Wednesday, 25 October 2017

Singida United kuutumia uwanja wa namfua

Uongozi wa Singida United umedhamiria kuanza kuutumia Uwanja wake wa Namfua mkoani Singida kwa mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Novemba 4, mwaka huu.
Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba baada ya ukarabati wa kiwango cha juu, uliohusisha pia eneo la kuchezea mpira (pitch), Namfua sasa upo tayari kwa matumizi.
Festo amesema kwamba baada ya Uwanja huo kukamilika, Singida United FC wataanza kutumia Namfua Novemba 4 katika mchezo wao dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Yanga.
“Ushirikiano wa TFF na Bodi ya Ligi kuhakikisha Namfua unaanza kutumika ni wa kiwango cha juu, viongozi wakuu wa soka nchini wanafanya kazi bega kwa bega na uongozi wa Singida United kuhakikisha kipute cha Ligi Kuu kinaanza kutimka pale Namfua,”amesema Festo.
Historia ya timu ya Singida United inaanzia kwenye timu nguli kipindi hicho ikijulikana kama Mto Singida FC na inashiriki Ligi Kuu kwa mara ya pili baada ya kupanda msimu huu, kufuatia awali kucheza ligi hiyo miaka ya 2000.

No comments:

Post a Comment