Friday, 27 October 2017

Chebukati ataja idadi ya Wakenya waliopiga kura

Chebukati ataja idadi ya Wakenya waliopiga kura

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amedai kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba Wakenya wapatao 6,553,858 wamejitokeza na kupiga kura. Hii idadi imejumuishwa kutoka kwa maeneo bunge 267 nchini.

Awali alitangaza kuahirisha uchaguzi kwenye gatuzi nne za mkoa wa Nyanza baada ya wafuasi wa Raila wamekinukisha kule na kuvuruga shughuli za upigaji wa kura kufanyika. Hivyo ameahirisha hadi Jumamosi.

Dkt. Kigwangalla afanya kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama Ngorongoro

Dkt. Kigwangalla afanya kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama Ngorongoro

Waziri wa maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigangwala amesema kuwa watoa huduma mbalimbali za utalii watatakiwa  kufuzu mtihani kabla ya kupewa leseni mpya kuanzia Januari 2018 ambapo Serikali itaandaa utaratibu mpya katika sekta hiyo.

Ambapo alisema kuwa Wizara yake iko katika mchakato wa kuandaa mwongozo kwa ajili ya makampuni ya utalii nchini pamoja na kufunga mashine maalumu ambayo itadhibiti mapato yatokanayo na utalii.

Aliongeza kuwa wizara yake itarekebisha mfumo wa watoa huduma katika sekta hiyo ambao umekuwa ukilalamikiwa na wadau mbalimbalui hasa watoa huduma za utalii wanaowashawishi watalii kutoka nchi mbalimbali za nje kuja kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini.

Dk. Kigangwala aliyasema hayo jana wakati alipokuwa anazungumza na watumishi wa Shirika la hifadhi la Taifa (Tanapa)katika ziara yake ya kutembelea ofisi mbalimbali za shirika hilo.

Alisema lengo hasa lakuanzisha mchakato huo utakaoanza kutumika mapema mwakani nikuweka vigezo vitakavyotolewa na Serikali kwa makampuni ili kuhakikisha wanakuwa na wahudumu watakaothibitishwa na wizara yake na kutoa cheti maalum kwa kila anaetoa huduma hiyo ya utalii.

Waziri huyo alisema lengo nikuboresha huduma za utalii ili kuwezesha upatikanaji bora wa huduma za utalii na mapato ambayo yanainua uchumi kwani Tanzania sasa inashindana na nchi mbalimbali katika kuvitangazavivutio vya utalii ili kuhakikisha watalii wenguwanakuja zaidi nchini kwetu.

Pia aliongeza kuwa watoa huduma za utalii wanapaswa kuzungumza vizuri kutoka nchi mbalimbali ili waweze kuja lakini pia waangalie jinsi ya kuboresha huduma za utalii ikiwemo mapatona mfumo huu mpya wa kukusanya mapatio ua sekta ya utalii kuboreshwa kuongeza mapato kwa mfumo wa kieletronik.

Aliongeza kuwa maeneo wanayoweka mkazo zaidi ni ukusanyaji wa mapato hiyvyo kutakuwa na dirisha moja litakalounganisha taasisi za utalii kujua mapato yanayoingia nikiasi gani na mtalii anakaa nchini kwa muda gani na hoteli ip na kujua mapato yamnayokusanywa kwa sekta ya utalii yanakuwa kwa kiasi gani.

Kwa upande wake Mkurugeni wa Tanapa Allan Kijazi alisema kuwa utaratibu huo utakuiwa mzuri na kpia wako katika mchakato wa kufungua ofifi katika mkoa wa dodoma ili kuweza kusogeza huduma mbalimbali zinazotoklewa nashirika huilo ili kuboresha sekta ya utalii na kuongeza pato la nchi kupitia sekta hiyo.

CHADEMA kwenda Mahakamani kumnasua Mkurugenzi wake Polisi

CHADEMA kwenda Mahakamani kumnasua Mkurugenzi wake Polisi

Baada ya Polisi kuendelea kumshikilia Mkurugenzi wa Chadema wa Operesheni na Mafunzo, Kigaila Benson chama hicho kimesema kimekwenda Mahakama Kuu kuiomba itoe amri kwa jeshi hilo kumfikisha kortini.

Wakati Chadema ikisema hayo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa jana  Alhamisi Oktoba 26,2017 alisema, “Upelelezi unaendelea na huenda kesho(Ijumaa hii) akafikishwa mahakamani.”

Kigaila anashikiliwa na polisi tangu Jumatatu Oktoba 23,2017 aliporipoti Kituo Kikuu cha Polisi cha kanda hiyo kuitikia wito wa jeshi hilo.

Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene iliyotolewa jana Oktoba 26,2017 imesema baada ya kumaliza mahojiano, askari kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO), waliokuwa wakimhoji Kigaila walisema hawana mamlaka ya kumwachia kwa dhamana.

Makene alisema sababu waliyoitoa ni kwamba wakubwa na wenye mamlaka ya kuruhusu dhamana au kutoa dhamana hawakuwepo ofisini.

“Juhudi za mawakili waliokuwepo polisi kumpatia Kigaila msaada wa kisheria, kueleza kuwa dhamana ni haki yake kwa mujibu wa sheria, huku wakihoji ni kwa nini kusifanyike mawasiliano ili hao wakubwa watoe ruhusa hiyo hata kama wako nje ya ofisi, hazikufua dafu!” alisema Makene.

Alisema tuhuma alizohojiwa Kigaila zilihusu kauli za uchochezi anazodaiwa kuzitoa Septemba 12,2017 siku chama hicho kilipotoa tamko la maazimio ya kikao cha dharura cha Kamati Kuu iliyoketi kujadili tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa  mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu.

Makene alisema kwa kuitikia wito wa Jeshi la Polisi na kwenda mwenyewe kituoni, ni sababu inayojitosheleza kuonyesha kuwa Kigaila ni mwaminifu na anatoa ushirikiano kwa sheria za nchi.

“Bila kumfikisha mahakamani au kumwachia huru, tafsiri yake ni kwamba Kigaila anashikiliwa na jeshi hilo kinyume cha sheria za nchi,” alisema.

Alisema Chadema imeagiza Kurugenzi ya Katiba na Sheria kuratibu na kusimamia hatua za kisheria ili kuhakikisha Kigaila anapata haki zake za msingi kwa mujibu wa sheria za nchi.

Meli ya uvuvi ya K Kusini yaachiwa huru Korea Kaskazini

Meli ya uvuvi ya K Kusini yaachiwa huru Korea Kaskazini

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi katika eneo hilo huku pande zote mbili zikifanya mizururu ya mazoiezi ya kijeshi.

Korea Kaskazini inasema kuwa itaiachilia meli ya uvuvi ya Korea Kusini ilioikamata siku sita zilizopita kwa kuingia katika himaya yake kinyume cha sheria, chombo cha habari kimesema.

Meli hiyo na wafanyikazi wake itaachiliwa katika mpaka wa kijeshi katika bahari ya mashariki kulingana na chombo cha habari cha KCNA.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya wafanyikazi hao kuomba msamaha kwa kufanya makosa hayo, kiliongezea.

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi katika eneo hilo huku pande zote mbili zikifanya mizururu ya mazoiezi ya kijeshi.

Korea Kaskazini imesema kuachiliwa kwa meli hiyo ya uvuvi, baadaye siku ya Ijumaa inafuatia hatua ya kukiri makosa kwa wale waliokuwa wakiabiri chombo hicho ambao walitaka serikali ya Korea Kaskazini kuwavumilia.

Uchunguzi, kulingana na Korea Kaskazini, ulithibitisha kuwa wavuvi hao waliingia maji ya taifa lake siku ya Jumamosi.

Msemaji wa serikali ya Korea Kusini alisema ni afueni kwamba wavuvi hao watarudi kulingana na chombo cha habari cha reuters.

Rais Magufuli kuwaapisha viongozi wapya walioteuliwa leo

Rais Magufuli kuwaapisha viongozi wapya walioteuliwa leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Oktoba, 2017 saa 8:00 mchana atawaapisha Makatibu Wakuu wapya, Naibu Makatibu Wakuu wapya na Wakuu wa Mikoa wapya baada ya jana tarehe 26 Oktoba, 2017 kufanya mabadiliko katika safu ya uongozi wa nyadhifa hizo.

Kufuatia mabadiliko hayo safu ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu itakuwa kama ifuatavyo;

Ofisi ya Rais Ikulu.

Katibu Mkuu – Bw. Alphayo Kidata

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Katibu Mkuu (Utumishi) – Dkt. Laurian Ndumbaro

Naibu Katibu Mkuu – Dorothy Mwaluko (ATAAPISHWA)

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Katibu Mkuu – Mhandisi Mussa Iyombe

Naibu Katibu Mkuu(Afya) – Dkt. Zainabu Chaula

Naibu Katibu Mkuu(Elimu) – Bw. Tixon Nzunda

Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Katibu Mkuu – Mhandisi Joseph Kizito Malongo (ATAAPISHWA)

Naibu Katibu Mkuu – Bi. Butamo Kasuka Phillipo (ATAAPISHWA)

Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Katibu Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) – Bw. Erick Shitindi
Katibu Mkuu(Bunge na Waziri Mkuu) – Maimuna Tarishi

Katibu Mkuu(Sera na Uratibu) – Prof. Faustine Kamuzora

Wizara ya Kilimo.

Katibu Mkuu – Mhandisi Methew Mtigumwe

Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Thomas Didimu Kashililah (ATAAPISHWA)

Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Katibu Mkuu (Mifugo) – Dkt. Maria Mashingo

Katibu Mkuu (Uvuvi) – Dkt. Yohana Budeba

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Katibu Mkuu (Ujenzi) – Mhandisi Joseph Nyamuhanga

Katibu Mkuu (Uchukuzi) – Dkt. Leonard Chamriho

Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Dkt. Maria Sassabo

Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Mhandisi Anjelina Madete

Wizara ya Fedha na Mipango.

Katibu Mkuu – Doto James Mgosha

Naibu Katibu Mkuu (Utawala) – Bi. Susana Mkapa (ATAAPISHWA)

Naibu Katibu Mkuu (Fedha za Nje) – Bi. Amina Shaaban

Naibu Katibu Mkuu (Sera) – Dkt. Khatibu Kazungu

Wizara ya Nishati.

Katibu Mkuu – Dkt. Hamis Mwinyimvua

Wizara ya Madini.

Katibu Mkuu – Prof. Simon S. Msanjila (ATAAPISHWA)

Wizara ya Katiba na Sheria.

Katibu Mkuu – Prof. Sifuni Mchome

Naibu Katibu Mkuu – Amon Mpanju

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Katibu Mkuu – Prof. Adolf F. Mkenda

Naibu Katibu Mkuu – Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Katibu Mkuu           – Dkt. Florence Turuka

Naibu Katibu Mkuu – Bi. Immaculate Peter Ngwale

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Katibu Mkuu           – Meja Jen. Projest Rwegasira

Naibu Katibu Mkuu – Balozi Hassan Simba Yahaya

Wizara ya Maliasili na Utalii.

Katibu Mkuu – Meja Jen. Gaudence Milanzi

Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Aloyce K. Nzuki

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Katibu Mkuu – Dorothy Mwanyika (ATAAPISHWA)

Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Moses M. Kusiluka

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Katibu Mkuu – Prof. Elisante Ole Gabriel

Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) – Ludovick J. Nduhiye (ATAAPISHWA)

Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) – Prof. Joseph Buchwaishaija (ATAAPISHWA)

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

Katibu Mkuu – Dkt. Leonard Akwilapo

Naibu Katibu Mkuu – Prof. James Epiphan Mdoe

Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Ave-Maria Semakafu

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Katibu Mkuu (Afya) – Dkt. Mpoki Ulisubisya

Katibu Mkuu (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) – Bi. Sihaba Nkinga.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Katibu Mkuu – Bi. Suzan Paul Mlawi (ATAAPISHWA)

Naibu Katibu Mkuu – Nicholaus B. William (ATAAPISHWA)

Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Katibu Mkuu – Prof. Kitila Mkumbo

Naibu Katibu Mkuu – Mhandisi Emmanuel Kalobelo

Mhe. Rais Magufuli atawaapisha Wakuu wa Mkoa 6 aliwateua jana kama ifuatavyo;


Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Mnyeti alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Joel Bendera ambaye amestaafu.

Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Joackim Leonard Wangabo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya uteuzi huu Bw. Wangabo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Zelote Stephen ambaye amestaafu.

Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Robert Gabriel Luhumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huu Bw. Luhumbi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe na anachukua nafasi ya Meja Jen. Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu.

Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Bw. Adam Kigoma Malima anachukua nafasi ya Dkt. Charles Mlingwa.

Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bi. Christine Solomon Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Mndeme alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini na anachukua nafasi ya Bw. Jordan Rugimbana.

Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Gelasius Gasper Byakanwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Bw. Byakanwa alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai na anachukua nafasi ya Bi. Halima Dendego.

Tukio la kuapishwa kwa viongozi hawa litarushwa moja kwa moja (Live) kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam kupitia vyombo vya habari vya Redio na Televisheni pamoja na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Oktoba, 2017

Serikali yakanusha kupokonya wafugaji mifugo

Serikali yakanusha kupokonya wafugaji mifugo

Naibu waziri mifugo na uvuvi Abdallah Ulega (Aliyevalia shati la rangi ya njano) akizungumza na wafugaji mkoani Tanga.

Serikali imewatoa  hofu wafugaji  nchini kuhusu  mchakato  wa  upigaji  chapa wa  mifugo  na kusema kuwa mpango huo haulengi kuchukua mifugo bali Serikali inataka kubaini  mifugo iliyopo.

Naibu Waziri  wa  Mifugo  na  Uvuvi, Abdallah  Ulega  ametoa hofu jana wakati akizungumza  na wakulima na wafugaji wa kijiji  cha  Perani  wilayani  Mkinga mkoa wa Tanga.

Kauli hiyo ya Ulega imekuja baada  wafugaji wa Perani kumweleza kwamba hawana elimu ya kutosha kuhusu mchakato huo na kwamba wanahisi kama mifugo yao inachukuliwa na Serikali .

Ulega  amesema Serikali ya Awamu ya Tano, ni sikivu na imedhamilia kuwatumikia vyema Watanzania na siyo kuwanyonya wananchi wa Taifa.

"Rais wetu ni mtu wa wanyonge, hakuna mtu yoyote atakayechukuliwa ngo'mbe zake.Bali tunataka  kujua mifugo yote iliyopo ili kuzuia mwingiliano na ile inayotoka nchi za jirani,"amesema  Ulega. 

Naibu waziri huyo, ametumia nafasi hiyo kuwasihi wafugaji na wakulima wa  eneo hilo kuacha mapigano baina yao kwani siyo jambo zuli na halileti taswira nzuri

"Naomba muishi kwa amani na utulivu kuanzia leo tatizo lenu nitalifikisha ngazi ya juu kuanzia kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela  ili atume wataalamu waje kuangalia namna ya kusimamamia  vyema mpango kazi,"amesema Ulega.

Awali mwenyekiti wa kijiji hicho, Letinga Oyaya alimweleza naibu waziri huyo kwamba wanaomba kuelimishwa namna ambayo mchakato wa upigaji chapa utakavyotekelezwa na madhumuni yake.

Nafasi za kazi leo October 27

Joti kuuaga ukapela

Joti kuuaga ukapela

Mchekeshaji mkongwe Bongo, Joti hatimaye ameamua kuachana na utani wa kudai anaoa na kuamua kufanya kweli kwa kudhihirisha yupo serious kidogo kwa jambo la mahusiano kwa kutarajia kuvuta jiko hivi karibuni.

Joti ambaye anafahamika kwa kufanya matangazo mengi ikiwemo ya kufunga ndoa , aliambatana na  watu wake wa karibu  katika sendoff  yake  iliyofanyika siku ya jana( Alhamisi) akiwa na mchekeshaji Seki.

Mchekeshaji huyo mwenye dili kibao town anatarajia kufunga ndoa rasmi  hivi karibuni na atakuwa ameingia kwenye orodha ya mastaa wa Bongo waliopo  katika ndoa kama Babuu wa Kitaa, Mx Carter, Kenedy The Remedy, Professa Jay, ZamaradI Mketema na Frola Mbasha.

Jokate kujikita kutetea haki za watoto na wanawake

Jokate kujikita kutetea haki za watoto na wanawake

MWANAMITINDO maarufu Bongo, Jokate Mwegelo amesema kuwa, atahakikisha anapambana vilivyo kwa ajili ya kutetea haki ya mwanamke pamoja na watoto kwa ujumla.

Akizungumza na Star Mix, Jokate alisema, kuna umuhimu sana kila mmoja mwenye nafasi kwenye jamii atambue nafasi ya mwanamke kwani wao ndio wenye nafasi kubwa kwenye jamii na pia kukazania kuwapa elimu.

“Unajua watu wengi wanajisahau kuhusu mwanamke na watoto lakini kwa upande wangu naona thamani kubwa sana ya mwanamke hasa akipatiwa elimu bora na kupewa nafasi nyingi za kuongoza huku watoto wakipewa haki inayostahili,” alisema Jokate.

Ajibu: Nitainyoosha Simba

Ajibu: Nitainyoosha Simba

MSHAMBULIAJI tegemeo hivi sasa wa Yanga, Ibrahim Ajibu amewaondoa hofu mashabiki kwa kutamka: “Waacheni watani wetu Simba wachonge na mwisho wa mechi watakaa kimya.”

Kauli hiyo, ameitoa akiwa ametoka kufunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Stand United iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga katika ushindi wa mabao 4-0 huku mengine yakifungwa na Obrey Chirwa na Pius Buswita.

Nyota huyo alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Simba baada ya mkataba wake kumalizika, akichota kitita cha shilingi milioni 50 na gari aina ya Toyota Brevis.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Ajibu aliwaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo akidai wana kikosi imara kitakachopata matokeo mazuri ya ushindi kwenye mechi hiyo itakayochezwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Ajibu alisema katika mechi hiyo atahakikisha anatengeneza au anafunga bao katika mechi hiyo ili iwe shukrani kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kumpokea vizuri tangu atue Jangwani.

“Mechi hii dhidi ya Simba ni muhimu kwetu kupata pointi tatu ili tukae kileleni katika msimamo wa ligi kuu, ninaamini ndiyo malengo yetu makubwa katika kuutetea ubingwa wetu.

“Hivyo, basi kikubwa nilichokipanga ni kuwa nitapambana kuhakikisha ninafunga bao au ninatengeneza nafasi ya bao kwa wachezaji wenzangu, kikubwa tunachokiangalia ni pointi tatu pekee.

“Timu yetu bila kuangalia nani kafunga, sisi tunaangalia ushindi utakaotuwezesha pointi tatu pekee, niwaondoe hofu Wanayanga wajitokeze kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kutusapoti, ninaamini uwepo wao utafanikisha mengi,” alisema Ajibu.

Aidha, kuona mahojiano hayo tembelea mtandao wa YouTube, kisha andika Global Tv Online, hapo utashuhudia mahojiano yote

Simba kutua Dar kwa ndege za kukodi

Simba kutua Dar kwa ndege za kukodi

Kikosi cha Simba kinatarajia kurejea jijini Dar es Salaam leo kwa maandalizi ya mwisho ya mechi yao ya kesho dhidi ya Yanga.

Simba walikuwa kambini mjini Zanzibar kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinaeleza, Simba watawasili kwa kutumia ndege za kukodi tayari kwa ajili ya mechi hiyo.

Kikosi hicho kitaingia kambini jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.


Hata hivyo, Simba wamekuwa wakifanya uficho kuhusiana na sehemu watakayokaa jijini Dar es Salaam wakimalizia maandalizi yao hayo ya mwisho kabla ya kesho.

Maneno ya Christina Shusho kwa viongozi Tanzania

Maneno ya Christina Shusho kwa viongozi Tanzania

Msanii wa muziki wa Injili Tanzania Christina Shusho, amewataka watanzania kuwaombea viongozi wetu wa kitaifa, kwani tuna kila sababu ya kujivunia watu hao kutokana na uongozi wao uliotukuka.

Christina Shusho ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, na kusema kwamba Tanzania tuna bahati kupa viongozi wenye hekima ambao wanaliongpoza taifa kwa amani, tofauti na nchi zingine za jirani kwa Afrika Mashariki.

"Najivunia sana viongozi wetu, tena niwaambie tu watanzania tuwaombee sana, tuna bahati ya kupata viongozi wenye upendo, na pia tudumishe upendo wetu tuwe na subira kwenye mambo yetu tudumishe hii amani, Mungu ametupendelea sana nchi za wenzetu wanalia na amani yao", amesema Christina Shusho.

Kauli hiyo ya Shusho imefuatia baada ya kuporomoshewa matusi na wakenya, kutokana na mihemko waliyonayo kipindi hiki cha uchaguzi, na kusema kwamba Wakenya wanahitaji  maombi pia kwani wanapitia kipindi kigumu.

Wauawa kwa Mapanga Usiku

Wauawa kwa Mapanga Usiku

Mume na mke wameuawa kwa kukatwa mapanga wakiwa wamelala nyumbani kwao.

Wanandoa hao walikuwa na kesi mbili za kugombea ardhi katika baraza la aridhi la Kata ya Hunyari, Tarafa ya Chamriho wilayani Bunda.

Ofisa Tarafa ya Chamriho Boniphace Maiga, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 22, mwaka huu.

Aliwataja waliouawa  kuwa ni Magina   Masengwa (61) na mke wake, Sumaye Sebojimu (58) ambao wote ni wakazi wa kitongoji cha Kiborogota Kijiji cha Mariwanda wilayani Bunda.

Maiga alisema   wanafamilia hao walivamiwa usiku na watu wasiojulikana na wakiwa wamelala na kukatwa mapanga kabla ya wavamizi hao  kutoweka na kuacha maiti za watu hao ndani ya nyumba hiyo.

Maiti hao waligundulika kesho yake asubuhi na mjukuu wao aliyekuwa anakwenda shambani.

“Ofisi yangu ilipokea taarifa ya mauwaji hayo kwamba watu wawili mume na mke wameuawa kwa kukatwa mapanga.

“Kwa hiyo chanzo cha mauaji hayo inasadikika huenda kinatokana na mgogoro wa shamba kwa sababu  walikuwa na kesi mbili katika baraza la ardhi la Kata ya Hunyari,” alisema Maiga.

Alisema   polisi walimkamata   Nyangi Nyabirumo, mkazi wa kijiji hicho kwa mahojiano na anaendelea kushikiliwa Kituo cha Polisi Wilaya ya Bunda.

Maiga alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.

Alisema  hali hiyo inaweza kusababisha upande wa pili nao kukasirika na kulipiza kisasi jambo ambalo  ni kinyume cha sheria.