Friday, 19 January 2018

Ndege yatetemeka angani

Ndege moja ya Malaysia ililazimika kutua katika eneo la Australia ya kati baada ya tatizo la kiufundi kuifanya kuanza kutetemeka ikiwa angani, wamesema abiria.

Ndege hiyo aina ya MH122 ilikuwa inasafiri kuelekea Kuala Lumpur kutoka Sidney siku ya Alhamisi wakati iliporudi katika eneo ambalo haliko mbali na Broome, kaskazini Magharibi mwa Australia.

Ndege hiyo iliokuwa ikiwabeba watu 224 ilitua salama katika uwanja wa ndege wa Alice Springs Airport.

Abiria wanasema kuwa ndege hiyo ilikuwa ikitetemeka na kutoa sauti kubwa.

Katika taarifa yake, kampuni ya ndege ya Malaysia Airline ilisema kuwa ndege hiyo ilibadilsha safari kutokana na tatizo la kiufundi.

Hatahivyo haikusema ni matataizo gani. Abiria Sanjeev Pandev alisema kuwa ndege hiyo ilionekana kuwa na tatizo hilo saa nne kabla ya safari kuanza.

''Ilikuwa ikitetemeka na kelele zilikuwa kubwa '', aliambia BBC.

''Watu walikuwa wakiomba na wengine walikuwa wakitokwa na machozi'', aliambia BBC.

Alisema kuwa abiria walionyeshwa njia za kubaliana na dharura na wafanyikazi wengi wao wakionekana kuogopa na kushtuka.

Simba kukutana na waliokwamisha mipango

Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC leo alfajiri wameondoka kwa ndege kuelekea mjini Bukoba mkoani Kagera kwaajili ya mchezo wao wa raundi ya 14.

Simba ambayo jana ilishinda mchezo wake wa raundi ya 13 kwa mabao 4-0 dhidi ya Singida United kwenye uwanja wa Uhuru, inakwenda kukutana na Kagera Sugar ambayo ilikwamisha mipango yake ya ubingwa msimu uliopita.

Kagera Sugar ilitibua mipango hiyo April 2 mwaka jana baada ya kuifunga Simba mabao 2-1 kwenye mechi iliyopigwa uwanja wa Kaitaba hivyo kuinyima nafasi ya kurejea kileleni ikibaki na alama 55 katika nafasi ya pili na kuwaacha Yanga wakiwa na alama 56 kileleni.

Endapo Simba ingeshinda mchezo huo ingefikisha alama 58 hivyo huenda ingetwaa ubingwa kutokana na bingwa wa msimu uliopita kupatikana kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, baada ya timu hizo mbili za Kariakoo kufungana pointi.

Simba ambayo kwasasa inaongoza ligi kwa alama 29 mbele ya Azam FC yenye alama 27, itashuka dimbani Kaitaba siku ya Jumapili.


Thursday, 18 January 2018

Audio | Jacko Beatz Ft Moni Centrozone – Baby | Mp3 Download

Audio | Jacko Beatz Ft Moni Centrozone – Baby | Mp3 Download
Audio | Jacko Beatz Ft Moni Centrozone – Baby | Mp3 Download

Batuli awataka mastaa kumrudia Mungu


Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.

MSANII mwenye mvuto Bongo Muvi, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amewasihi wasanii wenzake wajaribu kumrudia Mungu japo mara moja kwa wiki.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Batuli alisema kuwa anatambua mastaa wengi wamesahau kusali kabisa na kujua kama kuna Mungu huku wakiendelea kufanya vingi vya kidunia.

“Jamani hakuna kitu kizuri kama kuona staa akiwa kanisani au msikitini yaani hata jamii inakuchukulia kwa mtazamo wa tofauti kabisa, tumrudie Mungu,” alisema Batuli.


Picha ya Selfie kwenye Facebook yasababisha muuaji kupatikana Canada


Mkanda unaovaliwa na Cheyenne Antoine (kushoto) unaonekana kwenye picha na rafiki yake Brittney Gargol

Mwanamme mmoja nchini Canada amepatikana na hatia ya kumuua rafiki yake baada ya polisi kugundua kuwa kifaa kilichotumiwa kuua kilichokuwa kwenye picha ya kujipiga (selfie) ya wawili hao iliyokuwa katika mtandao ya kijamiii.

Cheyenne Rose Antoine, 21, alikiri siku ya Jumatatu kumuua Brittney Gargol, 18, Machi mwaka 2015.

Gargol alipatikana amenyongwa karibu na Saskatoon, Saskatchewan, huku mkanda wa Antoine ukiwa kando na mwili wake.

Antoine alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa mauaji

Alitajwa kama mshukiwa baada ya kuchapisha picha ya selfie kwenye mtandao wa Facebook, ikionyesha amevaa mkanda uliotumika saa kadhaa kabla ya Gargol kuuliwa.

Alisema walikuwa wamekunywa pombe na pia wakavuta bangi kabla kuanza kuzozana.

Polisi wanasema kuwa taarifa ambayo alikuwa amewapa, kuwa Gargol aliondoka na mwanamume mmoja huku naye akionda kumuona shangazi yake.

Ndipo wakatumia picha zake za Facebook kufuatilia mienendo ya wawili hao usiku huo.



Hii ndio Treni inayobweka kama mbwa ili kuwafukuza swara kwenye reli



Watafiti nchini Japana wameiwekea treni kipasa sauti ambacho kinabweka kama mbwa na kutoa mlio wa swara ili kuzuia treni kugonga swara njiani.

Gazeti la Asahi Shimbun lilisema kuwa sauti hizo zinatumiwa kuwafukuza swara kutoka kwa reli kwa lengo la kupunguza idadi ya wanaogongwa na kuuawa na treni.

Maafisa kutoka kwa taasisi ya reli wanasema kuwa mlio wa sekunde tatu wa swara humfanya swara kuwa makini na kusikiliza, ukifuatiwa na sekunde 20 za mbweko wa mbwa, inaweza kusababisha swara kukimbia.

Watafiti wanasema kuwa majaribio ya usiku wakati swara wanakusanyika kando ya reli yamesababisha swara hao kupungua.

Swara hukaribia reli nyakati za usiku kulamba chuma za reli wakitafuta virutubishi muhimu vya madini ya mwili.

Wizara ya uchukuzi nchini Japan inasema kuwa kulikuwa na visa 613 vya treni kugonga swara na wanyama wengine mwaka 2016.

Abiria wasota Kivukoni


Dar es Salaam. Abiria wanaotumia kivuko eneo la feri wamejikuta wakisota kituoni hapo leo Alhamisi baada ya kivuko kikubwa cha MV Magogoni kupata hitilafu hivyo kubaki vivuko viwili ambavyo vinabeba idadi ndogo ya abiria.

Mwananchi ilifika eneo la kivukoni na kukuta msongamano mkubwa wa abiria wakiwa wanasubiri usafiri huo na wengine wakiamua kuondoka kutokana na kusubiri kwa muda mrefu.

Mmoja wa wasimamizi wa ufundi aliejitambulisha kwa jina moja la Ndunguru amesema tatizo hilo limeanza toka usiku kutokana na MV Magogoni kubeba idadi kubwa ya abiria lazima usumbufu ujitokeze.

“Tatizo limeanza tangu usiku ingawa mimi sio msemaji ila unavyoona mafundi wanaendelea na kazi kuhakikisha tatizo linaisha, kivuko hiki ni kikubwa na kinabeba idadi kubwa ya abiria hivyo kikiaribika lazima usumbufu ujitokeze,” amesema Ndunguru.

Makonda: Dar Kujengwa Kiwanda Kikubwa Zaidi Barani Afrika


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda leo amekutana wawekezaji kutoka China kujadiliana kuhusu mambo ya uwekezaji nchini Tanzania.

Mhe Makonda akizungumza katika mkutano huo Mhe. Makonda amesema kuwa  kutokana na malengo yaliyo wekwa na Wizara ya TAMISEMI maelekezo kutoka kwa Rais John Pombe Magufuli kuwa kila Mkoa uhakikishe unajenga viwanda 100 hivyo wawekezaji hawa wanakwenda kuwekeza Tanga na kunduchi jijini Dar es Salaam na wana wekeza miradi yenye  thamani ya Dola  bilioni 3dola.

Aidha amewataka wanachi wa mkoa huo kuchangamkia fursa za uwekezaji
"sisi kazi yetu  kama serikali ni kuweka mazingira ya uwekezaji na hawandugu zetu wametoka jimbo la  nilizungumza nao nilipotembelea huko kwao mwakajana"Amesema Makonda.

Pamoja na hayo Makonda  amesema kuwa kuna clip ina zungunguka mtandaoni ikieleza kuwa Ethiopia wana kiwanda kikubwa zaidi kuliko nchi zote barani Afrika na kusema kuwa wananchi wasihofu kwani Dar es Salaam itajenga kiwanda kikubwa zaidi ya mara tatu ya hicho chenye  mita za mraba Milion Tano na uwekezaji huu utafanyika wilayani Kigamboni.

"Kuna mwekezaji mwingi ameonyesha nia ya kuwekeza kiwanda cha sukari nawaomba wafanyabiashara wetu mchangamkie fursa hizo za kibiashara   na vijana pia mchangamkie fursa za ajira" Amesema Makonda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa jimbo la Gwangzou , Xie zhenghy kutoka China amesema wao wako tayari kwa uwekezaji na katika nchi ambazo zitaendana kiutamaduni kama ilivyo kwa Tanzania.
Hata hivyo amesema kuwa China imekuwa na nafasi kubwa ya kuwekeza barani Afrika ambapo imekuwa na uwekezaji mkubwa nchini Misri.

Akizungumzia uwekezaji hapanchini amesema kuwa uwekezaji watakaofanya ni ule unaendana na kaulimbiu ya Rais John Pombe Magufuli.

Bunduki ya kivita yenye skafu ya Chadema yakamatwa Shinyanga


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha silaha aina ya AK-47 yenye namba 18116428 na mafuta ya kulainishia silaha yaliyotupwa na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Jielong

 Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata silaha ya kivita aina ya AK-47 iliyotupwa na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa wanataka kuvamia kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong Holdings (Tanzania) Ltd kilichopo Nhelegani katika kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamis Januari 18,2018 Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema walikamata silaha hiyo usiku wa kuamkia leo majira ya saa tano eneo la Tinde wakati majambazi hao wanafuatiliwa na polisi ndipo wakaamua kutupa bunduki hiyo.

“Silaha hii aina ya AK-47 yenye namba 18116428 ilikuwa imefungwa kwenye skafu yenye rangi ya nembo ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiwa na risasi 25 ndani ya magazine yake na risasi zingine 8,zikiwa kwenye mfuko mdogo wa nailoni”,alieleza Kamanda Haule.

“Majambazi wawili pia walitelekeza pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili MC 856 BPF,mafuta ya cherehani ya kulainishia silaha,tochi mbili na koti zito”,aliongeza.

Alisema jeshi la polisi lilipata taarifa za majambazi hao kutaka kuvamia kiwanda hicho kinachomilikiwa na raia wa China tangu tarehe 6.01.2018 kisha kuanza kuwafuatilia na kubaini kuwa baadhi yao ni wakazi wa Kahama na Ushirombo ambapo amewataka kujisalimisha polisi.

Magari zaidi ya 200 yakiwepo ya Watalii yakwama Monduli




Arusha. Magari zaidi 200 yakiwepo ya watalii yaliyokuwa yanaelekea Karatu kwenda Hifadhi ya Ngorongoro na Serengeti yamekwama katika eneo la Makuyuni baada ya daraja kusombwa na maji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi, Kamanda ya Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema jitihada za kutengenezwa njia ya muda zinaendelea.

Amesema daraja hilo limesombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Wilaya ya Monduli.

"Hadi sasa hakuna vifo ambavyo vimetokea ila ni kusombwa kwa daraja ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa," amesema.

Baadhi ya madereva waliokwama Ismail Kessy na John Michael wamesema tangu saa 12 alfajiri wamekwama katika eneo hilo.

"Hii si mara ya kwanza daraja hili kusombwa na mafuriko tunaomba Serikali kuingilia kati kwani tuna watalii ambao walipaswa kuwa Serengeti lakini wamechelewa," amesema.

Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii (TTGA), Khalifa Msangi ameomba daraja hilo kujengwa kwa ubora unaostahili ili kuondoa adha ya kuharibiwa na mafuriko mara kwa mara.

RC Iringa atoa agizo kwa Wakuu wa Shule

Iringa. Siku moja baada ya Rais John Magufuli kupigilia msumari wa mwisho suala la michango kwa wanafunzi mashuleni, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amewataka walimu wakuu wa shule zote mkoani kwake kuandika barua kueleza aina ya michango iliyopo shuleni kwao na sababu za uwepo wake.

Masenza ameonya mwalimu ambaye atatoa taarifa za uongo katika barua yake hatua zitachukuliwa dhidi yake ikiwamo ya kuondolewa katika nafasi yake.

"Kwenye waraka ambao kila mtu anao unazungumzia elimu bila malipo, tayari Serikali ilishaelekeza namna ya kuendesha elimu bila malipo, waraka namba 3 wa 2016 unaozungumzia elimu bila malipo na waraka wa elimu namba 8 wa 2011 kuhusu michango mbalimbali wanayopaswa kutoa wazazi kupitia kamati na bodi za shule," amesema Masenza na kuongeza;

"Mimi ninajua katika kamati na  bodi za shule ninyi ni makatibu, ikifika katika jambo hili, tafadhali kila mwalimu aone hahusiki na jambo lolote linalozungumzia michango katika shule za msingi na sekondari na kama kuna hitaji lolote libainishwe na jamii," amesema.

Amesema shule ni za jamii na jamii ikibainisha yenyewe nje ya utaratibu wa mwalimu mkuu juu ya nini wanataka kufanya na kusimamia wao wenyewe hilo linaruhusiwa.

"Sasa nimewaita ili nijiridhishe, nitamtaka kila mwalimu mkuu wa shule kwa mkono wake mwenyewe aandika barua ya kueleza kama shule yake ina mchango ama la na barua sote ziandikwe kwa mkuu wa mkoa," amesema Masenza.

Masenza amesema barua hizo zitapitiwa na ofisi yake na kisha ukaguzi utafanyika katika kila shule  zikihojiwa kamati na bodi za shule kubaini michango kama ipo sababu za uwepo na namna amehusika kuwepo kwa michango hiyo.

Katika hatua nyingine mkuu huyo amewaagiza wakuu wa shule kuwapokea wanafunzi wote wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza bila kujali wana sare za shule ama la.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amewataka wakuu wa shule zote za binafsi mkoani humo kuwarejesha wanafunzi waliowaondoa shuleni mwao kutokana na kutofikia wastani wa ufaulu wanaoutaka la sivyo shule zao zitafungwa.

Simba SC yamtangaza rasmi Kocha mpya


Pierre Lechantre

Klabu ya Simba leo imemtangaza rasmi Mfaransa Pierre Lechantre, kuwa Kocha mpya atakayekinoa kikosi hicho ambacho kilikuwa hakina mwalimu baada ya kumfukuza aliyekuwa kocha wake, Joseph Omog mwishoni mwa mwaka jana.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Klabu hiyo, Haji Manara imeeleza kuwa kocha huyo ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo na Mfaransa huyo atashuhudia mchezo wa Simba SC dhidi ya Singida United leo Januari 18, 2018 katika Uwanja wa Taifa.

Mfaransa huyo alishawahi kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Cameroun kilichoshinda ubingwa wa Afrika mwaka 2000 na ameshawahi kushinda tuzo ya kocha bora wa bara la Afrika 2001.

Soma zaidi taarifa hiyo kutoka Simba SC;

                                          TAARIFA KWA UMMA

Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya,Mfaransa Pierre Lechantre.

Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo

Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.

Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.

Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi, Na leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa.


VIDEO: Kiwanda Kikubwa Afrika Chatua Kigamboni



Dar es Salaam kujenga kiwanda kikubwa zaidi ya mara tatu ya ya Kiwanda cha Ethiopia chenye  mita za mraba Milion Tano na uwekezaji huu utafanyika wilayani Kigamboni.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KU SUBSCRIBE