Saturday, 9 December 2017

Waziri Kigwangalla ateua kamati ya Kitaifa ya Utambulisho wa Tanzania



Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangalla  jana Desemba 8,2017 Mjini Dodoma, ameunda kamati ya kuongoza maandalizi ya namna watanzania na wageni wa Tanzania watakavyosherehekea Utanzania wao  kwenye mwezi maalum utakaojulikana kama ‘TANZANIA HERITAGE MONTH’.

Akielezea wakati wa kutangaza kamati hiyo iliyojumlisha wadau mbalimbali wakiwemo wanahabari, wanamichezo na wadau wengine mbalimbali na wafanyabishara, alisema:

“Kwenye mwezi huu kila kitu kitakuwa cha kitanzania na tutataka kwenye kila ofisi ya umma, ofisi binafsi, shule, chuo, hotel, balozi zetu n.k mtu akifika tu, ‘utanzania’ wetu uonekane!” alieleza Dk.Kigwangalla.

Utanzania huo ambapo kila mwezi huo utakapofika ambapo moja ya mambo hayo ni pamoja na aina ya mavazi maalum, vyakula,  na mambo mengine yanayobeba na kujumuisha Utanzania.


Zitto Kabwe azungumzia hatima ya ACT- Wazalenddo



Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amefunguka kuwa  ndani ya chama chake (ACT) kuna watu wengi wakiwemo wanachama wa kutosha  akimaanisha hajabaki mwenyewe.

Zitto amefunguka hayo akimjibu mfuasi wake wa kwenye mtandao wa kijamii ambaye alitoa maoni yake kwa kumuuliza Mh. Kabwe haoni kama amebaki peke yake, ikiwa ni muda mfupi baada ya aliyekuwa Mgombea urais wa chama chake Anna Mghwira kujiunga na CCM huko Dodoma.

Akimjibu mfuasi huyo Zitto amesema "Chama chetu ACT Wazalendo kina madiwani 42, kina wenyeviti wa mitaa, vitongoji na wajumbe wa Serikali za Vijiji/Mitaa 507, Viongozi kila mkoa na jimbo, wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu. Ni dhahiri tuna watu wengi na wanachama wengi wa kutosha"

Hivi karibuni CCM ilijivunia wanachama wapya ambao waliwahi kuwa na nafasi ya uongozi ACT Wazalendo ambapo baadhi yao ni Prof Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba, Alberto Msando na jana  Anna Mghwira.

Wabunge wa Chadema waachiwa kwa Dhamana



Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro imetupilia mbali hati ya kiapo cha kupinga dhamana ya wabunge Suzan Kiwanga(Mlimba), Peter Lijualikali (Kilombero) na washtakiwa wengine 37 waliofikishwa mahakamani hapo kwa makosa nane.

Mbele ya Hakimu, Ivan Msaki mahakama ilitupilia mbali kiapo hicho na kueleza kuwa washtakiwa wote dhamana yao iko wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja watakaosaini dhamana ya Sh 5 milioni na pia barua za dhamana lazima zisainiwe na wenyeviti wa vijiji ama maofisa watendaji.

Katika kiapo kilichowasilishwa awali mahakamani hapo na upande wa mashtaka kupitia wanasheria wa Serikali, Sunday Hyera na Edga Bantulaki ulieleza sababu walizodai kuwa ni za msingi za kupinga dhamana na kwamba kuwepo nje kwa washtakiwa  kunaweza kuharibu upelelezi wa kesi hiyo.

Kufuatia hoja hiyo upande wa utetezi unaowakilishwa na mawakili wanne wakiongozwa na wakili Peter Kibatala uliamua kuwasilisha hati ya kupinga kiapo hicho kwa madai kuwa  kiliandikwa bila ya kuzingatia misingi na matakwa ya kisheria.

Wakili Kibatala alidai kuwa miongoni mwa mapungufu yaliyokuwemo kwenye kiapo hicho ni pamoja na kutokuonyesha majina ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Malinyi (OCD) ambaye alitajwa kwenye kiapo hicho kama chanzo kilichotoa taarifa zilizotengeneza mashtaka yanayowakabili wabunge hao na wenzao.

Alidai kuwa mapungufu mengine yaliyokuwepo kwenye kiapo hicho ni utofauti wa tarehe ya kuandika kiapo hicho na kusainiwa na hivyo waliiomba mahakama kuzingatia mapungufu hayo.

Kutokana na mvutano huo wa kisheria baina ya pande hizo mbili Hakimu Msaki aliamua kupitia hoja za msingi za kisheria na hivyo kubaini mapungufu yaliyopo kwenye kiapo hicho na kueleza kuwa mapungufu hayo hayawezi kurekebishwa na kwamba kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria na si kufundisha namna ya kuandika kiapo.

Kwa msingi huo Hakimu Msaki alitupilia mbali hati hiyo ya kiapo cha kupinga dhamana na kueleza kuwa washtakiwa hao watakuwa nje kwa dhamana wakati kesi yao ikiendelea.

Kabla ya kupewa dhamana washtakiwa hao walikaa rumande kwa siku 12 hali iliyosababisha kesi hiyo kuvuta hisia za watu hususani viongozi na wanachama Chadema waliokuwa wakifulika mahakamani hapo.

CHUO CHA ST DAVID KIMARA DAR KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO




CHUO CHA ST DAVID COLLEGE OF HEALTH KILICHOPO KIMARA TEMBONI DSM NI CHUO CHA KIPEKEE KATIKA UKANDA HUU WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KINACHOTOA KOZI ZA AFYA KWA NGAZI ZOTE ZA CHETI NA DIPLOMA.

SIFA KUU NI UFAULU MASOMO YA SAYANSI IKIWEO HESABU NA KIINGEREZA ANGALAU ALAMA D.

ADA ZETU NI NAFUU UTALIPA KIDOGO KIDOGO KUKIDHI UWEZO WAKO, KWA MAWASILIANO 0626 231 364 / 0783 785 747 /  0716 044 610 / 0718 229 977 AU INGIA MTANDAONI  www.stdavidcollege.ac.tc

WAHI SASA MUHULA MPYA TAYARI UMEANZA.
PIA KUNA KOZI MAALUMU KWA WOTE WASIO NA VIGEZO KAMILI KUMUWEZESHA KUPAMBANA MPAKA AFIKIE VIWANGO NA KUJIUNGA NA MEDICINE..CA/CO

JIUNGE NA KOZI INAYOTOLEWA ST DAVID COLLEGE PEKEE IITWAYO PRE-MEDICINE PROGRAME KWA KUSHIRIKIANA NA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA NECTA TUMEKUANDALIA NJIA RAHISI KABISA.

FIKA SASA KIMARA TEMBONI ZAMANI MOA AU OFISI ZETU ZILIZOPO MWANANYAMALA A CCM MINAZINI KWA DR DAVID B.MWANGANDA.

CHUO NI CHA KUTWA NA BWENI.





Breaking News: Papii Kocha na Babu Seya wapata msamaha wa Rais



Rais Dkt. John Magufuli ametoa msahama kwa wasanii Papii Kocha na baba yake Nguza Viking a.k.a Babu Seya waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela.

Rais Magufuli amesema hayo leo mjini Dodoma wakati wa sherehe za miaka 66 ya Uhuru. Pia Rais Magufuli ametoa msamaha kwa watu 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Nguza Viking na Papii Kocha walikuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto wadogo wa shule ya msingi.

Mzungu mwenye asili ya Israel afuata nyayo za AliKiba



Msanii wa muziki kutoka Kenya mwenye asili ya Israel Gilard Millo, amesema msanii wa bongo fleva Alikiba ndiye aliyemu-'insipire' kuimba Kiswahili, kitu ambacho kimempa mafanikio makubwa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television, Gilard ambaye hivi sasa ametua bongo, amesema wimbo wa 'Cinderela' wa Alikiba ndio ulimfanya azidi kupenda kuimba kwa lugha ya Kiswahili, baada ya kuona mashabiki wakimshangilia kwa nguvu alipoimba wimbo huo jukwaani.

"Cinderela ndio wimbo ulionifanya mimi nianze kuimba Kiswahili, nilikuwa nauimba na band live, na ndio wimbo wa kwanza wa Kiswahili nilioanza kuimba, sasa nikiimba watu wakawa wanashangilia huyu ni mzungu lakini anaimba Kiswahili, nikapenda nikaanza kuimba na zingine kwa Kiswahili, na mpaka leo naimba nyimbo zangu kwa Kiswahili", amesema Gilard.

Gilard ana kazi mbali mbali ambazo zimemfanya achukue tuzo za kimataifa, ambazo zimeimbwa kwa lugha ya Kiswahili, ikiwemo Unajua, Nairobi Yangu, Mapenzi, Sema milele na nyinginezo.

Spika Ndugai atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya wanajeshi


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ametuma salamu za rambi rambi kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, kufuatia vifo vya askari 14.

Spika Ndugai amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya askari hao ambao walikuwa wakilinda amani nchini Kongo, pamoja na wengine 44 waliojeruhiwa kufuatia mashambulizi yanayotekelezwa na askari waasi nchini humo.

Kufuatia tukio hilo, Spika Ndugai ametoa pole kwa familia za askari hao waliouawa, na kuwaombea wale waliojeruhiwa kupona haraka na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.

Lwandamina agoma wachezaji vijana kutolewa kwa mkopo



ocha George Lwandamina ameonekana kuwa na imani kubwa na wachezaji vijana wa kikosi hicho.

Lwandamina âmezuia kuondoka kwa wachezaji wote vijana walio katika kikosi chake hasa wale waliokuwa wakiombwa kwa mkopo.

Kocha huyo raia wa Zambia, ameuisisitiza uongozi wa Yanga wachezaji wa Yanga walio katika kikosi hicho wanapaswa kuendelea kubaki.

“Kocha amekataa kabisa wachezaji vijana wasiondoke, amesisitiza waendelee kubaki hadi hapo baadaye kwa kuwa ana programu nao,” kilieleza chanzo.

Timu kadhaa, zilionekana kuanza kuwanyemelea wachezaji makinda wa Yanga katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo lakini Lwandamina ameonekana kuendelea kuwahitaji.

Lwandamina amekuwa ni muumini wa vijana na tokea ametua Yanga amekuwa akitoa nafasi kwa wachezaji vijana ambao wamekuwa wakionekana kufanya vema.

Bosi wa Ndemla ashindwa kutua Bongo kumalizana na Simba


BOSI wa Klabu ya AFC Eskelistuna ameshindwa kuwasili nchini wiki hii kumalizana na Simba kuhusu usajili wa timu hiyo, Said Ndemla baada ya mmoja kati anayehusika na ujio wake kupata msiba.

Kiongozi huyo alitarajiwa kuwasili nchini wiki hii kwa ajili ya suala la mchezaji huyo pamoja na masuala mengine ya kisoka lakini imeshindikana.

Ndemla alifanikiwa kufuzu majaribio mwezi uliopita katika klabu hiyo ya Sweden ambayo ilikuwa
 inashiriki ligi kuu na sasa imeshuka daraja.

Akizungumza na Championi Jumamosi, meneja wa Ndemla, Jamali Kisongo alisema kiongozi huyo ameshindwa kuwasili kutokana na matatizo hayo aliyoyapata mwenzao.

“Yule kiongozi alitakiwa kuwasili nchini wiki hii lakini imeshindikana kwa sababu mmoja kati ya watu anayehusika na ujio wake amepata msiba, hivyo sijafahamu baada ya hapo ratiba zake zitakuwaje.

“Lakini kama kutakuwa na lolote tutaweka wazi. Kwa upande wa mchezaji licha ya timu kushuka daraja lakini dili liko palepale, atajiunga nayo tu,” alisema Kisongo.

Rais Magufuli atoa msamaha kwa wafungwa 61 wa kunyongwa


Rais wa Tanzania John Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo amewasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Hata hivyo idadi ya wafungwa wengine walioachiwa huru kutokana na makossa mbali mbali ni 1,821 ambao amesema kuwa wanapaswa kuachiwa mara baada ya tangazo lake.

Wafungwa wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao. Idadi hiyo ya msamaha kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha.

Jeshi la Israel lashambulia maeneo matatu Ukanda wa Gaza



Jeshi la anga la Israel lashambulia mapema asubui maeneo matatu tofauti katika Ukanda wa Gaza.

Katika mashambulizi hayo yaliolenga Kusini mwa Gaza, mpalestina mmoja mwenye umri wa kati ya maika 20 na 30 ameripotiwa kufariki.

Majira ya jioni Ijumaa jeshi la Israel lilishambulia Kaskazini mwa Gaza na kuwajeruhi watu 15.

Wasanii washirikikatika sherehe za Uhuru Dodoma



 Baadhi ya Wasanii wa kizazi kipya wanaounda kundi la Tanzania All Stars wakiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara,yanayoendelea kufanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.


tumia Asali Kwa Urembo Wa Nywele na Ngozi



Asali hutumika kulainisha Ngozi
Asali ina asili ya kuvuta unyevu kutoka kwenye hewa na kuipa ngozi uwezo wa kuhifadhi unyevu hivyo ni faida kwa mtu mwenye ngozi kavu.
Jinsi ya kuandaa
Chukua asali mbichi kijiko kimoja cha chai kisha paka usoni, kaa nayo kwa dakika 15 hadi 20 kisha safisha uso wako.
Asali katika kusafisha ngozi, kutibu na kuzuia chunusi
Kutokana na uwezo wa asali katika kuua bacteria na kuvuta uchafu katika matundu ya ngozi asali itakusaidia kutatua tatizo la chunusi.
Jinsi ya Kuandaa
Chukua asali mbichi Kijiko kimoja cha chakula changanya na mafuta ya nazi vijiko viwili changanya mchanganyiko uwe mlaini kisha paka usoni huku ukisugua taratibu kwa kufanya kama viduara huku ukiepuka kufikisha machoni. ukimaliza kusugua uso na mchanganyiko wako osha uso wako.
Jinsi ya kuandaa kama kisafisha ngozi, exfoliator
Changanya kijiko kimoja asali na kijiko kimoja baking soda. tumia mchanganyiko huu kusugua ngozi yako. Asali inaongeza lishe na chembe chembe kuzuia madhara yanayotokana na sumu za hewani zinazozeesha ngozi. Baking soda inasaidia kusafisha matundu ya ngozi.
Asali inasaidia ngozi iliyoungua na jua kujirudi na kung'aa.
Jinsi ya kutumia asali katika nywele
Asali inatibu nywele kavu zilizopauka, na kulainisha ngozi kavu ya kichwa na kutibu muwasho kichwani.
Jinsi ya kufanya
Changanya kijiko kikubwa cha asali na maji ya uvuguvugu kisha paka kichwani Acha kwa muda wa saa 1 iwe kama conditioner kisha safisha nywele zako.
Unaweza kuchanganya asali kiasi cha kijiko kimoja mpk viwili katika maji vikombe vitano kisha safishia nywele zako taratibu, yaani yapitishe tu hayo maji kwenye nywele zako ambazo ni safi.
Tahadhari: Asali kwa kiasi kikubwa hupausha weusi wa nywele kutokana na Hydrogen Peroxide inayopatikana ndani ya asali.
Ni vema ukatumia asali mbichi kujihakikishia faida za asali katika mwili wako.
Iwapo unavutiwa na matumizi ya kitu cha asili katika urembo wako unaweza kuongeza kitu hicho katika kitu kingine unachotumia mfano katika steaming yako au scrub unayotumia