Monday, 23 October 2017

RC Makonda Apinga bomoabomoa ya karne Dsm

Ndugu Zangu Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Naomba kuwatoa hofu, Mimi Paul Makonda nikiwa Mkuu wenu wa Mkoa na mtumishi wa serikali ya awamu ya tano, Napenda kuwataarifu kwamba serikali hii inayoongozwa na Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli HAIVUNJI Nyumba ya mtu Bali inaendelea kurasimisha Makazi kama ambavyo ilifanya kimara kwa kuwapatia Hati elfu Sita (6000) kwa Wananchi waliokuwa wamejenga kwenye makazi yasiyo rasmi, jitihada zinaendelea na ndivyo itakayofanyika tarehe 27/10/2017 kwa Wananchi waliojenga katika maeneo ya makongo juu.
Naomba niseme, na kama nimemuelewa vizuri alichokisema _Mhe William Lukuvi_ ambae ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi ni kuwa wananchi wasiendelee kujenga bila vibali vya ujenzi jambo ambalo linawanyima haki yao ya kukopeshwa, kulipa kodi ya majengo, na mwishoni kuwa na miji isiyopangwa vizuri.
Naomba kukiri kuwa apo awali kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa vibali vya ujenzi jambo ambalo haliwezi kuwa Adhabu kwa Wananchi waliojenga miaka ya nyuma iliyopita kwani ilifika hatua Mwananchi ana Hati ya Kiwanja chake na amekamikisha michoro kwa Mujibu wa Sheria na ana fedha za kuanza Ujenzi kwa ajili ya Makazi ya kuishi, unakuta Mwananchi huyo analazimika kufuatilia manispaa kwa zaidi ya miaka miwili mpaka mitatu bila kupata kibali cha ujenzi na hata akipata kibali baada ya miaka Mitatu na kuanza ujenzi, unakuta ndani ya muda mfupi watakuja baadhi ya watu wa OSHA kumsimamisha kwa madai hawana taarifa ya ujenzi jambo linalotengeneza mianya ya Rushwa, akimalizana na watu wa OSHA Wanakuja baadhi ya watu wa kikosi cha zimamoto (fire) nao inabidi atafute utaratibu wa kumalizana nao, jambo linalokera wananchi na kuwafanya wakose hamasa ya Kutafuta vibali vya ujenzi na Hatimae kujenga kiholela.
Kututokana na jambo hili, baadhi ya watu wasiowaaminifu wanatumia mwanya huu kuvamia maeneo ya watu na kujenga Kiholela na kuibua Migogoro Mikubwa ya Ardhi.
TULICHOFANYA KAMA MKOA
Kutokana na sababu hizo na changamoto nilizozielezea hapo juu, serikali ya Mkoa tulifanya kikao na wataalamu wa Ardhi na nikatoa maelekezo kuwa vitengo vyote nane vinanavyohusika na Utoaji wa vibali vya ujenzi VINAPASWA kuwa na mfumo Mmoja wa mawasiliano (one stop center) ili Mwananchi atakapoomba kibali cha ujenzi Idara zote nane zifikiwe kwa wakati Mmoja na kupunguza usumbufu wa Mwananchi kwenda kufuatilia vibali na wakati mwingine unaambiwa wahusika hawapo.
Ili mfumo huo uanze kufanya kazi wataalamu wangu walihitaji vitendea kazi ambavyo nimewawezesha vifaa hivyo zikiwemo Computer Hamsini (50) katika manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam na kuwataka kutoa vibali ndani ya mwezi Mmoja tangu kupokea maombi kutoka kwa Mwananchi tofauti na awali ambapo Mwananchi alikuwa akichukua muda wa miaka miwili kufuatilia kibali cha ujenzi, lengo Likiwa kuwawezesha wananchi kufuata Sheria ili kuendana na Mpango wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na makazi Chini ya _Mhe William Lukuvi_ katika kuhakikisha tunapanga miji yetu.
Kwa maelezo Haya mafupi, Naomba niseme kwenye Mkoa wa Dar es Salaam HAPATAKUWA na bomoa bomoa ya KARNE wala Nyumba ya mtu kuvunjwa ISIPOKUWA wananchi wanaojenga sasa ni vyema wakafuata utaratibu kama alivyoelekeza Mhe William Lukuvi waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, ili kuepuka kuvunjiwa Nyumba ambayo umeijenga kwa jasho jingi, na kujinyima uku ukikesha ili utimize ndoto ya kuwa na makazi bora.
Niwatakie kazi njema, na kwa pamoja tushirikiane katika Kupanga na kuendeleza Mkoa wetu wa Dar es Salaam kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa na vizazi vyetu.
Mhe Paul C. Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
23/10/2017

Sunday, 22 October 2017

Rais Magufuli aombwa Amtumbue Haraka Mkurugenzi Ruvuma

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga mji mkoani Ruvuma, wamemkataa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Bw. Robert Mageni na kumuomba rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli kumuondoa katika halmashauri hiyo haraka wakimtuhumu kuvuna miti katika msitu wa Mbambi, kuchana mbao na kisha kuziuza kinyume cha sheria na kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya zaidi ya milioni 800.
Baraza hilo la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga mji katika mkoa wa Ruvuma, limefikia maamuzi hayo baada ya kamati maalumu iliyoundwa na baraza hilo julai mwaka huu kuchunguza ubadhilifu wa fedha zilizotokana na kuvuna miti na kuuza mbao katika msitu wa Mbambi kinyume cha sheria, huku kamati hiyo ikimtia hatiani mkurugenzi huyo Bw. Robert Mageni kuingia katika tuhuma 10 ikiwemo ya kuuza mali za halmashauri bila kupitisha kwenye vikao vya halmashauri na kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya milioni 880.
Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Mhe. Cosmas Nshenye amepongeza uchunguzi wa uliofanywa na kamati hiyo na kuahidi kwamba kamati yake ya ulinzi na usalama ya wilaya inafanyia kazi mapendekezo hayo.
Hata hivyo mtuhumiwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya mbinga mji. Bw. Robert Mageni amesema kwa sasa hana cha kueleza kutokana na tuhuma hizo.
Baraza hilo pia limetoa mapendekezo ya kufukuzwa kazi kwa afisa misitu wa halmashauri hiyo, Bw. David Hyera kwa tuhuma za kushirikiana na mkurugenzi huyo kujiandikia mikataba feki ya kuvuna miti katika msitu wa Mbambi bila kushirikisha vikao vya halmashauri

Bomoa Bomoa Kuipitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Halmashauri, Tanesco, CCM

Wamiliki wa nyumba wa maeneo ya mjini waliojenga kwenye maeneo ya serikali Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wamepewa notisi ya mwezi mmoja kubomoa nyumba hizo ambazo tayari zimewekewa alama X baada ya kubainika nyumba hizo pamoja na Ofisi za serikali ziko ndani ya hifadhi ya barabara.
Meneja wa Wakala wa barabara TANROADS Mkoa wa Ruvuma Razack Alinanuswe ameiambia Channel ten katika mahojiano maalum kuwa baadhi ya nyumba za wananchi na ofisi za serikali ikiwemo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Jengo la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Ruvuma na Jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Songea zote zinapaswa kubomolewa.
Aidha Bustani inayoendelea kujengwa huku ikionekana kutumia gharama kubwa kupitia mkopo uliotolewa na Benki ya Dunia nayo imewekewa alama X kwa kuwa ujenzi wake unafanyika ndani ya hifadhi ya barabara.
Mbali ya maeneo hayo ya serikali, mashirika na nyumba za wananchi, Channel ten pia imeshuhudia baadhi ya vibanda vya biashara vinavyomilikiwa na Chama cha mapinduzi ccm Mkoa wa Ruvuma navyo vikiwa vimewekewa alama x inayomaanisha kuondolewa kwa kujengwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara.

Saturday, 21 October 2017

VIDEO : Mwana FA Ft Ay & Fid Q _ Upo Hapo | Mp4 Download

https://cloudup.com/files/iKBl1xkibP8/download

AUDIO | Mwana FA Ft AY & Fid Q – Upo Hapo | Mp3 Download

AUDIO | Mwana FA Ft AY & Fid Q – Upo Hapo | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/283095/by/rsNQEQDqxY

Wanafunzi watishia kuchoma shule Geita

Geita. Vurugu kubwa zimeibuka katika Shule ya Sekondari Geita baada ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita kutishia kuchoma shule kushinikiza wenzao wanne wanaoshikiliwa na polisi waachiwe.
Polisi Geita inawashikilia wanafunzi wanne wa shule hiyo tangu Alhamisi baada ya kumpiga, kumjeruhi na kutishia kumuua mwenzao wa kidato cha tano.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Isaya Busagwe amesema mwanafunzi huyo alipigwa Jumamosi iliyopita na walimu waligundua tukio hilo baada ya aliyepigwa kuugua na kuomba ruhusa ya kwenda nyumbani kutibiwa.
Jana Ijumaa Oktoba 20, wanafunzi hao waligoma kuingia darsani, badala yake, waliandamana kwenda kituo cha polisi kushinikiza wenzao kuachiwa huru.
Baada ya juhudi zao kugonga mwamba kwa polisi kuendelea kuwashikilia wenzao, wanafunzi hao walirejea shuleni na kuanza kurusha mawe wakitishia kuchoma moto majengo wakishinikiza wajumbe wa bodi waliokua wakiendelea na kikao shuleni hapo kutatua suala hilo.
Leo Jumamosi asubuhi, wanafunzi hao walianzisha vurugu zingine, hali iliyolazimisha jeshi la polisi kuingilia kati na kufanikiwa kuzidhibiti.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita(OCD), Ally Kitumbo aliyeongoza kikosi cha kutuliza ghasia kudhibiti vurugu hizo hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo akisema yeye siyo msemaji na kazi yake ni kulinda amani na utulivu.
Katika vurugu hizo mwandishi wa habari hii naye amejikuta akiwekwa chini ya ulinzi na kunyang'anywa simu na askari polisi kabla ya kunusuriwa na OCD na kuruhusiwa kuendelea na kazi.

Friday, 20 October 2017

AUDIO | Come Dash _ Haitowezekana | Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/283017/by/vJHK6UaW3X

Breaking News: Matokeo ya darasa la saba yatangazwa


Bonyeza link hapo chini kuanaglia matokeo ya Darasa La Saba mwaka 2017

http://www.necta.go.tz/matokeo/2017/psle/psle.htm

Juma Nature Awafungukia Wasanii Wachanga

Msanii Juma Nature ambaye ni mkongwe kwenye game ya bongo fleva, amewataka wasanii wachanga kufuata sheria pale wanapotaka kutumia nyimbo za wasanii wakongwe jukwaani, ikiwemo kuomba kibali kwa muhusika na ikiwezekana amlipe fedha
Juma Nature ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Radio, na kueleza kwamba msanii mchanga kuimba nyimbo za msanii mkongwe jukwaani sio jambo baya na inaonyesha heshima, lakini ni vyema wakawa na makubalino maalum kabla hajafanya hivyo kuepusha migogoro.

Askofu Afariki Akiwa Safarini

Dar es Salaam. Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi limempoteza askofu wake, Castory Msemwa aliyefariki jana Alhamisi Oktoba 19,2017 saa saba mchana nchini Oman.
Kwa mujibu wa Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki Tunduru Masasi, Padri Jordan Liviga, Askofu Msemwa amefariki dunia mjini Muscat akiwa safarini kwenda nchini India kwa matibabu.
Taarifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) imesema Askofu Msemwa alikuwa na tatizo la kiafya kwa kipindi cha miaka miwili na amekuwa akipata tiba na kuendelea na utume kama kawaida.
TEC imesema Askofu Msemwa aliondoka nchini Jumatano Oktoba 18,2017 kuelekea nchini India kwa matibabu kabla hajafariki dunia.
Padri Liviga amebainisha kuwa utaratibu wa kuuleta nchini mwili wa marehemu Askofu Msemwa Jumapili Oktoba 22,2017 unafanyika. Amesema taarifa zaidi za utaratibu wa mazishi zitatolewa baadaye.
Askofu Msemwa amezaliwa mwaka 1955 katika Kijiji cha Kitulira, Parokia ya Matola Jimbo Katoliki Njombe.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya Motola, kisha sekondari katika Seminari Kuu ya Peramiho ambako alisomea Falsafa na Teolojia kati ya mwaka 1981 na 1987. Alipata daraja ya upadri Juni 7,1987. Amekuwa Paroko Msaidizi, kiongozi wa vijana parokiani jimboni Njombe, mwalimu na amesoma katika Chuo cha Teresianum Pontifical College for Spirituality huko Roma na kuhitimu mwaka 1996.
Alipata Daraja ya Uaskofu Januari 30,2005 kisha kusimikwa kuliongoza Jimbo Katoliki Tunduru Masasi Agosti 25,2005.

Nassari ashangaa kuwaona viongozi ofisini


Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesema kuwa bado anashangaa kuendelea kuwaona ofisini viongozi ambao aliowataja kwenye ushahidi wa kutumia rushwa kununua madiwani wa Chadema mkoani Arusha kwani watakuwa na nafasi kubwa ya kuharibu ushahidi huo. Mh. Nassari amesema kwamba hofu yake kwa viongozi hao ni kwamba watakuwa na nafasi kubwa ya kuuharibu ushahidi huo kwa kuwa bado wamekalia madaraka hivyo wanaweza kufanya lolote kuhakikisha ushahidi ulioneshwa unaharibika ikiwa ni pamoja na upelelezi kufanyika kwa mashaka. "Kinachonishikisha ni kuendelea kuwaona viongozi wale bado wapo ofisini. Huko nyuma tumeona watu wakiwajibika kisiasa pale wanapopata tuhuma kuhusu rushwa, huwa wanawajibika au kuwajibshwa. Hapa naona inakuwa ngumu kidogo kuhusu upelelezi wa kesi hii kufanyika . Mfano tunaona sehemu kwenye video Mkurugenzi anasikika akieleza ni namna gani ataelekeza wale madiwani waanze kulipwa kidogo kidogo lakini bado yupo ofisini hii inanisikitisha kwani upelelezi unakuwa na mashaka kidogo" Nassari Aidha Nassari amesema ameshangazwa na kauli ya Mkurugenzi wa Takukuru, Valentino Mlowola kwamba yeye anaingilia upelelezi wao na kudai kwamba anachoamini yeye ni kwamba hajavunja sheria wala hajaingilia upelelezi wao kwani anachokifanya ni kuutaarifu umma kila hatua anayokua anaifanya. Nassari ameongeza kwamba kauli zinazotolewa na Mlowola kama zina lengo la kumtia hofu basi kwake hofu hiyo anaamini haitafanya kazi kwake kwani kama ni kuzungumza na wanahabari wakati akiwa anapeleka ushahidi hataacha kwani huwa hazungumzii ushahidi alioubeba bali huwa anazungumzia hatua anazopiga. Pamoja na hayo Nassari amesema hawezi kuzungumza kama haki itapatikana au la bali anachoamini Takukuru ni taasisi inayojitegemea hivyo hawataona haya kutenda haki ili ijulikane wateule wa rais wana hatia au vinginevyo.

Mexime asema Kagera Sugar bado inatafuta ushindi

Kocha wa klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara Meck Mexime amesema timu yao bado inatafuta ushindi.
Meck ameyasema hayo leo kuelekea mchezo wa raundi ya 7 dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.
“Kikubwa sisi tunatafuta ushindi kwasababu hatujaupata tangu ligi ianze, hivyo tumejiandaa kutafuta ushindi na pointi tatu”, amesema Meck Mexime.
Mexime ambaye ni mchezaji na kocha wa zamani wa timu ya Mtibwa Sugar ameshindwa kuonesha makali ya msimu uliopita tangu ligi ya msimu wa 2017/18 ianze ambapo hajafanikiwa kupata ushindi kwenye mechi Sita za mwanzo.
Hadi sasa Kagera Sugar inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 2. Wakata Miwa hao wa Kaitaba wamepoteza mechi 4 na kutoa sare mechi mbili. Wakati Mwadui wanashika nafasi ya 12 ikiwa na alama 6 baada ya michezo Sita.

Umoja wa Mataifa Umesitisha Shughuli Zake Zote Nchini Kenya Kuhofia Uchaguzi

Umoja wa Mataifa (UN) umesitisha shughuli zake zote nchini Kenya katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26.
Taarifa iliyotolewa Ijumaa na Msaidizi wa Katibu mkuu kanda ya Afrika Mashariki, Peter Drennan imesema umoja huo utasitisha kwa muda programu zake zote ambazo hazikuwa muhimu sana.
“Baada ya kufanya tathmini ya hali ya usalama nchini Kenya, ofisa mteule (DO) kwa ushauri kutoka Timu ya Usimamizi wa Usalama, ameshauri kusitishwa kwa warsha, mikutano, semina na makongamano na jumbe mbalimbali zisizo za lazima nchini Kenya walau kwa wiki moja kabla na wiki moja baada ya uchaguzi wa marudio kwa kura ya urais,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
“Ninakubaliana na ushauri wa DO na mamlaka husika kusitishwa kwa programu hizo ambazo hazina ulazima kuanzia leo Oktoba 19 hadi Novemba 2.”
Jana Alhamisi serikali ilitangaza kwamba Alhamisi ya Oktoba 26 itakuwa siku ya mapumziko kwa ajili ya kuruhusu wananchi kushiriki uchaguzi wa marudio.
Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani, Fred Matiang’i alitangaza kwamba siku hiyo imeandikwa katika Gazeti la Serikali kwamba itakuwa siku ya mapumziko kuwezesha Wakenya kushiriki kwa uhuru uchaguzi huo.
Tangazo hilo limekuja katikati ya mnyukano wa kisiasa na kuiweka uchaguzi huo katika hatihati ya kufanyika.
Jumatano, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati alielezea kukerwa kwake katika maandalizi ya uchaguzi wa marudio na akatangaza wazi kuwa hawezi kuhakikisha uchaguzi wa kuaminika.
Chekubati alisema kutokana na kupanda sana kwa hofu ya kisiasa nchini, alipendekeza Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wakutane kwa mazungumzo kabla ya uchaguzi huo