Monday, 16 October 2017

Lissu Amfaliji Nyalandu,,,,

Baada ya kukaa hospitali kwa zaidi ya mwezi mmoja Lissu
akipatiwa matibabu, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amekiri kuona tabasamu la Mbunge huyo aliyepigwa risasi mwezi uliopita na kuwataka watanzania waendelee na maombi.
Kupitia mtandao wake wa Instagram Nyalandu amesema kwamba shauku aliyonayo Lissu ndani ya moyo wake ni kuiona siku iliyo njema pia kufurahia siku kila asubuhi.
Nyalandu ameandika "Tuendelee kumwombea ndugu yetu Tundu Lissu. Nimeliona tabasamu la uso wake leo, na hakika Mungu anaendelea kujibu maombi ya Watanzania, na wote wanaomkumbuka katika sala na dua zao katika majira na saa hii ya kujaribiwa kwake".
"Tusimame pamoja naye, kwa kuwa shauku ya moyo wake ni kuiona siku iliyo njema, aweze kuifurahia kila asubuhi kama apendavyo Mungu".
Lissu alipigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa wasiojulikana tangu Septemba 07 akiwa mjini Dodoma nje ya nyumba yake alipokuwa ametoka Bungeni kutekeleza majukumu yake na sasa bado yupo hospitali ya Nairobi nchini Kenya akiendelea na matibabu.

Mwanafunzi Aua wenzie 5 kwa Risasi,,,,

Wanafunzi watano na mlinzi wa shule wameuawa kwa kupigwa risasi na mwanafunzi mwenzao, huku wengine 17 wakijeruhiwa katika shule ya sekondari ya Lokichogio iliyopo kaunti ya Turkana, nchini Kenya.
Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki hii ambapo mwanafunzi huyo aliyetambulika kwa jina la Abraham mwenye asili ya SUdan Kusini alikwenda shuleni akiwa na wenzake, na kuanza kuwamiminia risasi wanafunzi ambao walikuwepo kwenye shule hiyo, kwa kinachoaminika kuwa ni kulipiza kisasi baada ya kusimamishwa sule kwa utovu wa nidhamu.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwanafunzi huyo alifanikiwa kuingia shuleni hapo baada ya kumuua mlinzi na kisha kuingia bwenini, na kufanya shambulio lililopelekea vifo hivyo na kujeruhi wengine.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema kuna ulazima wa kukagua wanafunzi wanaotoka maeneo ya karibu kabla hawajawasajili kwenye shule zao, ili kujiepusha na matukio kama hayo kuendelea kutokea.
Mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza alikamatwa na polisi akijaribu kukimbia kuelekea kwenye kambi ya wakimbizi ya SUdan Kusini, na kumpeleka kituo cha polisi, lakini baada ya muda wananchi walivamia kituo hiko na kukishambulia, wakitaka kumuua kwa mawe.
Kufuatia tukio hilo uongozi wa shule hiyo umetangaza kuifunga shule hiyo kwa muda, ili wanafunzi wakae sawa kisaikolojia, kufuatia kile walichokishuhudia.

Austria kumchagua kiongozi mwenye umri mdogo zaidi duniani,,,,,

Mkuu wa chama cha kihafidhina nchini Austria cha People's Party, Sebastian Kurz, anaelekea kuwa kiongozi wa taifa mwenye umri mdogo duniani, baada ya ushindi wake katika uchaguzi mkuu hapo jana.
Kurz aliye na umri wa miaka 31 amepungukiwa na uwingi , lakini yupo katika nafasi nzuri ya kuunda serikali ya muungano.
Haijulikani wazi iwapo atafikiria kuunda serikali ya muungano na chama kinachopinga uhamiaji Freedom Party, kilichoibuka nafasi ya tatu kwa kishindo katika uchaguzi huo.
Akihutubia wafuasi wake Bw Kurz alisema: "Ni wakati wa kuleta mabadiliko kati nchi hii. Leo ni siku muhimu kwetu kuibadilisha nchi hii na ninasema asante kwa wale wamewezesha hili".
"Nina furaha, nimejitolea kuifanyia kazi Austria."
Sebastian Kurz ni nani?
Kabla ya uchaguzi Bw. Kurz lihudumu kama waziri mwenye umri mdogo zaidi wa mashauri ya nchi za kigeni barani ulaya, baada ya kuteuliwa mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 27.
Mwezi Mei mwaka 2017 akawa kiongozi wa chama cha People's Party. Alianza taaluma yake ya siasa katika tawi la vijana wa chama kabla ya kwenda kuhudumu katika baraza la manispaa la mji wa Vienna.
Akipewa jina "Wunderwuzzi" linalomaanisha mtu anayeweza kutembea juu ya maji, amefananishwa na viongozi vijana wa Ufaransa na Canada, Emmanuel Macron na Justin Trudeau.
Sawa na Macron, Bw Kurz amejiundia wafuasi wanaomzunguka, kukibadilisha chama cha People's Party, ambacho kimekuwa madarakani kwa miaka 30

Muda wa kiongozi wa Catalonia kutangaza msimamo waelekea kuisha

Kiongozi wa eneo la Catalonia amesalia na saa chache kabla ya kumalizika muda wa mwisho uliowekwa na serikali kuu kuthibitisha wazi ikiwa ametangaza uhuru au la.
Ikiwa atakiri kuwa ametangaza, atakuwa na hadi Alhamisi kufuta tangazo hilo au Catalonia ambayo imekuwa ikijisimamia iongozwe moja kwa moja na Uhispania, Tarehe ya mwisho iliyotolewa kwa Carles Puigdemont ni leo 08:00 GMT.
Baada ya kura ya maoni ya uhuru wiki mbili zilizopita ambayo ilitangazwa kuwa iliyo kinyume na sheria na mahakama ya katiba ya nchi hiyo, Bw Puigdemont alisaini tangazo la uhuru lakini akafuta kutekelezwa kwake, Alisema alitaka mazungumzo na serikali ya Madris lakini hilo halijafanyika.

7,602 wakutwa na saratani ya shingo ya kizazi

Jumla ya wanawake 187,267 wamefanyiwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi huku 7,602 wakipatiwa matibabu katika mradi uliofadhiliwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates baada ya kukutwa na ugonjwa huo.
Mradi huo uliokuwapo kwa miaka mitano ulikuwa ukitekelezwa na taasisi za Marie Stopes Tanzania (MST), Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (Umati) na PSI.
Akizungumza wakati wa kufunga mradi huo juzi, Mkurugenzi Mkazi wa MST, Anil Tambay alisema idadi hiyo ya wanawake imetoka katika mikoa 22 ambako mradi huo ulikuwa ukitekelezwa.
“Mradi huu ulijikita kupunguza athari za saratani na shingo ya kizazi kwa wanawake, tumefanya uchunguzi na kutoa matibabu,” alisema Tambay.
Alifafanua kuwa wakati wa kuanza kwa mradi huo walitoa mafunzo na kupata watoa huduma 210 waliohudumia vituo 79 vilivyoanzishwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Afya ya Uzazi wa Wizara ya Afya, Dk Hussein Kidanto alisema asilimia 38 ya wagonjwa waliofika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road mwaka 2015 walikuwa na saratani ya shingo ya kizazi.

Uchaguzi Liberia: Weah na Boakai kuelekea duru ya pili ya uchaguzi wa rais

Nyota wa zamani wa soka George Weah na makamu wa rais Joseph Boake, wanaelekea duru ya pili ya uchaguzi kwenye uchaguzi wa rais nchini Liberia.
Karibu matokeo yote kwenye uchaguzi wa siku ya Jumanne yamehesabwa, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.
Bw. Weah ambaye ni mwafrika wa kwanza kushinda tuzo la kandanda la Ballon D'Or, anaongoza kwa asilimia 39 huku Bw. Boakai akiwa wa pili kwa asilimia 29, Duru ya pili kati ya wawili hao inatarajiwa mwezi ujao.
Wanaongoza wagombea wengine 20 ambao wanataka kuchukua nafasi ya Ellen Johnson Sirleaf, mwanamke wa kwanza kuchaguliwa rais barani Afrika na mshindi wa tuzo la amani la Nobel, Weah na Boakai wote walikuwa wametabiri kuwa wangeshinda duru ya kwanza.
Meneja wa zamani wa Bw. Weah akiwa mcheza kandanda, Arsene Wenger, mapema wiki iliyopita alipotoshwa na habari kuwa Weah tayari alikuwa amechaguliwa rais.

Rais MagufuliJP atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya KADCO, Balozi Kibelloh



Mchezaji afariki kwa kugongana uwanjani Indonesia

Mlinda mlango wa klabu ya ligi kuu ya Indonesia amefariki baada ya kugongana na mchezaji mwenzake uwanjani.
Choirul Huda, mwenye miaka 38, alikimbizwa hospitalini siku ya Jumapili lakini muda mfupi baadae ilitangazwa kwamba amefariki dunia.
Katika taarifa iliyotolewa na tovuti ya klabu yake Persela FC , daktari wa timu Yudistiro Andri Nugroho amesema mchezaji huyo alifariki baada ya kupata madhara makubwa kifuani.
Anasema mgongano huo ulisababisha kushindwa kupumua kwa Huda.
Ameongeza kuwa madaktari walijaribu kuokoa maisha yake bila mafanikio, Mchezo huo uliisha kwa Persela kuifunga Semen Padang 2-0.
Maelfu ya mashabiki wamefika hospitalini alipofia mchezaji huyo aliyecheza michezo 500 ya ligi kuu kwa klabu yake pekee.

VIDEO : Harmonize Ft Korede Bello _ Shulala | Download

Bovya link ku Download ==>  https://cloudup.com/files/iA5c60-Yzkc/download

MAGAZETI YA LEO 16/10/2017



Sunday, 15 October 2017

Mourinho: sikwenda Anfield kumburudisha mtu yeyote bali tulikwenda kucheza soka.

Msimu wa ligi kuu Uingereza wakati unaanza kila mtu alimsifu Jose Mourinho kwa kuibadilisha United, walionekana wanacheza soka la kuvutia sana tofauti na msimu wa mwaka juzi.
Lakini baada ya mechi 7 ambazo hawakucheza na timu ngumu sana, jana United walipata kipimo chao cha kwanza baada ya kukanyaga katika uwanja wa Anfield kucheza dhidi ya majogoo wa London Liverpool.
Mambo yalibadilika na United walicheza ambavyo hakuna aliyetarajia, wakawa United wale wale wa kurudi nyuma kusubiri mipira ije huku wakiwaacha Liverpool kuushikilia mchezo wote.
Baada ya mchezo huo kuisha sasa sio mashabiki tu bali hata wachambuzi wa soka walianza tena kubeza mfumo wa kocha Mourinho dhidi ya timu kubwa na kudai kwamba unaboa sana kuangalia kama walivyocheza jana.
Mourinho mwenyewe amewaambia wanaoponda kwamba kila mtu auchukulie huo mchezo auchukuliavyo na hakwenda Anfield kujaribu kumburudisha mtu yeyote bali walikwenda kucheza soka.
Mourinho anadai kama kipindi cha pili aliona ugumu kufanya mabadiliko kutokana na Liverpool walivyokuwa wakicheza huku baadhi ya wachezaji wake muhimu akiwemo majeruhi mpya Eric Bailly wakiwa hawamo ndio maana akacheza mchezo huo unaokera kuangalia.
Cha kushangaza zaidi kuhusu Mou na Manchester United yake ni mashuti mawili tu waliyopiga golini kwa Liverpool katika michezo miwili, yaani shuti moja kila mchezo suala linaloonesha ni jinsi gani United wamekuwa wanajilinda tu.
Liverpool hawako katika kiwango kizuri sana na ni wazi kwamba kwa uwezo wa United ilitarajiwa jana wangejaribu kuwasukuma na kucheza mpira lakini wao wakacheza kama wanacheza na Barcelona au Real Madrid.
Mou anaonekana labda ni muoga kufungwa kutokana na alivyoanza msimu kwa mbwembwe lakini pamoja na yote United wamepata alama 1 Anfield inayowaweka nafasi ya pili nyuma ya vinara wa ligi Manchester City.

AUDIO | Jah Prayzah Ft Diamond Platnumz – Poporopipo | Download

AUDIO | Jah Prayzah Ft Diamond Platnumz – Poporopipo | Download

Bovya hapa kudownload ==>
https://my.notjustok.com/track/download/id/280813/by/okTklUXBQ0

AUDIO | HARMONIZE FT KOREDE BELO_SHULALA | MP3 DOWNLOAD

Bovya hapa kudownload ==>https://my.notjustok.com/track/download/id/280898/by/UP~oEGWQ61