Wednesday, 25 October 2017

Mahakama kuu Kenya kutoa uamuzi kesi ya dharura ya kupinga kufanyika uchaguzi kesho

Mahakama ya Juu nchini Kenya, inasikiliza kesi ya dharura iliyowasilishwa siku ya Jumanne na wapiga kura watatu, wakitaka Uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika kesho kuahirishwa kwa siku tisini. Wapiga kura hao wanasema mazingira ya kisiasa nchini Kenya sio rafiki kuwezesha kufanyika kwa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki. Wakili wao Harun Ndumbi amesema ana imani Mahakamani itawapa ushindi. “Uchaguzi huu hauwezi kufanyika na kuwa huru na haki kwa sababu ya mazingira mabaya, tunataka Mahakama ya Juu iahirishe Uchaguzi huu kwa siku tisini,” amesema Harun Ndumbi. Jaji Mkuu David Maraga alikubali kusikiliza kesi hiyo na kuwaagiza Majaji wengine kusikiliza kesi zote kuhusu Uchaguzi hivi leo, pamoja na kwamba, leo ni siku ya mapumziko. Kesi hii imezua wasiwasi nchini humo kuhusu hatima ya Uchaguzi wa kesho. Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga wanasubiri tangazo la kiongozi wao huku wafuasi wa chama cha Jubilee wakisema wako tayari kupiga kura. Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati, amemteua Consolata Maina kuwa Naibu msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa urais, uteuzi ambao umezua hisia mseto. Naye mlinzi na dereva wa Naibu Jaji Mkuu wa Kenya Philomena Mwilu alivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa risasi jijini Nairobi. Tukio hilo lilitokea baada ya mlinzi huyo kumfikisha nyumbani Naibu Jaji Mkuu huyo ambaye pia ni Jaji katika Mahakama ya Juu. Waziri wa Usalama Fred Matiang'i amesema uchunguzi unaendelea kubaini waliotekeleza shambulizi hilo lakini akawahakikishia wafanyikazi wa Mahakama na hasa Majaji kuwa, wako salama.

China yatangaza kuachana na mila za urithi

China yatangaza kuachana na mila za urithi

China imetangaza kamati mpya ya viongozi wakuu na kuachana na mila ya kutomtangaza mrithi wa rais Xi Jinping.

Kutotangazwa mrithi kunaashiria kuongezeka ushawishi wa Xi madarakani katika kipindi cha miaka mitano inayokuja, siku moja baada ya jina lake kujumuishwa katika katiba.

Uteuzi huo ulifanywa kwa kamati ya watu inayojulikana kama Politburo, ambayo ina nguvu zaidi nchini China.

Kamati hiyo mpya ilizinduliwa kwenye ukumbi mashuhuri wa watu wa China.

Kando na Xi mwenye umri wa miaka 64, waziri mkuu Li Keqiang, 62, ndiye mwanachama pekee wa kamati ambaye alidumisha nafasi yake.

Viongozi wa China miongo ya hivi karibuni wamekuwa wakimteua mrithi mmoja ua kadhaa katika kamati kuu, wakati wa kuanza kwa muhula wa mwisho kuonyesha warirhi watakaochukua usukani.
kumekuwa na uvumi kuwa Bw Xi anaweeza kuwainua wanachama Chen Miner na Hu Chunhua, wote ambao wana umri wa miaka ya 50 kuweza kuwa warithi wake.

Kamati kuu ya kijehi nayo ilitangazwa. Itaongozwa na Xu Qiliang ambye anadumisha cheo hicho na Zhanga Youxia mshirika waa karibu wa Bw. Xi.

Wajumbe pia waliteua kamati kuu ya nguvu ya wanachama 200 ambao hukutana mara mbili kwa mwaka.

Mashirika ya habari ya kimataifa likiwemo la BBC yalinyimwa vibali vya kuingia ukumbi wa matangazo.
Hatua ya kutoteuliwa kwa warithi wa kamati kuu inampa nguvu zaidi Bw Xi katika miaka mitano inayokuja na kuashiria kuendelea kuwepo kwake baada ya mwaka 2022.

USHAHIDI: Daktari ataja magonjwa mengine ya Kanumba

Mbele ya Jaji Sam Rumanyika leo Oktoba 25, 2017 katika mahakama kuu Kanda ya Dar es salaam, imemaliza kusikiliza ushahidi wa kesi namba 125/2012 inayomuhusu Msanii Elizabeth Michael maarufu kama 'Lulu' ya kumuua mpenzi wake Steven Kanumba bila kukusudia, ambapo kesho Oktoba 26 Mahakama hiyo itasikiliza maoni ya Baraza la wazee wa mahakama sambamba na kupanga tarehe ya hukumu.
Kwamujibu wa maelezo ya shahidi namba 2  na wa mwisho kwa upande wa mshitakiwa, aliyefahamika kama Josephine Mshumbus yaliyosomwa kwaniaba yake na Staff Sajenti wa polisi Detective E103 Aitwaye Nyangea, aliyotoa 23/04/2012, ameeleza kuwa yeye alimfahamu Marehemu Steven Kanumba Kama Mgonjwa wake katika kituo chake cha tiba mbadala cha Precious Clinic kilichokuwepo karibu na Jengo la Mawasiliano Jijini Dar es sala.
 "Steven Kanumba alikuwa ana matatizo ya sumu mwilini na alikuwa anakuja kwenye kituo changu cha Kliniki Ambapo alikuwa akifanya vipimo vya mwili mzima na aligundulika kuwa na tatizo la Mafuta (Cholestrol), tatizo la Moyo, Upungufu wa Hewa ya Oksijeni kwenye Ubongo ambayo yalimsababishia maumivu makali.
Hata hivyo niligundua kuwa wakati akiendelea na tiba alikuwa akifanya mazoezi ya kutanua misuli, nilimkataza mara moja kwakuwa angeweza kupoteza maisha au Kupooza baadhi ya sehemu za mwili wake.
Kuna siku alikuja kunilalamikia kuhusu maumivu makali anayopata kwenye Moyo, lakini kulingana na wingi wa wateja sikuweza kumuhudumia lakini tulipanga kuonana siku nyingine lakini haikuwezekana tena" Maelezo ya Shahidi yameeleza.
Upande wa Mstakiwa uliongozwa na Wakili msomi Peter Kibatala, Huku Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Faraja George.
Upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi Nne, na Upande wa Mstakiwa uliwasilisha mashahidi Wawili. 

Msajili wa Vyama Nchini Awataka watumishi Kufuata sheria

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi amewataka watumishi kutoka ofisi yake kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuleta weledi katika kazi.
Hayo ameyazungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa kwa ajili ya watumishi watakaoshiriki katika usimamizi wa utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Gharamaza Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa na wagombea yaliyofanyika Jana na Leo katika ukumbi wa Bunge Jijini Dar esa Salaam.
“Chapeni kazi na kuwa vinara wa kusimamia gharama za uchaguzi na maadili ya Vyama vya Siasa ili kubaini wagombea ambao hawafuati matakwa ya sheria ” amesisitiza Jaji Mtungi.
Naye Bi Piencia Kiure, Msajili Msaidizi wakati akitoa mada juu Elimu ya maadili ya Vyama vya Siasa ,amewasisitiza watumishi kuendelea na utamaduni wa kufanya kazi kwa weledi.
Sheria namba 6 ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2015 kupitia Amri ya Gharama ya uchaguzi inaweka wazi viwango vya juu vya matumizi kwa wagombea, kudhibiti matumizi ya fedha zinazotumika wakati wa uchaguzi kuanzia katika mchakato wa uteuzi, kampeni na kupiga kura ili kuweka uwanja sawa wa kisiasa na kudhibiti vitendo vya rushwa.
Sheria hii hubainisha wajibu wa Mgombea na Chama cha Siasa kujaza fomu maalumu za gharama za uchaguzi ili kubainisha bajeti yake ambayo ni mapato na vyanzo vya mapato na kurejesha katika ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ndani ya siku saba baada ya uteuzi wa wagombea unaofanywa na Tume ya uchaguzi .
Fomu maalumu ya kubainisha marejesho ya matumizi ya uchaguzi inayoambatana na kumbukumbu na stakabadhi za malipo hujazwa na mgombea na kurejeshwa kwenye chama chake ndani ya siku sitini baada ya uchaguzi, chama cha siasa kina wajibu wa kuiwasilisha fomu hiyo kwenye ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ndani ya siku 180 baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi
Hata hivyo ukiukwaji wa sheria hii unaambatana na adhabu kali ambayo hutolewa kwa chama ambacho kitashindwa kuwasilisha mapato na matumizi ya kila mgombea ambayo ni pamoja na kufutiwa kushiriki uchaguzi endapo kitashindwa kutoa maelezo ya kuridhisha.
Usimamizi wa Sheria ya gharama za Uchaguzi katika uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika tarehe Novemba 26 mwaka huu ni mwendelezo wa usimamizi wa sheria hii ambao hufanywa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakati wa uchaguzi wa Urais, Wabunge na Madiwani. Kwa mara ya kwanza sheria hii ilianza kutumika katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010

Singida United kuutumia uwanja wa namfua

Uongozi wa Singida United umedhamiria kuanza kuutumia Uwanja wake wa Namfua mkoani Singida kwa mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Novemba 4, mwaka huu.
Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba baada ya ukarabati wa kiwango cha juu, uliohusisha pia eneo la kuchezea mpira (pitch), Namfua sasa upo tayari kwa matumizi.
Festo amesema kwamba baada ya Uwanja huo kukamilika, Singida United FC wataanza kutumia Namfua Novemba 4 katika mchezo wao dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Yanga.
“Ushirikiano wa TFF na Bodi ya Ligi kuhakikisha Namfua unaanza kutumika ni wa kiwango cha juu, viongozi wakuu wa soka nchini wanafanya kazi bega kwa bega na uongozi wa Singida United kuhakikisha kipute cha Ligi Kuu kinaanza kutimka pale Namfua,”amesema Festo.
Historia ya timu ya Singida United inaanzia kwenye timu nguli kipindi hicho ikijulikana kama Mto Singida FC na inashiriki Ligi Kuu kwa mara ya pili baada ya kupanda msimu huu, kufuatia awali kucheza ligi hiyo miaka ya 2000.

Harmorapa: Sijapotea kwenye Muziki

Msanii ambaye hakauki vituko mitandaoni Harmorapa, amewa
jibu watu wanaomsema kuwa amepotea pamoja na kiki zake zote, na kusema kwamba hajapotea isipokuwa yuko busy na biashara.
Harmorapa ameyasema hayo kwenye eNewz ya East Africa Television, na kusema kwamba watu wanatakiwa wajue licha ya muziki Harmorapa ana maisha yake mengine ambapo pia ni mfanyabiashara, na sasa hivi yuko busy na kazi za biashara ikiwemo kusafiri, lakini mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani muda si mrefu atawapa kazi mpya.
"Watu waelewe sipo kimya, sasa hivi nipo busy na biashara nasafiri sana, ile kuonanana tu ni bahati, project zangu za muziki zinaendelea kama kawaida wiki ijayo naachia dude jipya, watu wajue tu mimi nipo, wamemzoea Harmorapa leo kafanya hiki mara hiki, sasa hivi niko busy na muziki wangu bado upo, kama kutrend kila siku natrend, naingia Instagram nakuta tu mtu amenipost bado machoni mwa watu naonekana, bado mimi nipo na nitakuwepo na vitu vitaendelea", amesema Harmorapa.
Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba msanii huyo ameshapotea kwenye game, kwani hawezi kufanya muziki na anachotegemea yeye ni kiki ambazo anazifanya na kuchekesha w

AUDIO | Moni Centrozone – Tunaishi Nao Remix (Diss Kwa Roma ) | Mp3 Download

AUDIO | Moni Centrozone – Tunaishi Nao Remix (Diss Kwa Roma ) | Mp3 Download


https://my.notjustok.com/track/download/id/284278/by/wQ~zUOP4NM

AUDIO | Rosa Ree _ Down | Mp3 Download

AUDIO | Rosa Ree _ Down | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/284335/by/szj2UH_cIL

Audio | Beka Flavour Ft Gentle – Naona Kiza | Mp3 Download

Audio | Beka Flavour Ft Gentle – Naona Kiza | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/284464/by/R3JAF4MUP0

Tuesday, 24 October 2017

Kenya: Watu 3 waenda mahakamani kusitisha uchaguzi

Mahakama ya juu nchini Kenya itatoa uamuzi wa muda wa mwisho kuamua iwapo marejeleo ya uchaguzi wa urais yanaweza kufanyika siku ya Alhamisi.
Mahakama hiyo itasikiza ombi la dharura siku ya Jumatano kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafutiliwa mbali siku moja kablka ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
Hatua hiyo inajiri baada bya mahakama hiyo kufanya uamuzi wa kihistoria ilipofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais na kutaka uchaguzi huo kurejelewa.
Sasa inatakiwa kuingilia kati kwa mara nynegine na itaamua , ikiwa imesalia chini ya saa 24 kabla ya uchgauzi huo kufanyika kuhusu iwapo uchaguzoi huo unafaa kuendelea.
Kuna utata kati ya sheria za uchaguzi, katiba na vile mahakama ilivyofafanua sheria hizo.
Kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga ametumia mojawapo ya uamuzi wa mahakama kujiondoa katika uchaguzi huo akiutaja kuwa usio huru na haki na hautatoa maono ya Wakenya.
Rais aliyepo sasa Uhuru Kenyatta amesema kuwa uchaguzi huo ni sharti ufanyike, huku akiwa na muswada wa uchaguzi katika meza yake unaotarajiwa kutiwa saini
Mahakama ya juu imekubali kusikiliza ombi hilo la muda wa lala salama ambalo linahoji iwapo tume ya uchaguzi na mwenyekiti wake wataweza kufanya uchaguzi ulio huru na haki siku ya Alhamisi.
Inataka uchaguzi huo kubadilishwa na uchaguzi mpya hatua ambayo huenda ikaongeza muda wa uchaguzi huo kwa kipindi cha mwezi mmoja .
Wapiga kura watatu wameelekea katika mahakama ya juu wakitaka kusimamisha uchaguzi huo wa Alhamisi.
Bwana Khalef Khalifa , Samuel Mohochi na Gacheke Gachuhi wanadai kwamba tume ya uchaguzi imegawanyika na haiwezi kufanya uchaguzi ulio huru na haki.
Wanadai kwamba makamishna wa IEBC wanahudumu kwa upendeleo na mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amekiri hadharani kwamba hawezi kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki.
Walalamishi hao watatu ,wanaowakilishwa na Harun Ndubi pia wanataka mahakama kuamua kuhusu hatua ya Raila Odinga kujiondoa katika uchaguzi huo.
Wanavyoelewa ni kwamba hatua ya Raila Odinga kujiondoa katika uchaguzi huo inamaanisha kwamba uchaguzi huo unafutiliwa mbali.
Wanahoji kwamba ilani ya gazeti rasm la serikali lililotangaza uchaguzi huo imepitwa na wakati kufuatia hatua hiyo ya Odinga.
Wanadai kwamba tume ya IEBC huenda isiweze kusimamia uchaguzi huo kama ilivyoagizwa na mahakama ya juu kutokana na maadalizi hafifu.
Kuna hatari kwamba uchaguzi huo huenda usifanyike katika idadi kubwa ya kaunti hatua itakayoweka hatma na maisha ya Wakenya katika matatizo.
Watatu hao wameagizwa kuwakabidhi wahusika agizo la kesi hiyo kufikia saa kumi na mbili jioni.
Wakati wa kuchapishwa kwa taarifa hii wakili wa rais Uhuru Kenyatta Tom Macharia na wale wanaowakilisha IEBC walikuwa washakabidhiwa agizi hilo.
IEBC na wengine wanatarajiwa kujibu kufikia kesho saa mbili alfjiri .
Kusikizwa kwa kesi hiyo kunatarajiwa kuanza saa nne ya alfajiri siku ya Jumatano.
Wakitoa uamuzi wao manmo tarehe mosi Septemba, majaji sita wa mahakama ya juu waliunga mkono ombi lililowasilishwa na Raila Odinga kwa majaji 4-2 aliyedai kwamba mfumo wa kielektroniki ulidukuliwa na kuingiliwa kwa lengo la kumsaidia rais Uhuru Kenyatta.
Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa kura hiyo kwa asilimia 54.
Majaji hao walisema: Tume ya uchaguzi ilishindwa ama hata kukataa kufanya uchaguzi wa urais katika hali ambayo inalingana na katiba .
Hatahivyo mahakama hiyo haikumlaumu rais Kenyatta ama hata chama chake.
Kenyatta alisema kuwa anajutia kwamba watu sita wameamua wataenda dhidi ya matakwa ya raia lakini hatopinga uamuzi huo. Kenya: Watu 3 waenda mahakamani kusitisha uchaguzi

Darasa: Azungumzia ujio wake mpya,,,

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Darassa amezungumzia ujio wake mpya.
Rapper huyo ambaye mara mwisho alisikika na ngoma ‘Hasara Roho’ ameiambia Dj Show ya Radio One yupo katika maandalizi ya kufanya hivyo ila kwa sasa asingependa kulizungumzia sana kwani yeye siku zote siyo muongeaji zaidi ya kazi.
“Kwenye single mpya watu wananijua mimi siyo mtu wa kuongea ongea kama sina kitu cha kuongea mara nyingi huwa nakuja kuongea nikiwa na kitu, kwa sasa naandaa project ambazo naamini nitakuja kufunga nazo mwaka watu wakae tayari tunakuja tuko poa kabisa” amesema Darassa.
Mwishoni mwa mwaka jana Darassa alifunga mwaka na ngoma Muziki ambayo alimshirikisha Ben Pol ambayo inatajwa kuwa ndio ngoma pekee kuwa hit ya kutisha kutoka kipindi hicho hadi mwaka huu.

Giggs Asema anazitamani Everton na Leicester City

Kocha msaidizi wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs amesema anatamani kuchukua mikoba ya makocha Ronald Koeman na Craig Shakespeare katika klabu za Everton na Leicester City.
Giggs ambaye alikuwa msaidizi wa Louis Van Gaal ndani ya Manchester United ameweka wazi nia yake hiyo wkaati akifanya mahoajiano na Sky Sports kuhusiana na uelekeo wake kwenye kufundisha soka.
“Hizi ni klabu zinazonivutia kuzifundisha kutoakana na aina yake ya uchezaji na zina wachezaji ambao wana viwango bora”, amesma Giggs
Hata hivyo Giggs amegoma kuweka wazi endapo atatuma maombi kwa uongozi wa timu hizo ili kumpatia nafasi hiyo ya kuongoza benchi la ufundi.
Leicester City ilimfuta kazi kocha Craig Shakespeare wiki iliyopita kabla ya jana Everton kumfuta kazi Ronald Koeman. Giggs amekuwa nje ya masuala ya ukocha kwa kazi ya juu tangu alipoondoka Manchester United mwaka 2016 baada ya mkuu wake Van Gaal kuondolewa.

Serikali kuboresha shule 85 za kata...

Serikali imetoa takribani Shilingi Bilioni 21 kwa ajili ya kuboresha shule 85 za Kata hapa nchini ili ziwe na Kidato cha Tano na Sita hali itakayoongeza ubora wa kiwango cha elimu na kuimarishwa kwa miundombinu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Selemani Jafo wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) siku za Jumatatu na Alhamisi.
Akifafanua Waziri Jafo amesema kuwa dhamira ya Serikalini katika kuboresha sekta ya elimu ambapo kila mwezi imekuwa ikitoa takribani Bilioni 23 zinazotumika kugharimia elimu bure hali inayochochea kuongezeka kwa wanafunzi wanaojiunga katika shule za msingi na Sekondari .
“Tumejenga madarasa mengi na vyoo vingi ili kuendana na kasi ya udahili wa wanafunzi na pia tutahakikisha kuwa kuna kuwa na uwiano katika mgawanyo wa walimu katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Aliongeza kuwa Serikali katika kuboresha huduma za Afya imeshapeleka fedha katika vituo 172 kote nchini ili kuboresha huduma zinazotolewa na pia watumishi katika sekta hiyo wataajiriwa kwa kuzingatia mahitaji kutokana na nafasi zilizoachwa wazi baada ya zoezi la ukaguzi wa vyeti feki.
Aidha Waziri Jafo aliwataka Viongozi wote katika Mikoa na Halmashauri kusimamia vizuri miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao ili thamani halisi ya fedha zilizowekezwa ionekane. “Nawasihi watanzania walipe kodi kwa kuwa fedha zinazotokana na kodi ndizo zinazotumika kutekeleza miradi ya maendeleo na ni matumaini yangu kuwa maelekezo niliyotoa kwa wakurugenzi kuhusu ukusanyaji wa mapato yatazingatiwa na watasimamia kazi hiyo vyema na kubuni vyanzo vipya vya mapato”Alisisitiza Jafo.
Aidha Waziri Jafo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kuwa hadi sasa watumishi zaidi ya 300 wameshachukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu kwa kushindwa kutimiza wajibu wao.
Kwa upande wa sekta ya Viwanda amebainisha kuwa wamejipanga vyema kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kutenga maeneo maalum ya uwekezaji katika Halamashauri na Mikoa.