Mume na mke wameuawa kwa kukatwa mapanga wakiwa wamelala nyumbani kwao.
Wanandoa hao walikuwa na kesi mbili za kugombea ardhi katika baraza la aridhi la Kata ya Hunyari, Tarafa ya Chamriho wilayani Bunda.
Ofisa Tarafa ya Chamriho Boniphace Maiga, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 22, mwaka huu.
Aliwataja waliouawa kuwa ni Magina Masengwa (61) na mke wake, Sumaye Sebojimu (58) ambao wote ni wakazi wa kitongoji cha Kiborogota Kijiji cha Mariwanda wilayani Bunda.
Maiga alisema wanafamilia hao walivamiwa usiku na watu wasiojulikana na wakiwa wamelala na kukatwa mapanga kabla ya wavamizi hao kutoweka na kuacha maiti za watu hao ndani ya nyumba hiyo.
Maiti hao waligundulika kesho yake asubuhi na mjukuu wao aliyekuwa anakwenda shambani.
“Ofisi yangu ilipokea taarifa ya mauwaji hayo kwamba watu wawili mume na mke wameuawa kwa kukatwa mapanga.
“Kwa hiyo chanzo cha mauaji hayo inasadikika huenda kinatokana na mgogoro wa shamba kwa sababu walikuwa na kesi mbili katika baraza la ardhi la Kata ya Hunyari,” alisema Maiga.
Alisema polisi walimkamata Nyangi Nyabirumo, mkazi wa kijiji hicho kwa mahojiano na anaendelea kushikiliwa Kituo cha Polisi Wilaya ya Bunda.
Maiga alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.
Alisema hali hiyo inaweza kusababisha upande wa pili nao kukasirika na kulipiza kisasi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

No comments:
Post a Comment