Sunday, 19 November 2017

Chelsea yaitwanga West Bromwich 4-0

Chelsea imeshangilia ushindi mwingine wa EPL kwa kuichapa Wes Borm kwa mabao 4-0.

Wakati inashinda kwa idadi hiyo, kiungo wake Eden Hazard anaonekana kuamka baada ya kufunga mabao mawili.

Wengine waliofunga ni Alvaro Morata na Alonso ambao kila mmoja alifunga bao moja.

Msafara wa Lowasa wapigwa mabomu Moshi



Polisi Mkoa wa Kilimanjaro wamelazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi kumwezesha mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kupata nafasi ya kupita mjini Moshi.

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi waliokuwa wamefunga barabara.

Takriban mabomu manne ya kutoa machozi yalifyatuliwa saa 10:30 jana jioni ya  Jumamosi Novemba 18,2017  katika eneo la Soko la Manyema ambako Lowassa na msafara wake alikuwa apokewe ili kuelekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani eneo la Pasua Relini.

Kabla ya Lowassa kufika, vijana madereva wa bodaboda walipita katika Barabara ya J.K. Nyerere.

Vijana hao walipopita mzunguko wa magari wa Coca Cola saa 10:15 jioni, gari la polisi aina ya Toyota Land Cruicer likiwa na polisi wenye mabomu ya machozi lilionekana likiwafuata.

Haikupita dakika 15, ndipo kulisikika milio ya mabomu katika eneo la Manyema ambalo ni njia panda ya kuelekea eneo la mkutano.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema ambaye yuko katika msafara wa Lowassa, alisema eneo la Manyema lilikuwa halipitiki kutokana umati wa watu.

Lema alisema ni kutokana na hali hiyo, ili kumwezesha Lowassa na msafara wake kupita, FFU walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alisema mabomu hayo yamepigwa ili kupunguza idadi ya watu waliokuwa wamefurika kwenye eneo hilo na kumuwezesha Lowassa kupita.

“Alikuwa hana njia ya kupita, watu walifurika kiasi kwamba hata Lowassa mwenyewe asingeweza kupita, tulifanya hivyo kuwapunguza na ameshapita ameenda zake kwenye mkutano,” alisema.

Lema : Nipo tayari kuuza figo yangu kugharamia matibabu ya Lissu




Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amesema hata kama gharama za  matibabu ya Tundu Lissu yakifika Trilioni  moja, watakuwa tayari kuuza figo zao.

Akizungumza jana  Novemba 18 katika kata ya Siuyu iliyopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Lema alisema utekelezaji wa  majukumu ya kisiasa ukiwa upinzani wakati huu ni ngumu kutokana na kuwindwa kila uchao.

Alisema  pamoja na ugumu huo hawajarudi nyuma na kisasi cha wasiopenda mabadiliko na wanaochukia kukosolewa   kimedhihirika  kwa vitendo alivyotendewa Lissu.

"Lissu yupo kitandani risasi mwili mzima, gharama za matibabu yake ni kubwa, lakini hata ikifika trilioni moja na tukawa hatuna fedha tutauza figo zetu kuendelea kugharamia matibabu yake" alisema Lema.

Alisema Lissu amekuwa alama ya haki katika taifa kutokana na kuamua kuwa upande wa haki.

Mama huyu avunja rekodi “Madrid Derby” iliyodumu kwa miaka 86



Ukiachana ns ile Derby ya kaskazini mwa London itakayopigwa pale nchini Uingereza hii leo, kule katika ligi kuu nchini Hispania katika dimba la Wanda Metrpolitana kutakuwa na derby nyingine.

Real Madrid ambao msimu huu wanaonekana kuchechemea watakuwa wageni wa Atletico Madrid ambao nao toka msimu uanze wanaonekana kutokuwa vizuri kama ilivyo kwa majirani zao.

Py Laurance anaweza kuwa mtu pekee ambaye anakwenda katika mchezo huu akiwa na presha kubwa kwani hatapenda timu yoyote kati ya Atletico Madrid au Real Madrid ipoteze mchezo wa hii leo.

Py ni mama mzazi wa mlinzi wa kushoto wa Atletico Madrid Theo Hernandez lakini vile vile Py huyuhuyu ndio mama mzazi wa mlinzi wa Real Madrid Lucas Hernandez jambo linalomfanya kushabikia timu zote mbili.

Katika mahojiano na jarida la Marca mwanamama huyu ameeleza kwamba kabla ya mechi ya leo aliwaita na kuwaambia kwamba anawapenda sana na akiwasisitiza wasipigane kwa kuwa wao ni ndugu.

Py anakuwa mzazi wa kwanza kukutanisha watoto wake katika mchezo wa Madrid Derby tangu jambo kama hili lilipotokea katika msimu wa mwaka 1929/1930 na tangu kipindi hicho hakuna aliyeweza kuvunja rekodi hiyo.

Real Madrid na Atletico Madrid wote wana alama sawa (23) na atakayeshinda katika mchezo wa leo atakaa juu ya mwenzake na kupunguza pengo la alama na vinara Barcelona

Wazimbabwe waandamana kumtaka Mugabe ajiuzulu



Maelfu ya raia wa Zimbabwe jana walijitokeza barabarani hasa mjini Harare wakijiandaa kwa mkutano mkubwa unaoungwa mkono na chama tawala ZANU-PF katika jitihada za kuongeza shinikizo la kumtaka rais Mugabe ajiuzuulu,wakishikilia mabango yaliyoandikwa 'Mugabe Must Go'.

Zanu-PF ndio chama kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini kwa takriban miaka 40.

Lakini sasa inabidi wamshinikize ajiuzulu kufuatia mpasuko mkubwa katika chama tawala.

Kikubwa kinachodhaniwa ni nani atakayemrithi rais Mugabe atakapoochia madaraka.

Jeshi la nchi hiyo lilichukua hatamu za kiserikali na kumuweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kina.

Mugabe angependelea mkewe kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na uhasama mkubwa baina yake na mkewe rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa madaraka.

Zaidi ya hayo Rais Mugabe angependa kuendelea kuwa uongozini hadi chama kitakapofanya mkutano wao mkuu mwezi ujao.

CHUO CHA ST DAVID KIMARA DAR KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO



CHUO CHA ST DAVID COLLEGE OF HEALTH KILICHOPO KIMARA TEMBONI DSM NI CHUO CHA KIPEKEE KATIKA UKANDA HUU WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KINACHOTOA KOZI ZA AFYA KWA NGAZI ZOTE ZA CHETI NA DIPLOMA.

SIFA KUU NI UFAULU MASOMO YA SAYANSI IKIWEO HESABU NA KIINGEREZA ANGALAU ALAMA D.

ADA ZETU NI NAFUU UTALIPA KIDOGO KIDOGO KUKIDHI UWEZO WAKO, KWA MAWASILIANO 0626 231 364 / 0786 658 535 /  0716 044 610 / 0718 229 977 AU INGIA MTANDAONI  www.stdavidcollege.ac.tc

WAHI SASA MUHULA MPYA TAYARI UMEANZA.
PIA KUNA KOZI MAALUMU KWA WOTE WASIO NA VIGEZO KAMILI KUMUWEZESHA KUPAMBANA MPAKA AFIKIE VIWANGO NA KUJIUNGA NA MEDICINE..CA/CO

JIUNGE NA KOZI INAYOTOLEWA ST DAVID COLLEGE PEKEE IITWAYO PRE-MEDICINE PROGRAME KWA KUSHIRIKIANA NA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA NECTA TUMEKUANDALIA NJIA RAHISI KABISA.

FIKA SASA KIMARA TEMBONI ZAMANI MOA AU OFISI ZETU ZILIZOPO MWANANYAMALA A CCM MINAZINI KWA DR DAVID B.MWANGANDA.

CHUO NI CHA KUTWA NA BWENI.







Mbunge Nassari atumia CD kufanya kampeni

Mbunge Nassari atumia CD kufanya kampeni



Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemnadi kitofauti mgombea udiwani wa Kata ya Ambureni, Dominick Mollel kwa kugawa CD anazodai zinaonyesha baadhi ya madiwani wa chama hicho wilayani Arumeru walivyoshawishiwa kupokea rushwa.

Nassari aligawa zaidi ya nakala 500 katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Kwa Pole wilayani hapa huku akiwataka wananchi kutowachagua wagombea wa CCM kwa kudai baadhi yao wanatuhumiwa kupokea rushwa.

Nassari amefafanua kwamba pamoja na kuwasilisha ushahidi wake Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ameamua kugawa nakala hizo kuwafungua macho wananchi waelewe kwamba wagombea kutoka CCM hawafai.

Akizungumzia kitendo cha baadhi ya wagombea wa CCM kutoa ahadi ya kuyakomboa baadhi ya mashamba yaliyotwaliwa na wawekezaji wilayani humo, Nassari amesema kwamba wakati hao wanatoa ahadi jukwaani wao wataingia shambani kudai haki.

“Wakati wao wanaahidi kushughulika na nyaraka sisi watatukuta shambani tunaendelea na kazi sawa,” alisema Nassari.


John Heche aamua kujisalimisha polisi



Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche amesema kesho ataripoti polisi mkoani Morogoro kuitikia wito wa jeshi hilo.

Heche alisema jana kuwa ana taarifa kwamba anatafutwa na jeshi hilo na anatakiwa kwenda kuhojiwa mkoani Morogoro.

Heche, pia alidai kuwa polisi walikuwa wamkamate, hata hivyo hilo halikufanyika.

Mbunge huyo alisema hajui kosa alilotenda, isipokuwa anatakiwa kuhojiwa kwa kauli alizotoa alipomsindikiza mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali kutoka gerezani.

Akizungumza na gazeti hili, kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema kwamba mbunge huyo alifanya mkutano wa hadhara wilayani Kilombero Aprili 8, 2017.

Alisema kwamba wanamtafuta kwa tuhuna za kutotii amri za viongozi na kufanya mkutano kisha kutoa lugha za matusi zilizotaka kusababisha vurugu.

Alisema tangu siku ya tukio, jeshi hilo limekuwa likimtafuta mbunge huyo bila mafanikio ndipo lilipoamua kulishirikisha Bunge.

Polisi iliandika barua kwa Spika wa Bunge kumtaarifu kuwa mbunge huyo anatafutwa kwenda kujibu tuhuma zinazomkabili mkoani Morogoro.

“Barua ni mambo ya siri kati ya jeshi na Bunge, tunachotaka sisi ni kumuona Heche hapa na asitake tutumie nguvu,” alisema Kamanda Matei.

Mwananchi:

Aliyezikwa akidaiwa mtu mzima abainika kuwa ni mwanafunzi aliyekuwa amepotea

Aliyezikwa akidaiwa mtu mzima abainika kuwa ni mwanafunzi aliyekuwa amepotea



Kama ni kuumbuka, basi walioidhinisha kuzikwa kwa maiti iliyodaiwa kuwa ni ya mtu mzima na mwenye ndevu, wameumbuka; maiti hiyo ni ya Humphrey Makundi, mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Scolastica ya Himo wilayani Moshi.

Hayo yalibainika baada ya kutekelezwa kwa amri ya kufukua maiti hiyo iliyotolewa na Hakimu Idan Mwilapo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na baadaye kufanyiwa uchunguzi. Uchunguzi umebaini kuwa maiti hiyo ni ya mtoto na hakuwa na ndevu.

Amri ya kufukua maiti hiyo ilitolewa baada ya Jamhuri kuwasilisha maombi kupitia kwa Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka ukitaka mwili uliozikwa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Novemba 12 kwa kukosa ndugu ufukuliwe.

Maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani juzi yakiambatanishwa na kiapo cha Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kilimanjaro (RCO), Doto Mdowe na Mahakama iliridhia ombi hilo.

Mwanafunzi huyo alitoweka shuleni katika mazingira ya kutatanisha Novemba 6 na baadaye mwili wake ukaokotwa Mto Ghona, umbali wa mita 300 kutoka shule hiyo.

Kutokana na mwili huo kuharibika, polisi na daktari waliufanyia uchunguzi wa awali na kueleza kuwa haukuwa wa mtoto huyo bali ni wa mtu mzima na kuruhusu halmashauri kuuzika.

Ingawa haielezwi katika shauri hilo ni nani aliyetoa hoja mwili huo ufukuliwe, lakini RCO katika kiapo chake alitaka ufukuliwe ili uchunguzwe kama ni wa Humphery aliyetoweka Novemba 6.

Watu 11 wakamatwa

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Hamis Issah alisema wanawashikilia watu 11, akiwemo mmiliki wa shule hiyo iliyopo mji mdogo wa Himo kwa ajili ya mahojiano.

Kwa mujibu wa Kamanda Issah, ingawa mtoto huyo aliondoka Novemba 6 kutoka shule hiyo iliyozungushiwa ukuta na walinzi na kwenda kusikojulikana, taarifa za kutoweka kwake zilitolewa polisi Novemba 11.

“Mtoto alitoweka shuleni tarehe 6.11.2017 wao wakaendelea na taratibu zao hadi tarehe 10.11.2017 ndio walizifikisha taarifa hizo polisi. Tulianzia uchunguzi papo hapo,” alisema.

“Katika hatua za awali za uchunguzi tulimkamata mmiliki wa shule kwa usalama wake kwa sababu wazazi tayari walikuwa wanamtuhumu kuhusika na kifo cha mtoto wao.”

Kamanda Issah alisema wakati wakiendelea na uchunguzi, walipata taarifa kuwa kuna mwili wa mtu uliokotwa Novemba 7 na ukahifadhiwa Hospitali ya Mawenzi hadi Novemba 12 ukazikwa.

“Baada ya kupata taarifa ndipo tukaomba kibali cha kufukua huo mwili na wakati unafukuliwa wazazi walikuwepo. Nawahakikishia haki ya huyu mtoto haitapotea,” alisema.

Kamanda Issah hakutaka kuzungumzia kwa undani kuhusu kile kilichobainika katika uchunguzi huo, lakini alisema umefikia asilimia 50.

“Tunataka kujua ilikuwaje mwanafunzi akatoka shuleni na shule ina geti na ina walinzi. Hapo nje kuna mama lishe,” alisema kamanda huyo.

“Niwaonye wamiliki wa shule, wasimamie vizuri maisha ya wanafunzi.”

Mwili ulivyotambuliwa

Watu walioshuhudia ufukuaji wa mwili huo katika makaburi ya Karanga mjini Moshi juzi saa 8:30 mchana, walilieleza gazeti hili kuwa baba mzazi wa mtoto huyo, Jackson Makundi aliishiwa nguvu na kuanguka.

Taarifa zinasema kabla ya ufukuaji kuanza, maofisa wa polisi walimuuliza mzazi huyo ataje alama zitakazomfanya amtambue kuwa huyo ni mwanaye naye alitoa alama mbili ambazo ni jino moja kukatika nusu na kidole kimoja cha mkononi kuwa na kucha iliyong’oka, alama ambazo zilionekana.

“Baada ya mwili kufukuliwa na baba na ndugu wengine kutambua alama alizozisema, yule baba aliishiwa nguvu na kukaa chini ikabidi aondolewe eneo lile,” alisema mmoja wa walioshuhudia tukio hilo.

Kwa mujibu wa mtu aliyeshuhudia uchunguzi huo, mwili wa mtoto huyo umekutwa na jeraha kwenye fuvu la kichwa ikiashiria alipigwa na kitu kizito kichwani.

Mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Alichosema baba mzazi

Jackson Makundi, baba mzazi wa mtoto huyo amedai kuna mchezo uliofanywa baina ya uongozi wa shule na polisi wa Himo ili kuficha ukweli kuhusu ukatili aliofanyiwa mtoto wake.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, baba huyo alidai alipewa taarifa za kupotea mwanawe Novemba 8, ikiwa ni siku mbili baada ya kudaiwa ametoweka shuleni katika mazingira ya kutatanisha.

Makundi alidai taarifa ambazo baadhi ya walimu wanazitoa kuhusu kutoweka kwa mwanafunzi huyo zinatofautiana na taarifa za wanafunzi.

“Baada ya mwili kufukuliwa nilijiridhisha kwa asilimia 100 kuwa mtoto ni wangu kutokana na kwamba vichwa vyetu vinafanana na nyuso zetu,” alisema.

Alidai taarifa alizozipata kutoka kwa wanafunzi wenzake ni kwamba mtoto wake aliondoka shuleni akiwa amevaa bukta, fulana na soksi.

Makundi amehoji iweje mwanafunzi atoweke shule halafu apewe taarifa baada ya siku mbili, wakati shule hiyo ina ulinzi na utaratibu mkali wa kuingia na kutoka.

“Ninaamini na dhamira ya moyo wangu inanituma kuamini uongozi wa shule na polisi wa kituo cha Himo wana jambo wanalificha kuhusu kifo cha mtoto wangu,” alisema.

Hata hivyo, alimpongeza Kamanda Issah na wasaidizi wake kwa namna wanavyompa ushirikiano katika uchunguzi, akiamini kila kitu kitajulikana.

Maswali kuhusu uchunguzi

Tangu kufukuliwa kwa mwili huo na kubainika ni wa Humphrey, kumeibuka maswali kuhusu namna polisi na daktari wa Hospitali ya Mawenzi walivyoruhusu mwili uzikwe.

Taarifa kutoka eneo ambalo mwili huo uliokotwa zilidai polisi hawakupiga picha pande zote za mwili huo ili iwe rahisi kwa mtu yeyote kuutambua.

Imeelezwa polisi walitafuta picha na kupata kutoka kwa mwananchi aliyezipiga kwa kutumia simu zikionyesha mwili huo ukiwa umelala kifudifudi.

“Ndiyo maana ukitazama polisi siku mwili unaokotwa wana picha moja ya marehemu akiwa amelala kifudifudi. Huu ndio utaratibu wa kiuchunguzi?” Alihoji mmoja wa wajumbe wa Serikali ya Mji wa Himo.

Swali jingine ambalo baadhi ya watu wamekuwa wakihoji ni jinsi polisi na daktari wa Hospitali ya Mawenzi walivyoruhusu mwili huo uzikwe wakidai ni wa mtu mzima mwenye ndevu wakati ni wa mtoto.

Pia, wanahoji ilikuwaje mwanafunzi atoweke shuleni tangu Novemba 6, lakini taarifa za kutoweka kwake zikafikishwa polisi siku tano baadaye.

Swali jingine ni kwanini polisi waliofika mahali sehemu ulipookotwa mwili huo, hawakuchukua sampuli za vipimo vya vinasaba (DNA) ili atakapojitokeza ndugu, waweze kuoanisha.

Utaratibu unataka maiti isiyojulikana inapookotwa yatolewe matangazo katika maeneo yote ya jirani, lakini katika tukio hilo, mwili ulichukuliwa na kupelekwa hospitali na baadaye kuzikwa.

Mwananchi

Yanayojiri nchini Zimbabwe




Baada ya jeshi kuchukua utawala nchini Zimbabwe,mkutano wa pili untarajia kufanyika kwa ajili ya kumshauri rais Robert  Mugabe kuyaachia madaraka.

Kwa mujibu wa habari,katika mkutano ujao padri wa Katoliki Fidelis Mukonor,Waziri wa Ulinzi Aaron Nhepera na msemaji wa Mugabe George Charamba watahudhuria.

Ripoti zimeonyesha kuwa wananchi wamekuwa wakikusanyika barabarani wakimtaka rais Mugabe ajiuzulu.

Toka Jumatano jeshi kuu la Zimbabwe limechukua utawala wa nchi hiyo mpaka pale hatma itakapojulikana.

CCM walia kufanyiwa fujo na upinzani K'njaro

CCM walia kufanyiwa fujo na upinzani K'njaro


Wakati kampeni za udiwani zikiendelea katika maeneo mbalimbali nchini, Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kilimanjaro kimedai kufanyiwa fujo na wafuasi wa upinzani pindi wafuasi wao wanapomaliza mikutano yao.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Katibu wa chama hicho mkoani hapa, Jonathan Mabihya katika mkutano wa kampeni za marudio ya uchaguzi wa udiwani Kata ya Bomambuzi.

Mabihya aliliomba Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua za kisheria wafuasi hao wa upinzani, huku akiwasisitiza wanachama wa CCM kutowajibu kwa fujo.

Katibu huyo aliwataka wanachama wote wanaoshiriki kwenye kampeni kufanya siasa safi na kunadi sera za chama hicho kwa kuzingatia sheria ikiwamo kufuata kanuni.

Pia, Mabihya aliwataka wananchi wa Kata ya Bomambuzi kutokubali kudanganywa kwa kilo moja ya nyama na sukari wanazopewa na wapinzani ili kuuza kura zao, badala yake wafanye uamuzi sahihi wa kuchagua kiongozi atakayewatumikia.

Pia, katibu huyo aliliomba jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kuingilia kati suala hilo akidai limekuwa likiwafifisha wafuasi wa chama hicho kushiriki katika mikutano yao kwa kuhofia kufanyiwa fujo.

Katibu msaidizi wa oganizesheni ya chama hicho, Steven Kazidi aliwataka wakazi wa Bomambuzi kutunza shahada zao za kupigia kura kwa ajili ya Novemba 26.

Aliwataka wananchi kutodanganyika na wapinzani kwa madai kwamba maendeleo yaliyopo wameyaleta.

“Wapo wanaopita majukwaani na kujitapa kuwa wao ndiyo wamewezesha maendeleo kwenye halmashauri zilizopo chini yao, ila si kweli, ukweli ni kwamba chama tawala ndicho kinachotoa fedha, kinatambua katika halmashauri kuna wananchi wao,” alisema Kazidi.

Aliwashauri wananchi kutokumchagua kiongozi kwa kuangalia fedha wala kabila bali wamchague mgombea wa CCM ili aweze kuwaletea maendeleo na kusimamia ilani ya uchaguzi inayoongoza dola.

Mgombea udiwani kupitia chama hicho, Juma Rahibu aliwataka vijana kutokubali kutumika na viongozi wa vyama vya siasa kwa lengo la kuhatarisha amani ya nchi.

Aliwashauri vijana kuungana ili kuhakikisha wanaleta maendeleo katika kata ya Bomambuzi.

Pia, aliwataka wakazi wa eneo hilo kuwa na msimamo katika shughuli za maendeleo huku akiahidi kuhakikisha anasimamia ilani ya uchaguzi pindi watakapompa ridhaa ya kuongoza.

“Mimi ni kijana mwenzenu, mkinichagua nitasimamia ilani ya chama changu pamoja na kuhakikisha asilimia tano zinazotengwa na halmashauri kwa ajili ya vijana zinawafikia vijana wote ndani ya kata hii,” alisema Rahibu.

Mwananchi.


Watu 19 wapoteza maisha kwenye ajali ya moto



Moto umeripotiwa kuteketeza jumba moja Pekin na kusababisha vifo vya watu 19.

Kwa mujibu wa habari,moto huo umetokea katika mji mkuu wa Pekin na kupelekea watu wengine nane kujeruhiwa.

Polisi wamekamata wale wote walioshtukiwa kuhusika na moto huo.

Majeruhi wamefikishwa hospitali haraka iwezekanavyo.

Uchunguzi zaidi wa chanzo hasa cha moto huo unafanyika.

Kumbe Dk Shika anajuana na Abromovich, ni shabiki wa Chelsea

Kumbe Dk Shika anajuana na Abromovich, ni shabiki wa Chelsea



Yule ' Bilionea wa nyumba za Lugumi'  Dk Louis Shika ambaye hivi karibuni alisema kuwa ni shabiki wa Chelsea kwa kuwa mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich ni rafiki yake, amefafanua zaidi.

Shika ambaye kitaaluma ni Daktari amesema kwamba, alikuwa akikutana na Abramovich mara kadhaa katika mikutano ya wadau.

Amesema kwa kuwa yeye ni mmiliki wa kampuni ya masuala ya kilimo, walikuwa wakikutana na Abramovich mara kwa mara katika mikutano ya viwanda.

“Mimi nilikuwa ninashughulika na masuala ya kilimo na yeye masuala ya mafuta. Sasa kule Urusi kuna kawaida ya makampuni kukutana.

“Kunakuwa na mikutano ya kuwakutanisha wamiliki kujadili mambo mbalimbali. Unajua kilimo pia kinahitaji mafuta na wauza mafuta wanawahitaji watu wa kilimo na makampuni mengine. Sasa pale nilikuwa ninakutana naye (Abramovich).

“Niliposikia kuwa yeye ndiye mmiliki wa Chelsea, basi nikaanza kuifuatilia na mwisho nikawa naipeda,” alifafanua