Thursday, 18 January 2018

VIDEO: Mwenyekiti Bavicha Amvaa Magufuli


Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Patrick Ole Sosopi amesema kitendo cha Rais John Pombe Magufuli Kumuita Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa Ikulu na Kumshawishi kujiunga na CCM sio kitendo ambacho kinafaa kufumbiwa macho.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE


Mtulia sasa kupambana na meneja wake Kinondoni


Aliyekuwa meneja kampeni wa Maulid Mtulia kwenye uchaguzi wa 2015 Kinondoni, Rajabu Salim Jumaa leo Alhamisi amechukua fomu kugombea ubunge jimbo hilo.

Mwaka 2015 mgombea wa CUF Mtulia alishinda ubunge wa jimbo hilo lakini alijivua uanachama wa CUF na kuhamia CCM na hivyo kupoteza sifa ya ubunge.

Akizungumza leo Alhamisi, Juma amesema atamshinda Mtulia katika nafasi hiyo kwa sababu anaisababishia Serikali hasara.

"Gharama kubwa za uchaguzi zinasababishwa na Mtulia ambaye alishakuwa mbunge lakini amejiuzulu na kutaka tena ubunge.”


Afariki Dunia kwa kugongwa na ndege Mwanza



Mkazi mmoja wa mkoa wa Mwanza amefariki dunia baada ya kuigonga ndege ya Fastjet iliyokuwa ikiruka katika Uwanja wa Ndege Mwanza kuelelea jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari 18, 2018 Kaimu MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela amesema tukio hilo la aina yake limetokea jana usiku.

Amesema ndege hiyo ilikuwa njia moja kuelekea jijini Dar es Salaam, kubainisha kuwa mtu huyo ndiye aliyeigonga ndege hiyo.

“Ingawa ndege ndio ilimgonga mtu huyo ambaye jina lake hatulifahamu, kisheria mtu au kitu chochote kinachokuwa kwenye njia ya kurukia  na kutua ndege ndiyo kinahesabiwa kuigonga ndege. Ni kama ilivyo kwa treni,” amesema Mayongela.

Amesema kabla ya ndege hiyo kuruka,  taratibu zote za kiusalama zilifuatwa ikiwemo kukagua njia kujiridhisha hakuna kitu chochote.

“Haijulikani mtu huyo alitokea wapi. Vyombo vya ulinzi na usalama vipo eneo la tukio kuchunguza tukio hilo kwa kina na tutatoa taarifa kamili uchunguzi utakapokamilika,” amesema kaimu mkurugenzi huyo.

Amesema kitendo cha mtu huyo kuwepo katika njia ya kurukia ndege licha ya ukaguzi kufanyika kinawaumiza vichwa viongozi na wataalam wa usalama uwanjani hapo.

 “Pengine tatizo la muda mrefu la kukosa uzio tunaloanza kukabiliana nalo kwa ujenzi na upanuzi wa uwanja linaweza kuwa chanzo cha mtu huyo kuingia katika njia ya kurukia ndege,” amesema.

Ili kukabiliana na matukio ya aina hiyo, amesema wataimarisha mifumo ya usalama kwenye viwanja vya ndege nchini.

Majaliwa ampa maagizo RC Mghwira kuhusu KNCU



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira asitishe uuzwaji wa mali za Chama cha Ushirika cha Kilimanjaro (KNCU).

Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 17, 2018) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Serengeti, wilayani Tarime.

Hatua hiyo imekuja baada ya KNCU kutangaza kuuza shamba lake kwa ajili ya kuiwezesha benki yake ya KCBL  kutimiza sharti la mtaji la Benku Kuu ya Tanzania (BoT).

Benki hiyo ya KCBL inatakiwa kutimiza sharti la kuwa na mtaji kamili unaotosha wa shilingi bilioni  tano (5) katika kipindi cha miezi sita tangu kutolewa kwa tangazo hilo.

Waziri Mkuu alisema ni marufuku kuuza mali za Ushirika huo, hususan katika kipindi hiki ambacho Serikali inafanya uhakiki wa mali za vyama mbalimbali vya Ushirika nchini.

Alisema Serikali imedhamiria kuimarisha Ushirika nchini na sasa inafanya uhakiki wa mali za vyama vya Ushirika na watakaobainika kuhusika na ubadhilifu watachukuliwa hatua.

Januari 4, 2018 BoT ilizipa miezi sita benki tatu ili ziweze kuongeza kiwango cha mtaji unaohitajika kutokana na matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji kamili wa kutosha.

Benki hizo ni Kilimanjaro Co-Operative Bank Limited, Tanzania Women Banki Plc na Tandahimba Community Bank Limited, zitakaposhindwa kutekeleza agizo zitachukuliwa hatua.

BoT ni itazifutia leseni na kusimamisha shughuli za kibenki chini ya ufilisi, iwapo benki hizo zitashindwa kutekeleza agizo hilo ihadi kufikia Juni 30, 2018.

Walcott atuma ujumbe wa mwisho kwa Arsenal



Inauma ukiondoka sehemu ambayo umeizoea kwa muda mrefu. Theo Walcott ametuma ujumbe kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal baada ya kuhamia Everton.

Mchezaji huyo ambaye amesajiliwa na Everton kwa ada ya uhamisho wa paund milioni 20 na kukabidhiwa jezi namba 11, amedumu Arsenal kwa miaka 12 na ameichezea jumla ya michezo 397 na kushinda magoli 108.

Huu ndio ujumbe ambao Walcott amewatumia mashabiki wa Arsenal:
Ninataka tu kusema shukrani kubwa kwa mashabiki wote wa Arsenal. Nimekuwa nimesumbuliwa na ujumbe ambao nimepata leo kheri na siwezi kukushukuru kwa kutosha, na hasa kwa miaka 12 iliyopita. Nataka tu kuwatakia kila mmoja katika klabu kila la kheri kwa siku zijazo.

Mashindano ya elimu kuanza kutimua vumbi Februari 28



Katika kuonesha kwamba wanaunga mkono suala la elimu bora nchini Taasisi ya Teacher's Junction imeandaa mashindano kwa shule za binafsi nchini ambapo wanafunzi wa darasa la nne, sita la saba watafanya mitihani ya kujipima nguvu lengo likiwa ni kuongeza ufanisi baina ya wanafunzi hao na pia kuwarahisishia walimu kujua wapi wanapaswa kuongeza nguvu.

Mashindano hayo yamepangwa kufanyika kuanzia Februari 28 hadi Machi 1 na kushirikisha takribani shule 120 nchini.

Akizungumza na wandishi wa habari leo, Afisa Mradi wa taasisi hiyo, Njama Salum alisema walianzisha mradi huo ili kuongeza kiwango cha elimu nchini kwa wanafunzi wa shule za msingi lakini pia wakiwa na mpango wa kupeleka mradi huo hadi kwenye shule za Sekondari.

" Kiu ya taasisi yetu ni kuona kiwango cha elimu kinaongezeka nchini, hivyo kwa kushirikiana na wadau wa elimu hasa wamiliki wa shule tukaja na wazo hili la kufanya mashindano ambayo tunaamini yanawajenga wanafunzi kuanzia kiakili hadi kujiamini pale wanapofanya mitihani ya Kitaifa.

" Kikubwa tunatoa zawadi za medali kwa wanafunzi wanaofanya vizuri lakini shule ambazo zitafanya vizuri tunatoa zawadi za ngao. Na mitihani hii hufanyika mara tatu kwa mwaka ambapo kwa kuanzia tunaanza mwezi Machi kisha tutafanya mwingine Mei halafu Agosti tutafanya mwingine," alisema Njama.

Alisema tayari washapata zawadi lakini bado anatoa fursa kwa wadau wengine wa elimu kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono ili kuweza kuzalisha kizazi bora cha vijana wenye elimu ambao watakuja kuwa msaada mkubwa kwa Taifa hapo baadaye.

Akizungumzia sababu za kutohusisha Shule za Serikali, Njama alisema sio kwamba wamezitenga shule hizo lakini wao kama taasisi waliangalia ni wapi wanaweza kupenyeza wazo lao kwa haraka zaidi na kwamba taratibu za kuonana na viongozi wa kiserikali ili kuangalia uwezekano wa kupeleka mradi huo kwenye shule hizo unafanikiwa kusudi kila mwanafunzi nchini aweze kunufaika nao.

Kwa upande mwingine Njama alisema taasisi yake pia imekuwa ikisaidia walimu ambao wapo mitaani bila ajira kwa kuwatafutia kazi kwenye shule za binafsi ambazo wana ushirika nazo lengo likiwa ni kumaliza tatizo la ajira nchini.

" Sisi pia tunasaidia vijana wenzetu ambao wana taaluma ya ualimu ambao wapo mitaani ambapo kwa mwaka uliopita zaidi ya vijana 356 ambao wana taaluma ya ualimu tuliwatafutia kazi katika shule mbalimbali nchini," alisema Njama.

Mwanamke mjamzito atolewa kopo la mafuta sehemu za siri



Veronica Paschal (29) mkazi wa Kishili jijini Mwanza ametolewa kopo la mafuta ya kujipaka mwilini katika sehemu za siri, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuwaeleza ndugu zake kuwa anataka kujifungua kopo.

Licha ya kutolewa kopo hilo, daktari aliyekuwa zamu katika kituo cha afya Igoma jijini hapa, Zaitun Lionge amelieleza Mwananchi leo Januari 18, 2018 kuwa mimba ya miezi sita ya mwanamke huyo ipo salama.

Tukio hilo la aina yake limetokea jana Januari 17, 2018 baada ya Veronica kufikishwa katika kituo hicho cha afya na ndugu zake waliomtoa kwenye zahanati binafsi.

“Mwanzoni hawakuonyesha ushirikiano ndio tukawambia tutafanyaje. Wakasema kuna kopo kwamba ndugu yao anataka kujifungua kopo, tukauliza kopo linazaliwaje? Amehoji na kuongeza,

“Tukawambia hilo kopo halijaingia lenyewe mtakuwa mmeliweka wenyewe. Kopo lilikuwa halionekani lakini anavyojaribu kusukuma likatokezea.”

Amesema walipomchunguza kwenye vipimo ndipo walipolibaini kopo hilo la mafuta ya kujipaka mwilini, kwamba baada ya kulitoa waliita Polisi kuchukua maelezo ya mhusika na ndugu zake.

Amesema ujauzito wa mwanamke huyo uko salama kutokana na njia kutofunguka baada ya kuondolewa kopo hilo.

Bunge lahoji mkataba wa UDSM na Kampuni ya Mlimani Holding



Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeutaka uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kurekebisha mkataba kati yake na kampuni ya Mlimani Holding Ltd kutokana na upungufu uliojitokeza, huku ikihoji sababu ya mwekezaji huyo kuja na mtaji wa Sh150,000 tu.

Wakizungumza katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi eneo la Mlimani City jijinj Dar es Salaam leo Januari 18 wajumbe wa PAC walikosoa pia gawio la asilimia 10 la mapato yote kwa mwaka ambapo Mlimani  City wamekuwa wakikata gharama zao kabla ya kulipa.

Jambo la tatu lililolalamikiwa ni umri wa mkataba ambapo UDSM imetaka upunguzwe kutoka miaka 50 hadi miaka 35.

Mbunge wa Magomeni (CCM) Zanzibar, Jamal Kassim amehoji sababu za chuo hicho kumpokea mwekezaji akiwa na mtaji wa Sh150,000.

"Ukisoma mkataba huu utaona mtaji wa mwekezaji ni Sh150,000 yaani Dola 75. Maana yake mwekezaji hakuja na pesa bali alichukua pesa za upangishaji na kuzifanya kuwa mkopo na anajilipa riba ya mabilioni ya fedha," amesema Kassim.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka amehoji: "Je, Chuo kikuu cha Dar es Salaam kilimkubalije mwekezaji mwenye mtaji wa Dola 75 tu? Dhamana ilikuwa nini?"

Hoja hiyo ilimwibua Mbunge wa CCM (Vijana)  , Khadija Naasir akihoji sababu ya mwekezaji huyo kutuma barua pepe kila anapotakiwa kutoa maelezo na UDSM.

Mbunge wa Ulanga Magharibi Dk Haji Mponda amesema mkataba huo ni mbovu kwa sababu umeshindwa kuna ardhi iliyopangishwa bila kutumika kwa muda mrefu.

Baada ya hoja za wabunge hao, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Hilal Aeshi ameitaka kamati kuwaita watumishi wa UDSM walioshiriki kusaini mkataba huo ili wahojiwe na kuchukulia hatua.

"Kwa kuwa waliotia saini mkataba huo wapo, tuwaite Dodoma, wajieleze ili wachukuliwe hatua na Rais. Mimi nilikuwa mjumbe wa kamati ya madini ya Spika, tuliwaita waliohusika wakajieleza," amesema Aeshi.

Hata hivyo baadhi ya wabunge walitaka viongozi wa sasa wa UDSM  wajieleze kabla ya kuwaita wa zamani.

Tofauti na mtazamo wa wabunge hao, Naibu Makamu mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia utawala, Profesa David Mfinanga amekiri kuwa mkataba huo una mapungufu na kwamba wana mgogoro na Mlimani Holding.

Mwanasheria wa Chuo hicho, Profesa Bonaventure Rutinwa amesema tangu alipoteuliwa alianza kuupitia mkataba huo.

"Tangu nilipoteuliwa mwaka jana nilifika ofisini kwa Profesa Rwekaza Mukandala nikamuomba vipaumbele vitano vya kisheria, mojawapo akaniambia ni kuupitia mkataba wa Mlimani," amesema Profesa Rutinwa.

Akifafanua zaidi, Kaimu Katibu wa Baraza la Chuo hicho, Dr Saudin Mwakaje alikiri kuwepo tatizo la mtaji na kwamba walishaiambia kamati hiyo.

Awali Mkurugenzi wa mipango na maendeleo wa chuo hicho, Pancras Pujuru amesema Mlimani Holding iliingia mkataba huo mwaka 2004 ukiwa katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ulihusu kati yake na UDSM na sehemu ya pili ilikuwa kati yake na Serikali kupitia kituo cha

Mkali wa tennis Uingereza atupwa nje ya michuano



Mchezaji tennis namba moja kwa viwango vya ubora nchini Uingereza mwanadada, Johanna Konta ameondolewa kwenyemichuano ya Australia Open baada ya kufungwa na mchezaji anaeshikilia nafasi 123 duniani, Bernarda Pera.

Mmarekani, Bernarda Pera amemshinda Konta kwa jumla ya seti 6-4 7-5 katika kipindi cha pili cha mchezo.

Mara baada ya kutolewa katika mashindano hayo Konta amesema “Ni jambo la kusisimua lakini tunaendelea vizuri na benchi langu la ufundi, siji sikii vizuri lakini kwa namna yoyote lazima nikubali matokeo,”Konta.

Konta ameongeza “Nimecheza kila namna mpaka kufikia pale kwa hakika sikuhitaji rejea nyumbani mapema.”

Video | Korede Bello – Melanin Popping | Mp4 Download

Video | Korede Bello – Melanin Popping | Mp4 Download
Video | Korede Bello – Melanin Popping | Mp4 Download



Audio | Korede Bello – Melanin Popping | Mp3 Download

Audio | Korede Bello – Melanin Popping | Mp3 Download
Audio | Korede Bello – Melanin Popping | Mp3 Download


Audio | Belrino Ft Nana – Si Umesema | Mp3 Download

Audio | Belrino Ft Nana – Si Umesema | Mp3 Download

Audio | Belrino Ft Nana – Si Umesema | Mp3 Download

DOWNLOAD

Waziri Mkuu amewaasa Wanaume wa Wilaya ya Tarime


Tarime.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaasa wanaume wa wilaya ya Tarime kujiepusha na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kuachana na kilimo cha bangi.

Ametoa  kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Januari 17, 2018) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Serengeti, wilayani Tarime.

Waziri Mkuu amesema  vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kilimo cha bangi vinaitia doa wilaya hiyo, hivyo hawana budi wakaepukana navyo.

“Serikali inakemea vitendo vya ukatili, achaneni navyo. Mtu unamchapa mtoto makofi hadi anazimia, kitendo hicho hakiwezi kuvumilika na pia kinaitia doa wilaya yenu.”

Wakati Huohuo, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa wilaya hiyo, Glorious Luoga kuendelea na msako wa mashamba ya bangi na mirungi na kuchukua hatua kwa watakaobainika kuendesha kilimo hicho.

Amesema ardhi ya wilaya hiyo ni nzuri na inahimili kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara kama mahindi, mihogo, ndizi, kahawa, pamba, ni marufuku kulima bangi.

Pia Waziri Mkuu ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wakandarasi waliotekeleza ujenzi wa maji mkoani Mara kwa sababu miradi hiyo wameijenga chini ya kiwango.

Waziri Mkuu amesema hayo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kupitia mabango wakidai kutonufaika na miradi ya maji katika maeneo yao licha ya Serikali kutoa fedha.