Sunday, 19 November 2017

Yanga yasema mechi itakuwa ngumu lakini watapambana



Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema mechi yao ya raundi ya 10 ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mbeya City itakuwa ngumu lakini watapambana washinde.

Lwandamiza amesema ni lazima wajitahidi washinde mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Uhuru leo jioni ili wasiachwe mbali na mahasimu wao Simba katika mbio za ubingwa.

“Tunaingia kwenye mchezo mgumu, lakini tutapigana tushinde, Mbeya City ni timu nzuri na kwa sababu imefungwa mechi mbili mfululizo leo watakuwa wakali sana, lakini tutajitahidi tushinde,”amesema Lwandamina.

Kwa matokeo ya ushindi wa bao 1-0 iliyopata Simba jana dhidi ya Tanzania Prisons yanainyima Yanga nafasi ya kukaa kileleni hata ikishinda leo. Simba sasa ina alama 22 ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga yenye alama 17. Ili kuipiku Simba, Azam FC yenye alama 19 inahitaji kushinda mabao 13-0 dhidi ya wenyeji Njombe Mji FC leo jioni.

Mechi nyingie ya kukamilisha mzunguko wa 10 leo itapigwa Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar wakiwakaribisha ndugu zao Kagera Sugar.

Ufaransa: Chama tawala chachagua kiongozi mpya

Ufaransa: Chama tawala chachagua kiongozi mpya




Chama tawala cha rais wa sasa Emmanuel Macron kimemchagua kiongozi wake mpya.

Kwa mujibu wa habari,ni miezi 19 toka chama hicho cha LREM(La Republique En Marche) kiundwe.

Msemaji wa serikali Christophe Castaner ndie amechaguliwa kama kiongozi mpya wa chama hicho.

Chama hicho kimefanya mkutano wake wa kwanza mashariki mwa mji wa Lyon.

Mgombea pekee wa nafasi hio, Castaner, 51, amechaguliwa kama kiongozi wa chama hicho na viongozi waliochaguliwa, mawaziri, watendaji wa chama na wanachama 200 wa chama.

Christophe Castaner hakuchaguliwa moja kwa moja na wanachama  380,000 wa LREM.

Atatumikia nafasi yake kwa muda wa miaka mitatu

Zanzibar kujenga Jengo jipya la Uwanja wa Ndege



Waziri wa Fedha na  Mipango Dkt Khalid Salum Mohamed (pichani) amesema ujenzi wa jengo jipya la uwanja wa ndege unatarajiwa kuanza tena  Disemba Mwaka huu chini ya ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China  kupitia Exim Bank.

Alisema ujenzi wa  jengo jipya ni miongoni mwa miradi  mitatu mikubwa ya maendeleo katika kukiimarisha kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume kiliopo Kisauni ambacho kinaumuhimu mkubwa kwa uchumi wa  Zanzibar.

Hayo aliyasema katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu changamoto zilizojitokeza ambazo zilisababisha kushindwa kukamilika ujenzi huo .

Alisema kutokamilika kwa muda mrefu jengo jipya la kuhudumia abiria kulipelekea changamoto ya kumudu kuhudumia ndege kubwa aina ya Code E kulingana na mahitaji ya sasa na uwezo wake wa idadi ya abiria wataohudumiwa kwa mwaka .

Aidha alisema utengenezaji wa jengo kuligana na mahitaji mapya ya shirika la usafiri wa anga la duniani (ICAO) na mkabala wake wa maeneo ya kuegesha ndege yaliojengwa kwa ufadhili wa benki ya dunia .

Alieleza kutokana na kadhia hiyo Serikali ililazimika  kuajiri mshauri maalumu kutoka kampuni ADPi kutoka ufaransa ili kuweza kuishauri vizuri juu ya utatuzi wa changamoto zilizobainika  .

Hata hivyo alisema marekebisho yaliyopendekezwa na kukubaliwa na Serikali yalipelekea kuongezeka kwa gharama za mradi kutoka dola 70.4 millioni hadi 128.7 million .

Alieleza gharama hiyo ni kwa ajili ya ujenzi wa jengo lenyewe eneo Zaidi la maegesho ya ndege la mita za mraba 38,000 na eneo la kuegesha gari za watumiaji wa uwanja ,abiria pamoja na wapokeaji abiria .

Waziri wa fedha alisema tatizo hasa lililojitokeza ni upatikanaji wa fedha za ziada ambapo awali Benki ya Exim ilitaka atafutwe mfadhili mwengine kwa kiasi hichi lakini baada ya mashauriano ya muda mrefu baina ya  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja  na Serikali ya Watu wa China hatimae walikubaliana kudhamini kwa mkopo wa kibiashara .

Alifahamisha kuwa kutokana  na jitihada kubwa za  Serikali na Rais wa Zanzibar  Dkt Ali Mohamed Shein Benki ya Exim ilikubali kudhamini mkopo wote wa kugharamia ujenzi huo kwa utaratibu wa mkopo nafuu.

“Benki ya Exim kwa sasa imekubali kudhamini gharama zote za dola 128.7 million kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo na kwa masharti ya  mkopo nafuu .“alisema Waziri .

Alifafanua kuwa tayari wiki hii Benki hiyo imeshamlipa mkandarasi madai yake ya dola 17.6 millioni kwa kazi ambazo ameshazifanya awali na kuidhinishwa na mshauri dola nyengine 17.6 millioni kwa kazi kama hizo lakini zenye dhamana mpya ya mkandarasi na tayari mkandarasi amelipwa jumla ya dola 35.2 millioni .

Nae Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji  Balozi Ali  Karume (pichani) alisema mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa na kufanikiwa kwa wakati uliopangwa kwa muda wa miezi 18 hadi 20.

Aidha alisema Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano itahakikisha inasimamia vizuri ujenzi huo na kuhakikisha inatatua matatizo madogo madogo yatakayojitokeza ili  lengo la serikali la kuhakikisha jengo hilo jipya la abiria linauwezo wa kuchukua abiria 1,
200,000 mpaka 1,600,00 kwa mwaka .

Hata hivyo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweza kuwashukuru Wananchi wa eneo la Chukwani   kwa ustahamilivu wao na imani yao kwa muda wote wakati serikali ikilitafutia ufumbuzi suala la mradi huo

Mugabe kukutana na makamanda wa jeshi leo



 Washirika wa karibu wa Rais Robert Mugabe kwenye chama alichokianzisha wanamtaka ajiuzulu wakati shinikizo dhidi yake zikiongezeka kufuata hatua za jeshi kutwaa madaraka.
Maafisa wa vyeo vya juu chamani wameanza kuwasili kwenye mkutano wa Zanu PF, ambapo watajadili ikiwa watamtimua chamani Mugabe.

Kitengo cha vijana wa chama ambacho awali kilkuwa mtiifu kwake Mugabe sasa kimemgeuka.
Nao makamanda wa jeshi wanatarajiwa kukutana na Mugabe baadaye leo.

Mkuu wa chama chenye nguvu cha wale waliopigania uhuru Chris Mutsvangwa, aliiambia Reuters kuwa Bw Mugabe anawea kuondolewa kutoka uongozi wa chama mke wake kupokonywa wadhifa wa mku wa kitengo ya wanawake.

Bw Mugabe amekuwa akizuiliwa nyumbani tangu jeshli litwae madaraka siku ya Jumatano.
Jeshi lilingilia kati baad ya Mugabe 93, kumfuta makamu wa rais Emmerson Mnangagwa.

Maelfu ya watu wakiwemo kutoka chama tawala na upinzani waliingia mitaani siku ya Jumamosi kushrehekea hatua ya jeshi na kumtaka Mugabe ang'atuke


Wanajeshi walidhibiti kituo kikuu cha matangazo cha serikali siku ya Jumatano.
Afisa mmoja wa jeshi jenerali Sibusiso Moyo, kisha akasoma taarifa kwenye televisheni akiihakikishia nchi kuwa Mugabe na familia yake walikuwa salama.

Jeshi linasema kuwa likuwa likiwalenga waalifu wanaomzunguka Mugabe na kukana kuwa hayo sio mapinduzi ya kijeshi.
Ijumaa Mugabe alionekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu aweke nchini ya kuzuizi cha nyumbani na jeshi, wakati alihudhuria sherehe za kufuza kwenye chuo cha Harare.

Hata hivyo Grace Mugabe hakuwa. Ilifikiriwa kuwa alikuwa ameondoka nchini humo lakini iliiibuka Alhamisi kuwa alikuwa nyumbani na Mugabe.


DC Handeni atoa onyo kwa wafugaji


Watendaji wa kata na vijiji wilayani Handeni mkoani Tanga, wameonywa na kutakiwa kuacha kuwaruhusu wafugaji kuingiza mifugo kwenye maeneo yao bila kufuata utaratibu. Atakaebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Onyo hilo limetolewa Novemba 18 na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, wakati akizindua zoezi la upigaji chapa mifugo (ng’ombe) wilayani humo katika kijiji cha Sua.

Gondwe amesema zipo taarifa kuwa kuna watendaji wa kata na vijiji bado wanapokea mifugo kinyemela.

Mkuu huyo wa wilaya alisema zoezi la kupiga chapa mifugo hiyo litasaidia kubaini mfugo katika kila eneo kutokana na alama zinazowekwa.

Alisema zipo taratibu za kupokea mifugo hivyo ni vizuri zifuatwe ili kuweza kuibaini mifugo ambayo inaweza kuingia na magonjwa na kusababisha maambukizi ya magonjwa.

Akielezea dhumuni ya zoezi hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Makufwe, alisema hikolo ni zoezi la kitaifa lililoagizwa kutoka ngazi za juu likiwa na nia ya kuondoa migogoro ya mara kwa mara, hivyo ni muhimu wafugaji wote kushiriki.

Alisema kwa halmashauri ya Handeni zaidi ya ng’ombe 30,000 wanatarajiwa kupigwa chapa ili iwe rahisi kutambuliwa, kuweza kusajiliwa na  kudhibiti mifugo iliyopo wilayani humo.

Aidha, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Handeni, Athumani Malunda, amewataka wafugaji kuepuka migogoro na wakulima kwa kulisha mifugo yao kwenye mashamba huku wakitoa lugha za maudhi  kwa wenzao.

Mmoja wa wafugaji mkazi wa Mkata, Omari Bigo, ameipongeza serikali  kwa kuendesha zoezi hilo na kusema kuwa litasaidia udhibiti wizi wa mifugo.

Serikali wilayani Handeni imetoa siku 45 hadi Disemba 31 kwa wafugaji wote kuhakikisha wamepeleka ng’ombe wao kupigwa chapa na atakayeshindwa kufanya hivyo atatozwa faini isiyozidi Sh1 milioni kwa kukiuka agizo.

Mwananchi.



Barnaba uzalendo umemshinda Mama Steve



Mwanamuziki anayefanya poa kwenye game ya Bongofleva Barnaba Classic ameshindwa kujizuia kwenye siku ya kuzaliwa mama wa mtoto wake Zuwena ambaye kwa sasa hawapo pamoja kwa kumshukuru kuwepo na kumpatia zawadi ya mtoto.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Barnaba amesema kwamba upendo wake juu ya zawadi mwanadada huyo aliyempati ipo palepale na kusisitiza kwamba anamuheshimu huku akimsisitizia kwamba anapenda kumuona akiwa furaha.

"Wewe ni rafiki Yangu na ndugu yangu Uvungu wa moyo wangu unakushukuru kwa kuwa daraja kwenye maisha yangu na nashukuru nimevuka salama matatizo ni sehemu ya kila mwanadamu upendo wangu juu ya zawadi uliyonipatia Iko pale pale/STEVE Na Kitu kizuri ninakuheshimu Sana mbali Na mambo Yote Na Kitu kingine Furaha Yangu kuona unaendela Kutabasamu Hata kama ilo Tabasamu Silitengenezi Mimi," Barnaba

Aidha Barnaba ameongeza kwamba anamtakia kila la kheri mwanadada huyo ambaye tayari amekwishaingia kwenye mahusiano na kumwambia anapenda yeye awe shuhuda wa maisha ya mzazi mwenzake huyo kwa kila jambo.

"Nakutakia maisha mema yenye baraka, nawaombea heri Katika Familia yako, nakuombea heri na uwahi uwe shuhuda wangu nami niwe shuhuda wako wa kila jambo heri ya siku yako ya kuzaliwa mzazi mwenzangu mama yake Steve, Zuunamela mama watoto ! Damu Ya yesu ikuangazie Amina,"  Barnaba

Mtanzania mwingine afuzu majaribio timu ya AFC ya Sweden

Mtanzania mwingine afuzu majaribio timu ya AFC ya Sweden



Kiungo mshambuliaji Rashid Chambo ,17, amefuzu kucheza kuitumikia timu ya AFC ya Sweden.

AFC ndiyo timu anayofanya majaribio Mtanzania, Said Hamis Ndemla.

Chambo kutoka JKT Ruvu alikwenda kufanya majaribio katika timu hiyo mwezi uliopita na sasa amefuzu.

Pamoja na kufuzu timu ya vijana, kocha amependekeza awe anapewa nafasi katika timu ya wakubwa.

“Kocha kaona ana kipaji, hivyo atakuwa akitumiwa pia na timu ya wakubwa. Lakini timu ya vijana inapokuwa na mechi, basi anakwenda kucheza,” kilieleza chanzo kutoka Sweden

Mbowe kumnadi mgombea aliye mahabusu

Mbowe kumnadi mgombea aliye mahabusu



Wakati Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe akitarajiwa kuwahutubia wakazi wa Kata ya Mhandu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani, mgombea wa chama hicho, Godfrey Misana yupo mahabusu kutokana na kukabiliwa na shitaka la kujeruhi.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Boniphace Nkobe  amesema Mbowe ameambatana na aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu.

Amesema mkutano huo pia utahudhuriwa na aliyekuwa mbuge wa Nyamagana, Ezekia Wenje na utafanyika saa kumi jioni.

Misana (46), mgombea udiwani wa Chadema katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Novemba 26,2017 na kampeni meneja wake, Charles Chinjibela (37) Ijumaa Novemba 17,2017 walipandishwa kizimbani wakidaiwa kumjeruhi meneja wa kampeni za CCM katika kata hiyo, Thomas Warioba.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, mbele ya hakimu Ainawe Moshi wanadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 14,2017.

Akisoma mashtaka katika shauri hilo namba 540/2017, mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Elizaberth Barabara alidai washtakiwa walitumia visu na mawe kumjeruhi Warioba.

Upande wa Jamhuri uliomba Mahakama kuzuia dhamana ya washtakiwa kwa kile ilichoeleza ni kwa usalama wao.

Ombi hilo la Jamhuri limepingwa na wakili wa utetezi, Gasper Mwanaliela.

Wakili Mwanaliela alisema dhamana ni haki ya wateja wake na kwamba, kuwanyima kutawazuia kushiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26,2017.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu Moshi alisema Mahakama itatoa uamuzi kuhusu dhamana Novemba 21,2017. Washtakiwa walipelekwa mahabusu


Profesa Lumumba awakingia kifua JPM, Kagame


MWANAZUONI maarufu barani Afrika, Profesa Patrick Lumumba, amesema Rais Dk. John Magufuli na Rais wa Rwanda, Paul Kagame si madikteta bali wanachokifanya ni kuhakikisha kunakuwa na siasa za miiko na maadili.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana katika Mkutano wa Pan African Humanitarian wa mwaka huu ulioandaliwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (Yuna) uliokuwa na kaulimbiu ya “amani inawezekana jana, sasa na kesho” na kuwakutanisha vijana kujadili nafasi zao katika kuleta amani barani Afrika.

Profesa Lumumba ambaye ni raia wa Kenya, alisema katika miaka ya hivi karibuni, wamekuja viongozi wenye mwelekeo na uchungu wa kuhakikisha mataifa yao yanaendelea, lakini baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwaita madikteta.

“Tunapaswa kujua hawa watu tunaowaita madikteta ni akina nani, kwa sababu kuna viongozi wameibuka katika miaka mitatu hadi 20 iliyopita, wakiwa na mwelekeo na kuona uchungu wa kuhakikisha mataifa yao yanaendelea, lakini baadhi ya watu wengine wanawaita eti ni madikteta,” alisema na kuongeza:

“Lakini viongozi hao ni watu wazalendo na wakereketwa wa maendeleo endelevu, hivyo watu kama hawa lazima tujiulize mienendo yao ni ya kidikteta? Au ni ya kuhakikisha mataifa yao yanapiga hatua za haja na hoja. Mfano wengine wanasema Kagame, Dk. Magufuli ni dikteta, sikubaliani nao kwa sababu kile ambacho wanakifanya, wanajaribu kusema kwamba lazima kuwe na siasa za miiko na maadili.

“Nakubali kwamba udikteta ni jambo ambalo halistahili, lakini ni muhimu kuhoji kwamba uhuni ndiyo demokrasia? Kwa sababu kumeibuka wimbi la watu ambao ni wababaishaji hata sio wapinzani, kila kitu anachokifanya (rais) wao kazi yao ni kupinga.”

Akizungumzia suala la amani, hasa katika vipindi vya uchaguzi, alisema ni wakati wa kujiuliza ni aina gani ya uongozi inahitajika barani Afrika ili kuwe na njia ya kubadilisha uongozi isiyoleta vurugu tofauti na ilivyo sasa.

“Pia tunapaswa kuangalia hivi vitu tunavyoviita vyama, ni vyama kweli au ni vikundi tu, genge tu la vibarua waliokuja kujitafutia nyadhifa ili kupora mali za Waafrika. Vijana ndio wataibua hoja hii na kutathimini kuwa mataifa yetu tunayaandaa kwa minajili ya kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo,” alisema.

Pia alisema anaamini Afrika itakuja kuwa na amani na utulivu kwa sababu jitihada mahsusi zimeshaanza kufanywa na viongozi wake na tayari wamekwisha kutoa tamko kwamba kufikia mwaka 2020, lazima vitu vinavyoleta migogoro vitolewe na kila mtu anatakiwa kushiriki kwa nafasi yake.

Mtanzania


Zimbabwe: Chama cha Zanu-PF kimemfuta Mugabe kama kiongozi wake

Zimbabwe: Chama cha Zanu-PF kimemfuta Mugabe kama kiongozi wake


Chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF kimefuta Robert Mugabe kama kiongozi wake.

Kimemtua aliyekuwa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa ambaye alifutwa wiki mbili zilizopita kama kiongozi wake.

Kufutwa kwa Bw. Mnangawa kumezua mambo mengi huku jeshi likitwaa madaraka na kumzuia Mugabe 93, kumteua mke wake Grace kama makam wa rais.

Maelfu ya watu nchini Zimbabwe waliingia barabarani siku ya Ijumaa kuandamana kumpinga Bw. Mugabe.

Bw. Mugabe anatarajiwa kukutana na makanda wa jeshi na msafara wa magari umeonekana ukiondoka makao ya rais.

Mkuu wa chama chenye nguvu cha wale waliopigania uhuru Chris Mutsvangwa, aliiambia Reuters kuwa chama kilikuwa kinaanza mchakato wa kumuondoa Mugabe madarakani kama rais

Bifu la Ronaldo na Ramos lafikia mwisho

Bifu la Ronaldo na Ramos lafikia mwisho


KOCHA wa klabu ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, Zinedine Zidane, ameweka wazi kuwa nyota wake, Cristiano Ronaldo na nahodha Sergio Ramos, wamemaliza tofauti zao.

Uongozi wa klabu hiyo uliwakutanisha wachezaji hao juzi, kabla ya kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid kwenye Ligi Kuu nchini Hispania.

Sababu za wawili hao kuwa kwenye mgogoro ni baada ya Real Madrid kukubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Tottenham kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Novemba 1, kwenye Uwanja wa Wembley, hivyo Ronaldo akatupia lawama kwa uongozi wa klabu hiyo kwa kudai kwamba, walifanya makosa makubwa kuwauza wachezaji wao, James Rodriguez na Alvaro Morata.

Kauli hiyo ya Ronaldo ilionekana kumchukiza sana Ramos na ndipo nahodha huyo alisema kuwa, Ronaldo ni mchezaji mbinafsi sana na hakupaswa kuongea kauli kama hiyo na alitakiwa kushirikiana na wenzake ili kuisaidia timu.

Hata hivyo, baada ya mgogoro huo kuwa mkubwa, Ronaldo aliweka wazi kuwa, hana mpango tena wa kuendelea kuwa na timu hiyo mara baada ya kumaliza mkataba wake.

“Ni wazi kwamba Sergio Ramos ni miongoni mwa wachezaji wenye akili sana ndani na nje ya uwanja, anaweza kumwambia kitu mchezaji yeyote hata kama ni Cristiano Ronaldo, isitoshe wachezaji hao wamekuwa pamoja kwa muda mrefu na wamezoeana.

“Mchezaji huyo alistahili kumwambia hivyo Ronaldo kutokana na kauli yake, lakini ukweli ni kwamba kila kitu kipo sawa kwa sasa, uongozi wa klabu uliamua kukaa pamoja na wachezaji hao kwa ajili ya kumaliza tofauti zao na kila kitu kinakwenda sawa sasa.

“Kwa pamoja naweza kusema nina wachezaji wawili kwenye kikosi ambao wanatengeneza historia ndani ya timu hii, wamekubali kumaliza tofauti zao ili kuweza kuipigania timu yao katika michezo inayofuata,” alisema Zidane.

Wababe hao wa soka barani Ulaya, msimu huu wanaonekana kuwa wameuanza vibaya kutokana na kiwango chao na ushindi wanaoupata, huku baadhi ya mshabiki wakidai kuwa, mshambuliaji wao huyo ambaye ana tuzo nne za Ballon d’Or, amekuwa kwenye kiwango cha chin

Diego Simeone: Griezmann anaweza kuondoka baada ya kuzomewa Jana



KOCHA Diego Simeone amedokeza kwamba Antoine Griezmann anayetakiwa na Manchester United, anaweza kuondoka Atletico Madrid.

Simeone amesema hayo baada ya kuulizwa mustakabali wa Griezmann kufuatia kuzomewa wakati Atletico Madrid ikilazimishwa sare ya 0-0 na Real Madrid jana katika La Liga.

Kocha huyo wa Atletico alimpumzisha mshambuliaji wake huyo Mfaransa kwa mara ya pili mfululizo kwenye mechi ya ligi na akazomewa kipindi cha pili wakati anakwenda benchi.

Simeone alisema: "Nyumbani nilifundishwa kwamba wakati mmoja wenu anapokuwa sehemu ya familia unapaswa kuwasimamia hadi kifo,".

Na kwa sababu mashabiki wa Atletico Madrid wamekwishaanza kuhisi siki za Griezmann zinahesabika kutokana na kutakiwa na United waliokaribia kumsajili msimu huu na Barcelona wanamtaka pia kwa mwakani.

Griezmann amefunga mabao mawili tu msimu huu katika mechi 10 alizocheza na Simeone amerudia mara mbili kusema katika mkutano na Waandishi wa Habari.

"Unamsapoti mtu hadi kifo hadi atakapokuwa si sehemu ya familia yako tena,".

Kiungo Saul amesema: "People wanatakiwa kumtetea. Greizman ni mchezaji wetu muhimu na tunatakiwa kumsapoti wakati wote,".

Dau la kumnunua Griezmann lilikuwa Euro Milioni 200 January mwaka huu, lakini litapungua hadi Milioni 100 msimu ujao.

Manchester United ilikaribia kumsajili msimu huu, lakini ikashindwa kutokana na Atletico Madrid kufungiwa kusajli mchezaji mpya hadi mwaka 2018.

Nyota ya Sane yazidi kung'aa Epl


Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Leroy Sane, amefanikiwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini England wa Oktoba, baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda michezo mitatu mfululizo mwezi huo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, amekuwa tegemeo kwenye kikosi cha kocha Pep Guardiola na amekuwa akipachika mabao mengi pamoja na kupiga pasi za mwisho katika michezo mbalimbali. Katika michezo mitatu ya Oktoba, ameweza kufunga kila mchezo na kutoa pasi ya mwisho.

Kutokana na mabao sita aliyoyafunga mchezaji huyo na kutoa pasi tano za mwisho ndani ya Ligi Kuu, mchezaji huyo ameingia kwenye orodha ya wachezaji wanaotengeneza nafasi nyingi msimu huu akiungna na mshambuliaji wake Sergio Aguero ambaye ana mabao nane na pasi tatu za mwisho.

Katika ushindi wa mabao 7-2 dhidi ya Stoke City, alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya mwisho, huku ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burnley, alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya mwisho, sawa na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya West Brom.

Sane anakuwa mchezaji wa pili kutoka nchini Ujerumani kuchukua tuzo hiyo, huku mchezaji wa kwanza akiwa Jurgen Klinsmann, ambaye aliwahi kuichukua wakati anakipiga katika kikosi cha Tottenham, Agosti 1994.

Katika tuzo hiyo, Sane alikuwa anashindana na wachezaji watano ambao ni pamoja na mchezaji mwenzake wa timu hiyo, kiungo Kevin De Bruyne, beki wa klabu ya Arsenal, Nacho Monreal, Glenn Murray kutoka Brighton, kipa wa klabu ya Burnley, Nick Pope na nyota wa klabu ya Crystal Palace, Wilfried Zaha.

“Ninashukuru sana kwa ushirikiano ninaoupata kutoka kwa wachezaji wenzangu, ninaamini kwa hali hii tunaweza kufanya makubwa msimu huu, nawashukuru wote kwa sapoti,” alisema Sane.

Hata hivyo, kutokana na mchango wa Sane ndani ya Man City, amemfanya kocha wake, Guardiola na yeye kuchukua tuzo ya kocha bora wa Oktoba nchini England