa muuaji Loliondo ambaye yeye kazi yake ni kulenga shabaha na silaha anachukua kwa mtu mwingine.

“Tumetengeneza utaratibu wa kuwafuatilia katika ngazi tofauti tofauti hadi tuvunje mtandao mzima wa ujangili hapa nchini, na sasa tunawatambua kwa ngazi tano za ujangili na biashara haramu na tunawabainisha majangili kwa madaraja yao, daraja la anayeenda kuua, kulenga shabaha, kusafirisha, wakala, anayefadhili, anayevuka mipaka kwenda nchi nyingine, mitandao ya kuuza nyara nje ya nchi,” alisema.

Hizi ndizo sababu za Kagera Sugar kutomuadhibu Nyoso



JUMA NYOSO.

SIKU chache baada ya kuachiwa kwa dhamana beki wa kati wa Kagera Sugar, uongozi wa timu hiyo umetoa sababu kwa nini hawatamchukulia hatua mchezaji huyo anayetuhumiwa na madai ya kumpiga shabiki wa soka.

Nyoso, alikamatwa na Jeshi la Polisi mara baada ya mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Simba uliofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na wenyeji kulala kwa mabao 2-0.

Akizungumza jana na kituo kimoja cha redio, Mratibu wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein, alisema kuwa klabu hiyo haitamchukulia hatua yoyote Nyoso kutokana na kitendo hicho kwa sababu jambo hilo lilifanyika nje ya uwanja na pia shabiki huyo Shabaan Hussein alimfanyia vitendo vya ‘kumpandisha hasira’ Nyoso.

“Nyoso kwa sasa yupo nje kwa dhamana na amejiunga na kambi ya timu, lakini niweke wazi hatotumchukulia hatua yoyote sisi kama klabu,” alisema Hussein.

Alisema kuwa Nyoso ni binadamu na kitendo cha shabiki yule kumpulizia Vuvuzela sikioni na kumtukana kilimtia hasira.

“Hatukubaliani na kitendo cha kupiga shabiki, lakini kama ni adhabu basi vyombo vya dola au Shirikisho (TFF),” aliongeza kusema.

Nyoso aliwekwa mahabusu kuanzia Jumatatu mpaka juzi baada ya hali ya shabiki huyo kuwa mbaya katika kipindi hicho.