Saturday, 9 December 2017

Breaking News: Papii Kocha na Babu Seya wapata msamaha wa Rais



Rais Dkt. John Magufuli ametoa msahama kwa wasanii Papii Kocha na baba yake Nguza Viking a.k.a Babu Seya waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela.

Rais Magufuli amesema hayo leo mjini Dodoma wakati wa sherehe za miaka 66 ya Uhuru. Pia Rais Magufuli ametoa msamaha kwa watu 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Nguza Viking na Papii Kocha walikuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto wadogo wa shule ya msingi.

Mzungu mwenye asili ya Israel afuata nyayo za AliKiba



Msanii wa muziki kutoka Kenya mwenye asili ya Israel Gilard Millo, amesema msanii wa bongo fleva Alikiba ndiye aliyemu-'insipire' kuimba Kiswahili, kitu ambacho kimempa mafanikio makubwa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television, Gilard ambaye hivi sasa ametua bongo, amesema wimbo wa 'Cinderela' wa Alikiba ndio ulimfanya azidi kupenda kuimba kwa lugha ya Kiswahili, baada ya kuona mashabiki wakimshangilia kwa nguvu alipoimba wimbo huo jukwaani.

"Cinderela ndio wimbo ulionifanya mimi nianze kuimba Kiswahili, nilikuwa nauimba na band live, na ndio wimbo wa kwanza wa Kiswahili nilioanza kuimba, sasa nikiimba watu wakawa wanashangilia huyu ni mzungu lakini anaimba Kiswahili, nikapenda nikaanza kuimba na zingine kwa Kiswahili, na mpaka leo naimba nyimbo zangu kwa Kiswahili", amesema Gilard.

Gilard ana kazi mbali mbali ambazo zimemfanya achukue tuzo za kimataifa, ambazo zimeimbwa kwa lugha ya Kiswahili, ikiwemo Unajua, Nairobi Yangu, Mapenzi, Sema milele na nyinginezo.

Spika Ndugai atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya wanajeshi


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ametuma salamu za rambi rambi kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, kufuatia vifo vya askari 14.

Spika Ndugai amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya askari hao ambao walikuwa wakilinda amani nchini Kongo, pamoja na wengine 44 waliojeruhiwa kufuatia mashambulizi yanayotekelezwa na askari waasi nchini humo.

Kufuatia tukio hilo, Spika Ndugai ametoa pole kwa familia za askari hao waliouawa, na kuwaombea wale waliojeruhiwa kupona haraka na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.

Lwandamina agoma wachezaji vijana kutolewa kwa mkopo



ocha George Lwandamina ameonekana kuwa na imani kubwa na wachezaji vijana wa kikosi hicho.

Lwandamina âmezuia kuondoka kwa wachezaji wote vijana walio katika kikosi chake hasa wale waliokuwa wakiombwa kwa mkopo.

Kocha huyo raia wa Zambia, ameuisisitiza uongozi wa Yanga wachezaji wa Yanga walio katika kikosi hicho wanapaswa kuendelea kubaki.

“Kocha amekataa kabisa wachezaji vijana wasiondoke, amesisitiza waendelee kubaki hadi hapo baadaye kwa kuwa ana programu nao,” kilieleza chanzo.

Timu kadhaa, zilionekana kuanza kuwanyemelea wachezaji makinda wa Yanga katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo lakini Lwandamina ameonekana kuendelea kuwahitaji.

Lwandamina amekuwa ni muumini wa vijana na tokea ametua Yanga amekuwa akitoa nafasi kwa wachezaji vijana ambao wamekuwa wakionekana kufanya vema.

Bosi wa Ndemla ashindwa kutua Bongo kumalizana na Simba


BOSI wa Klabu ya AFC Eskelistuna ameshindwa kuwasili nchini wiki hii kumalizana na Simba kuhusu usajili wa timu hiyo, Said Ndemla baada ya mmoja kati anayehusika na ujio wake kupata msiba.

Kiongozi huyo alitarajiwa kuwasili nchini wiki hii kwa ajili ya suala la mchezaji huyo pamoja na masuala mengine ya kisoka lakini imeshindikana.

Ndemla alifanikiwa kufuzu majaribio mwezi uliopita katika klabu hiyo ya Sweden ambayo ilikuwa
 inashiriki ligi kuu na sasa imeshuka daraja.

Akizungumza na Championi Jumamosi, meneja wa Ndemla, Jamali Kisongo alisema kiongozi huyo ameshindwa kuwasili kutokana na matatizo hayo aliyoyapata mwenzao.

“Yule kiongozi alitakiwa kuwasili nchini wiki hii lakini imeshindikana kwa sababu mmoja kati ya watu anayehusika na ujio wake amepata msiba, hivyo sijafahamu baada ya hapo ratiba zake zitakuwaje.

“Lakini kama kutakuwa na lolote tutaweka wazi. Kwa upande wa mchezaji licha ya timu kushuka daraja lakini dili liko palepale, atajiunga nayo tu,” alisema Kisongo.

Rais Magufuli atoa msamaha kwa wafungwa 61 wa kunyongwa


Rais wa Tanzania John Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo amewasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Hata hivyo idadi ya wafungwa wengine walioachiwa huru kutokana na makossa mbali mbali ni 1,821 ambao amesema kuwa wanapaswa kuachiwa mara baada ya tangazo lake.

Wafungwa wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao. Idadi hiyo ya msamaha kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha.

Jeshi la Israel lashambulia maeneo matatu Ukanda wa Gaza



Jeshi la anga la Israel lashambulia mapema asubui maeneo matatu tofauti katika Ukanda wa Gaza.

Katika mashambulizi hayo yaliolenga Kusini mwa Gaza, mpalestina mmoja mwenye umri wa kati ya maika 20 na 30 ameripotiwa kufariki.

Majira ya jioni Ijumaa jeshi la Israel lilishambulia Kaskazini mwa Gaza na kuwajeruhi watu 15.

Wasanii washirikikatika sherehe za Uhuru Dodoma



 Baadhi ya Wasanii wa kizazi kipya wanaounda kundi la Tanzania All Stars wakiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara,yanayoendelea kufanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.


tumia Asali Kwa Urembo Wa Nywele na Ngozi



Asali hutumika kulainisha Ngozi
Asali ina asili ya kuvuta unyevu kutoka kwenye hewa na kuipa ngozi uwezo wa kuhifadhi unyevu hivyo ni faida kwa mtu mwenye ngozi kavu.
Jinsi ya kuandaa
Chukua asali mbichi kijiko kimoja cha chai kisha paka usoni, kaa nayo kwa dakika 15 hadi 20 kisha safisha uso wako.
Asali katika kusafisha ngozi, kutibu na kuzuia chunusi
Kutokana na uwezo wa asali katika kuua bacteria na kuvuta uchafu katika matundu ya ngozi asali itakusaidia kutatua tatizo la chunusi.
Jinsi ya Kuandaa
Chukua asali mbichi Kijiko kimoja cha chakula changanya na mafuta ya nazi vijiko viwili changanya mchanganyiko uwe mlaini kisha paka usoni huku ukisugua taratibu kwa kufanya kama viduara huku ukiepuka kufikisha machoni. ukimaliza kusugua uso na mchanganyiko wako osha uso wako.
Jinsi ya kuandaa kama kisafisha ngozi, exfoliator
Changanya kijiko kimoja asali na kijiko kimoja baking soda. tumia mchanganyiko huu kusugua ngozi yako. Asali inaongeza lishe na chembe chembe kuzuia madhara yanayotokana na sumu za hewani zinazozeesha ngozi. Baking soda inasaidia kusafisha matundu ya ngozi.
Asali inasaidia ngozi iliyoungua na jua kujirudi na kung'aa.
Jinsi ya kutumia asali katika nywele
Asali inatibu nywele kavu zilizopauka, na kulainisha ngozi kavu ya kichwa na kutibu muwasho kichwani.
Jinsi ya kufanya
Changanya kijiko kikubwa cha asali na maji ya uvuguvugu kisha paka kichwani Acha kwa muda wa saa 1 iwe kama conditioner kisha safisha nywele zako.
Unaweza kuchanganya asali kiasi cha kijiko kimoja mpk viwili katika maji vikombe vitano kisha safishia nywele zako taratibu, yaani yapitishe tu hayo maji kwenye nywele zako ambazo ni safi.
Tahadhari: Asali kwa kiasi kikubwa hupausha weusi wa nywele kutokana na Hydrogen Peroxide inayopatikana ndani ya asali.
Ni vema ukatumia asali mbichi kujihakikishia faida za asali katika mwili wako.
Iwapo unavutiwa na matumizi ya kitu cha asili katika urembo wako unaweza kuongeza kitu hicho katika kitu kingine unachotumia mfano katika steaming yako au scrub unayotumia

Tambua Madhara ya Ulaji Wa chipsi



Chips ni aina ya chakula ambacho hupendwa na watu wengi na pia ni miongoni mwa vyakula vyenye mafuta mengi. chips pia inasemekana ni miongoini mwa vyakula ambavyo hupikwa katika joto la juu zaidi ya 300 degree.
Chips ni chakula chenye mafuta mengi na mafuta yanapoingia mwilini huenda kuzunguka sehemu ya mwili wa mwanadamu. kama ni mtu ambaye mazoezi pia hufanyi madhara yake ni kupata magonjwa ya moyo. hivi sasa idadi kubwa ya vijana wanaugua magonjwa mengi yanayo sababishwa na mkusanyiko wa mafuta katika miili yao amabayo huchangiwa na kuto kufanya mazoezi madhara yake mafuta kuziba mirija
Mafuta yakiliwa sana husababisha kuzidi mwilini.
Pia inasadikika mafuta yaliyopo katika chipsi katika sahani moja ya chisi ya moto endapo utaamua kuchuja kuna uwezekano wa kupata nusu glasi ya mafuta ya kupikia. Kwa hali hii ujue ni hatari.
Na mwili huwa hatupi kinachofaa, na badala yake kama hakitumiki wakati huo basi huhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye. Ndio maana tunapokula vyakula vyingi vyenye mafuta mengi hutupelekea kuongeza unene na uzito.
Unene huwa ni chanzo cha magonjwa mengi ,Kwani (High Blood pressure) hutokana na kuwa na mafuta mengi mwilini ambayo hupelekea mirija ya kusafirisha damu kuwa na mafuta. Hii husababisha njia ya kupitia damu kuwa nyembamba hivyo kusababisha nguvu ya ziada itumike kusukuma damu hiyo ili isambae mwilini kama inavyotakiwa. Nguvu hii ya ziada huongeza au kupunguza mapigo ya moyo.
Mapigo ya moyo yanapoongezeka sana ni hatari na yanapo pungua sana pia ni hatari.
Hivyo basi ni vizuri kwa watumiaji wa chipsi kujitahidi kutumia kwa kiasi kidogo au kuacha kabisa vile vile mazoezi pia ni muhimu ili kupunguza mrundikano wa mafuta katika mwili.
Pia inasemekana kuwa wanasayansi wamegundua kuwa chipsi husababisha kukuza hips hivyo kwa wanaume wengi hawatapenda kuwa katika hali hiyo, hivyo ni muhimu kujiepusha na pia isije ikawa kichocheo kwa wanawake kutumia sana ili kukuza sehemu hizo za maumbile bali wapunguze kutumia chipsi pamoja na kufanya mazoezi ili kuweka mwili katika hali ya kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.pia ulaji wa chips kupita kiasi husababisha wanaume na wanawake kuzeeka mapema.

Friday, 8 December 2017






Mwanza. Sakata la mwanamke aliyemvisha pete ya uchumba mwanamke mwenzake limechukua sura mpya baada ya jeshi la polisi kufanikiwa kuwatia mbaroni watu wengine watatu akiwemo aliyevishwa pete.
Sura mpya ya kwanza ni mtuhumiwa Milembe Suleiman (36), anayedaiwa kumvalisha pete mwanamke mwenzake Janeth Shonza, aliyekuwa akishikiliwa na polisi mkoani Geita kuhamishiwa mkoani Mwanza.
Pili, jeshi la polisi pia limefanikiwa kumtia mbaroni mwanamke aliyevishwa pete, Janeth Shonza (25), mwanafunzi wa mwaka wa nne wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa akiwa mafichoni eneo la Puma mkoani Singida.
Amewataja wengine wanaoshikiliwa na kutarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote uchunguzi utakapokamilika kuwa ni Richard Fabian (28), mkazi wa Buzuruga jijini Mwanza aliyepiga na kusambaza mitandaoni picha za wanawake hao wakivishana pete mitandaoni.
Kamanda Msangi amemtaja mwingine anayeshikiliwa kuwa ni Aneth Mkuki (24), mkazi wa Nyasaka jijini Mwanza, mpenzi mwingine wa Janeth aliyemsaidia kutoroka kukwepa kutiwa mbaroni na polisi baada ya video yao kusambazwa mitandaoni.

Kanisa la Mch Gwajima Labomolewa usiku

Kufuatia zoezi la serikali la kupanua na kuboresha miundo mbinu mbalimbali nchini hususan ya barabara katika jiji la Dar es Salaam ambapo imelazimu baadhi ya maeneo kubomolewa ili kupisha zoezi hilo la upanuzi, Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima nalo limekumbwa na kadhia ya kubomolewa.
Kanisa hilo lililoko jirani kabisa na Barabara ya Morogoro ambayo serikali imepanga kuipanua ili kurahisisha usafiri na kupunguza foleni, lilitakiwa kubomolewa kutokana na kuwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara hiyo.
Mchungaji Biyagaza wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko chini ya Askofu Gwajima, ameeleza kuwa serikali iliwapatia notisi ya siku 30 ili wabomoe kipande cha jengo la kanisa hilo kilichopo ndani ya eneo la hifadhi ya barabara.
“Ni kweli tunayo notice ya mwezi mmoja ya kuhakikisha kwamba eneo ambalo ni hifadhi ya barabara tunaliacha. Na hifadhi ya barabara ni mita 90 kuanzia katikati. Bahati nzuri wale waliokuja kuweka alama zao walipofika hapa na wahandisi , mafundi na baadhi ya watu wa kanisani walikuwepo. Basi tukawaambia wapime mita 90 zinapoishia. Kwa hiyo wakapima mita 90 zilipoishia wakaweka alama, wakasema basi nyie mnaweza mkabomoa upande huu na upande huu mkauacha kwa ajili ya hifadhi ya barabara,” alisema Mchungaji Biyagaza.
“Sisi baada ya hapo tukaona tujipange kwa ajili kuachia eneo la barabara ili shughuli nyingine ambazo ni mpango wa maendeleo ya serikali ziweze kuendelea na sisi tuweze kuendelea na eneo letu vizuri. Kwa hivyo kile kipande chote ambacho ni cha barabara na tukaongeza ndani kidogo chote tumekiondoa. Na hili eneo linalobaki tunapaimarisha ili nyumba ya Bwana iweze kufanya kazi yake ya kutoa huduma za kiroho,” aliongeza.
Mchungaji Biyagaza alieleza japokuwa eneo la jengo limepungua, eneo lililobakia linaimarishwa ili kanisa hilo liweze kuendelea kutoa huduma za kiroho kwa waumini wake.
Aidha kufuatia zoezi hilo la upanuzi wa barabara ya Morogoro ambalo linaenda sambamba na ujenzi wa barabara za juu (fly-over) katika makutano ya barabara eneo la Ubungo, umepelekea kubomolewa kwa majengo mbalimbali ikiwemo majengo ya wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na jengo la Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania ambayo yamebomolewa kufuatia agizo la Rais Dkt. John pombe Magufuli.

Jerry Muro amesema uwezowake ajilinganisha na Wabunge 10 Chadema




Aliyekuwa Msemaji wa Yanga SC, Jerry Muro amesema kutokana na uwezo wake katika mambo mbali mbali anaweza kujilinganisha na wabunge 10 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika mahojiano na kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm, Jerry amesema kutokana na uwezo wake suala la ubunge kwake ni jambo rahisi tu sawa na kubofya button.

“Mimi Jerry Muro mmoja ni sawa na wabunge 10 wa Chadema, nimewazidi kifikra, kinguvu, kipesa, maadili, kihoja na mambo mengine mengi sana” amese Jerry.

Katika hatua nyingine Jerry amesema mwaka 2020 si ajabu kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Edward Lowassa wakirejea katika Chama cha Mapinduzi (CCM).