Monday, 20 November 2017

Makonda aiungamkono Kampuni ya ukamataji kazi za Wasanii



MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameipiga jeki Kampuni ya Msama Auction Mart inayojishughulisha na ufuatiliaji na ukamataji wezi wa kazi za wasanii kwa kuchoma CD feki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, Alex Msama alisema Makonda ameamua kuipiga jeki kampeni hiyo kutokana na matunda anayoyaona ya zoezi hilo kuendelea vizuri kwani amezunguka katika jiji lake hasa maeneo ya Kariakoo na kujionea biashara hiyo haramu ya kuchoma CD feki ikiwa imepungua na kuwaomba waendelee na zoezi hilo.

Alisema kutokana na kutiwa moyo na mkuu huyo wa mkoa, Kampuni ya Msama Auction Mart sasa imezidi kupata nguvu ya kuendelea na zoezi hilo popote pale, iwe mafichoni ama pembezoni mwa mji lazima wezi wa kazi za wasanii wakamatwe.
Stori zinazo husiana na ulizosoma

Rais Kenyatta kuapishwa jumanne wiki ijayo





Rais Kenyatta.

Rais Kenyatta sasa anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais kwa muhula wa pili baada ya Mahakama ya Juu kufutilia mbali kesi ambazo zilikuwa zinapinga ushindi wake katika uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 26 Oktoba.

Kifungu 141(1b) cha Katiba ya Kenya kinasema Rais anafaa kuapishwa siku ya saba inayofuata siku ya kutolewa kwa uamuzi wa mahakama wa kuidhinisha uchaguzi iwapo kulikuwa na kesi iliyokuwa imewasilishwa.

Rais, kwa mujibu wa katiba, anafaa kuapishwa hadharani mbele ya Jaji Mkuu au Naibu Jaji Mkuu

Kauli ya Omog kuhusu Ibrahim Mo





Kama ulisikia, hivi karibuni baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa, uongozi wa Yanga ulidaiwa kuwa katika harakati za kumuwinda kiungo mshambuliaji wa Simba, Mohammed Ibrahimu ‘Mo’.

Yanga ilifikia hatua hiyo baada kuona kiungo huyo mbunifu uwanjani hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha Simba kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Hata hivyo, baada ya Simba kupata taarifa hizo ilidai kuwa mchezaji huyo ambaye mkataba wake na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu huu haendi popote, lakini pia kocha mkuu wa timu hiyo Mcameroon, Joseph Omog amepigilia msumari juu ya hilo kwa kusema kuwa Mo haondoki klabuni hapo.

Omog amesema kuwa Mo ni mmoja kati ya wachezaji anaowahitaji zaidi katika kikosi chake, kwa hiyo hayupo tayari kumuona akiondoka klabuni hapo.

“Kama kuna timu yoyote inamhitaji Mo kwa sasa hawezi kuondoka, bado tunamhitaji zaidi katika kikosi chetu na uongozi nimeshauambia juu ya hilo.

“Nilikuwa simtumii kwa sababu alikuwa ni majeruhi na sasa amepona, ndiyo maana unaona nimeanza kumtumia na matunda yake yanaonekana uwanjani, sipo tayari kuona akiondoka kikosini kwangu kwa sasa kama hao Yanga wanamtaka basi wasubiri lakini siyo sasa,” alisema Omog.

Aliyeongoza mauaji ya kiitikadi Marekani Charles Manson amefariki jela


Kiongozi wa kikundi chenye itikadi kali za imani Charles Manson - ambaye aliongoza mauaji ya kikatili miaka ya 1960 - amefariki dunia katika jimbo la California baada ya kuwa gerezani kwa zaidi ya miongo minne .

Alikuwa na umri wa miaka 83.

Mwezi Agosti 1969 wafuasi wa kundi lake waliwauwa watu saba, akiwemo mcheza filamu wa Hollywood actress Sharon Tate, ambaye alikuwa akitarajia kupata mtoto na mumewe mwongozaji wa filamu Roman Polanski.

Waandamana tena Marekani kupinga mauaji

Maadhimisho ya mauaji ya mweusi Marekani

Kwa Picha: Mauaji Las Vegas, Marekani

Manson alihukumiwa kifo mwaka 1971, lakini kifungo chake kilibadilishwa na kuwa cha maisha jela.

Aliamuini mauaji hayo yangeanzisha vita vya kijamii na hivyo kumuwezesha kuchukua mamlaka.
Manson alilazwa katika hospitali ya Bakersfield iliyoko California mapema mwezi huu na baadae akafa kifo cha kawaida Jumapili.

Mmoja wa wafuasi wa Manson, Susan Atkins, alimdunga kisu Tate hadi kufa na kuuburuza mwili wake uliokuwa ukichuruzika damu hadi mbele ya mlango wa nyumba ya mchezaji filamu huyo.

Wengine wanne waliokuwa nyumbani kwa Tate waliuliwa kinyama kwa kuchomwa visu.

Siku iliyofuatia, matajiri wawili wa Los Angeles- mke na mume , Leno na Rosemary LaBianca, pia waliuliwa na wafuasi wake.

Mauaji hayo yalitambuliwa kwa ujumla kama mauaji ya Tate-LaBianca.

Katika tukio jingine tofauti Donald Shea, mchezaji filamu mwingine wa Hollywood , na Gary Hinman, pia waliuliwa na wajumbe wa familia ya Manson.

Manson hakuwepo kwenye tukio la mauaji, lakini alipatikana na hatia ya kuongoza mauaji ya wafuasi wake katika mauaji yote saba.
Alihukumiwa mwaka 1971.



Mkenya ashinda taji la malkia wa urembo Afrika



Shindano la malkia wa urembo duniani la 2017 lilikamilika mjini Sanya China siku ya Jumamosi huku Mkenya Magline Jeruto akishinda taji la malkia wa urembo barani Afrika.

Hatua hiyo inajiri baada ya mwanadada huyo kutoka eneo la Elgeyo Marakwet nchini Kenya kuchukua nafasi ya tano.

Taji la malkia wa urembo duniani lilichukuliwa na mwanadada wa India Manushi Chhillar.

Andrea Meza wa Mexico alichukuwa nafasi ya pili akifuatiwa na Muingereza Stephanie Hill huku naye Aurore Kichenin wa Ufaransa akishinda nafasi ya nne.




Magline Jeruto ambaye ndiye malkia wa urembo wa Elgeyo Marakwet alichukua nafasi ya tano miongoni mwa wagombea 118 katika shindano la malkia mrembo dunia.

Mwanadada mwengine wa Afrika ambaye aliorodheshwa katika nafasi kumi bora ni Ade van Heerden wa Afrika Kusini ambaye alimaliza katika nafasi ya tisa.

Mahakama ya Kenya yafanya uamuzi huu



Mahakama ya Juu nchini Kenya imetupilia mbali kesi zilizofunguliwa na wafuasi wa NASA za kupinga ushindi wa Urais wa Uhuru Kenyatta, kwenye uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26, 2017

Kesi hiyo ambayo ilikuwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari, iliongozwa na majaji 6 akiwemo Jaji Mkuu David Maraga, na kutoa uamuzi kuwa Uhuru Kenyatta ni mshindi halali wa uchaguzi wa Oktoba 26.

Kufuatia uamuzi huo wa mahakama ya Juu nchini Kenya, Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo, na kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa muhula wa pili.

Ikumbukwe uchaguzi wa marudio ulifanyika baada ya Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya Urais ya uchaguzi wa kwanza wa Agosti 8, 2017 na kutaka urudiwe mara ya pili.

Upimaji afya waibua msongamano




 Upimaji afya bure unaofanywa na madaktari kutoka China katika Bandari ya Dar es Salaam umesababisha foleni kwa watumiaji wa barabara.

Upimaji wa afya unafanyika kwenye meli iliyotia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam.

Katika Barabara ya Kilwa, magari yanayoelekea Posta na Gerezani yamekuwa yakitembea mwendo wa taratibu na kusimama kwa takriban kwa dakika 20 kabla ya kusogea.

Kondakta wa daladala linalofanya safari kati ya Mbagala Rangi Tatu na Stesheni, Yasin Yusuph amesema leo Jumatatu Novemba 20 kuwa wametumia zaidi ya saa mbili kwa safari.

"Sisi tumetoka Mbagala saa 1:30 hadi sasa saa 3:40 hatujafika na mwendo ni huuhuu unaouona wa taratibu. Magari yakishasimama unasahau. Tatizo ni kuwa hakuna utaratibu maalumu, watu wamejaa kila sehemu na wanaruhusu magari njia mbili," amesema Yusuph.

Amesema ni vyema lingetafutwa eneo kubwa ambalo watu wanaweza kukaa na kusubiri huduma badala ya kusimamishwa pembezoni mwa barabara.

"Watu ni wengi, eneo la kupumzika hakuna. Hapa hakuna miti ya kutosha jua likiwa kali litawachoma," amesema.

Mtoto wa Rais Mugabe amkingia kifua baba yake



Mtoto wa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na mkewe Grace, Chatunga Bellarmine Mugabe amemsifu baba yake na kukitukana chama cha Zanu-PF.


Rais Robert Mugabe akiwa na mkewe Grace pamoja na mtoto wao wa tatu Chatunga

Mtoto huyo ambaye ni watatu katika familia ya Rais huyo ametoa maneno hayo kupitia mtandao wake wa Facebook kwa kukiambia chama hiko kuwa hakiwezi kufanya lolote bila Rais Mugabe.

Kupitia mtandao huo, Chatunga ameandika:

“You can’t fire a Revolutionary leader ! Zanu Pf is nothing without President Mugabe ✊ Gushungo will always remain the champion of champions! Proud of you Gushungo Proud of Dad. Gushungo always and forever to death✊ People like Wellence Mujuru celebrate and march became of Jealous and ruchiva acting as if he cares for the people and unnecessary attacks !

We all grow up in life and take up our responsibility to serve our country. We all have a responsibility to keep this country safe and guard our sovereignty. God bless all who sacrifice for our nation Zimbabwe

Chama cha Zanu-PF kimemtaka Mugabe kujiuzulu Urais wa nchi hiyo mpaka kufikia leo mchana.

Nafasi za kazi leo November 20

Huu ndio muonekano mpya wa Dkt Shika

Huu ndio muonekano mpya wa Dkt Shika

Maisha ya Dk Louis Shika ambaye hivi karibuni aliingia kwenye headline baada ya kushindwa kutoa asilimia 25 ya mnada wa nyumba za Lugumi muda mchache baada ya kushinda mnada huo, yameanza kubadilika taratibu kutokana na kupata deal kadhaa za matangazo.

DK Shika ambaye alikuwa katika muonekano ambao haufananii na utajiri anaoutangaza kuwa nao, weekend hii ameonekana akiwa amevaa suti kali.

Wadau wa mambo wanadai kuwa mzee huyo mashuhuri mitandaoni amepata deal kubwa katika kampuni moja kubwa la michezo ya kubashiri.

Huwenda akapata deal nyingi zaidi kutoka na umaarufu alionao kwa sasa

Kala Jeremiah ataka kufanya kazi na Dk Shika



Msanii wa muziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah amedai atafanya jitihada za kumtafuta Dk Louis Shika ili apate madini kutoka kwa mzee huyo ambaye anadaiwa kuwa  ni msomi wa udaktari.

Akimzungumzia 'tajiri mtata' , Kala alisema mzee huyo anaonekana kuwa ni msomi mkubwa na tayari ana mambo mengi amejifunza akiwa nje ya nchi alipokuwa alisoma na kufanya kazi enzi za ujana wake.

“Binafsi nitamtafuta kwaajili ya kujifunza, yule ni mzee mwenye mambo mengi, aliyopitia, ni mafunzo tosha kwa vijana kama mimi na wengine. Kwahiyo nitamtafuta ili nijifunze,” alisema Kala.

Kala alidai kwa kuwa nyimbo zake ni za kijamii zaidi, ataangalia uwezekano wa kumtumia katika baadhi ya project zake kama akipata nafasi.

Pia rapa huyo aliitaka serikali kumtumia mzee huyo katika Tanzania ya Viwanda kwa kuwa anaonekana ana mambo mengi ambayo anayafahamu.

Dk Louis Shika hivi karibuni aliingia kwenye headline baada ya kushindwa kutoa asilimia 25 ya mnada wa nyumba za Lugumi muda mchache baada ya kushinda mnada huo na kudai pesa zake zipo Urusi.

Mtoto wa Rais Mugabe amkingia kifua baba yake na kuitukana Zanu-PF



Rais Robert Mugabe akiwa na mkewe Grace pamoja na mtoto wao wa tatu Chatunga

Mtoto wa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na mkewe Grace, Chatunga Bellarmine Mugabe amemsifu baba yake na kukitukana chama cha Zanu-PF.

Mtoto huyo ambaye ni watatu katika familia ya Rais huyo ametoa maneno hayo kupitia mtandao wake wa Facebook kwa kukiambia chama hiko kuwa hakiwezi kufanya lolote bila Rais Mugabe. Kupitia mtandao huo, Chatunga ameandika:

“You can’t fire a Revolutionary leader ! Zanu Pf is nothing without President Mugabe ✊ Gushungo will always remain the champion of champions! Proud of you Gushungo Proud of Dad. Gushungo always and forever to death✊ People like Wellence Mujuru celebrate and march became of Jealous and ruchiva acting as if he cares for the people and unnecessary attacks !
We all grow up in life and take up our responsibility to serve our country. We all have a responsibility to keep this country safe and guard our sovereignty. God bless all who sacrifice for our nation Zimbabwe

Chama cha Zanu-PF kimemtaka Mugabe kujiuzulu Urais wa nchi hiyo mpaka kufikia leo mchana.

Mahakama ya Kenya kuamua juu ya kesi ya urais leo

Jaji Mkuu wa Mahakama ya juu zaidi nchini kenya David Maraga

Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya Jumatatu inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi zilizowasilishwa kwenye mahakama hiyo kupinga uchaguzi wa marudio wa tarehe 26 Oktoba ambapo rais wa sasa Uhuru Kenyatta alitangazwa kama mshindi.

Katika Kesi majaji watatakiwa kutoa uamuzi kuhusu masuala yafuatayo:

Wataamua iwapo tume huru ya taifa ya chaguzi na mipaka (IEBC ) ilifaa kuteuwa upya wagombea urais au la.

Uamuzi pia utatolewa na mahakama hiyo juu zaidi juu ya ya ikiwa kujiondoa kwenye uchaguzi huo kwa kiongozi Muungano wa upinzani Raila Odinga na Makamu wake Kalonzo Musyoka kuliathiri uchaguzi huo.

Majaji pia watatoa uamuzi kuhusu ikiwa baada ya tume ya IEBC kushindwa kuendesha uchaguzi katika ameneo bunge 25 kati ya 290 kunahalalisha ama kubatilisha matokeo ya uchaguzi.

Aidha Mahakama hiyo itawaeleza waKenya ikiwa tume ya uchaguzi (IEBC) ilikuwa na uwezo wa kuandaa uchaguzi wa haki na huru baada ya kugubikwa na mgawanyiko miongoni mwa wajumbe wake.

Kwa upande mwingine Wakenya watasubiri kusikia uamuzi wa mahakama kuhusu kama ghasia zilizotokea kabla na baada ya uchaguzi wa marudio wa urais ziliathiri ama hazikuathiri matokeo ya uchaguzi na kuufanya kuwa usio wa haki na huru au la.

Mahakama itatoa ufafanuzi juu ya dosari ya karatasi za kupigia kura, maarufu kama form 34A ziliathiri matokeo ya uchaguzi.

Hukumu hii inasubiriwa kwa shauku kubwa na raia wa Kenya pamoja na kwingineko duniani, huku wengio wakijiuliza hatma ya Kenya.

Tangu kufanyika kwa uchaguzi wa marudio wa urais tarehe 26 Oktoba, baadhi ya miji mikuu nchini Kenya ukiwemo mji mkuu Nairobi, pamoja na mji wa magharibi wa Kisumu imekuwa ikikumbwa na ghasia za maandamano ambazo zilizosababisha mauaji ya watu na wengine kujeruhiwa.