Tuesday, 21 November 2017

Real Madrid yamuacha Ramos




Nahoda wa Real Madrid Sergio Ramos ameachwa kwenye kikosi kilichosafiri kwenda nchini Cyprus kucheza na Apoel Nicosia leo kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Sergio Ramos alivunjika pua kwenye mchezo wa La Liga jumamosi iliyopita wakati timu yake ya Real Madrid ilipotoka sare ya bila kufunagana na Atletico Madrid kwenye uwanja wa Wanda Metropolitano.
Mlinzi huyo wa kati mwenye miaka 31, bado haijajulikana atarejea lini uwanjani. Ramos anaongeza idadi ya majeruhi kwenye timu hiyo akiwemo winga Gareth Bale pamoja na golikipa Keylor Navas.

Mabingwa hao watetezi wa UEFA wameshinda mechi moja tu katika michezo yao minne iliyopita kwenye mashindano yote.

Katika kundi H Real Madrid ina nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya 16 bora pamoja na timu ya Tottenham Hotspurs ambayo itakuwa ugenini leo nchini Ujerumani kukipiga na wenyeji Borussia Dortmund.

Nasa kuzuiwa kuanzisha Mabaraza ya Wananchi



Nairobi, Kenya. Mahakama Kuu imetoa amri ya kuzuia mabaraza yote ya kaunti kupitisha au kutekeleza hoja ya kuanzishwa mabaraza ya wananchi, jambo ambalo linatajwa kuwa pigo kwa muungano wa upinzani (Nasa).

Jaji Lilian Mutende alitoa amri ya muda Jumatatu hadi ilitakapokamilika kusikilizwa kesi iliyofunguliwa na wanaharakati Counties Development Group.

"Amri hii inatolewa kuwazuia walalamikiwa kuanzia wa nne hadi 50 na wanachama na wajumbe wa mabaraza ya kaunti kutoanzisha mchakato wa kuteua wajumbe, timu na waangalizi wa Baraza la Watu,” inasema amri.

Kesi iliyofunguliwa Jumatatu mchana ikiomba kuwazuia wawakilishi kutoatekeleza hoja iliyowasilishwa na kufikishwa mbele yao kwa ajili ya kuteua au kuchagua wanachama au wajumbe au waangalizi wa mabaraza ya wananchi.

Amri ya Jeji Mutende itadumua hadi Januari 28 mwaka ujao wakati usikilizwa wa kesi ukiendelea. Hata hivyo, mkuu wa sekretarieti ya Nasa walioanzisha utaratibu wa kuunda mabaraza ya wananchi, Norman Magaya alitupilia mbali amri hiyo akisema “upuuzi".


Sophia Simba arudi CCM



Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanawake CCM (UWT), Sophia Simba aomba radhi na kuomba kurejea CCM baada ya kufukuzwa uanachama.

Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli amesoma barua ya Sophia kuomba radhi mbele ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na kuwahoji wajumbe kama wanakubali kumsamehe jambo lililokubaliwa.

"MwanaCCM aliyefukuzwa uanachama amekuwa akiandika barua nyingi za kuomba radhi lakini tumekuwa tukinyamaza,  kikao hiki ndiyo kilimfukuza," amesema Rais Magufuli katika kikao hicho kinachofanyika leo Jumanne.

Baada ya kuwahoji wajumbe na kukubaliwa Rais Magufuli aliandika kwenye barua hiyo kuwa amekubaliwa kurudi CCM.

Ruge kukutana na Makonda Kuhusu Tamasha la Fiesta



Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, Jumatatu hii amefunguka kuzungumzia tetezi ya kwamba Tamasha la Muziki la Fiesta litaishia 6 usiku tofauti na miaka iliyopita kutokana na hali ya usalama.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda hivi karibuni akiwa katika kituo cha redio cha EFM kuzungumza juu ya matukio ya burudani kutotakiwa kufanyika zaidi ya saa sita usiku kwenye maeneo ya wazi Dar es salaam.

Tamasha la FIESTA 2017 linatarajiwa kufanyika Leaders Club Jumamosi hii November 25 huku ticket tayari zikiwa zimeshazagaa mitaani.

Ruge ambaye ni Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group amesema “Tunafanya juhudi za kujaribu kuona kama tunaweza tukampata Mkuu wa Mkoa”

Zelothe azungumza kimasai wakati akiomba kura




    Arumeru. Vituko na vioja vimezidi kutawala kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani Kata ya Musa mkoani hapa baada ya mgombea udiwani kupitia CCM, Flora Zelothe kuamua kuongea kimasai kwa lengo la kuwashawishi wananchi wampe kura.

Zelothe, aliamua kutumia lugha hiyo juzi wilayani Arumeru kama njia mojawapo ya kuwashawishi wapigakura wa eneo hilo ambao kwa asilimia kubwa ni makabila ya Wameru na Wamasai.

Akizungumza katika mkutano huo, Zelothe alisema wananchi wakimchagua atatekeleza mradi wa maji uliokuwa unagharamiwa na Benki ya Dunia eneo la Makutian ambao umesimama baada ya kuvurugwa na baadhi ya wanasiasa.

Akinadi sera zake kwa kimasai huku akiwa na mtafsiri wake pembeni aliwaambia wapigakura amejipanga kujenga shule ya sekondari.

Alisema kwa miaka mitano akiwa diwani wa viti maalumu alifanikiwa kuchonga barabara zote za vitongoji ndani ya Kata ya Musa kwa kiwango cha changarawe.

“Tutaboresha Shule ya Sekondari ya Kata ya Musa na kuleta walimu wa masomo ya sayansi na sanaa,” alisema Zelothe huku akishangiliwa.

Awali akimkaribisha jukwaani mwenyekiti wa CCM mkoani Arusha, Lekule Laiser alisema mgombea huyo ni mwanamke lakini ni jasiri na anajenga hoja.

Laiser alisema Zelothe aliwahi kwenda kupinga matokeo ya uchaguzi wa udiwani wa kata hiyo mwaka 2015 mahakamani na kusimamia kesi bila kuyumba na hilo linaonyesha dhahiri anafaa kuwa kiongozi.   

Breaking News: Clouds Media Group inawaka moto



Sehemu ya jengo la kituo cha Chouds Media Group linaungua moto muda huu. Juhudi za kuuzima moto huo bado zinaendelea.

MAGAZETI YA LEO 21/11/2017

MAGAZETI YA LEO 21/11/2017























Rais Magufuli hajatengua uteuzi wa Dkt. Laurian Ndumbaro


Taarifa zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurian Ndumbaro sio za kweli na zipuuzwe.

Wananchi endeleeni kupokea taarifa rasmi kutoka kwenye mamlaka na vyombo rasmi vya Serikali, na pia watumiaji wa mitandao ya kijamii mnakumbushwa kuwa kueneza taarifa za uongo ni makosa kisheria.

Serikali itawafuatilia wote waliozusha taarifa hizi na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


Baada ya Polisi kushikilia simu yake, Zitto ajipanga kuwashitaki




Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe, amesema anajipanga kulifungulia kesi ya kikatiba jeshi la polisi nchini kutokana na kushikilia simu yake.

Zitto ameeleza kuwa simu yake inashikiliwa tangu Novemba 7 mwaka huu alipokamatwa kwa tuhuma za kuvunja sheria ya takwimu  na sheria ya makosa ya mtandao.

“Walisema watahitaji simu hiyo kwa siku mbili tu, nilikwenda polisi KAMATA siku tatu baadaye nikaelezwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi. Nimerudi leo tarehe 20, Polisi wanasema bado wanahitaji simu yangu hiyo”, amesema Zitto.

==>Aliyoyasema Zitto kupitia akaunti yake ya Facebook:

Ndugu, Jamaa na Marafiki, mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 7/11/2017 Jeshi la Polisi walichukua Simu yangu kwa ajili ya uchunguzi wao kuhusu tuhuma dhidi yangu kwa mujibu wa sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya mtandao. Walisema watahitaji simu hiyo kwa siku 2 tu.

Nilikwenda polisi KAMATA siku 3 baadaye nikaelezwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi. Nimerudi leo tarehe 20/11/2017, Polisi wanasema bado wanahitaji simu yangu hiyo.

1) Nawakumbusha kuwa msitumie simu ile 0767777797 kwani bado imeshikiliwa na Polisi

2) Katiba ya Nchi yetu kifungu cha 16(1) na (2) imeweka msingi wa nguvu sana haki ya FARAGHA kwa raia na kwamba hata sheria ikitaka haipaswi kuingilia mawasiliano binafsi ya Raia.

Nina mashaka kuwa Jeshi la Polisi linakaa na Simu yangu muda wote huu kwa sababu za zaidi ya uchunguzi wao wa makosa wanayonituhumu nayo. Nimeamua kuwaachia Simu mpaka hapo watakapotosheka lakini wajiandae na kesi ya kikatiba ambayo pia italinda haki za wananchi wengi wanaothirika na matumizi mabaya ya sheria ya Mtandao ( cybercrime act ).
Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe, amesema anajipanga kulifungulia kesi ya kikatiba jeshi la polisi nchini kutokana na kushikilia simu yake.

Zitto ameeleza kuwa simu yake inashikiliwa tangu Novemba 7 mwaka huu alipokamatwa kwa tuhuma za kuvunja sheria ya takwimu  na sheria ya makosa ya mtandao.

“Walisema watahitaji simu hiyo kwa siku mbili tu, nilikwenda polisi KAMATA siku tatu baadaye nikaelezwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi. Nimerudi leo tarehe 20, Polisi wanasema bado wanahitaji simu yangu hiyo”, amesema Zitto.

==>Aliyoyasema Zitto kupitia akaunti yake ya Facebook:

Ndugu, Jamaa na Marafiki, mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 7/11/2017 Jeshi la Polisi walichukua Simu yangu kwa ajili ya uchunguzi wao kuhusu tuhuma dhidi yangu kwa mujibu wa sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya mtandao. Walisema watahitaji simu hiyo kwa siku 2 tu.

Nilikwenda polisi KAMATA siku 3 baadaye nikaelezwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi. Nimerudi leo tarehe 20/11/2017, Polisi wanasema bado wanahitaji simu yangu hiyo.

1) Nawakumbusha kuwa msitumie simu ile 0767777797 kwani bado imeshikiliwa na Polisi

2) Katiba ya Nchi yetu kifungu cha 16(1) na (2) imeweka msingi wa nguvu sana haki ya FARAGHA kwa raia na kwamba hata sheria ikitaka haipaswi kuingilia mawasiliano binafsi ya Raia.

Nina mashaka kuwa Jeshi la Polisi linakaa na Simu yangu muda wote huu kwa sababu za zaidi ya uchunguzi wao wa makosa wanayonituhumu nayo. Nimeamua kuwaachia Simu mpaka hapo watakapotosheka lakini wajiandae na kesi ya kikatiba ambayo pia italinda haki za wananchi wengi wanaothirika na matumizi mabaya ya sheria ya Mtandao ( cybercrime act ).



Kinga ya VVU kutolewa mwakani

Serikali inatarajia mwakani, kuanza kutoa dawa za kujikinga na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), ikiwa ni mkakati za kuwazuia watu kutopata maradhi hayo



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile

Dawa hiyo ni Truvada na utaratibu huo utakuwa wa majaribio na utahusisha watu 12,000 wanaojidunga dawa za kulevya, machangudoa na wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gazeti la Serikali la Habari Leo, imeeleza kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alisema: “Hii ni tiba kama kinga na tutawapima kwanza wote 12,000 na wale wasiokuwa na maambukizi ya VVU ndiyo tutawapa dawa ambao tunajua wanaendelea na ngono zembe, kisha tutafuatilia mienendo yao kwa mwaka mmoja na ikibidi kuongeza iwe miaka miwili.”

Watu hao watakaofanyiwa utafiti huo wa majaribio ni kutoka mikoa ya Njombe, Kagera, Iringa, Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam. Dk Ndugulile alisema kutakuwa na timu ya wataalamu ya kufuatilia mienendo yao na afya zao wote watakaokuwa kwenye majaribio hayo. Alisema timu hizo zitagawanywa katika kanda tatu ikiwemo Kanda ya Ziwa.

Alisema dawa hizo watakuwa wakipewa kila mwezi. Vidonge hivyo serikali haijanunua, bali imepata taasisi za Presidents Emergency Plan for Aids Relief (PEPFAR) na Global Fund. “Hizi dawa ni katika mkakati wa kidunia wa kuzuia maambukizi mapya na sisi tumepewa na taasisi hiyo ya Marekani ya PEPFAR na Global Fund,” alieleza Dk Ndugulile.

Dk Ndugulile alisema wanakamilisha taratibu za kuanza kwa majaribio hayo ikiwemo kupata vibali, hivyo hawajajua rasmi lini wataanza kazi hiyo isipokuwa itakuwa mwakani. Sasa hivi nchi nyingi zinatumia Truvada kama kinga dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi na miongoni mwao ni pamoja na Kenya, Uganda, Peru na Marekani.

Kwa mujibu wa mtandao wa Truvada.com, utumiaji wa dawa hizo ambao umeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) una mafanikio makubwa, unaweza kuleta madhara kama ya matatizo ya figo, kuwepo asidi ya lactic nyingi, maumivu ya tumbo, maumivu ya misuli.

Athari nyingine ni kuhema kwa kasi au kasi ya kuhema kuwa chini, kutapika, mapigo ya moyo kuwa katika hali isiyo ya kawaida, tatizo la ini, kichwa kuuma na kupungua uzito. Dawa hiyo ya Truvada imeingizwa nchini mwaka 2013 na imekuwa ikitumika kwenye tiba kama sehemu ya dawa za kufubaza Virusi Vya Ukimwi (ARVs). Inakadiriwa watu milioni 1.4 wanaishi na VVU nchini na maambukizi mapya yameonekana kupungua kila mwaka.

Takwimu zilizotolewa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) zinaonesha mwaka 2013 maambukizi hayo mapya yalikuwa kwa watu 72,000, mwaka uliofuata yalikuwa watu 69,603 na mwaka 2015 yameshuka na kuwa watu 48,000. Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Tacaids, Dk Jerome Kamwela amesema katika semina ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi kadiri dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs) zinavyoongezeka, vifo vitokanavyo na Ukimwi vinapungua.

Alisema hali ya maambukizi kwa Tanzania ni asilimia 5.3 huku Manyara na Tanga kwa Tanzania Bara, kiwango cha maambukizi kikiwa chini zaidi na Zanzibar, Pemba kipo chini. Makundi yaliyo hatarini zaidi kwa maambukizi na asilimia yao kwa wastani wa kitaifa yakiwa kwenye mabano ni makahaba (26), wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja (22.2) na wanaojidunga dawa za kulevya (15). Mengine yaliyo hatarini ni madereva wa malori ya masafa marefu, wafungwa na wafanyakazi wanaohama kufuata ajira.

Waliokwapua fedha Saudi Arabia watakiwa kurejesha



Mamlaka za Saudi Arabia zimewataka watoto wa kiume wa familia za kifalme na baadhi ya wafanyabiashara wanaoshikiliwa kurudisha mali walizojipatia kwa njia isiyo halali ili waweze kuachiwa huru, vyombo vya habari vimeripoti.

Shirika la habari la Bloomberg limesema watu 201 wakiwemo wafanyabiashara, mawaziri na wana wa ufalme miongoni mwao mwana mfalme Alwaleed bin Talal anayemiliki jengo refu la ghorofa katika mji mkuu, Riyadh wanashikiliwa na mamlaka za Saudi Arabia katika kampeni yake ya kukabiliana na rushwa. Pia, mamlaka zimefunga akaunti zao za benki.

Taarifa za vyombo vya habari zinasema kuwa mamlaka nchini Saudi Arabia zimewataka wanaoshikiliwa kurudisha mali walizopata kwa njia ya rushwa ikiwa wanataka kuachiwa huru na wasifunguliwe mashitaka. Inakadiria kuwa kati ya dola za Marekani 50 bilioni na 100 bilioni zitahamishwa kwenda hazina ya taifa.

Mapambano dhidi ya mafisadi yanaongozwa na mwana mfalme Mohammed bin Salman anayejaribu kuimarisha nguvu yake ya kimamlaka kabla ya kuapishwa rasmi kuwa mrithi wa ufalme.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaamini kuwa anataka kukusanya fedha anazohitaji kwa ajili ya kufanya mageuzi ya kiuchumi nchini.

Rose Ndauka awafungukia watoa mimba


Rose Ndauka.

MSANII wa Filamu Bongo, Rose Ndauka amewarushia dongo wasichana wa kizazi kipya ambao wengi wao wakipata mimba wanakimbilia kutoa badala ya kujifungua.

Ndauka ameiambia Full Shangwe, kuwa wanawake wengi wakipata ujauzito hutoa bila kujua kuwa mtoto ni faraja ya mwanamke na uhusiano kwa ujumla. “Nawashangaa wasichana wengi ambao wakipata mimba wanakimbilia kutoa.

I wish kama wangejua furaha, faraja na thamani ya mwanamke ni mtoto, wasingefanya hivyo,” alisema. Aliongeza: “Huwezi amini furaha ya kuwa na mtoto kwa mzazi ni zaidi ya changamoto.”

Jaji Warioba, Serukamba waumizwa kichwa na Mfumo wa elimu

Jaji Warioba, Serukamba waumizwa kichwa na Mfumo wa elimu



   Dar es Salaam. Waziri mkuu mstaafu, Joseph Warioba na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo na Huduma za Jamii, Peter Serukamba wamesema mfumo wa elimu unaotolewa sasa una kosoro hivyo unahitaji kufumuliwa na kuundwa upya.

Mbali ya Jaji Warioba na Serukamba, wadau wengine wamesema Tanzania ya viwanda haitafanikiwa ikiwa elimu itolewayo haiwaandai wahitimu kujitegemea badala yake wanakuwa tegemezi.

Hayo waliyasema jana katika kongamano litakalomalizika leo ambalo limeandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Taasisi ya HakiElimu linalojadili kuelekea Tanzania ya viwanda na Sera ya Ujamaa na Kujitegemea.

Jaji Warioba ambaye ni mwenyekiti wa kongamano hilo, alisema elimu inayotolewa inapaswa kuendana na mazingira ya wakati huu na kujibu mahitaji ya wahitimu.

Alisema licha ya mafanikio yanayofanywa na Serikali, kuna changamoto kubwa hususan ubora wa elimu inayotolewa kutowaandaa wahitimu kujitegemea kama ilivyokuwa awali.

“Uwiano wa wanafunzi wanaomaliza shule na wanaoendelea sekondari ni mdogo, wanaomaliza sekondari na kwenda chuo mdogo zaidi. Zamani mtu akimaliza darasa la nne anajua kusoma, kuandika na kuhesabu lakini sasa mtu anamaliza darasa la saba hajui kusoma, kuandika na kuhesabu,” alisema Warioba ambaye ni Jaji mstaafu na kuongeza: “Kuna matatizo makubwa ya miundombinu katika shule na vyuo kama madarasa na nyumba za walimu. Vitendea kazi na idadi ya walimu katika ngazi zao na maslahi ya walimu ni tatizo, haya yote yanatakiwa kupata majibu.”

Jaji Warioba aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alisema: “Siku hizi watu wanamaliza lakini hawana la kufanya, lazima tujiulize elimu yetu ni bora kwa mazingira ya baadaye?

Naye Serukamba ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM) akichangia mada alisema: “Wote tunakubali tatizo lipo ila hatujui lini tunalimaliza. Umefika wakati tukae tuangalie mfumo, tuangazie elimu ya awali hadi vyuo vikuu.”

Alitaja maeneo yanayohitaji kuangaliwa kuwa ni ubora wa elimu inayotolewa, ufundishaji, uongozi, muda wa kusoma na maudhui kuanzia chini hadi juu.

“Tukifikia hapo tutaweza kujibu challenges (changamoto). Tunapaswa kuufumua mfumo wetu tuunde tume ya elimu ambayo itakuja na majibu ya wapi tuboreshe... leo wanaokwenda kusoma ualimu si waliofaulu vizuri, ukiangalia Finland anayekwenda kusoma kafaulu vizuri na mtumishi anayelipwa vizuri ni mwalimu,” alisema Serukamba.

Makamu mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala alisema elimu bora ni ile inayomfanya mtu aweze kutumia maarifa na ujuzi alioupata kupambana na mazingira yake.

“Elimu sahihi ni ile inayoondoa pengo kati ya maarifa ya kinadharia yanayotolewa darasani na yale ya vitendo yanayopatikana katika jamii. Elimu mwafaka ni elimu ya kujitegemea,” alisema.

Akizungumza kwenye kongamano hilo, mkuruenzi mtendaji wa HakiElimu, John Kalage alisema: “Tunahitaji kuuangalia mfumo, je unajibu mahitaji ya sasa, je mfumo gani tuutumie sasa, kwani uliopo umeshindwa kuwaandaa wahitimu watakaokwenda kujitegemea na si kuwa tegemezi?”

Akifungua kongamano hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi (Tamisemi), Suleiman Jafo alisema Serikali itayachukua mapendekezo yote watakayofikia na kuyafanyia kazi.

“Tupo pamoja, Rais John Magufuli amefurahishwa na ninyi wasomi kukutana kujadili ikiwamo suala la uchumi wa viwanda na yeye amesema atakuwa tayari kupokea mapendekezo mtakayoyafikia na kuyafanyia kazi,” alisema Jafo.

“Taifa hili litajengwa na sisi wenyewe, tutumie kongamano hili kujadili kwa kina bila woga kwani tusipojenga msingi mzuri wa elimu yetu katika ushirikiano huu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, tutakuwa wasindikizaji,” alisema.

Naye Waziri wa viwanda, Charles Mwijage alisema: “Hakuna hofu mtu kujitathmini wapi ametoka, yupo wapi na anakwenda wapi.”

Mwigage alisema tayari ameagiza uongozi wa Chuo cha Biashara (CBE) kutoa kozi kwa kila mwanafunzi ya ujasiriamali ili kuwawezesha wanapohitimu waweze kuwa wajasiriamali.