Sunday, 29 October 2017

Wabunge waibua hoja hii

Wabunge waibua hoja hii

Dodoma.Hoja ni kiongozi gani kati ya wabunge, wakuu wa wilaya na mikoa ni mkubwa kwa cheo imeibuka kwenye semina ya wabunge mjini Dodoma.

Hoja hiyo imeibuka leo Jumapili Oktoba 29,2017 katika semina ya wabunge wa kamati mbili za Bunge kuhusu masuala ya kidiplomasia na itifaki.

Semina hiyo imeandaliwa na Bunge kupitia mradi wa kujengea uwezo wabunge na wawakilishi unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP).

Washiriki wa semina ni wajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama; Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na wawakilishi kutoka vyama vya kibunge.

Akizungumza katika majadiliano, Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeshi Hillal ametoa mfano wa ziara za kikazi akisema mbunge huwekwa wa mwisho, akitanguliwa na mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya.

“Unakuta mkoa katika ziara gari la mbele yupo RC ameweka bendera, linalofuatia ni la DC naye ameweka bendera na la mbunge linakuwa nyuma. Tunaomba utufafanulie katika hilo,” amesema.

Katika hilo, Mbunge wa Morogoro Kusini-Mashariki (CCM), Omary Mgumba amesema mkuu wa wilaya anamwakilisha Rais na katika wilaya nyingine huwa zina majimbo mawili ya uchaguzi, hivyo kumfanya mbunge kuwa na eneo dogo la kiutawala ikilinganishwa na mkuu wa wilaya.

“Siku zote ukweli ni mchungu na hasa ukiwa hutaki kuusikia. Utakuta wilaya moja ina majimbo mawili, mbunge wa jimbo moja utawala wake ni kwenye jimbo lake tu lakini mkuu wa wilaya ni mtawala katika majimbo yote mawili yaliyo katika wilaya yake,” amesema.

Akizungumzia hilo, Mbunge wa Mtambile (CUF), Mosoud Abdallah, amehoji itifaki inazungumzaje kuhusu mbunge wa jimbo na wa viti maalumu wanapokuwa jimboni.

“Tunapokuwa jimboni ni mbunge gani anakuwa mkubwa kwa cheo kati ya mbunge wa viti maalumu na wa jimbo,” amehoji.

Akijibu hoja hizo, ofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Kitengo cha Uhusiano wa Kimataifa, Ally Masabo amesema kiitifaki mkuu wa mkoa ndiye mwenye mamlaka katika mkoa, hivyo ndiye anayetakiwa kuwa mbele katika msafara mkoani.

"Suala hili wabunge wana wajibu wa kuangalia, na utatuzi upo kwenu wabunge," amesema Masabo ambaye ametoa mada katika semina hiyo.

Mwananchi:

Uchebe aahidi kumfanyia makubwa Shilole kwenye 'honeymoon'

Uchebe aahidi kumfanyia makubwa Shilole kwenye 'honeymoon'

Mume mtarajiwa wa msanii ambaye ni mfano wa kuigwa kwa mabinti kutokana na juhudi zake za kupambana na maisha, Zuwena Mohamedi au Shilole, ameweka wazi matarajio ya kumpeleka Ulaya kula 'honey moon' mke wake huyo mtarajiwa.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, mwanaume huyo anayejulikana kwa jina la Uchebe, amesema ndoa yake na msanii huyo itakuwa mwezi wa 12 mwaka huu kwa kuwa ameshakamilisha taratibu zote za kuhalalisha mahusiano yake na msanii huyo.

"Mwenyezi Mungu afanyie wepesi sasa hivi tupo kwenye maandalizi, na akipenda mwezi wa 12 itakuwa ndoa kwani taratibu zote nishafuata, mahari mi nishamaliza sidaiwi, na honey moon nampeleka Ulaya", amesema Uchebe ambaye ndiye shemeji yetu kwa Shilole.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kwamba wawili hao wameachana, na Shilole kukanusha taarifa hizo na kusema kwamba wawili hao bado wapo pamoja.

Fahamu kwamba pamoja na vituko vyake vingi, Shilole ni mfano bora kwa mabinti kutokana na bidii anazoonyesha kwenye kupambana na maisha, ambapo mpaka sasa ni mjasiriamali mkubwa, kwa kuwa na mgahawa wa chakula, bidhaa ambayo ni brand yake pamoja na kusimamia wasanii wengin
e.

MAGAZETI YA LEO 29/10/2017

Milipuko miwili yatokea mji mkuu wa Somalia

Milipuko miwili imetokea mjini Mogadishu nchini Somali chini ya wiki mbili baada ya shambulio kubwa la bomu kuwaua watu 350.

Mlipuko wa kwanza ulitokea baada ya gari lililokuwa limetegwa bomu kuvurumishwa na kuingizwa kwa nguvu hotelini.

Wanamgambo wenye silaha kisha walifuata na kuingia ndani ya jengo hilo.

Milio ya risasi ingali ikiendelea kusikika ndani ya hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, ambao ulishambuliwa na kundi la kigaidi la kiislamu, la Al- Shabaab. Yamkini watu 17 wanasemekana kuuwauwa kufikia sasa. Wanamgambo hao wanasemekana kuvamia jumba la Hoteli hiyo, mara tu baada ya mabomu mawili kulipuka nje ya majengo hayo.

Duru zinasema kuwa watu kadhaa wamepigwa risasi ndani ya hoteli hiyo, wakiwemo watoto na mbunge mmoja wa zamani.

Hoteli hiyo ilipangiwa kuandaa mkutano wa kiusalama leo Jumapili.

Majuma mawili yaliyopita, mji wa Mogadishu, ulikumbwa na shambulio baya zaidi la bomu kuwahi kutokea nchini Somalia, amabapo zidi ya watu 350 waliuwawa.

Mlipuko wa pili ulitokea karibu na majengo ya zamani ya bunge ambayo yamo hapo karibu.
Bado haijabainika idadi ya waliofariki.

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabaab ambalo lililaumiwa kwa shambulio hilo la wiki mbili zilizopita, ingawa halikujitokeza kukiri, limejitokeza na kusema lilitekeleza mashambulio hayo ya leo.

Afisa wa polisi Mohamed Hussein ameambia shirika la habari la Reuters kwamba: "Watu zaidi ya saba wamefariki wakiwemo wanajeshi na raia."

Shirika la huduma ya dharura la Aamin mjini humo limesema tayari limesafirisha majeruhi 15 hadi hospitali na kwamba kulikuwa na "miili mingi ya waliofariki".

Afisa wa polisi Ibrahim Mohamed ameambia AFP kwamba katika mlipuko wa pili, gari lililokuwa limejazwa vilipuzi lililipuka karibu na makutano ya barabara.

Shambulio hilo limetekelezwa huku viongozi wa mkoa wakikutana mjini Mogadishu kwa mkutano Jumapili kukubaliana kuhusu mkakati wa pamoja wa kukabiliana na al-Shabab.

Shambulio lililotekelezwa tarehe 14 Oktoba lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 358.
Watu 56 bado hawajulikani walipo

Joshua amdunda Mfaransa, Zlatan ashuhudia pambano

Bondia Carlos Takam kutoka Ufaransa ambaye alionekana kama sugu hivi, mwisho alishindwa kuvumilia ukali wa makonde ya Anthony Joshua katika raundi ya 10.

Joshua amemshinda Takam katika pambano la uzito wa juu kuwania mkanda wa IBF lililomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Cardiff.

Kabla Joshua alikuwa azichape na Kubrat Pulev lakini aliumia na kujitoa na Takam akachukua nafasi yake

England watwaa kombe la Dunia


Wachezaji wa England wakishangilia ubingwa wa Kombe la Dunia la Vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya ushindi wa 5-2 dhidi ya Hispania leo mjini  Kolkata, India. Mabao ya England yalifungwa na Rhian Brewster, Morgan Gibbs White, Phil Foden mawili na Marc Guehi, wakati ya Hispania yalifungwa na Sergio Gomez.

Messi atupia bao la 12< Barca yashinda 2-0

Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la kwanza dakika ya 36 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao usiku wa Jumamosi Uwanja wa San Mamés Barria mjini Bilbao, ambalo linakuwa bao lake la 12 katika mechi 10 za La Liga msimu huu. Bao la pili la Barca lilifungwa na Paulinho dakika ya 90 na ushei.

Goli la Kichuya lanunuliwa kwa Tsh. 500,000

Mashabiki wa Simba kundi la Simba Kwanza (SK) wamekabidhi shilingi 500,000 Shiza Kichuya baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi ‘Man of the Match’ ikiwa ni kutokana na goli alilowafunga watani wao wa jadi mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana 1-1.

Mashabiki hao wamemchagua Kichuya kuwa Man of the Match wakiwa wameridhishwa na kiwango alichokionesha kwenye mchezo huo.

Kichuya aliifungia Simba bao la kuongoza lakini baadae goli hilo lilisawazishwa na Obrey Chirwa na kulazimisha timu hizo za Kariakoo kugawana pointi.

Mmoja wa viongozi wa kundi hilo amesema, huo utakuwa ni utaratibu wao wa kila mechi kutoa zawadi ya pesa kwa mchezaji atakaefanya vizuri kwenye mechi.

Ameahidi kuwa, mechi ijayo ya Simba (Mbeya City vs Simba November 5, 2017) watatoa kisasi cha shilingi 2,000,000

Cuba yakanusha kuwashambulia kwa sauti wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani

Cuba yakanusha kuwashambulia kwa sauti wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani


iC uba inasema kuwa hakujakuwa na mashambulizi ya kutumia sauti dhidi ya wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani kwenye mji wake mkuu Havana, ikisema kuwa madai hayo ni kisiasa yenye lengo la kuharibu uhusiCuba inasema kuwa hakujakuwa na mashambulizi ya kutumia sauti dhidi ya wafanyakazi wa ubalozi ano kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Cuba Bruno Rodriguez alipinga madai hayo ya kuwepo mashambulizi ya sauti akiyataja kuwa kuwa uwongo.

Marekani inasema kuwa karibu wafanyakazi wake 20 katika ubalozi wake walikumbwa na matatizo ya kiafya na kuwapunguza wafanyakazi wake kutokana na kisa hicho.

Ripot zinasena kwa hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na mashambulizi ya sauti lakini hata hivo hakuna kile kimethibitishwa.

Marekani haijailaumu Cuba kwa mashambulizi hayo, na serikali ya Cuba imekana mara kwa mara kuwalenga wafanyakazi wa ubalozi. wa Marekania mjini Cuba.

Marekani iliwatimua wanadiplomasia watano wa Cuba, ikisema kuwa Cuba ilishindwa kuwalinda wafanyakazi wake.

Serikali ya Marekani pia ilifuta shughuli za utoaji visa katika ubalozi wake mjini Havanna
Akizungumza mjini Washington wakati wa mkutana na raia wa Cuba wanaoishi nchini Marekani, Bw. Rodriguez alisema kuwa madai hayo yamesababisha kuharibika kwa uhusiano kati ya serikali hizo mbil

Mtibwa Sugar yaweza kurejea Kileleni leo

MTIBWA Sugar inaweza kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo kama itashinda dhidi ya Singida United.

Wakata Miwa hao wa Manungu wanawakaribisha Singida waliopanda Ligi Kuu msimu huu kwenye Uwanja wa Manungu Arena, Morogoro kuanzia Saa 10:00 jioni.

Na baada ya mahasimu wa jadi, Simba na Yanga kumalizana kwa sare ya 1-1 jana Uwanja wa Dar es Salaam na wote kufikisha pointi 18 baada ya mechi nane, wastani wa pointi mbili kwa mcheszo, Mtibwa wanahitaji kushinda kurudi juu.

Kwa sasa, Mtibwa Sugar ya kocha Zuberi Katwila ina pointi 15, baada ya kucheza mechi saba, maana yake ikishinda leo itafikisha pointi 18.

Lakini hilo halitarajiwi kuwa jepesi mbele ya Singida, inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm ambayo ni mshindani kweli.

Kwa ujumla, Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea leo baada ya mechi mbili za Raundi ya nane kuchezwa juzi na jana, nyingie Azam FC wakiifunga Mbeya City 1-0 Ijumaa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mechi nyingine za leo, Maji Maji wanaikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Lipuli FC wanaikaribisha Mbao FC Uwanja wa Samora mjini Iringa, Kagera Sugar wanaikaribish Ndanda FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Njombe Mji FC wanaikaribisha Stand United Uwanja Saba Saba, Njombe na Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine mjini Iringa.

DRC: Watu milioni 3 wamo hatarini ya kufaa nja

Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi ya watu milioni tatu wamo katika hatari ya kufa njaa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kiongozi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia mpango wa chakula Duniani- WFP, ametoa wito wa msaada wa dharura wa kimataifa, ili kumaliza matatizo ya baa la njaa, nchini DR Congo.

David Beasley, ambaye anafanya ziara yake ya kwanza kabisa, katika jimbo linalokumbwa na msukosuko wa mapigano na uasi la Kasai, ameiambia BBC kuwa, zaidi ya watu milioni tatu, wanakabiliwa na baa la njaa.

Anasema kwamba, timu ya wafanyikazi wake, wameshuhudia watoto ambao wanakabiliwa na matatizo ya utapia mlo, huku mamia kwa maelfu yao, wakiwa katika hatari ya kufa, katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo, ikiwa msaada hautawafikia.

Mapigano mabaya yalianza katika jimbo hilo la Kasai mwezi Agosti mwaka 2016, baada ya kiongozi mmoja wa kitamaduni kuuwawa, katika mapigano na wanajeshi wa kulinda amani.

Ghasia mpya imesababisha mauwaji ya watu elfu tatu na kuwafurusha zaidi ya watu milioni moja, wengi wao wakiwa ni watoto kutoka nyumbani kwao.

BBC

Nape Nnauye na Waziri Nchemba walikuwepo jana kushuhudia mechi ya Simba na Yanga

Waziri wa zamani wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakifuatilia mechi ya mahasimu wa jadi, Simba na Yanga.

Jakaya Kikwete amtumia salamu za heri ya kuzaliwa Rais Magufuli

Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amemtumia ujumbe Rais wa sasa wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kuhusu siku yake ya kuzaliwa ambayo ni leo Oktoba 29.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Jakaya Kikwete ameandika ujumbe huo wa kumtakia heri, huku akizidi kumuombea kwa Mungu, ampatie afya na siha njema.

"Nakutakia kila la kheri Mhe Rais Magufuli unaposherehekea siku yako ya kuzaliwa. Nakutakia afya na siha njema na umri mrefu zaidi", ameandika Jakaya Kikwete.

Leo Oktoba 29, Rais Magufuli anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo anatimiza miaka 57, tangu alipozaliwa mwaka 1959 huko wilayani Chato mkoani Geita