Thursday, 25 January 2018

New VIDEO: DJ Big N ft Reekado Banks, Iyanya & Ycee – The Trilogy

New VIDEO: DJ Big N ft Reekado Banks, Iyanya & Ycee – The Trilogy

New VIDEO: DJ Big N ft Reekado Banks, Iyanya & Ycee – The Trilogy


DOWNLOAD VIDEO

New VIDEO: Samklef ft. Akon – Skelebe

New VIDEO: Samklef ft. Akon – Skelebe

New VIDEO: Samklef ft. Akon – Skelebe


DOWNLOAD VIDEO

Audio | Vinny Roy – Niende | Mp3 Download

Audio | Vinny Roy – Niende | Mp3 Download

Audio | Vinny Roy – Niende | Mp3 Download

DOWNLOAD

Jaji Ramadhan ataka majaji kumuenzi Jaji Kisanga

Jaji Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhani amemzungumzia Jaji Robert Kisanga kuwa mtu aliyebobea katika taaluma na hakuwahi kujihusisha na rushwa.

Amesema hayo leo Alhamisi Januari 25,2018 Oysterbay jijini Dar es Salaam alikokwenda kuhani msiba wa Jaji Kisanga (85).

Jaji Ramadhani amesema hakuna hata siku moja aliwahi kusikia malalamiko dhidi ya Jaji Kisanga kutokana na uadilifu wake.

"Mimi ni miongoni kwa watu waliopitia kwenye mikono yake, yeye ndiye aliyenifundisha masuala ya Mahakama ya Rufaa," amesema.

Amesema, “Alikuwa mahiri kwenye kazi na kama uko naye kwenye kesi ni muhimu usome sana kwa sababu alikuwa anasoma na kila jambo alilichimba kwa undani."

Jaji Ramadhani amesema, "Naweza kusema ni miongoni mwa majaji waadilifu, kwake rushwa ilikuwa mwiko, hakuwahi kujihusisha na vitendo hivyo ndiyo sababu sikuwahi kusikia malalamiko dhidi yake."

Amesema majaji wanatakiwa kujifunza tabia hiyo kutoka kwa Jaji Kisanga.

"Majaji wanapaswa kutambua kuwa hakuna kitu kibaya kama kuuza utu wa mtu, mwenzetu Kisanga alizingatia mno sheria na hata mawakili waliokuwa wanapangiwa kesi kwake walikuwa wanajipanga," amesema.

Jaji Kisanga alifariki dunia Jumanne Januari 23,2018 katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya saratani.

Dk. Mabodi atuma salam za rambi rambi kwa magufuli

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ametuma salamu za rambi rambi kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Omar Kinana amfikishie Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli, kufuatia kifo cha Mtumishi wake    Marehemu Bi. Nakia Khamis Abdalla aliyefariki leo Januari 25, 2018.
Bi. Nakia amefariki dunia akiwa nyumbani kwake mtaa wa Sogea Zanzibar baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Katika Salamu zake  Dk. Mabodi amesema  CCM Zanzibar  imepokea taarifa ya kifo cha mtumishi huyo  kwa Mshutuko, Majonzi na Simanzi kubwa, kwani Marehemu enzi za uhai wake alikuwa Mwadilifu aliyefanya kazi kwa bidii na ubunifu wa hali ya juu katika utumishi wake.
Pamoja na hayo alitoa pole kwa familia Wanachama, Viongozi na Watendaji Wote wa CCM, Marafiki pamoja na Jamaa wa karibu walioguswa na msiba huo, na   kuwaomba waendelee kuwa na uvumilivu katika kipindi chote cha msiba huo.
“ Marehemu alikuwa ni mfano wa kuigwa enzi za uhai wake hasa kwa kujitolea na kukipigania Chama cha Mapinduzi muda wote wa uhai wake, hivyo  tumepoteza mtu muhimu sana ndani ya Chama na Taifa kwa ujumla.
Pia nawaomba watumishi na wanachama na Familia ya Marehemu kuwa na Subra katika kipindi hiki kigumu cha Msiba huo, na tuendelee kumuombea dua mwenzetu ili Mwenyezi Mungu amuweke pahala pema peponi Amin.”, alieleza Dk. Mabodi.
Marehemu Bi. Nakia Khamis Abdalla amefariki leo Tarehe 25/1/2018 Nyumbani kwake Mtaa wa Sogea Zanzibar baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu, amezaliwa Januari 6,1965 katika Kijiji cha Ndagaa Wilaya ya Kati Unguja.
Alipata elimu yake ya Sekondari ya Kidato cha Tatu katika Shule ya Ben-Bella Mjini Zanzibar.
Enzi za uhai wake Marehemu Bi. Nakia amehudumu katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kwa  nafasi mbali mbali zikiwemo Ukarani wa Simu (Telephone Operator), Ulinzi pamoja na nyinginezo.
Marehemu ameolewa na ameacha Mume na Watoto Wawili. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu pahala Pema Peponi Amin.
Source: Zanzibar24

Watu watano wanusurika kuungua na moto

Watu watano wamenusurika kifo baada ya nyumba wanayoishi kuteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Alhamisi Januari 25,2018 eneo la Mitondooni wilayani Magharibi B, Unguja.

Chanzo cha moto kinaelezwa kuwa ni hitilafu ya umeme ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali amesema moto ulitokea saa moja usiku.

Mayasa Makame aliyenusurika katika janga hilo amesema moto ulizuka ghafla walipokuwa wakipika.

Amesema wamepoteza kila kitu kilichokuwamo ndani.

Kuhusu chanzo cha moto imeelezwa huenda ikawa ni hitilafu ya umeme kwenye jokofu.

Mayasa ameiomba Serikali na wananchi kwa jumla kuwasaidia kwa kuwa hawana chochote kwa sasa

JPM amwagiwa pongezi na Rais wa Benki ya maendeleo

Rais John Magufuli amepongezwa na mjumbe maalum wa Rais wa Rwanda na aliyewahi kuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Donald Kaberuka kwa kuweza kuweza kusimamia ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

Pongezi hizo zimetolewa leo wakati Rais Magufuli alipokutana na mjumbe na kufanya mazungumzo katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Tanzania na umoja wa Afrika (AU), yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

"Nimefurahi sana jinsi Tanzania inavyokwenda mbele, maendeleo yanakwenda kwa kasi na Mhe. Rais anafahamu kabisa kwamba katika Afrika nchi zetu zinahitaji kuwa na uchumi bora, ningependa kumpongeza Mhe. Rais na watanzania wote kwa kazi nzuri wanayofanya", alisema Dkt. Kaberuka.\

Aliyekamatwa akisafirisha dola ajidhamini

Mfanyabiashara Boniface Mbilinyi (32) ambaye hivi karibuni alikamatwa na jeshi la polisi akitaka kusafirisha kiasi kikubwa cha Dola za Marekani kwenda nje ya nchi kinyume na utaratibu, amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kudanganya kiasi cha fedha alichokuwa akitaka kusafiri nacho.

Mbilinyi anadaiwa kutamka kuwa na kiasi cha Dola 40,000 wakati alikuwa na Dola 123,000.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Awamu Mbagwa, amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, kuwa Januari 13, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi umekamilika na wapo tayari kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Baada ya kusomewa kesi inayomkabili, Hakimu Shaidi alisema kwa kuwa kiasi hicho cha fedha zipo mikononi kwa serikali, aliamuru mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua na kitambulisho na kwamba fedha hizo zitasimama kama bondi na kesi imeahirishwa hadi Februari 7, mwaka huu.

Yondani, Chirwa kamili kuivaa Azam

Yanga wao wameamua kufanya mambo yao kimyakimya wakijiandaa na mechi ya Jumamosi.

Sasa hawana wanachoweza kulaumu maana mechi yao dhidi ya Azam FC itachezwa saa 10 jioni, Jumamosi.

Wanachotaka ni kushinda na Kocha Mkuu, George Lwandamina aliagiza mazoezi makali yafanyike na juzi wachezaji walikuwa hoi.

Sasa wamelegeza ukali wa mazoezi na wanaendelea na mazoezi ya mbinu zaidi kuhakikisha ushindi unapatikana Jumamosi.

Pamoja na kwamba watamkosa Pius Buswita ambaye ana kadi tatu za njano, mshambuliaji Obrey Chirwa kamaliza adhabu yake anarejea.

Lakini Yanga watakuwa na uhakika kwamba ukuta utaimarika tena wakati Kelvin Yondani anarejea pia.

Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu kubwa, Yanga wakitaka kupunguza pengo lao kubwa dhidi ya Simba na Azam pia lakini Azam FC wakitaka kushinda wazidi kuipa presha Simba iliyo kileleni mwa msimamo.

Rais Magufuli amkaribisha mrithi wa Mugabe nchini

Rais John Magufuli amemkaribisha Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe kutembelea nchini.

Dk Magufuli ametoa mwaliko huo leo Alhamisi Januari 25,2018 alipoagana na Balozi wa Zimbabwe nchini anayemaliza muda wake Edzai Chimonyo.

“Naomba umwambie Rais Mnangagwa kuwa namkaribisha atembelee Tanzania na namtakia heri katika majukumu yake, natarajia ataendeleza uhusiano na ushirikiano wetu ili tuweze kujiimarisha zaidi kiuchumi kwa manufaa ya nchi hizi mbili,” amesema Rais Magufuli katika taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amempongeza Balozi Chimonyo kwa uwakilishi mzuri alioufanya kwa miaka 10 aliyoiwakilisha Zimbabwe nchini.

Pia, Dk Magufuli amemuomba Balozi Chimonyo kumfikishia pongezi Rais Mnangagwa kwa kuchaguliwa kuongoza Zimbabwe.

Amemhakikishia kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria na kidugu uliopo kati yake na Zimbabwe.

Balozi Chimonyo ameshukuru Rais kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chake cha ubalozi nchini na amempongeza kwa namna anavyoiongoza nchi.

Ametaja baadhi ya mambo yanayofanywa kwa mafanikio kuwa ni mapambano dhidi ya rushwa, ujenzi wa miundombinu na hasa barabara, madaraja na viwanja vya ndege.

Balozi Chimonyo aliyekuwa kiongozi wa mabalozi wa Afrika na kaimu kiongozi wa mabalozi wote wanaowakilisha nchi zao Tanzania amesema wanafurahishwa na wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli, ikiwemo kuhamia makao makuu Dodoma.

VIDEO: Kibano Kwa Wanaohusika uteswaji wa Vijana

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Mwigulu Nchemba ameagiza kutafutwa na kukamatwa mara moja kwa watu wote wanaohusika na uteswaji wa vijana wanaopelekwa nje ya nchi kutafuta ajira.


TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KU SUBSCRIBE HAPA CHINI

Makonda Azindua Jengo La Upasuaji Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezindua jengo la upasuaji katika Hospitali ya Mwananyamala lililojengwa kwa msaada wa kampuni ya GSM.

Katika uzinduzi huo Makonda amesema kuwa Serikali itaandaa mpango wa kuwezesha wananchi kupata matibabu kwa kutumia kadi ya bima ya afya katika hospitali zote za umma.

Aidha amesema mwananchi mkoani Dar es Salaam ambaye hatakuwa na kadi hiyo hataweza kupata huduma.
Amesema lengo la mpango huo ni kuwawezesha wananchi kuwa na uhakika wa matibabu hata wakati hawana fedha.

"Ni muhimu tuingie kwenye mfumo wa matibabu kwa kadi badala ya kuchangishana na kusumbua watu kwenye simu. Itafikia wakati mtu ambaye hana kadi hatatibiwa kwenye hospitali zetu," amesema.

Serikali inaendelea kuboresha mazingira na miundombinu ili kuwapatia wananchi huduma bora ya afya.

Makonda aliyefanikisha ujenzi wa jengo hilo kwa kutafuta wafadhili ameahidi mwaka huu ataanza ujenzi wa wodi za wagonjwa na hasa akina mama.

Akizungumzia jengo hilo jipya, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk Festo Bugange amesema kukamilika kwake kutapunguza msongamano wa akina mama waliokuwa wakisubiri kwa muda mrefu kufanyiwa upasuaji.
Dk Bugange amesema jengo hilo lina vyumba viwili vya upasuaji tofauti na kimoja kilichokuwepo awali. Amesema sasa watahudumia wagonjwa wengi zaidi na kwa muda mfupi.

Amesema Hospitali ya Mwananyamala inahudumia wagonjwa kati ya 1,800 na 2,000 kwa siku. Pia, inahudumia wajawazito kati ya 1,500 na 2,000 kwa mwezi.

"Asilimia 25 ya wajawazito wanaokuja Mwananyamala wanahitaji kufanyiwa upasuaji, kwa hiyo walikuwa wanasubiri kwa muda mrefu lakini sasa tuna vyumba vya upasuaji vitatu," amesema Dk Bugange.

Lava Lava – Kilio (Behind The Scene)

Lava Lava – Kilio (Behind The Scene)

Lava Lava – Kilio (Behind The Scene)