Wednesday, 13 December 2017

TBC1: Waliosamehewa na JPM, Sasa Wamuomba Mtaji!

TBC1: Waliosamehewa na JPM, Sasa Wamuomba Mtaji!

Mazoezi ya Yanga Yashusha Majembe Mawili ya Kimataifa


Mazoezi ya Yanga Yashusha Majembe Mawili ya Kimataifa


Afanya sherehe ya kuagwa kabla hajafariki


Satoru Anzaki akiwa kwenye karamu hiyo

Mfanyabiashara mmoja nchini Japan ambaye anaugua saratani na anatarajiwa kufariki karibuni aliwashangaza watu baada ya kuandaa karamu kubwa ya kuaga.

Satoru Anzaki aliwaalika wageni karibu 1,000 wakiwemo marafiki zake, watu waliosoma naye, washirika wake wa kibiashara na wafanyakazi wake.

Satoru, 80, ambaye ni mkuu wa zamani wa kampuni ya kuunda mashine ya Komatsu alipatikana na saratani ya kibofu cha nyongo Oktoba.

"Nimeridhika kwamba niliweza ksuema 'asante' kwa watu niliokutana nao maishani," aliwaambia wanahabari baada ya sherehe hiyo.

"Kwa kuwa nilitaka kufurahia kabisa sehemu ndogo ya maisha niliyobaki nayo, nimeamua nisipokee matibabu baada ya kuzingatia madhara ya tiba," alisema.

Alitangaza mpango wake wa kufanya sherehe hiyo kupitia tangazo gazetini, taarifa ambazo zilisambazwa sana mtandaoni watu wakitaniana kuhusu ingelikuwa wao wangewaalika nani.

Satoru alikodisha chumba katika hoteli moja Tokyo na akaipamba kwa picha za kumbukumbu ya maisha yake.


Marekani iko tayari kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini


Rex Tillerson

Marekani iko tayari kwa mazungumzo wakati wowote na Korea Kaskazini bila ya masharti yoyote, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson amesema.

Taaarifa yake ilionekana kuwa tofauti na msimamo wa awali wa Marekani kuwa Korea Kaskazini ni lazima iharibu zana zake kabala ya mazungummzo yoyote kufanyika

Lakini saa chache baadaye Ikulu wa White House ilisema msimamo wake Trump kwa Korea Kaskazini haujabadilika.

Hatua ya Korea Kaskazini ya kuunda zana za nyuklia imesababisha Marekani kuongoza vikwazo vikubwa dhidi ya nchi hiyo.

Jordan yaitaka Marekani isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel
Kando na hilo mkuu wa masuala ya siasa wa Umoja wa Mataifa ambaye hivi karibu alizuru Korea Kaskazini aliwaambia waandishi wa habari kuwa maafisa wa Korean Kaskazini wanaamini kuwa ni muhimu kuzuia vita.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Korea Kaskazini umeharibika kufuatia majaribio ya hivi karibuni ya mabomu ya nyuklia na makombora na kuwepo vita vya Maneno kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Akizungumza kwenye mkutano wa baraza la nchi za Atlantic siku ya Jumanne, Bw Tillerson alisema kuwa Marekani haiwezi kukubali Korea Kaskazini kujihami kwa silaha za nyuklia.



Viongozi wa ACT Wazalendo Singida watimkia CCM


 Mwenyekiti na katibu wa Chama cha ACT Wazalendo mkoani Singida, wamejivua uanachana na vyeo vyao na kuhamia CCM.

Viongozi hao ni aliyekuwa mwenyeketi Wilfred Noel Kitundu na katibu wa mkoa wa chama hicho, Loth Robert Thomas.

Viongozi hao wamechukua uamuzi huo mbele ya mkutano mkuu wa uchaguzi CCM mkoa wa Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Uhazili mjini hapa juzi.

Kwa nyakati tofauti walisema changamoto ambazo upinzani walikuwa wakizipigia kelele, Rais John Magufuli ameendelea kuzitatua kwa ufanisi.

Viongozi hao walikabidhi kadi za vyama vyao vya zamani, kwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Hadija Abood na kupewa kadi za CCM.

Katibu wa CCM mkoa wa Singida, Jimson Mhagama alisema kwamba wataendelea kuwapokea wanachama wanaorejea kutoka upinzani lakini ni lazima wafuate taratibu za chama.


Baada ya Askofu kuhojiwa Uraia wake, Bashe afunguka



 Bashe.

MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ameelezwa kusikitishwa kwake baada ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge, Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera, Severine Niwemugizi (61), kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji kuhusiana na uraia wake.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Bashe ameandika;

I know how it feels unapo ambiwa AMA kuanza kujazishwa Fomu na kuhojiwa juu ya Uraia Wako its like kujazishwa fomu kuambiwa huyu sio Mama yako or Baba yako Pole Askofu Severine Niwemugizi wanaofanya haya hawana hata Khofu ya Mungu.

Askofu Niwemugizi aliehojiwa na Idara ya Uhamiaji kuhusiana na uraia wake kwa mara ya kwanza Novemba 28 mwaka huu na mara ya pili alihojiwa Desemba 4, mwaka huu.

Askofu Niwemuzi aliingia kwenye headlines baada ya kueleza kuwa serikali itoe kipaumbele kwa katiba mpya ya nchi ili iweze kukamilika.



Askofu Niwemugizi


Mama Mjamzito ajifungulia kichakani


MKAZI wa Kijiji cha Ibondo, Kata ya Ludete, wilayani Geita, Ester Balele, amelazimika kujifungulia kwenye kichaka hatua chache kutoka kwenye nyumba anayoishi mkunga wa zahanati ya Ibondo, baada ya kukosa huduma kwa wakati.


Akizungumza na gazeti hili kijijini hapo, Balele alisema alikutwa na hali hiyo Novemba 29, majira ya saa 12.30 alfajiri alipo kwenda katika zahanati hiyo kujifungua na mkunga kugoma kufungua mlango.

Alisema kuwa siku hiyo majira ya saa tisa usiku akiwa amelala nyumbani kwake alipata dalili ya uchungu na kuamua kwenda kumuamsha mama mkwe na shemeji yake ili wampeleke zahanati akajifungue,  lakini baada ya kufika kwenye zahanati hiyo mkunga huyo aligoma kufungua licha ya kugongewa mlango mara kadhaa.

Alisema waliamua kumgongea mkunga huyo kwenye nyumba anayolala baada ya kukuta zahanati imefungwa.

Alisema ilipofika majira ya saa 12.30 alfajiri wakati wanaendelea kumgongea, hali ya uchungu ilizidi akalazimika kusogea kwenye kichaka ili ajifungue na alipomaliza mkunga huyo alitoka nje na kuwahoji kwa nini wanamsumbua usiku na kudai wanataka kumvamia.

Mkunga wa zahana hiyo, Aloyce Emmauel katika mahojiano na gazeti hili, amekiri kugoma kufungua mlango akihofia usalama wake huku akionyesha waandishi wa habari eneo la kichaka alipojifungulia mwanamke huyo .“Ni kweli nilisikia watu wanagonga mlango sikuweza kufungua kwa wakati huo, ilipofika majira ya saa 12.30 nilifungua mlango nikawakuta watu watatu nje wakiwa na mwanamkemmoja akihangaika kujifungua wakati narudi ndani kuchukua vifaa ghafla akawa amejifungua mtoto wa kiume,” alisema mkunga huyo.

Hata hivyo, zahanati hiyo kwa muda mrefu imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa lugha chafu kwa wagonjwa, kufanya kazi kwa mazoea na huku wakidaiwa kujihusisha na rushwa.

Wakati mkunga akikiri kutokea kwa tukio hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Geita, Solomon Shati, amekanusha kuwapo kwa mwanamke aliyejifungulia nje.

“Sijafika eneo la tukio, lakini nimewasiliana na mkuu wa zahanati ya Ibondo, Asteria Chekanabo, amesema hakuna mwanamke mjamzito aliyejifungulia kichakani,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mwalimu Hermani Kapufi, alipotafutwa kuelezea tukio hilo, ofisi yake imedai kuwa yuko safarini kikazi.

Source: Nipashe


Wanandoa wauawa kwa kupigwa mapanga na watu wasiojulikana


Mume na mke wakazi wa kitongoji cha Kidogue wilayani Mkalama wamefariki dunia kwa madai ya kukatwa mapanga shingoni na kichwani na watu wasiojulikana.

Mauaji ya wanandoa hao, Kija Kitundu (53) na mkewe Mwajuma Ramadhan (59) yalitokea Desemba 10 saa sita usiku nyumbani kwao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba alisema watoto wa wanandoa hao, Ramadhani (14) na Namagalu (12), wamepelekwa hospitali kwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika tukio hilo.

Magiligimba alisema siku ya tukio wauaji hao walitumia ngazi kupanda juu ya paa la nyumba ya Kija kisha kuingia chumbani kwa wanandoa hao na kuwacharanga mapanga.

Alifafanua kuwa kabla ya tukio hilo, kuna mtu alikwenda nyumbani kwa Kija kuomba pampu lakini aliponyimbwa ndipo ugomvi ukaanza baina yao.



Mbunge wa Chadema atofautiana na Ukawa


Dar es Salaam. Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu ametoa msimamo unaotofautiana na ule uliotolewa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuhusu ushiriki katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani.

Ukawa wamesema kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) haitaahirisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Januari 13 mwakani ili kuruhusu majadiliano, hawatashiriki uchaguzi huo. Lakini Komu amesema kufanya hivyo ni kosa kubwa linaloweza kuwaathiri katika chaguzi zijazo.

Viongozi wa Ukawa unaoundwa na Chadema, Chauma, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF waliitaka Nec kuahirisha uchaguzi huo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido, Songea Mjini na ule wa kata sita ili wadau wapate nafasi ya kujadili kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo kwenye kata 43 vinginevyo hawatashiriki.

Viongozi wa Ukawa; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Mwenyekiti wa Baraza Kuu la CUF, Julius Mtatiro; Kaimu Katibu wa Chauma, Eugene Kabendera na Katibu Mkuu wa NCCR- Mageuzi, Danda Juju walitoa msimamo huo juzi lakini jana Komu akizungumza na mwandishi wetu kuhusu uamuzi huo wa Ukawa alisema uamuzi ni halali kwa kuwa umepitia vikao halali, lakini unaweza kujadiliwa.

“Usahihi ni kitu kingine. Hatuko sahihi kususia uchaguzi haya ni mapambano, kwenye vita unapopigana unaonyesha wapi unakosea na kujisahihisha,” alisema mkurugenzi huyo wa fedha wa zamani Chadema.

“Hata hizo kata 43 hatukuonewa kote ndiyo maana tulishinda kata moja tuliyojipanga vizuri, kikubwa tunapaswa kujenga uwezo wetu na kupambana… kama tutasusia je, tumejipangaje kuhakikisha hicho tunachokipigania tutakipata?” alihoji.

Mbunge huyo alisema uamuzi huo unazua maswali mengi kwani CCM itapita katika majimbo yote bila kupingwa... “Watapata jukwaa la kueleza mambo yao sisi hatutapata, lakini je, kama huu hatutashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ule wa mwaka 2020 tutashiriki au la, haya ndiyo maswali yanayohitaji majibu.”

Juzi, Mbowe alisema kulikuwa na kasoro nyingi kwenye uchaguzi wa kata 43 ambazo zinahitaji kurekebishwa, lakini mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima katika taarifa yake aliyoitoa jana alisema chama cha siasa kutangaza kugomea uchaguzi hakuwezi kuifanya Tume iuahirishe.

“Ikitokea vyama vikasusa vyote kushiriki kwenye uchaguzi hapo ndipo unaweza kuahirishwa kwa kuwa hakutakuwa na mgombea,” alisema Kailima.



Mchezaji wa Simba apata msiba


Kiungo wa klabu ya Simba, Mohammed Ibrahim amepata pigo jana baada ya kumpoteza mtoto wake wa kiume aliyefariki dunia

Klabu ya Simba pamoja na mashabiki wa klabu hiyo wameungana na Watanzania wengine kumpa pole kiungo wao kwa pigo kubwa alilopata kumpoteza mtoto wake wa kiume ambaye bado alikuwa mdogo.

"Klabu ya Simba inatoa pole kwa kiungo wetu 'Mohammed Ibrahim' kwa kufiwa na mwanae mpendwa, tumeumia sote kwa msiba huu wa mtoto wetu mdogo kabisa. Klabu ya Simba inatoa pole kwa msiba huu mzito kwako na kwa famila nzima. Inna lillah wainna ilaihi Raajiun" alisema taarifa ya Simba



Kombe la ASFC kuzinduliwa na klabu ya Simba



Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho la TFF klabu ya soka ya Simba inatarajiwa kuzindua rasmi michuano hiyo kwa msimu wa 2017/18 itakapocheza na Green Warriors Desemba 22.

Kwa mjibu wa ratiba iliyotolewa na TFF raundi ya pili ya michuano hiyo itacheza kwa siku tano kuanzia Disemba 20 hadi 24. Michezo ya Desemba 20 mwaka huu itakutanisha timu za JKT Mlale na KMC, Toto African ya Mwanza na Eleven Stars ya Kagera.

Mechi zingine siku hiyo ni kati Ambassador na JKT Oljoro, Boma FC na Ndanda, Mvuvumwa na JKT Ruvu, Abajalo itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons wakati Milambo ya Tabora itacheza na Buseresere ya Geita.

Desemba 21, 2017 Mshikamano itacheza na Polisi Tanzania, Rhino ya Tabora na Alliance ya Mwanza, Majimaji Rangeres ya Lindi itapambana na Mbeya Kwanza ya Mbeya, Njombe Mji na Mji Mkuu ya Dodoma, Ashanti na Friends Rangers za Dar es Salaam, Kagera Sugar na Makambako wakati Stand United ya Shinyanga itacheza na AFC ya Arusha.

Desemba 22, kutakuwa na mechi ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo kati ya Green Warriors na Simba, Polisi Dar itapambana na Mgambo JKT ya Tanga, Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya Dar ila kwa sasa imeweka maskani Shinyanga, Biashara ya Mara itacheza na Mawenzi Market ya Morogoro, Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani itacheza na Madini FC ya jijini Arusha huku Mufindi United na Pamba ya Mwanza ilihali Singida United itacheza na Bodaboda FC.

Mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo Young Africans itacheza na Reha FC, Desemba 24, 2017 siku ambayo pia Burkina ya Morogoro itacheza na Lipuli ya Iringa,  Coastal Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma, Shupavu na Real Mojamoja wakati Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Hukumu ya Scorpion kusomwa January 10



Salum Njwete maarufu Scorpion akiwa chini ya ulinzi.

Kesi ya kumjeruhi mpaka kumtoboa macho kinyozi, Said Mrisho inayomkabili mwalimu wa sanaa ya kujihami, ‘Martial Arts’ na msanii wa filamu za kibongo, Salum Njwete maarufu Scorpion hatimaye imefikia tamati ambapo hukumu inatarajiwa kusomwa januari 10 mwakani.

Kesi hiyo iliendelea jana katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala jijini Dar ambapo Scorpion alikuwa akibanwa maswali na wakili wa utetezi, Nassoro Katuga kufuatia utetezi wake alioutoa kipindi kilichopita akiongozwa na wakili wake, Juma Nassoro.

Katika utetezi wake wa awali Scorpion alisema alishurutishwa kutoa maelezo katika kituo cha polisi cha Buguruni ambapo wakili Katuga alimuuliza kwanini alisaini.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Flora Haule aliifunga kwa kuahidi kuitolea hukumu Januari 10 mwakani ambapo kabla ya hukumu hiyo kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Desemba 27 mwaka huu.

Kula Blueberry Kunaongeza Uwezo Wa Ubongo



Utafiti mpya umegundua kuwa, kunywa vikombe viwili na nusu vya juisi ya blueberry kwa siku ( mie naziita kunazi za bluu) kunaongeza uwezo wa ubongo wa kufahamu, na kuondoa matatizo ya usahaulifu yanayotokana na utu uzima. Wataalamu wanasema kuwa

kunywa kila siku juisi hiyo kunamzuia mtu uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa kupoteza akili uzeeni au wendawazimu. Blueberry kwa kuwa na kiwango kikubwa cha phytochemical, tunda hilo lina limejaa anti oksidanti na lina uwezo wa kuzuia uvimbe. Vilevile kunazi za

bluu kwa kuwa na mada iitwayo Anthocyanin, huweza kusaidia kuongeza kumbukumbu katika ubongo. Pia tunda hilo husaidia kupunguza kasi ya kitendo cha kupungua kumbukumbu katika ubongo kwa kuondoa gulukosi zinazopatikana kwenye ubongo.

Uchunguzi huo umebaini kwamba, kula blueberry kupitia vidonge maalum vya kusaidia afya au supplements kunaweza kumpatia mtu faida kubwa katika ubongo. Hata hivyo wataalamu hao wameshauri kuwa ni bora tunda hilo liliwe katika hali ya kawaida.

Huko nyuma pia wataaamu walieleza kuwa, Blueberry husaidia kupunguza usongo wa mawazo pamoja na kiwango cha juu cha gulukosi katika damu.
Haya tena wadau…usichelewa kula tunda hili, najua katika nchi zetu za Afrika tunda hili

halipatikana na ndio sababu hata jina lake katika kamusi yetu haliko, lakini usife moyo unaweza kupata tunda hilo madukani na katika supermarkets ambapo huhifadhiwa katika makopo au kama juisi. Kwa wale walioko ughaibuni basi hakuna tabu hiyo na usikose kula tunda hilo tamu wakati wa msimu wake na wakati miwngine wowote.
Daima tuzilinde afya zetu!