Tanzania\'s leading online News Edition (The National Newspaper). Get access to the most current and latest authoritative news on local issues, politics, events, celebrations, editorial, columnists, features, people and business.
Wednesday, 22 November 2017
Clouds FM yapigwa faini ya Tsh milioni 12

MAMLAKA ya udhibiti wa mawasiliano nchini (TCRA) imekitoza kituo cha redio cha Clouds FM faini ya shilingi milioni 12 ikiwa ni pamoja na kupewa onyo kali kwa sababu ya kukiuka maudhui na kanuni za utangazaji kupitia vipindi vya Jahazi na XXL
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema Clouds FM imetozwa shilingi milino tano kwa kosa la kukiuka misingi na maudhui ya utangazaji kupitia kipindi cha Jahazi kwenye kipengele cha Mastori ya Town, shilingi milioni tano kupitia kipindi cha Jahazi kipengele cha Najua Wajua na shilingi milioni mbili kupitia kipindi cha XXL.
“Hata hivyo, tunaitaka Clouds Media Group kuwaomba radhi wasikilizaji wa vipindi hivyo kwa siklu tatu mfululizo na pia tunautaka uongozi wa Clouds Media Group kuwachukulia hatua za kinidhamu watangazaji wanaokiuka maadili, miiko na kanuni za utangazaji,” alisema Mapunda.
Masha afunguka baada ya kuruhusiwa Kurudi CCM Leo

Lawrence Kego Masha, aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amesema kuwa amefurahi sana kupewa ridhaa ya kujiunga rasmi na CCM leo, Novemba 21, na kwamba atahakikisha anakitumikia ipasavyo.
“Nimefurahi sana kwamba nimepewa ridhaa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi pamoja na Halmashauri Kuu kurejea nyumbani, kurejea CCM. Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kufuata ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuhakikisha kwamba nakitumikia chama na kulitumikia taifa jinsi inavyotakiwa. Kidumu Chama cha Mapinduzi,” amesema Masha.
Wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu cha CCM kinachoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais Magufuli, Masha alieleza kuwa yeye ni kada wa CCM tokea zamani kwani alilelewa na kukulia CCM, hivyo yeye kurudi CCM ni kama kurudi nyumbani na anajuta kufanya maamuzi ya kukihama chama hicho huku akitaka kutumiwa ili kukiendeleza chama hicho na kukiletea maendeleo.
“Mwaka 2015 nilifanya maamuzi ambayo sina sababu ya kueleza sana, nimezaliwa ndani ya chama hiki, nilipohama ilibidi nimfiche mzee Masha, akanipigia simu akanuliza umefanya nini? nikamuuliza kwani wewe chama gani? akaniambia mimi nilifukuzwa we umehama, amefurahi sana juzi nilipomwambia narejea CCM, Mheshimiwa Mwenyekiti na kamati yako, naomba mnikubali, naahidi nitakuwa mwaminifu kwa chama cha Mapinduzi na serikali yake, ukinihitaji nitumie“, amesema Lawrence Masha.
Masha ambaye alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mwaka 2015 akitokea CCM, alitangaza tena kukihama CHADEMA hivi karibuni kwa madai kuwa upinzani hauna nia ya dhati ya kutafuta nafasi ya kuunda serikali, badala yake umejikita katika kuikosoa serikali.
Wasanii wa Tanzania wasababisha kufungwa kwa tamasha Kenya

Kundi la wasanii wa muziki wa Tanzania kutoka visiwani Zanzibar, Off Side Trick, wamesababisha kufungwa kwa tamasha la utamaduni la Lamu huko Mombasa nchini Kenya, baada ya kucheza mtindo usiofaa wenye kukiuka maadili.
Taarifa kutoka Mombasa zinasema kwamba kitendo hiko kililalamikiwa na wakazi wa eneo hilo, viongozi wa dini na viongozi wa utamaduni wa Kenya, baada ya kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea jukwaani na kulazimu tamasha hilo kufungwa.
Baadhi ya watu walijaribu kuwaonya kundi hilo kuacha kucheza michezo hiyo ya uchafu ambayo sio maadili lakini walijifanya kutosikia, na ndipo waandaaji wa tamasha na viongozi wa eneo hilo kupanda jukwaani na kuwashusha kwa nguvu .
Baada ya tukio hilo Mkurugenzi Msaidizi wa Nyumba ya Maonyesho wa Kenya, Bwana Athman Hussein, amesema kuna haja ya kuwahakiki wasanii kabla hawajapanda jukwaani, kwani kitendo hiko kimedhalilisha jamii ya hapo na mji wa Lamu kiujumla, kwani mji huo ni maarufu kwa utalii na pia uko chini ya Urithi wa dunia wa UNESCO.
Sergio Ramos kukosa mchezo wa Champions League

Michuano ya Champions League inaendelea tena wiki hii huku tayari timh mbali mbali zimeshatangaza vukosi vyao vitakavyosafiri kwa ajili ya mechi za wiki hii, Real Madrid ni moja kati ya timu zilizotangaza vikosi vyao.
Lakini mlinzi Sergio Ramos ameachwa nje ya kikosi cha Real Madrid kitakachocheza dhidi ya APOEL kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuvunjika pua yake kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya Atletico Madrid.
Kikosi cha kocha Zinedine Zidane kimeundwa na wachezaji: Casilla, Moha, Carvajal, Vallejo, Varane, Nacho, Marcelo, Theo, Achraf, Kroos, Modric, Casemiro, Marcos Llorente, Asensio, Isco, Caballos, Ronaldo, Benzema, Lucas Vazquez, na Borja Mayoral.
Majeruhi wengine ukiachana na Ramos ambae anatarajiwa kuwa nje ya kikosi hicho kwa siku kumi ni Keylor Navas na Gareth Bale huku taarifa nzuri ni juu ya urejeo wa Kovacic licha ya kutojumuishwa kwenye kikosi hicho.
Ufaransa yathibitisha kuwapokea wahamiaji kutoka Libya watakao safirishwa na UNHCR

Ufaransa yatangaza kuwa itawapokea wakimbizi wa kwanza watakao safirishwa na shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoka nchini Libya
Serikali ya Ufaransa imetangaza kuwa utawapokea wakimbizi na wahamiaji wa kwanza watakaosafirishwa na shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoka nchini Libya.
Taarifa zinafahamisha kuwa wakimbizi watakao pokelewa na Ufaransa ni raia 25 kutoka Erytrea , Sudan na Ethiopia.
Wakimbizi hao watapokelea mwanzoni mwa Januari mwaka 2018.
Taarifa hiyo ilitolewa na Pascal Brice mkurugenzi wa ofisi inayosimamia haki za wakimbizi baada ya mkutano uliofanyika Vovemba 20 mjini Niamey nchini Niger.
Wambura awapa somo waamuzi

Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Michael Wambura amesema, kuna uwezekano mkubwa Bara la Afrika, likatoa idadi kubwa ya waamuzi katika fainali za michuano mikubwa hususani Kombe la Dunia.
“Waamuzi wa Afrika wana uwezo, Ninyi wakufunzi ni wa kufanya waamuzi wetu kuwa na uwezo zaidi. Ni Aibu kwa Bara kubwa kama Afrika lenye nchi wanachama 54 wa FIFA kuwa na waamuzi wachache katika fainali za Kombe la Dunia”, amesema Wambura.
Wambura ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua kozi ya Wakufunzi wa Waamuzi kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika.
Kozi hiyo itafanyika kwa muda wa wiki moja kwenye ukumbi wa ILO jijini Dar es salaam, ikiwafua waamuzi hatua ya tatu ‘Futuro III’ ambapo jumla ya washiriki 58 kutoka nchi 26 barani Afrika wanashiriki kozi hiyo.
Kozi hiyo ina wakufunzi sita akiwamo Carlos Henriques na Dominic Chiellens wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). Wambura amesisitiza kuwa lazima kama bara waazimie kuwa na waamuzi wa kutosha katika fainali kubwa duniani.
Dr. Shika kushiriki kwenye video ya Dogo Janja?

Kila siku umaarufu wa Dk.Luis Shika unazidi kuongezeka na hata baadhi ya watu na makampuni wameanza kumtumia katika biahara zao, hii ni pamoj na picha zilizoanza kusambaa zikimuonyesha yupo na msanii wa muziki Dogo Janja.
Kutokana na picha ambazo zimeanza na zinaendelea kusambaa mtandaoni zikimuonyesha Dk.Shika au Mzee wa 900 Itapendeza akiwa katika muonekano wa kipapa na huku akiwa ana kula bata na warembo, jambo linalohisiwa kuwa huwenda kukawa na video mpya ya muziki kutoka kwa msanii Dogo Janja hivyo ametumika kama muhusika mkuu.
Dk. Luis Shika amejipatia umaarufu kutokana na sakata la kuuzwa kwa nyumba za mfanyabiashara Said Lugumu, ambapo aliingilia katikwa kutaja kiwango kikubwa cha pesa ili aweze kununua nyumba hicho ila cha kushaa baada ya kuibuka mshindi hakuwa na 25% za kumfanya aweze kuwa mmiliki halali wa nyumba hizo na kufanya polisi wamkamate na kumuweka ndani ambapo alitoka baada ya siku kadhaa na kuanza kupata umaarufu mara dufu.

200 waomba kujiunga CCM

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema kuna wanachama wa vyama vya upinzani 200 ambao wameomba kujiunga na CCM.
Akizungumza leo Jumanne wakati wa kutangaza majina ya viongozi wa mikoa na kitaifa walioomba nafasi mbalimbali za uongozi CCM, Polepole amesema wapinzani walioomba kujiunga na chama hicho wamo wabunge na wenyeviti.
Amesema sababu waliyotoa ya kutaka kuhamia CCM ni kutokana na chama hicho kushughulika na matatizo ya watu.
Polepole amesema chama kimewapokea wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani.
Amewataja wanachama hao kuwa ni Samson Mwigamba, Albert Msando na Profesa Kitila Mkumbo kutoka ACT-Wazalendo. Wengine na Lawrence Masha na Protobas Katambi wa Chadema.
"Tutawajulisha siku tutakapowapokea wanachama hawa wapya," amesema.
Mwananchi:
Breaking News: Rais Robert Mugabe amejiuzulu
Breaking News: Rais Robert Mugabe amejiuzulu

Katika dakika chache zilizopita , spika wa bung la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu . Kumekuwa na shangwe miongoni mwa wabunge kufuatia tangazo hilo. harakati za kumuondoa madarakani rais huyo kupitia bunge kumesitishwa.
VIDEO:Ruge afunguka baada ya Jengo la Clouds kuwaka moto full Video.

Moto uliozuka katika ofisi za Clouds Media Group na kusababisha Television na Radio Clouds kutokuwa hewani kwa muda, Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group amesema bado huduma ya vipindi nitaendelea kama kawaida.
Moto huo ulianza saa 4 asubuhi katika chumba kimoja kwenye ghorofa ya kwanza uliosambaa kwenye jengo la kampuni hiyo.

Hata hivyo hadi sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana.
Magari ya Zimamoto yapatayo manne yalifika eneo la tukio kwa ajili ya kuzima moto huo.
Aidha Ruge Mutahaba amewashukuru Zimamoto kwa kuweza kuokoa vifaa na kuzima moto huo.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE
Subscribe to:
Comments (Atom)




















