Thursday, 23 November 2017

Tabia Ya Kuzoeana inavyoweza kuathiri maisha yako ya kimahusiano



kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa upande wa mwanamke kwa kutojali usafi wake, mavazi anayovaa, chakula anchopika, nidhamu ya nyumba na mpangilio kwa ujumla.

Matatizo mengi ndani ya nyumba yanaweza kusababishwa na moja au baadhi ya tabia hizo, ambazo huenda ikawa hazitokani na dharau, bali kuzoeana, kwa mfano, siku za mwanzo wa ndoa mwanamke huwa anajali sana usafi wa mwili wake, umaridadi wa nguo anazovaa, usafi wa nyumba na nidhamu ya hali ya juu, upishi wa chakula unaozingatia vionjo na ubunifu, mapokezi yenye bashasha na wakati mwingine hata kumkumbatia mumewe arudipo kutoka kazini.

Lakini baada ya kuzoeana yote hayo hubadilika, mwanamke huhisi kuwa hana jipya la kumuonyesha mumewe, hujiona wameishakuwa watu wazima sasa, na mara nyingi utakuta mwanamke huyu anashinda na sare (uniform) moja kuanzia asubuhi hadi anapopanda kitandani usiku, mambo ya Hinna, nguo za fashion, salon, manukato, kujipamba na dhahabu huyafanya pale anapotoka kwenda harusini na sio nyumbani. Huku ndio kuzoena, na tafsiri sahihi ni kudharau.

Hivyo ili kulinda kibarua cha chako cha mahusiano ni vyema ukajifunza kila wakati kutofanya vitu ambavyo vimekuwa havijayajengi mahusiano yako.

Asante kwa kuwa msomaji wa Muungwana Blog.

Ukipata mwanamke mwenye sifa hizi 16 usimwache




Hizi ni sifa halisi za mwanamke wa kweli

1. Ni nguvu ya mwanaume
2. Ni jasiri
3. Mchapakazi
4. Mwenye kujiamini
5. Tegemeo la familia
6. Mwalimu wa watoto na familia yake kiujumla
7. Mlinzi wa mwanaume.
8. Chanzo cha baraka ya familia.
9. Adui wa maadui wa familia.
10. Sauti ya familia.
11. Mponyaji wa familia yake na taifa.
12. Mlezi wa huduma.
13. Mkombozi wa familia na taifa.
14. Msaidizi wa Mungu tumfanyie msaidizi wa kufanana naye.
15. Mwombezi wa familia, huduma na taifa.
16. Mficha siri wa Mungu

Mwanamke Kama Unatabia Hii Basi Neno Ndoa Utalisikia Kwenye Bomba






Hivi unajua kwanini mahusiano mengi katika karne hii yanakufa sana ukilinganisha na miaka ya zamani? Nini ambacho kimetokea miaka ya hivi karibuni? Naomba utafakari kwa muda usiopungua dakika tano kisha majibu ubaki nayo.

Binafsi leo sikuja kwa leo ya kuzungumzia sababu hizo, ila leo nataka niseme  na wanawake wote wenye tabia ya kupenda ganda la ndizi kuteleza, unawajua wanawake wenye tabia za aina hii kwa watalam wa masuala ya mahusiano wamewapa jina jipya ambalo ni magolipa.

Wao kazi yao kubwa ni kusubiri wanaume zao waende kutafuta ili hali wao wamekaa nyumbani wakisubiri kuletewa, wanawake wa aina hii kiufupi ukiwachunguza kwa umakini huwa hawana uchu wa mafanikio na maendeleo hata chembe. Na wanawake wa aina hii huwa wana uhusiano mzuri na romote control za tv.

Nataka nikuibie siri wewe mwanadada mwenye tabia ya aina hii, hivi unajua wanaume wengi katika utawala huu wa sizonje  hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani ‘golikipa’? kama ulikuwa hujui basi leo nakupa makavu live.

Hivi unajua  Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa, kusugua miguu akimsubiria mwanaume arudi akutelee, sasa hivi imepitwa na wakati? Kama ulikuwa hujui basi leo nakupa ukweli wako bure pasipo kuchangia hata mia mbovu.

Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.

Kabla sijamaliza kicheni part ya  leo nataka kukwambia ya kwamba maisha ni kutafuta, punguza kufanya vitu visivyokuwa wa maana katika maisha yako,punguza muda wa kukaa vibalazan huku macho yakikutoka huku kazi ikiwa ni kuwasema watu wengine.

Wewe ni mtu mzima mwenye meno 32, una akili timamu buana, tafuta shughuli za kufanya ambayo itakufanya uweze kujikiingizia kipato, binafsi naamini unaweza kwani ule msemo wa wahenga wapya ya kwamba wanawake wanaweza upo kwa ajili yako.

Jifunze kupambana na hali yako kama young killer muhasisi ya hip-hop asemavyo. Kukaa ukimsubiri shemela akuletee sio mpango mzima pia nidhambi na chukuzi kwa mwenyezi mungu.

Punguza kilo tano kwa siku saba




NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha maradhi mbalimbali bali pia mwonekano wako unakuwa si mzuri. Makala haya yanaeleza namna ya kupunguza unene ndani ya siku saba.

Siku ya 1: Asubuhi kula matunda (lakini usile ndizi). Mchana chemsha kabichi, weka chumvi kidogo na nyanya, chemsha na upate supu. Kula mchanganyiko huo na utajiona umeshiba. Jioni kula tikiti maji na mbogamboga au kabichi uliyotengeneza mchana.

Siku ya  2: Kula mboga za majani asubuhi (usile mboga za majani zenye wanga kama karoti).  Mchana kula kabichi iliyochemshwa, tengeneza na kachumbari. Katika kabichi weka chumvi, pilipili na mafuta ya olive.  Jioni unaweza kula mlo kama wa mchana lakini unaweza kukaanga mboga nyingine za majani.

Siku ya 3: Kula mboga za majani na matunda, unaweza kuongeza kiazi kitamu kimoja.

Siku ya nne 4: Kula ndizi moja na unywe na maziwa ya mtindi wakati wa asubuhi. Mchana kula kabichi kama ulivyoitengeneza kwenye siku ya kwanza, usiku rudia mlo wa mchana.

Siku ya  5: Kula nyanya nne pamoja na samaki au kipande cha kuku asubuhi. Mchana unaweza  kula samaki wa kuchemsha kiasi ambaye amechanganywa na nyanya.  Wakati wa jioni unaweza kula chakula kama cha mchana.

Siku ya 6:  Unaweza kula chakula cha protini na mboga za majani. Anza kwa kula kachumbari asubuhi. Mchana kula tambi kiasi na kipande kidogo cha samaki. Usiku tengeneza supu ya kabichi.

Siku ya 7: Anza kwa matunda na juisi. Mchana kula mboga za majani na usiku kula supu ya kabichi na kiazi kimoja.

Kumbuka: Unatakiwa kunywa maji angalau glasi nne kila siku. Usiendelee kwa muda mrefu, kumbuka dayati hii ni ni kwa siku saba. pekee.

Jinsi ya Kuepuka Kunuka Mdomo



Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla. Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni uondoa haiba ya kupendwa kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea moja kwa moja na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni mwako.

Chakula unachokula kina athiri hewa inayotoka mdomoni au sehemu nyingine za mwili wako. Baadhi ya vyakula vina matokeo mabaya sana kwa hurufu unayotoa mdomoni. Harufu mbaya mdomoni si ugonjwa wa kuambukiza haina haja kuogopa ukikutana na mtu mwenye harufu mbaya mdomoni kwamba atakuambukiza.

Pia tatizo kubwa ni kwamba watu wenye harufu mbaya mdomoni hawajijui kwamba wana harufu mbaya. Asilimia 85 - 90% ya tatizo la harufu mbaya mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi).

Harufu nyingi mbaya mdomoni hutokana na vyakula vyenye asilia ya protein. Kuna zaidi ya aina 600 ya bacteria wanaoishi kwenye kinywa cha Binadamu (sehemu ya juu ya ulimi, fizi na kuzunguka meno).

KINACHO SABABISHA HARUFU MBAYA MDOMONI
Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kama vile kupiga mswaki vizuri kunakoacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya mdomoni. (Wengi hupiga mswaki haraka haraka na kuacha mabaki ya chakula). Maambukizi ya magonjwa kama vile fizi kutoka damu, mfumo wa upumuaji na kisukari. Kinywa kuwa kikavu kutokana na madawa (medications) Kuvuta sigara, kunywa kahawa, ulaji wa vyakula vyenye viungo vikali kama vile vitunguu maji au thaumu.

NAMNA YA KUJUA KAMA UNA HARUFU MBAYA MDOMONI
Wanasayansi wamekiri kwamba ni ngumu sana mtu kujijua mwenyewe kama ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea (habituation).

Ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine. Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu unayemuamini.

Pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa. Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama Halimeter, Gas Chromatography na BANA Test.

NAMNA YA KUJILINDA NA HARUFU MBAYA MDOMONI (TIBA) 
Kula vyakula vyenye afya na vyakula ambavyo wakati unakula vinaweza kusafisha kinywa vizuri. Kusafisha meno mara kwa mara au kwa uchache mara mbili kwa siku asubuhi na baada ya mlo wa usiku, hii usaidia kuondoa au kujikinga na harufu mbaya mdomoni.

Vilevile unashauriwa kutumia KISAFISHA ULIMI (tongue cleaner) kusafishia ulimi wako. Tumia bazooka (chewing gum) ambazo husaidia kuongeza kiasi cha mate kwenye kimywa kilichokauka.

Baadhi ya gums zina viungo vinavyoondoa harufu mbaya mdomoni na zingine husafisha kinywa na bacteria wanaosababisha harufu mbaya. Tumia dawa ya kusukutua mdomoni (mouthwash) kabla ya kulala usiku. Kuwa makini na afya ya kichwa chako kama vile kupiga mswaki vizuri, kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno na kumuona daktari kila unapoona una Matatizo ya meno au kinywa au kila baada ya miezi sita kwa uchache.

Kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku angalau glass mbili za maji.
Mwone daktari wako ukiona una tatizo la harufu mbaya mdomoni.

NAMNA YA KUJIKINGA NA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI!
Watu wengi husumbuliwa na tatizo la kunuka mdomo bila hata kujijua hivyo kuwa kero kwa wenzao na wakati mwingine hujishushia hadhi mbele ya jamii. Mara nyingi ugonjwa wa kunuka mdomo (Halitosis) husababishwa na uchafu wa kinywa na ulaji wa vyakula usiosahihi lakini ni tatizo linalotibika.

Ni rahisi kulizuia na kuliondoa tatizo la kunuka mdomo iwapo utaamua kufuata kanuni za usafi wa kinywa na unywaji wa maji kwa kufuata kwa makini muongozo ufuatao:

KUPIGA MSWAKI
Kitu cha kwanza kufanya ni kupiga mswaki kwa ukamilifu kila uamkapo asubuhi. Wakati wa kupiga mswaki, utatakiwa siyo tu kusugua meno, bali pia ulimi, sehemu ya katikati hadi karibu na koromeo kwa kusugua vizuri.

Vile vile kila uamkapo baada ya kulala mchana au jioni, hakikisha unapiga mswaki, kwani bakteria wa kinywani, hutawala kinywa kila ulalapo. Mara baada ya kupiga mswaki na kusugua ulimi sawaswa, hakikisha unasukutua vizuri kwa maji, kwani hapa ndipo baadhi ya watu hukosea kwa kupiga mswaki bila kusukutua kwa maji.

KUNYWA MAJI MENGI
Maji ni muhimu sana karibu kila eneo la mwili wa binadamu. Unywaji wa maji ya kutosha kila siku utakusaidia kudhibiti na hatimaye kuondoa tatizo la kunuka mdomo. Unywaji wa maji mengi ni muhimu, hasa kwa wale watu wenye ugonjwa wa kukauka midomo (xerostomia).

Mara nyingi harufu itokayo mdomoni, hutokea tumboni na siyo kinywaji peke yake kama unavyoweza kudhani. Hivyo, kama tumbo litakuwa chafu, hata kama utasafisha kinywa vizuri bado harufu mbaya inaweza kuendelea kutoka. Harufu mbaya ya tumboni hutokea pale tumbo linapokuwa chafu kutokana na kutopata choo kwa muda mrefu. Miongoni mwa mambo yanayochangia kukosekana kwa choo kwa muda mrefu ni pamoja na tabia ya kutokunywa maji ya kutosha kwa siku, hivyo hakikisha unakunywa maji, kiasi kisichopungua lita moja na nusu hadi mbili au zaidi, kutegemeana na kazi unazozifanya.

Ukiwa na tatizo la kukaukiwa maji mwilini kila mara, mwili hujaribu kutumia njia zake za kiasili kupunguza uzalishaji wa mate ili kuhifadhi maji kwa ajiili ya matumizi mengine, kitendo hicho huchangia kunukisha mdomo kwa sababu ndani ya mate huwa kuna kinga muhimu dhidi ya baktetria wanaonukisha kinywa.

Kwa upande mwingine, ili kuzuia kinywa kunuka pale mdomo unapokuwa umekaukiwa na mate, ni vizuri kutafuna vitu kama bazooka (chewing gum) yoyote ili kuzalisha mate ambayo huhitajika katika kudhibiti bakteria.

MWISHO: Hakikisha unasukutua sawaswa baada ya kula chakula chochote, hata kama ni juisi isipokuwa unapokunywa maji tu ya kawaida. Bila shaka, ukizingatia haya, tatizo ulilonalo la kunuka mdomo litataoweka na kubaki historia.

DR SHIKA AENDA KUPIMA TEZI DUME SIKIA ANACHOSEMA


Rostam ft Maua Sama - Kiba_100 [Official Music Video]


BREAKING: Nyumba za Lugumi kupigwa mnada tena, masharti yatajwa


Mhasibu feki atiwa mbaroni kwa wizi wa Tsh. 873,000


Na Nathaniel Limu, Singida
 Mhasibu wa hospitali ya mkoa mjini Singida aliyeachishwa kazi kwa kosa la kumiliki vyeti feki, Edith Talasi (49) mkazi wa Minga,anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kuvunja milango ya ofisi yake ya zamani na kuiba shilingi 873,000 taslimu, kwa kutumia funguo bandia.

Talasi  ambaye imelelezwa kwamba alifanya kazi hospitalini hapo kwa  muda na baadaye alirejeshwa kwenye kituo chake cha kazi manispaa ya Singida,kwenye wizi huo, alimshirikisha mlinzi wake wa nyumba ya kulala wageni Nandau, Antony Felix (51).Mlinzi huyo naye anashikiliwa na polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, ACP Debora Magiligimba, alisema tukio hilo limetendeka Novemba, 21 saa 6.30 usiku huko katika hospitali ya mkoa mjini hapa.

Alisema siku ya tukio muuguzi wa zamu Shamir Omari (27) akitokea maeneo ya mapokezi akielekea wodini, alimwona mtu akiwa amesimama karibu na ofisi ya mhasibu, alisimama akamsalimia na mtu huyo aliondoka.

“Muuguzi huyo aliamini kuwa mtu aliyemwona,huenda alikuwa  mgonjwa au mtu aliyeleta mgonjwa hospitalini.Lakini aliporudi,alimwona mtu yule yule amerudi eneo lile lile, kitendo kilichopelekea amshuku kuwa sio mtu mzuri,” alisema kamanda huyo.

Alisema muuguzi huyo baada ya kumtilia shaka mtu huyo, alitoa taarifa kwa mlinzi wa zamu wa hospitali hiyo, Abubakari Jumanne,ambaye alimweka chini ya ulinzi mtu huyo.

ACP Magiligimba alisema hata hivyo mtu huyo alijitetea kuwa amefika hospitalini hapo, kwa ajili kuchoma sindano na kuonyesha dawa ya unga na kichanganyio chake.

“Wakati wanaendelea na mahojiano hayo,waliona makufuli  mawili ya mlango wa nje/grili yapo chini na mlango huo wa chuma upo wazi. Mtuhumiwa mlinzi Antony alieleza kuwa bosi wake (mtuhumiwa Edith) kwa wakati huo,alikuwa ndani ya ofisi ya mhasibu amejifungia ndani,” alisema.

 Akifafanua  alisema  jeshi la polisi baada ya kupata taarifa ya wizi huo, liliweza kufika eneo la tukio na kukuta mlango wa ndani ukiwa umefungwa kwa ndani.

“Walipoamuru mhasibu afungue mlango huo kwa kutumia funguo zake,walimkuta mtuhumiwa (Edith) akiwa amejibanza kwenye kona ya mlango na watumishi wa hospitali hiyo, waliweza kumtambua. Alipohojiwa ameingiaje humo ndani,alionyesha funguo saba (07) na zilipojaribiwa ziliweza kufungua milango yote ya ofisi ya mhasibu,” alisema Magiligimba.

Alisema pamoja na wizi huo wa shilingi 873,000,imeelezwa kwamba aprili mwaka huu,wahasibu wa hospitali hiyo,walibaini upotevu wa shilingi 1,800,000.Oktoba mwaka huu,pia walibaini upotevu wa shilingi 3,600,000.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. David Mwasita,amekiri kutokea upotevu huo lakini wahasibu katika wakati huo,waliweza kuziba upotevu huo, kwa fedha zao za mishahara.

Ameeleza kuwa wahasibu hao walilazimika kutoa fedha zao binafsi, na wasingeweza kutoa taarifa ya upotevu huo, kwa vile milango na kasiki, ilikuwa imefungwa kama kawaida.

ACP Magiligimba amesema kwa sasa wanaendelea kuwahoji watuhumiwa hao na baada ya kumalizika kwa mahojiano hayo,watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.






GodBless Lema Amtaka Kafulila Amshauri Mkewe Naye Ajiondoe CHADEMA



Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA Godbless Lema, amefunguka kuhusu kitendo cha David Kafulila kuhama CHADEMA na kusema ana amini atamshauri mke wake naye afuate nyayo zake.

Kwenye ukurasa wake wa twiter Godbless Lema ameandika ujumbe akisema Kafulila ni rafiki yake wa karibu, lakini kwa namna alivyoamua hana shaka atamshauri mke wake ambaye ni mbunge kupitia chama cha CHADEMA, kufanya kama yale aliyoyafanya.

"David Kafulila ni rafiki yangu, nafikiri kwa namna hii alivyoamua ataweza bila shaka kumshauri Mbunge wa Chadema, Jesca Kishoa (mke wake) kufikiri kama yeye, hii inaweza kusaidia maoni yake juu ya uamuzi aliouchukua leo na kuthibitisha ukweli huu kama hupo", ameandika Godbless Lema.

Jana David Kafulila ametangaza kukihama chama cha CHADEMA akidai vyama vya upinzani havina nia ya kupambana dhidi ya ufisadi, lakini mke wake Jesca Kishoa ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA bado hajazungumza chochote.

Mchezaji wa Everton afungiwa mechi mbili



Mshambuliaji wa Everton Oumar Niasse amepigwa marufuku ya mechi mbili kwa kupatikana na hatia ya kujirusha.

Mshambuliaji huyo wa Senegal ni mchezaji wa kwanza katika ligi ya Uingereza kupewa adhabu chini ya sheria za shirikisho la soka nchini Uingereza ambazo zilizinduliwa mnamo mwezi Mei.

Niasse alikabidhiwa penalti iliozua utata na refa Ccott Dann wakati wa mechi ya Jumamosi ambapo timu yake ilitoka sare ya 2-2 dhidi ya Crystal Palace.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atakosa mechi ya Everton dhidi ya Southampton siku ya Jumapili na ile ya nyumbani dhidi ya West Ham tarehe 29 mwezi Novemba.

Tume huru ya shirikisho la soka nchini Uingereza ilitoa uamuzi huo kwa pamoja katika kumpata na hatia mchezaji huyo wakati ilipokutana siku ya Jumatano.

Niasse alikana kufanya makosa, hatua iliosababisha penalti kukabidhiwa katika dakika ya tano ya mchezo.

Leighton Baines alifunga mkwaju huo kabla ya Niasee kuifungia timu yake goli la kusawazisha katika uwanja wa Selhurst Park.

Lema afunguka kuhusu Kafulila



Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA Godbless Lema, amefunguka kuhusu kitendo cha David Kafulila kuhama CHADEMA na kusema ana amini atamshauri mke wake naye afuate nyayo zake.

Kwenye ukurasa wake wa twiter Godbless Lema ameandika ujumbe akisema Kafulila ni rafiki yake wa karibu, lakini kwa namna alivyoamua hana shaka atamshauri mke wake ambaye ni mbunge kupitia chama cha CHADEMA, kufanya kama yale aliyoyafanya.

"David Kafulila ni rafiki yangu, nafikiri kwa namna hii alivyoamua ataweza bila shaka kumshauri Mbunge wa Chadema, Jesca Kishoa (mke wake) kufikiri kama yeye, hii inaweza kusaidia maoni yake juu ya uamuzi aliouchukua leo na kuthibitisha ukweli huu kama hupo", ameandika Godbless Lema.

Hii leo David Kafulila ametangaza kukihama chama cha CHADEMA akidai vyama vya upinzani havina nia ya kupambana dhidi ua ufisadi, lakini mke wake Jesca Kishoa ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA bado hajazungumza chochote.



Mladic ahukumiwa maisha jela kwa mauaji ya kimbari Bosnia



Kamanda wa zamani wa jeshi la Boznia Jenerali Ratko Mladich amehukumiwa maisha jela na Mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu wa kivita-ICC.

Mladich alipatikana na hatia ya kutekeleza mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita pamoja na dhulma dhidi ya binadamu katika iliyokuwa utawala wa Yugoslavia.

Hukumu imepokelewa kwa hisia tofauti.

Kundi la wamama wa Srebrenitsa, limesema kuwa limefurahishwa mno na hukumu hiyo.

Lakini mwanamke mmoja Muislamu raia wa Boznia, ambaye wavulana wake wawili na mumewe waliuwawa katika vita hivyo, ameiambia bbc kuwa Bwana Mladich anastahili hukumu kubwa na kali zaidi.

Mwaandishi wa BBC huko Sarayevo, anasema kuwa watu wengi walitaka ahukumiwe kwa mauwaji yote yaliyotokea kote Boznia na wala sio eneo moja pekee.