Sunday, 22 October 2017

Rais Magufuli aombwa Amtumbue Haraka Mkurugenzi Ruvuma

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga mji mkoani Ruvuma, wamemkataa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Bw. Robert Mageni na kumuomba rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli kumuondoa katika halmashauri hiyo haraka wakimtuhumu kuvuna miti katika msitu wa Mbambi, kuchana mbao na kisha kuziuza kinyume cha sheria na kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya zaidi ya milioni 800.
Baraza hilo la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga mji katika mkoa wa Ruvuma, limefikia maamuzi hayo baada ya kamati maalumu iliyoundwa na baraza hilo julai mwaka huu kuchunguza ubadhilifu wa fedha zilizotokana na kuvuna miti na kuuza mbao katika msitu wa Mbambi kinyume cha sheria, huku kamati hiyo ikimtia hatiani mkurugenzi huyo Bw. Robert Mageni kuingia katika tuhuma 10 ikiwemo ya kuuza mali za halmashauri bila kupitisha kwenye vikao vya halmashauri na kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya milioni 880.
Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Mhe. Cosmas Nshenye amepongeza uchunguzi wa uliofanywa na kamati hiyo na kuahidi kwamba kamati yake ya ulinzi na usalama ya wilaya inafanyia kazi mapendekezo hayo.
Hata hivyo mtuhumiwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya mbinga mji. Bw. Robert Mageni amesema kwa sasa hana cha kueleza kutokana na tuhuma hizo.
Baraza hilo pia limetoa mapendekezo ya kufukuzwa kazi kwa afisa misitu wa halmashauri hiyo, Bw. David Hyera kwa tuhuma za kushirikiana na mkurugenzi huyo kujiandikia mikataba feki ya kuvuna miti katika msitu wa Mbambi bila kushirikisha vikao vya halmashauri

No comments:

Post a Comment