Saturday, 2 December 2017

Funguo Tano Za Mafanikio Ya Mjasiriamali Wakati Wote



Kitu kizuri kwa mjasiaramali yoyote yule uwe unaanza au tayari safari hiyo  ulishaanza ni kujiandaa kuwa mshindi. Ni muhimu sana kujua wewe ni mshindi kwa kile unachokifanya bila kujali ni changamoto zipi unakutana nazo.

Lakini hata hivyo huwezi kuwa mshindi kama hutaweza kujua siri ya ushindi huo utaupata vipi. Kutokana na hilo sasa hapo ndipo unalazimika kuzijua funguo tano za  mafanikio ukiwa kama mjasiriamali.

Hizi ni funguo tano kweli kwa mjasiriamali ambazo ukizitumia, zitakupa mafanikio na kukufikisha kule unakotaka kufika . Funguo hizo ni zipi, fuatana nasi katika makala yetu ya leo kujifunza.

1. Weka kushindwa nyuma kabisa.
Kwa kawaida huwa yapo makosa  na kushindwa kwingi hasa pale unapoanza biashara au hata pia unapokuwa unaendelea na biashara yako. Yote hayo yanapotokea ikiwa kweli wewe ni mjasiriamali uliyenuia hebu yasahau.

Kitu kukubwa kwako angalia kule unakokwenda. Makosa ni sehemu pia ya kukusaidia kufanikiwa kule unakokwenda ikiwa utajifunza. Acha kuamini kwamba utashindwa kirahisi. Amini utashinda kwa hicho unachokifanya.

2. Weka juhudi nyingi kila siku.
Anza siku yako kila siku kwa kujua kwamba unakwenda kuweka juhudi nyingi sana ambazo kwa vyovyote vile zitakuletea matunda. Jione mshindi kila iitwapo leo. Acha kujiona mnyonge.

Unapokuwa mjasiriamali unayejitambua ni lazima uelewe hili kwamba mafanikio yako yanategemea sana pia kutokana na juhudi unazoziweka. Hakuna kubahatisha ni kuweka juhudi ndiko kutakapokupa matokeo chanya.

3. Jifunze na jirekebishe kila siku.
Usiruhusu kutokujifunza, kila siku jifunze unapokuwa kwenye safari yako ya ujasiriamali. Kuna njia nyingi za kujifunza kama semina, mitandao na hata kutumia vitabu, hapo chagua njia iliyo bora kwako na ujifunze kila siku.

Kujifunza kunakusaidia sana kuchukua taarifa kutoka kwa wajasiriamali waliobobea kutoka sehemu mbalimbali duniani na kunakufanya na wewe kuzidi kuwa bora. Tumia muda hapo japo kidogo kujifunza na usiache.

4. Fuatilia biashara yako kwa ukaribu sana.
Ni vyema kutambua upo umuhimu wa wewe kuifatilia biashara yako kwa ukaribu sana kuliko unavyofikiri. Acha kufanya sana biashara yako kwa simu, kuwa karibu nayo.

Hata pale inapotokea umeajiri watu wengine, hiyo isiwe eti ndio basi kila kitu kimeishia hapo. Upo ulazima pia wa wewe kufatilia hatua zingine nazo kwa ukaribu zaidi kila wakati.

5. Kataa kushindwa mapema.
Kukutana na magumu katika kitu chochote ni jambo la kawaida. Sasa najua wewe ni mjasiamali mkomavu jipe ahadi kwamba hata ikitokea magumu vipi, kukata tamaa mapema  lisiwe jambo rahisi kwako.

Kila wakati ukijifunza kutumia funguo hizi tano za mafanikio katika safari yako ya mafanikio utafanikiwa.

Hii Ndiyo Sababu Kwa Nini Utangaze Biashara Yako



Watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mbalimbali ambayo yanahusiana na masuala ya kibiashara. Na miongoni mwa maswali ambayo wamekuwa wakiniuliza ni kuhusu ni nini faida ya kutangaza biashara kwa sehemu kubwa?

Swali hili ndilo limenifanya nishike kalamu yangu ili niweze kulijibu. Nakusihi twende sambamba ili niweze kueleza kwa kinagaubaga, kwa nini unapaswa kuitangaza biashara yako tena kwa nguvu zote.
Matangazo ni usambazaji wa taarifa  sahihi  kuhusu bidhaa au huduma kutoka kwa mfanyabiashara kwenda kwa mteja. Matangazo ndiyo roho ya biashara, kwani bila kufanya biashara yako bila matangazo ni sawa na bure.

Nafikiri pia utakubaliana nami ya kuwa ili uweze kufanya biashara  yenye tija ni lazima uitangaze biashara yako, kwani " biashara ni matangazo".  Matangazo ndiyo yatakuyokufanya uweze kuongeza mauzo ya kibiashara kila wakati.

Kwa kuzingatia hilo unaweza kuitangaza biashara yako kwa njia ambayo itakuwa ni rahisi kwako. Na sababu kubwa ya kuitangaza biashara yako ni kuongeza wateja wapya.

Leo na dhumuni kubwa la kutangaza biashara yako ni kukutana na na watu wapya,  ukiona umetangaza biashara yako na hakuna mteja mpya hata mmoja ujue fika kuna mahala ambapo umekosea.

Hivyo fanya tathimni upya na ujipange upya na kuona ni jinsi gani unaweza kuitangaza biashara hiyo. Vile vile katika upangaji wa malengo ya kibiashara hakikisha ya kwamba unapanga na mbinu za kukutana na watu wapya kila siku.

Nasisitiza juu ya kukutana na watu wapya, kwa sababu nimegundua ya biashara nyingi zimekuwa hazifanyi vizuri kwa sababu zimekuwa na watu ambao wanaizunguka biashara ile ni wale wale kila siku. Hivyo kila siku fanya tathimini juu wateja wapya ambao wamekuja katika biashara yako.

Asante kwa kutembelea mtandao huu wa dira ya mafanikio,  usisite kumshirikisha na mwingine ili aweze kujifunza

MAGAZETI YA LEO 2/11/2017

Friday, 1 December 2017

Audio | Nyashinski – Hayawani | Mp3 Download

Audio | Nyashinski – Hayawani | Mp3 Download

Audio | Nyashinski – Hayawani | Mp3 Download


                                                 DOWNLOAD HERE

Audio | Sholo Mwamba – Kama Ronaldo | Mp3 Download

Audio | Sholo Mwamba – Kama Ronaldo | Mp3 Download

Audio | Sholo Mwamba – Kama Ronaldo | Mp3 Download


                                                              DOWNLOAD HERE

Audio | Diamond Platnumz Ft. Rick Ross – WAKA | Mp3 Download

Audio | Diamond Platnumz Ft. Rick Ross – WAKA | Mp3 Download

Diamond Platnumz Ft. Rick Ross - WAKA

Audio | Diamond Platnumz Ft. Rick Ross – WAKA | Mp3 Download


                                                     DOWNLOAD HERE

Umeme wakatika karibia nchi nzima kuanzia jana



Dar es Salaam. Wakati umeme ukiwa umekatika nchi nzima kuanzia jana Alhamis, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema huduma hiyo imeanza kurejea kwenye mikoa ya Iringa, Dodoma na Tanga.

Akizungumza leo Ijumaa, Desema 1, 2017, Kaimu Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Leila Mhaji amesema umeme umekatika katika mikoa yote iliyounganishwa katika gridi ya Taifa.

Amesema wataalam wa shirika hilo wanaendelea kurekebisha mifumo ya gridi ya Taifa ili kufanya matengenezo ya hitilafu iliyotokea.

“Marekebisho ya mafundi wetu yamesababisha umeme kurejea katika mikoa ya Iringa, Dodoma na Tanga,” amesema.

Amesema wataalam wamegundua mfumo wa gridi haujatengemaa vizuri na hivyo wanaendelea na kazi ya kurekebisha usiku na mchana ili kuhakikisha huduma hiyo inarejea katika hali yake ya kawaida.

“Tutaendelea kuwapa taarifa na tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza,” amesema.

Amewatahadharisha wananchi kutokushika wala kukanyaga nyaya zilizokatika au kuanguka kwa kuwa ni hatari.

Ameitaja mikoa ambayo umeme haujakatika kuwa ni Kagera na Ruvuma ambayo haijaunganishwa na gridi ya Taifa.

Barcelona kuimaliza Livepool


Barcelona imemgeukia kwa mara nyingine kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho, safari ikimtengea Pauni 130 milioni na mshahara mnono.

Barcelone imerejea Liverpool kwa maa ya tatu, baada ya dau lake la awali kukataliwa na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Mbali na kutaka kumngoa kwa dau kubwa, Barcelona imepanga kumpa mshahara wa Pauni 137,000 kwa wiki ili kupata saini ya nyota huyo katika dirisha la usajili Januari, mwakani.

Barcelona imemuweka sokoni mchezaji Arda Turan ili kupata fedha za kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Brazil.

Endapo Barcelona itakosa saini ya kiungo huyo, imesema itamfuata katika usajili ujao wa majira ya kiangazi. Paris Saint Germain (PSG) nayo imejitosa kuwania saini ya Coutinho.

Nafasi za kazi leo Dec 1

TBA yasimamia Tanesco kuondoa vifaa vyao



Dar es Salaam. Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye amepewa kazi ya kubomoa jengo la Tanesco Ubungo, leo Ijumaa ameanza kusimamia shirika hilo litoe madirisha, vitu pamoja na viyoyozi ili waanze kazi ya kubomoa kama ilivyoagizwa na Rais John Magufuli.

TBA imechelewa kuanza ubomoaji wa jengo hilo baada ya Tanesco kuomba waondoe wenyewe madirisha, milango na AC, kazi ambayo amepewa kuifanya mpaka leo Ijumaa jioni kabla ya ubomoaji kuanza.

Akizungumza na gazeti hili leo Ijumaa wakati uondoaji wa madirisha ukiendelea, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Mhandisi Elius Mwakalinga amesema kazi waliyonayo ni kubwa lakini wamejipanga kuikamilisha kwa wakati.

"Mpaka sasa hatujapata mchoro wa jengo hili baada ya kujengwa, tunachofanya ni kupima na kuchora ili kuepusha madhara. Unaweza ukakata bomba la gesi hapa ikawa shida tena," amesema Mwakalinga.


Amesema suala kubwa wanalolizingatia kwenye ubomoaji huo ni usalama na kwamba watatoa mafunzo maalumu kwa wafanyakazi kuhusu kujikinga wakati kazi hiyo ikiendelea.

Amebainisha kwamba watabomoa jengo la mbele pekee bila kuathiri lile la nyuma. Hata hivyo, amekiri kwamba jengo litakalobaki litakosa mwonekano mzuri kwa sababu sehemu ya mbele inayobeba sura ya jengo itakuwa imeondolewa.

"Tutatumia teknolojia mbili katika kubomoa jengo hili ambazo ni manual na mechanical. Tungeweza kutumia njia ya kulipua lakini tumeona itaathiri shughuli nyingine za kiuchumi," amesema.

Mwakalinga amesema athari zitakazojitokeza wakati wa ubomoaji ni kelele pamoja na vumbi. Amesema wamefanya tathmini ya jengo na kuangalia athari za mazingira na kujiridhisha kwamba ni chache.

Kuhusu gharama za ubomoaji, Mwakalinga amebainisha kwamba bado hawajakubaliana kuhusu hilo lakini watakaa na Tanesco kuzungumza kuhusu gharama hizo.

"Sheria ya manunuzi ya umma inasema ukishampa mtu kazi bila kutangaza tenda mnapata fursa ya kukaa na kujadili gharama wakati kazi inaendelea. Kwa hiyo, tutakaa na kuzungumzia hilo, hii ni taasisi ya umma na agizo limetoka kwa Rais," amesema Mwakalinga.

Mke wa Kafulila kafunguka



November 30, 2017 Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA Jesca Kishoa ambaye pia ni Mke wa Mbunge wa zamani Kigoma Kusini David Kafulila amekuwepo kwenye headlines kwa zaidi ya wiki moja baada ya Kafulila kuhamia CCM na kumuacha CHADEMA.

Kupitia page yake ya Instagram Jesca ameandika yafuatayo…

UCHAGUZI HUU WA UDIWANI UTOSHE 
KUTOA PICHA HALISI YA TAIFA HILI KWA SASA.

Mungu katunyima binadamu kujua siri nyingi za dunia hii ili turudi kwake na kumtambua yeye peke yake kama Mfalme wa ulimwengu.

Ametunyima kuchagua wazazi wa kutuzaa (maana uwenda wengine wangetaka kuzaliwa na watu wa aina ya Trump au Dangote,) ametunyima kuchagua wapi pa kuzaliwa (maana wengine uwenda wangetamani kuzaliwa ulaya na sio Tanzania)

Ametunyima kuchagua malezi ya kulelewa na ndio maana kwa mazingira yoyote watoto wamekuwa wakiishi kutegemeana na mazingira ya wazazi.

Lakini Mungu ametupa nguvu moja kubwa ambayo ikitumika vema huleta matunda mema na majibu ya mambo yote niliotaja juu, Mwenyezi Mungu katika maandiko matakatifu amezitambua Serikali za wanadamu na kupitia hizo endapo kutapatikana viongozi sahihi waliochaguliwa na wengi, ambao kwa uwingi huo ni alama au tafsiri ya chaguo la Mungu, hakika nchi itaneemeka na itatulia.

Ikiwa kinyume chake kwamaana ya alieshinda kuanzia mbinguni sie aliepewa ushindi duniani hakika mambo hugeuka kuwa laana na mateso kwa viumbe wa Mungu, Anguko la Madiwani au Wabunge wanaoshinda chaguzi sio la kwao peke yao na vyama vyao ni anguko la watu wa Mungu waliopaza sauti zao kwa unyenyekevu kupitia sanduku la kura.

WOTE KWA PAMOJA TUKEMEE VIKALI UPINDISHAJI WA MATOKEO BILA KUJALI WEWE NI NANI NA UNA UHUSIANO GANI NA SIASA ZA NCHI ILI KULIOKOA TAIFA HILI.

Roho mtakatifu ana uwezo mkubwa na nafasi kubwa ya kunyoosha mambo sawasawa, ungana na mimi katika maombi maalum juu ya taifa hili usiku huu kabla hujalala popote ulipo – hayo ndio aliyoyaandika Jesca.


Wakwanza kupandikizwa Figo Muhimbili Aruhusiwa


Dar es Salaam. Mgonjwa wa kwanza kupandikizwa figo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prisca Mwingira  ameruhusiwa kurudi nyumbani leo Ijumaa baada ya kuwa chini ya uangalizi wa jopo la madaktari bingwa wa figo kwa siku 10.

Prisca (30) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mikese mjini Morogoro, amechangiwa figo na mdogo wake Batholomeo Mwingira (27).

Akizungumza na vyombo vya habari leo Ijumaa mara baada ya kutoka chumba cha uangalizi maalum (ICU), Prisca ameishukuru Serikali kugharamia matibabu yake na kuiomba kuwekeza zaidi katika matibabu ya kibingwa ili kusaidia Watanzania wengi wasio na uwezo wa kufuata gharama nje ya nchi.

“Kwa kipekee napenda kumshukuru sana ndugu yangu, kaka yangu Batholomeo kwa kupenda niendelee kuishi. Madaktari bingwa wa figo Muhimbili tangu wamenipokea wamekuwa wakinipa matibabu mbalimbali, nimesafishwa damu kwa muda wa mwaka mmoja wamenishauri na mpaka katika matibabu ya kupandikiza figo nyingine,"


Serikali yakanusha haijatoa ruhusa chuo kikuu huria kutoa kozi ya foundation



Singida. Serikali imesema  haijatoa ruhusa  Chuo Kikuu Huria (OUT) kiendelee kutoa kozi ya ‘Foundation’ kama ambavyo imedaiwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii.

Baadhi ya mitandao imetoa taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho: “Waziri Mkuu aruhusu kozi za 'Foundation' Chuo Kikuu Huria” kwa madai kuwa alitoa ruhusa hiyo jana (Alhamisi, Novemba 30, 2017) wakati akiwa mkoani Singida ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu hicho.

Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Singida waliohudhuria mahafali ya 33 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kanisa Katoliki mjini Singida, Waziri Mkuu amesema  Serikali bado inafanyia maboresho Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014.

“Kwa sasa Serikali inafanya maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo kwani sera tuliyonayo haifafanui vizuri jinsi ya kuwasaidia vijana wetu wajiendeleze kwa njia ya mfumo wa elimu huria na masafa,” amesema

“Programu kama zilizoelezwa na Makamu Mkuu wa Chuo za Foundation, zinahitaji pia kufafanuliwa kwenye sera yetu, ambayo kwa sasa wataalamu wetu wanaendelea kuiboresh’’amesema

Ameongeza kwamba ‘’ Pindi itakapokamilika, tutaitolea taarifa kwa Chuo Kikuu Huria na wataalamu wataweza kushirikiana na sekta zote ili kuhakikisha jambo hili linakwenda vizuri,” amesema

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifas Tozo Bisanda amesema wamepokea barua kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwaarifu juu ya nia ya Serikali kutaka kurejeshwa kwa kozi za Foundation katika chuo hicho.

“Tayari tumekwisha wasilisha mtaala wa Foundation ulioboreshwa ili kukidhi matakwa ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), na tunasubiri mrejesho kutoka Kamisheni baada ya kikao chao, mapema mwezi ujao,” amesema Prof. Bisanda.