Tuesday, 17 October 2017

Kampuni ya televisheni Uingereza yadukuliwa na Korea kaskazini,,,,

Wadukuzi wa Korea Kaskazini wamelenga kampuni moja ya vipindi televisheni nchini Uingereza ambayo inatengeneza kipindi wa kuigiza kuhusu nchi hiyo.
Kipindi hicho ambacho kilitarajiwa kuandikwa na mwandishi ambaye ashateuliwa kuwania tuzo za Oscar sasa kimesitishwa.
Mwezi Agosti mwaka 2014 Channel 4 ilitangaza kuwa kipindi hicho kitakuwa kipya na cha kuchokoza.
Kipindi hicho kinachojulikana kama Opposite Number, kinahusu mwanasayansi ya nyuklia muingereza ambaye amefungwa nchini Korea Kaskazini.
Mradi huo haujapiga hatua kutokana na kushindwa kupata ufadhili kwa mujibu wa kampuni hiyo.
Maafisa wa Korea Kaskazini walijibu kwa hasira wakati taarifa kuhusu kipindi hicho zilifichuka mara ya kwanza.
Pyongyang ilitoa wito kwa serikali ya Uingereza kuzima kipindi hicho ili kuzuia kuharibu uhusiano.
Korea Kaskazini kisha ikachukua hatua zaidi na kudukua kompiuta za kampuni husika.
Udukuzi huo haukusababisha uharibifu lakini, kuhusika kwa wadukuzi wa Korea Kaskazini mitandaoni kulizua hofu juu ya ni kipi wana uwezo wa kukifanya.
Hofu hiyo ilitokana sababu Sony Pictures ililengwa na udukuzi kama huo mwezi Novemba mwaka 2014.
Marekani ilisema kuwa udukuzi huo uliendeshwa na Korea Kaskazini.
Udukuzi huo nao ulikuwa ni jibu kwa filamu iliyopangwa kutolewa kwa jina The Interview, mchezo ambao kiongozi wa Korea Kaskazini aliuawa.

Malori ya Dangote yaua madereva

WATU watatu kati ya sita waliokuwa wakisafiri na malori yanayomilikiwa na kiwanda cha saruji cha Dangote mkoani Mtwara, wamekufa papo hapo na wengine kulazwa Hospitali ya Sokoine ya mkoa wa Lindi, baada ya magari hayo kugongana uso kwa uso.
Waliofariki ni Issa Rashidi Mbweso (28) ambaye ni dereva wa lori namba T 481 DJZ na mkazi wa mjini Mtwara, Haruni Nazir Mbonde (48) ambaye pia ni dereva wa lori la kiwanda hicho pamoja na utingo wake aliyefahamika kwa jina moja la Rajabu.
Majeruhi ni Ramadhani Nasoro (30) utingo na mkazi wa mjini Mtwara, Sophia Isumaili (35) na dada yake, Mawazo Omari (40) wakazi wa Kata ya Mandawa wilaya ya Kilwa.
Wakizungumza na Nipashe katika hospitali hiyo Lindi, majeruhi hao akiwamo utingo wa lori hilo namba T 481 DJZ lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mtwara, walisema ajali hiyo ilitokea eneo la kitongoji cha Mihambwe, kwenye barabara kuu ya Kibiti-Lindi juzi mchana.
Sophia Isumaili na dada yake Mawazo Omari waliokuwa wameomba lifti kutoka Mandawa kwenda Newala mkoani Mtwara, walisema walipofika kitongojini hapo na kukuta barabara imezibwa na wingu la moshi mzito, alimuomba dereva Issa ambaye ni marehemu asimamishe gari wasubiri kupungua kwa moshi huo, lakini alikaidi na kujitosa.
“Tulipofika eneo lile na kukuta moshi mwingi nilimshauri dereva wetu tusimame ili kupisha moshi, lakini hakuwa tayari na kujibu atapita tu bila shida,” alisema Sophia.
Utingo Ramadhani Omari alisema kutokana na dereva kukaidi ushauri huo, walijikuta wakigongana uso kwa uso na lori lingine lililokuwa limebeba saruji likiwa limesimama kando ya barabara kupisha kupungua kwa moshi huo.
Alisema baada ya malori hayo kugongana, kulijitokeza cheche za moto na kuteketea kwa magari yote hayo wakiwamo madereva na utingo, kabla ya gari la Zimamoto kutoka Manispaa ya Lindi kwenda eneo la tukio Mihambwe kuuzima moto.
Mganga wa zamu katika Hospitali ya Sokoine, Dk. Edgal Mlawa, alithibitisha kupokea miili na majeruhi watatu, lakini hakuwa tayari kutoa maelezo zaidi akisema hadi mkuu wake wa kazi atakapofika.
“Licha ya kuwa nipo zamu muda huu, lakini siwezi kuelezea zaidi kwani mwenye mamlaka ya kuzungumza na vyombo vya habari ni mkuu wangu wa kazi,” alisema Dk. Mlawa.
Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Renatha Mzinga, alipoulizwa kupitia simu yake ya mkononi, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza taarifa kamili ataitoa baada ya kupelekewa na vijana wake waliokuwapo eneo la tukio.

Audio | Mr Nana _ You Know Me | Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/281463/by/wt9QqBDHn_

VIDEO | Benjamin wa Mambo Jambo – Bang | Download

VIDEO | Benjamin wa Mambo Jambo – Bang | Download

Ben Pol Amwambia Ebitoke awe na subira,,,,

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ilikuwa inasemekana yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na muigizaji wa vichekesho Ebitoke, amemtaka msanii huyo kuwa na subira juu ya yale anayoona anamkosea na kusema muda utafka na kila kitu kitakuwa sawa.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ben Pol amesema anaamini mpenzi wake huyo anaelewa mazingira ya kazi zake jinsi yalivyo, na mchaka mchaka wa ubize ambao alikuwa nao kwenye kazi zake za muziki.
"Mimi naamini anaelewa, saa nyingine uko safarini hakuna mtandao, nafikiri tuwe na subira vitu vingine vingi tutapata ufumbuzi wa kila kitu, unajua kila mtu ana mapungufu yake, unaweza ukakosea sehemu baadaye mkaelewana mkasahau", amesema Ben Pol.
Hivi karibuni Ebitoke alisikika akisema kuwa Ben Pol hapokei simu zake wala hajibu message zake, na kuomba watu wamsaidie kumuuliza Ben Pol amekutwa na nini mpaka kufikia hatua hiyo.

Alichoongea RC Makonda baada ya ziara ya siku 1 Visiwani Zanzibar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amefanya ziara ya siku moja katika maeneo mbalimbali kwaajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu visiwani Zanzibar katika mkoa wa Mjini wa Magharibi.
Akiongozwa na mwenyeji wake ambaye ndiye Mkuu wa mkoa huo Ayoub Mahamoud ziara hiyo imeanzia katika Pango la Tumekuja lilijengwa enzi za utawala wa Sultan Said Said Barghash kwaajili ya kusafirishia watumwa.
Alitembelea makumbusho ya jengo ambalo lililkuwa likitumika kuuzia watumwa enzi za Ukoloni ambalo lilifungwa rasmi mwaka 1873 na sasa eneo hilo linatumika kama kanisa "Kanisa la Mkunazini" mbali na kutumika kama sehemu ya Historia visiwani humo.
Kabla ya kuelekea mtoni marine inakojengwa hoteli kubwa Afrika mashariki ambayo iko mjini na yenye uwezo wa kupokea wageni wenye meli zao 12, alitembezwa katika eneo darajani unapofanyika ukarabati wa Jumba la treni ambalo limo kwenye Orodha ya urithi wa dunia.
Pia alitembezwa katika eneo la Nyamanzi unakofanyika ujenzi ya makazi ya kisasa ya nyumba za mbao ambazo zinajengwa hadi kukamilika kwa muda wa siku tisa.
Baada ya hapo alitembelea kiwanda cha sukari cha Zanzibar Sugar Factory (ZSF) kilichopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B Unguja chenye uwezo wa kuzalisha tani 80 ya sukari kwa siku.
Ziara hiyo ilihitimishiwa kwenye shamba la Viungo la 'Spice Farm' la Kizimbani lenye viungo vya chakula na mboga mboga ikiwemo Tangawizi, Binzari, Pilipili Manga, Karafuu, mdalasini, Hiliki, mchaichai na kadhalika.
Mara baada ya ziara hiyo Mh: Makonda ameeleza sababu zilizomfanya afanye ziara hiyo licha ya kujifunza masula kadhaa ni pamoja na kujadili namna gani watabadilishana taarifa za kiusalama, ukomeshwaji wa biashara ya ngono, dawa za kulevya na kwa upande wake mwenyeji wa mkoa huo Mkuu wa mkoa RC Ayoub ameeleza kuwa baada ya Ziara hiyo wataanza rasmi kurasimisha mahusiano hayo.


Monday, 16 October 2017

Kesi ya msanii Lulu kuanza kusikilizwa tena Mahakama kuu

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam inatarajia kuanza kusikiliza kesi ya mauaji ya bila kukusudia inayomkabili Mwigizaji Elizabeth Michael maarufu kama Lulu October 19, 2017.
Lulu anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kumuua Msanii mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia, kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu (PC), April 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican.
Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji ya bila kukusudia iliyotolewa na Mahakama Kuu, kesi ya Lulu itaanza kusikilizwa siku hiyo ya October 19, 2017 mbele ya Jaji Sam Rumanyika.
February 18, 2014 akisomewa maelezo ya awali (PH) alikiri Mahakamani kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kanumba na pia kuwa kulikuwepo na ugomvi baina yao siku ya tukio la kifo cha Mwigizaji huyo.
Lulu aliachiwa kwa dhamana January 29, 2013 baada ya kesi hiyo kubadilishwa hati ya mashtaka kutoka kwenye kesi ya mauaji ya bila kukusudia ambapo badiliko hilo lilimpa nafasi ya kupata dhamana.
Katika kesi ya msingi namba 125 ya mwaka 2012, inadaiwa kuwa April 7, 2012 Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia.

Waziri Mkuchika kupeleka ombi Bungeni umri wa kustaafu uongezwe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema anakusudia kupeleka ombi maalum Bungeni kuomba umri wa kustaafu kwa Maprofesa uongezwe na kufikia 65 badala ya 55.
Waziri Mkuchika ameyasema hayo alipokwenda alipotembelea ofisi za Sekretarieti ya Ajira na kukutana na watendaji wa taasisi hiyo, na kusema kwamba umri wa kustaafu kwa sheria unawafanya wasomi hao washindwe kutumika vizuri kulijenga Taifa.
"Hawa maprofesa wengi wanaofikia hatua hiyo wanakuwa na miaka kuanzia 50 na kuendelea, halafu anafanya kazi kidogo anatakiwa kustaafu, tutapeleka bungeni maombi kuwe na mabadiliko kidogo katika baadhi ya maeneo, haitakuwa na maana kama wasomi wanatumia rasilimali za taifa kufikia hatua hiyo halafu baada ya kuhitimu wanafanya kazi kwa muda mfupi na kutakiwa kustaafu", amesema Waziri Mkuchika.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuchika ameahidi kushughulikia changamoto zinazoikabili sekta hiyo, ikiwemo sheria na utaratibu wa ajira unaopitia kwenye Sekretarieti ya ajira.

Pogba Aanza kujinoa,,,,


Diamond Afunguka kuhusu pochi ya Zari

Baada ya Zari kuonekana kwenye uzinduzi wa duka la vifaa vya nyumbani na Ofisini Danube Mlimani City baadhi ya mitandao na watu walianza kusema kwamba amebeba pochi ya bei rahisi, hilo limemfikia mpaka Diamond na akaamua kusema yafuatayo.
Diamond amezima taarifa hizo kwa kusema pochi hiyo alimnunulia Zari shilingi milioni 5 za Kitanzania hivyo haitakiwi kushushwa thamani.

Gigy money atangaza dau lake,,,,,

Msanii wa Bongo Fleva na Video Queen, Gigy Money amesema kwa sasa kama promota au mtu yeyote anayehitaji kumuita kutumbuiza kwenye tamasha/sherehe yake basi ni lazima uwe na kiasi cha milioni mbili za kitanzania.
Mkali huyo anayetamba kwa sasa na wimbo wake wa ‘Papa’ amesema wimbo huo ni ‘Hit Song’ na ni moja ya wimbo mkali kwa sasa kuliko nyimbo nyingine zilizotoka kwa muda huu.
“Na-perform stejini kwa milioni mbili, Papa is a hit song, bila milioni 2 siwezi kutoa Papa stejini, is a hit song.“amesema Gigy Money kwenye mahojiano yake na Bongo5.

Waziri Mkuu Amewaonya Mawaziri,,,,,

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya mawaziri na kuwataka watumie madaraka yao kwa manufaa ya Taifa na kamwe wasiyatumie kama fursa ya kujitajirisha wao binafsi.
Kassim Majaliwa amesema hayo leo Oktoba 16, 2017 alipozungumza na baadhi ya Mawaziri, Manaibu na Makatibu Wakuu katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Aidha Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza kwamba amewateua ili wafanye kazi na kamwe wasitumie madaraka waliyopewa kwa maslahi yao binafsi.
“Madaraka haya ya Uwaziri si fursa ya kujipatia utajiri, tunatakiwa tufanye kazi kwa weledi, uadilifu, bidii na uaminifu mkubwa ili kuondoa kero za wananchi kwa wakati.”
Waziri Mkuu amesema Mawaziri hao wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa Taifa wa miaka kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021. Pia utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 pamoja na ahadi alizozitoa Rais Dkt Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi.
Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka Mawaziri hao wakapunguze urasimu katika utekelezaji wa malengo ya Serikali kwa sababu wananchi wanahitaji kuhudumiwa kwa wakati Mawaziri waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Bw. Suileiman Jaffo pamoja na Manaibu wake Bw. Joseph Kandege na Bw. George Kakunda, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile.
Wengine ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu wake Bw. Jumaa Aweso, Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Charles Mwijabe na Naibu wake Mhandisi Stella Manyanya.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Naibu wake Bw. Josephat Hasunga, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Naibu wake Bw. William Ole Nasha, Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw. Abdallah Ulega pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo.

Idadi ya watu waliouawa kwenye mlipuko mkubwa Wa mabomu Mogadishu yafika 300

Idadi ya watu waliouawa kwenye ,lipuk

o mkubwa wa bomu katika eneo lenye shughuli nyingi kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumamosi, imefikia watu 300 hadi sasa, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la hahari la Reuters
Takriban watu wengine 300 walijeruhiwa kwa mujibu wa AFP, wakati lori lililokuwa limejazwa milipuko lilipolipuka karibu na lango la hoteli.
Reuters walimnukuu Ahmed Ali, muuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja akisema kuwa miili 160 haikuweza kutambuliwa na hivyo ilizikwa na serikali jana. Anasema kuwa miili mingini iliziwa na jamaa zao,.
Hilo ndilo shambulizi baya zaidi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007.
Rais Mohamed Abdullahi "Farmajo" Mohamed alilaumu kundi la al-Shabab kwa shambulizi hilo katili.
"Tumethibitisha kuwa watu 300 waliuawa kwenye mipuko huo. Idasi ya waliokufa huenda bado ikaongezeka na kuna watu kadha ambao bado hawajulikani waliko," Abdikadir Abdirahman, mkurugenzi wa idara ya magari ya kusafirisha wagonjwa aliliambia shiria la Reuters.