Friday, 27 October 2017

Maneno ya Christina Shusho kwa viongozi Tanzania

Maneno ya Christina Shusho kwa viongozi Tanzania

Msanii wa muziki wa Injili Tanzania Christina Shusho, amewataka watanzania kuwaombea viongozi wetu wa kitaifa, kwani tuna kila sababu ya kujivunia watu hao kutokana na uongozi wao uliotukuka.

Christina Shusho ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, na kusema kwamba Tanzania tuna bahati kupa viongozi wenye hekima ambao wanaliongpoza taifa kwa amani, tofauti na nchi zingine za jirani kwa Afrika Mashariki.

"Najivunia sana viongozi wetu, tena niwaambie tu watanzania tuwaombee sana, tuna bahati ya kupata viongozi wenye upendo, na pia tudumishe upendo wetu tuwe na subira kwenye mambo yetu tudumishe hii amani, Mungu ametupendelea sana nchi za wenzetu wanalia na amani yao", amesema Christina Shusho.

Kauli hiyo ya Shusho imefuatia baada ya kuporomoshewa matusi na wakenya, kutokana na mihemko waliyonayo kipindi hiki cha uchaguzi, na kusema kwamba Wakenya wanahitaji  maombi pia kwani wanapitia kipindi kigumu.

No comments:

Post a Comment