Thursday, 18 January 2018

Bunge lahoji mkataba wa UDSM na Kampuni ya Mlimani Holding



Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeutaka uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kurekebisha mkataba kati yake na kampuni ya Mlimani Holding Ltd kutokana na upungufu uliojitokeza, huku ikihoji sababu ya mwekezaji huyo kuja na mtaji wa Sh150,000 tu.

Wakizungumza katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi eneo la Mlimani City jijinj Dar es Salaam leo Januari 18 wajumbe wa PAC walikosoa pia gawio la asilimia 10 la mapato yote kwa mwaka ambapo Mlimani  City wamekuwa wakikata gharama zao kabla ya kulipa.

Jambo la tatu lililolalamikiwa ni umri wa mkataba ambapo UDSM imetaka upunguzwe kutoka miaka 50 hadi miaka 35.

Mbunge wa Magomeni (CCM) Zanzibar, Jamal Kassim amehoji sababu za chuo hicho kumpokea mwekezaji akiwa na mtaji wa Sh150,000.

"Ukisoma mkataba huu utaona mtaji wa mwekezaji ni Sh150,000 yaani Dola 75. Maana yake mwekezaji hakuja na pesa bali alichukua pesa za upangishaji na kuzifanya kuwa mkopo na anajilipa riba ya mabilioni ya fedha," amesema Kassim.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka amehoji: "Je, Chuo kikuu cha Dar es Salaam kilimkubalije mwekezaji mwenye mtaji wa Dola 75 tu? Dhamana ilikuwa nini?"

Hoja hiyo ilimwibua Mbunge wa CCM (Vijana)  , Khadija Naasir akihoji sababu ya mwekezaji huyo kutuma barua pepe kila anapotakiwa kutoa maelezo na UDSM.

Mbunge wa Ulanga Magharibi Dk Haji Mponda amesema mkataba huo ni mbovu kwa sababu umeshindwa kuna ardhi iliyopangishwa bila kutumika kwa muda mrefu.

Baada ya hoja za wabunge hao, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Hilal Aeshi ameitaka kamati kuwaita watumishi wa UDSM walioshiriki kusaini mkataba huo ili wahojiwe na kuchukulia hatua.

"Kwa kuwa waliotia saini mkataba huo wapo, tuwaite Dodoma, wajieleze ili wachukuliwe hatua na Rais. Mimi nilikuwa mjumbe wa kamati ya madini ya Spika, tuliwaita waliohusika wakajieleza," amesema Aeshi.

Hata hivyo baadhi ya wabunge walitaka viongozi wa sasa wa UDSM  wajieleze kabla ya kuwaita wa zamani.

Tofauti na mtazamo wa wabunge hao, Naibu Makamu mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia utawala, Profesa David Mfinanga amekiri kuwa mkataba huo una mapungufu na kwamba wana mgogoro na Mlimani Holding.

Mwanasheria wa Chuo hicho, Profesa Bonaventure Rutinwa amesema tangu alipoteuliwa alianza kuupitia mkataba huo.

"Tangu nilipoteuliwa mwaka jana nilifika ofisini kwa Profesa Rwekaza Mukandala nikamuomba vipaumbele vitano vya kisheria, mojawapo akaniambia ni kuupitia mkataba wa Mlimani," amesema Profesa Rutinwa.

Akifafanua zaidi, Kaimu Katibu wa Baraza la Chuo hicho, Dr Saudin Mwakaje alikiri kuwepo tatizo la mtaji na kwamba walishaiambia kamati hiyo.

Awali Mkurugenzi wa mipango na maendeleo wa chuo hicho, Pancras Pujuru amesema Mlimani Holding iliingia mkataba huo mwaka 2004 ukiwa katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ulihusu kati yake na UDSM na sehemu ya pili ilikuwa kati yake na Serikali kupitia kituo cha

Mkali wa tennis Uingereza atupwa nje ya michuano



Mchezaji tennis namba moja kwa viwango vya ubora nchini Uingereza mwanadada, Johanna Konta ameondolewa kwenyemichuano ya Australia Open baada ya kufungwa na mchezaji anaeshikilia nafasi 123 duniani, Bernarda Pera.

Mmarekani, Bernarda Pera amemshinda Konta kwa jumla ya seti 6-4 7-5 katika kipindi cha pili cha mchezo.

Mara baada ya kutolewa katika mashindano hayo Konta amesema “Ni jambo la kusisimua lakini tunaendelea vizuri na benchi langu la ufundi, siji sikii vizuri lakini kwa namna yoyote lazima nikubali matokeo,”Konta.

Konta ameongeza “Nimecheza kila namna mpaka kufikia pale kwa hakika sikuhitaji rejea nyumbani mapema.”

Video | Korede Bello – Melanin Popping | Mp4 Download

Video | Korede Bello – Melanin Popping | Mp4 Download
Video | Korede Bello – Melanin Popping | Mp4 Download



Audio | Korede Bello – Melanin Popping | Mp3 Download

Audio | Korede Bello – Melanin Popping | Mp3 Download
Audio | Korede Bello – Melanin Popping | Mp3 Download


Audio | Belrino Ft Nana – Si Umesema | Mp3 Download

Audio | Belrino Ft Nana – Si Umesema | Mp3 Download

Audio | Belrino Ft Nana – Si Umesema | Mp3 Download

DOWNLOAD

Waziri Mkuu amewaasa Wanaume wa Wilaya ya Tarime


Tarime.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaasa wanaume wa wilaya ya Tarime kujiepusha na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kuachana na kilimo cha bangi.

Ametoa  kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Januari 17, 2018) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Serengeti, wilayani Tarime.

Waziri Mkuu amesema  vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kilimo cha bangi vinaitia doa wilaya hiyo, hivyo hawana budi wakaepukana navyo.

“Serikali inakemea vitendo vya ukatili, achaneni navyo. Mtu unamchapa mtoto makofi hadi anazimia, kitendo hicho hakiwezi kuvumilika na pia kinaitia doa wilaya yenu.”

Wakati Huohuo, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa wilaya hiyo, Glorious Luoga kuendelea na msako wa mashamba ya bangi na mirungi na kuchukua hatua kwa watakaobainika kuendesha kilimo hicho.

Amesema ardhi ya wilaya hiyo ni nzuri na inahimili kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara kama mahindi, mihogo, ndizi, kahawa, pamba, ni marufuku kulima bangi.

Pia Waziri Mkuu ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wakandarasi waliotekeleza ujenzi wa maji mkoani Mara kwa sababu miradi hiyo wameijenga chini ya kiwango.

Waziri Mkuu amesema hayo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kupitia mabango wakidai kutonufaika na miradi ya maji katika maeneo yao licha ya Serikali kutoa fedha.



Mambosasa akanusha Polisi kuzuia Wanawake kuvaa nguo fupi




Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,  Lazaro Mambosasa amekanusha kutoa tamko la kuzuia wanawake kuvaa nguo fupi zisizo na heshima kwa maelezo kuwa  jambo hilo ni la kimaadili siyo sheria.

Amesema Jeshi la Polisi lina kazi ya kushughulikia makosa ya kisheria na si maadili.

Mambosasa ametoa kauli hiyo leo Januari 18, 2018 wakati akihojiwa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Redio Clouds, ikiwa ni siku mbili baada ya kunukuriwa katika mkutano wake na wanahabari kuwa amezuia uvaaji wa nguo fupi jijini Dar es Salaam.

 “Niliwaeleza wazi kuwa suala la mavazi bado halijatungiwa sheria hivyo polisi hatuhusiki nalo mtu anayevaa kimini katika maeneo kama kanisani au msikitini  ni ukiukwaji wa maadili,” amesema na kuongeza,

“Niliwaeleza  kuwa katika nyumba hizo za ibada kuna kamati ya ulinzi na usalama za eneo husika wao watakushughulikia lakini si polisi.”

Amesisitiza, “Nilikwenda mbali zaidi na kuwaeleza kuwa hivyo vimini kuna mahali vinahitajika kama ufukweni, sehemu za starehe. Ikitokea mtu amepigwa, amedhalilishwa au amekamatwa na askari kwa kuwa amevaa kimini ana haki ya kulalamika kuwa ameshambuliwa.”

NHIF yakanusha taarifa hii

Waziri Mkuu atoa agizo kwa Mghwira kusitisha uuzwaji wa mali za KNCU



Tarime. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Anna Mghwira asitishe uuzwaji wa mali za Chama cha Ushirika cha Kilimanjaro (KNCU).

Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 17, 2018) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Serengeti, wilayani Tarime.

Hatua hiyo imekuja baada ya KNCU kutangaza kuuza shamba lake kwa ajili ya kuiwezesha benki yake ya KCBL  kutimiza sharti la mtaji la Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Benki hiyo ya KCBL inatakiwa kutimiza sharti la kuwa na mtaji kamili unaotosha wa shilingi bilioni  tano (5) katika kipindi cha miezi sita tangu kutolewa kwa tangazo hilo.

Waziri Mkuu amesema  ni marufuku kuuza mali za Ushirika huo, hususan katika kipindi hiki ambacho Serikali inafanya uhakiki wa mali za vyama mbalimbali vya Ushirika nchini.

Amesema Serikali imedhamiria kuimarisha Ushirika nchini na sasa inafanya uhakiki wa mali za vyama vya Ushirika na watakaobainika kuhusika na ubadhilifu watachukuliwa hatua.

Januari 4, 2018 BoT ilizipa miezi sita benki tatu ili ziweze kuongeza kiwango cha mtaji unaohitajika kutokana na matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji kamili wa kutosha.

Benki hizo ni Kilimanjaro Co-Operative Bank Limited, Tanzania Women Banki Plc na Tandahimba Community Bank Limited, zitakaposhindwa kutekeleza agizo zitachukuliwa hatua.

BoT ni itazifutia leseni na kusimamisha shughuli za kibenki chini ya ufilisi, iwapo benki hizo zitashindwa kutekeleza agizo hilo hadi kufikia Juni 30, 2018.


Katibu UVCCM Iringa afunguka alivyonusurika kufa


KATIBU wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM), Alophance Myunga amenusurika kifo baada ya kitu chenye mlipuko kurushwa dirishani kwake na kufikia kitandani huku yeye akiwa amelala na kisha kusababisha moto ulioteketeza nyumba anayoishi yote.

Amesema kutokana na kurushwa kwa kitu hicho ambacho kilisababisha mlipuko mkubwa chumbani kwake na kisha moto kuanza kuwaka alichofanikiwa ni kuchukua simu yake ya mkononi tu huku vitu vingine vyote vikiteketea kwa moto.

 Myunga amesema yeye ni moja kati ya wapangaji saba wanaoishi kwenye nyumba ambayo wanaishi na chumba ambacho kilianza kuwaka moto ni cha kwake.

Katibu huyo wa UVCCM Wilaya ya Iringa amesema kuwa kwenye mida ya saa saba usiku akiwa amelala chumbani kwake alisikia dirisha lililopo chumbani kwake likivunjwa.Hata hivyo aliogopa kuchungulia kwani hakujua wanaofanya hivyo wanalengo gani dhidi yake.

Ameongeza wakati anaendelea kutafakari huku akiwa bado yupo kwenye kitanda chake alishangaa kuona amerushiwa kitu ambacho hawezi kukielezea ni cha aina gani lakini ghafla kikaangukia chini na kusababisha kulipuka na moto kuanza kuwaka.

“Naogopa kusema ni kitu aina ya bomu au laa.Maana si mtaalamu wa kutambua aina ya kitu ambacho kimerushwa chumbani.Niseme tu baada ya kitu hicho kurushwa kitandani na kudondokea chini, moto ukaanza kufuka na kisha kulipuka.Nilichofanikiwa ni kuchukua simu na Kompyuta mpakato na kisha kukimbilia nje.

“Nilipotoka nje na wapangaji wenzangu nao wakatoka na kuanza kuulizana nani amefanya tukio hilo.Tayari tumetoa taarifa Polisi jana(juzi) usiku baada ya nyumba kuungua na hivyo tunasubiri watakachobaini kilichosababisha nyumba kuchomwa na waliohusika kufanya tukio hilo,”amesema.

Alipoulizwa anahisi nini baada ya tukio hilo, Myunga alijibu kuwa anachoamini sababu kubwa itakuwa ni mambo ya siasa kwani yeye si mfanyabashara na hana kazi nyingine zaidi ya siasa na siku za karibuni kuna moja ya kiongozi wa kisiasa wa upande wa upinzani alimtishia kwa bastola.

“Mbali ya kunitisha kwa bastola aliniambia kuwa nitakiona na lazima atanihamisha Iringa kwani najifanya mjanja kwa kuwa nimetoka Dar es salaam.Huyu kiongozi(jina tunalo) ndio atakuwa adui yangu namba moja na ndio namhisi atakuwa kafanya tukio hilo.

“Inaonesha kabisa walikuwa wamedhamiria kuniuua mimi na ndio maana walivunja dirisha la chumbani kwangu na kurusha kitu hicho ambacho kilisaabisha mlipuko uliofanya moto kuanza kuwaka.Hata hivyo acha Jeshi la Polisi Iringa nalo lifanye kazi yake ya kuchunguza na ukweli utapatikana,”amesema.


Fid Q atoa somo kwa Wasanii



Mkali wa muziki wa hip hop Bongo, Fid Q ametoa somo kwa wasanii namna ya kujiweka mbali na msongo wa mawazo (stress) kutokana na kuyumba kwa uchumi.

Rapper huyo ameiambia Dj Show ya Radio One kuwa wasanii wanatakiwa kuwa wabunifu katika kazi zao na kuwa na njia tofauti tofauti za kuwaingizia kupato.

“Katika suala la ubunifu inakupa nafasi kubwa sana kwa sababu unakuwa na akili iliyotulia ambayo haipelekwi pelekwi na stress ndogo ndogo kama za kukosa show za hapa na pale, ni kitu poa na kinapaswa kufuatwa na kila msanii,” amesema Fid Q.

“Pia kuhakikisha anakuwa na njia zaidi ya moja ya kujiingizia kipato yaani mbali na muziki awe na vitu vingine ambayo vitamsaidia kujiingizia kipato,” amesisitiza Fid Q.

Fid Q kwa sasa anafanya vizuri na remix ya ngoma Fresh aliyowashirikisha Diamond na Rayvanny.


Davido kuwaanika anaowadai



Unaweza ukasema ugumu wa mwezi Januari kwa upande wa uchumi ni kwa watu wakawaida lakini kumbe haipo hivyo hili ni janga hata kwa watu maarufu, Hii ni baada ya msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido kutangaza kuwa ataweka hadharani majina ya watu wote anaowadai kama hawatarudisha fedha zake kuanzia leo.

Davido kupitia ukurasa wake wa Snapchat amesema ametoa siku ya leo Jumatano kwa watu wote anaowadai ambao wapo jijini Lagos kutii amri hiyo la sivyo atatangaza majina hayo bila kuogopa ukubwa wa majina yao.

“Kupitia posti hiyo Davido amesema “Nitaweka orodha ya majina ya watu wote ninao wadai hapa Lagos, Watu wengi nimewakopesha pesa lakini hawataki kunilipa mimi sio serikali, Kama hutanilipa leo jina lako nitaliweka hadharani,” ameandika Davido.

Hata hivyo, watu wengi wanasema huenda hasira hizo zimekuja kutokana na Mamlaka ya mapato jijini Lagos kumtaka Davido atoe risiti za malipo ya kodi aliyolipa kwenye tamasha lake la 30 Bilioni Concert.


Pluijm awafungukia Simba




KUELEKEA mchezo wa Alhamis hii dhidi ya vinara Simba, kocha mkuu wa timu ya Singida United, Hans van der Pluijm amesema anawachukulia mabingwa hao wa zamani kama washindani wake wengine katika ligi na atakiingiza kikosi chake katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa ‘tahadhari’ kubwa licha ya ukweli haihofii timu hiyo iliyofunga magoli 12 katika michezo 12 iliyopita.

“Naichukulia Simba kama timu nyingine. Siwezi kuweka akili yangu yote kwao.” Anasema Hans nilipofanya naye mahojiano Jumanne hii. Inatakiwa tuwe makini na tucheze mchezo wetu kwa kujitambua na kuimarisha morali ya timu nzima. Inatakiwa tufanye kazi yetu vizuri katika kila nafasi na katika uchezaji wa mpira pia.”

Singida wamepanda daraja msimu huu lakini namna timu hiyo inavyoendeshwa imesaidia kwa  kiasi kikubwa kusajili wachezaji mahiri kutoka ndani na ng’ambo, ikiwemo kumtwaa kocha Hans ambaye aliipa Yanga mataji mawili mfululizo ya ligi kuu.

Mudathir Yahya, Ken Ally, Deus Kaseke, Kiggy Makassy, Daniel Lyanga, golikipa Peter Manyika ni baadhi ya nyota wazawa ambao wamesajiliwa na klabu msimu huu. Mzimbabwe, Tafadzwa Kutinyu, Mganda, Shafiq Batambuze,  Wanyarwanda, Michael Rusheshangoga, Danny Usengimana wamefanya kikosi hicho kuwa imara na ushindi wowote utawafanya kuwa pointi sawa na Simba.

Hans ni kocha mwenye uzoefu mkubwa sasa hadi katika soka la Tanzania. Amewahi kuishinda Simba katika michezo yote miwili ya ligi kuu msimu wa 2015/16 ameendeleza aina ya soka lake la kushambulia katika kikosi cha Singida. Atawavaa Simba kwa mara ya kwanza akiwa nje ya kikosi cha Yanga huku akiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo mmoja tu vs Simba.

“Mpira hautabiriki. Kila kitu kinawezekana, Simba bado ni timu kubwa na nawaheshimu lakini siwaogopi. Tunajiandaa vizuri na timu ipo katika morali, natumaini tunaweza kuwashangaza siku ya mchezo. Hii mechi wachezaji wanatakiwa wawe makini wao wenyewe ili tupate matokeo mazuri. Ni mechi yetu muhimu.” Anasema Hans ambaye atamkosa mfungaji wake namba moja Usengimana.

Singida wamekusanya alama 23 katika michezo 12 iliyopita. Wakiwa nafasi ya nne ya msimamo pointi  tatu nyuma ya Simba, timu hiyo kutoka mkoani Singida imeonyesha mwanga kuwa huenda wakawa washindani wa kweli katika mbio za ubingwa msimu huu kutokana na uimara wa timu yao.

“Njia bado ngumu, chochote kinaweza kutokea muda wowote. Tunaichukulia ligi ‘mchezo kwa mchezo’ mwishoni tutajua tulipofika. Inatakiwa tufanye kazi yetu vizuri.” Anamaliza kusema Hans.