Thursday, 25 January 2018

Mzee Majuto amelazwa Muhimbili



Mchekeshaji Amri Athuman aka Mzee Majuto Jumatano hii amelazwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es saalam kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Habari wa Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii Asifa Habari huyo, Masoud kaftany, amesema muigizaji huyo alipelekwa hospitali hapo siku ya jana baada ya kuzidiwa.

“Ni kweli Mzee Majuto anaumwa na sasa hivi tupo naye hapa Muhimbili anaendelea na matibabu,” alisema Masoud kaftany. Kusema anaumwa nini ni mapema zaidi lakini baadae tutatoa taarifa rasmi baada ya kupokea taarifa ya madaktari,”

Afisa huyo amekiomba Chama cha Waigizaji, wadau wa filamu Tanzania na wa Tanzania wote wamuombee muigizaji aweze kupona haraka

Source: Bongo 5

DC ashtakiwa na Wenyeviti wa mitaa




  Dar es Salaam. Wenyeviti wa serikali za mitaa ya Kimara Baruti, Mavurunza na Makoka wamemshtaki katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Makori Kisare kwa madai ya kukiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kutumia mamlaka yake kuwaweka ndani bila sababu za msingi.

Wenyeviti hao wameliambia gazeti hili kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona vitendo hivyo vinazidi kukithiri, wanaitaka Tume ya Maadili iingilie kati.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mavurunza, Josephat Nehemia alisema mkuu huyo wa wilaya amekuwa akiwanyanyasa wenyeviti wa mitaa kwa kuagiza askari kuwakamata bila kuwaeleza makosa yao.

Nehemia alisema kwa muda mrefu amevumilia uonevu huo ila kwa sasa ameona awasilishe malalamiko yake katika sekretarieti ya maadili ili yaweze kushughulikiwa.

“Anachokifanya DC ni ukiukwaji wa maadili ya uongozi, kiongozi huwezi kuwa unasikiliza maneno bila kuyafanyia uchunguzi unaagiza mwenyekiti awekwe ndani, tunawekwa mahabusu bila kuambiwa makosa yetu, suala hili sasa basi,” alisema.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Kimara Baruti, Aloyce Kinyonga alidai kuwa DC huyo alimtukana hadharani kwa kumuita mtu asiye na maana.

“DC akiwa kwenye mkutano mtaa wa Kilungule A alitamka mbele ya wananchi kuwa mimi sina nidhamu, ni mtu wa hovyo kosa langu likiwa ni kuandika barua kuhusu suala la umeme, nimeona nami nilete malalamiko yangu tume ili waone viongozi wasiozingatia maadili,” alisema.

Akizungumzia suala hilo, mwenyekiti wa mtaa wa Makoka, Emmanuel Akyoo alisema kitendo cha kuwekwa ndani bila kuambiwa kosa alilofanya kinamsababishia kushindwa kutekeleza majukumu yake.

“Nashindwa kufanya kazi vizuri, muda wote nakuwa na wasiwasi na ninaamini hatuwezi kuendelea kwa mtindo huu, lazima viongozi tufanye kazi kwa uhuru,” alisema.

Kauli ya DC

Kisare alisema wenyeviti wote waliowekwa ndani walikuwa na makosa na kwamba hafahamu sababu za kumtuhumu.

Alisema wenyeviti wote ambao amewachukulia hatua walikuwa na makosa mbalimbali ikiwamo ubadhirifu, ukiukwaji wa taratibu na uonevu kwa wananchi.

“Hao ni watu wanaotaka kufanya siasa, sisi hatuna muda wa porojo lengo letu ni kuleta maendeleo hivyo hatuwezi kuvumilia wanaotumia nafasi zao kama mtaji,” alisema.

Akitoa mfano mtaa wa Golani ambako mwenyekiti wake aliwekwa ndani kwa kosa la kukiuka mwongozo uliotolewa na manispaa kwa ajili ya kufanya urasimishaji.

“Manispaa imeweka mwongozo kwa kila kata kuwe na urasimishaji wa makazi na gharama ya mpimaji isizidi Sh260,000 yeye akaenda kuleta mtu wa kufanya kazi hiyo kwa Sh450,000, akawa anawaweka ndani watu waliokuwa wanapinga gharama hizo,” alisema. 

Mensen Selekta na DJ Tito wamshambulia Man Fongo




Msanii na mtayarishaji muziki kutoka studio ya Defatality Mensen Selekta pamoja na DJ Tito wamemshambulia kwa maneno muimbaji wa singeli Man Fongo kutokana na tabia yake ya kutafuta kiki kwa kutumia majina yao kila anapotaka kutoa kazi zake mpya.

Mensen na DJ Tito wameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya msanii huyo kusema 'biti' anayolalamikiwa kuwa ameiba kwamba amepewa na DJ Tito ambae yupo chini ya Mensen.

"Mimi naomba tu, nimekanye Man Fongo maana naona muziki wake hawezi kuufanya bila ya Mensen kwa sababu haiwezekani kila anapotaka kuachia ngoma au 'video' amzungumzie Mensen ameenda amerudi kwa nini hawezi kuwazungumzia watu wengine ?. Kwa hiyo inaonesha kabisha Man Fongo bila ya Mensen hamna kitu, suala la kutoa 'instrument' ninavyojua mimi 'biti' sikutoa mimi bali alitengeneza kijana wangu", alisema Mensen.

Aidha, Mensen Selekta aliendelea kufafanua baadhi ya mambo na kusema siyo kweli kama anavyodai Man Fongo kuwa mdundo huo unaolalamikiwa amemuibia Sholo Mwamba kuwa umetolewa na DJ Tito.

"Cha kwanza akanushe kauli yake, DJ Tito hajagawa 'biti' kwa sababu yeye siyo 'producer' halafu ninavyojua mimi hawana mahusiano ya karibu ya kihivyo na Man Fongo", alisisitiza Mensen Selekta.

Kwa upande wake DJ Tito alisema alifuatwa na Man Fongo ili aweze kutengeneza 'kiki' kupitia mdundo huo kwa kumtaka aseme yeye ndio aliyempatia ili Sholo Mwamba akasirike.

"Mimi siwezi kupenda kumwambia kitu kizuri Man Fongo, sema namuelekeza kimazingira tu lakini yeye anayumba halafu kigege 360 kipo kwa ajili ya kazi na kupambana ili mambo yaende, muziki haufanywi hivyo anakiuka mazingira ya kimuziki", alisema DJ Tito.

DJ Tito aliendelea kwa kusema "Man Fongo yeye afanye kazi nzuri tu mbona watanzania watampokea vizuri, halafu hichi kigege 360 ndicho kilichomlea ila yeye ameleta dharau kwa Mensen na kwangu mimi ambaye niliyemtoa Tandale kwa hiyo Man Fongo ana laana na laana siyo lazima upewe na Baba au Mama hata masela kama sisi tunakuachia laana na hausongi mbele".

Malaika afungukia udhaifu wake



MWIMBAJI anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Diana Exavery ‘Malaika’, amefunguka kuwa, udhaifu wake mkubwa kwenye maisha ni kusimama mbele za watu na kujielezea yeye ni nani.

Akipiga stori na Showbiz-Xtra, Malaika alisema, katika maisha amekuwa na udhaifu tofauti tofauti lakini mkubwa kuliko wote ni kutokuwa na ujasiri wa kuweza kusimama mbele za watu na kujieleza.

“Nimewahi kufeli kwenye interview nyingi kwa sababu ya kutakiwa kujielezea, kwa kweli huu ni udhaifu wangu mkubwa, hali hii ni tofauti na nikiwa jukwaani niki-paform, kuimba jukwaani mbele ya mashabiki ni tofauti na kujielezea,” alisema Malaika

HOME AFYA BIASHARA MAHUSIANO KILIMO MAKALA TECNOLOG UREMBO CONTACT US Asilimia 75 waendao kupima JKCI wanakutwa na maradhi ya moyo




WATU 15 kati ya 20 wanaokwenda  kwa uchunguzi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), sawa na asilimia 75, wanakutwa na maradhi mbalimbali ya moyo, imefahamika.

Akizungumza  na waandishi wa habari jana, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo katika taasisi hiyo, Dk. Peter Kisenge, mbali na watu hao, alisema asilimia mbili hadi tatu  ya watoto wanaozaliwa nchini wana tatizo la moyo.

Kutokana na takwimu hizo, alisema ni vyema Watanzania wakafika katika taasisi hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati kwa ajili ya uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kujiunga na bima ya afya kwa kuwa huduma za matibabu ni kubwa.

Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo, alisema JKCI kwa kushirikiana na taasisi za Israel na Ujerumani, wameokoa Sh. milioni 800 ambazo zingetumika kuwapeleka nje ya nchi watoto 30 kwa matibabu ya moyo.

 Taasisi hizo ni Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto ya Israel na Kituo cha Moyo cha Berlin, Ujerumani, ambao hadi sasa wamewafanyia upasuaji wa bila kufungua kifua watoto 15.

 “Upasuaji unatumia mtambo wa Cathlab umefanyika katika kambi maalumu iliyoanza Januari 20, mwaka huu na itamalizika kesho (leo). Matibabu yaliyofanyika ni kuzibua matundu kwenye moyo na kutanua mishipa ya moyo kwa watoto wenye umri wa kuanzia mwezi mmoja hadi miaka 18,” alisema.

 Kwa mujibu wa Kisenge, kambi hiyo ilikwenda sambamba na uchunguzi wa moyo kwa watoto 32 ambao kati yao 20 watafanyiwa matibabu katika kambi hiyo na wengine 12 watatibiwa na madaktari hapa nchini kuanzia wiki ijayo.

 “Tumepanga kufanya matibabu kwa watoto 20, tunaamini hadi kambi itakapomalizika watakuwa wamepata matibabu. Watoto 15 waliopata matibabu wamesharuhusiwa na waliobaki wanaendelea vizuri,” alisema.

 “Tumetoa elimu ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa watoto, jinsi ya kuwahudumia waliofanyiwa upasuaji. Waliopata mafunzo ni madaktari, wauguzi, wataalamu wa kutoa dawa za usingizi na wataalamu wengine wa chumba cha upasuaji,” alifafanua.

 Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, asilimia 90 ya matibabu bila kufungua kifua yanafanywa na madaktari wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

 Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Naiz Majani, alisema wanawake wanapaswa kufanya uchunguzi wakiwa na mimba ya miezi minne, ili watakapojulikana na tatizo wajifungue katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hivyo kuwa rahisi kupata matibabu.

 Alisema kuna wanawake 35 wenye tatizo la moyo, kati yao watano wamejifungua mmoja mwanawe alifariki dunia kwa ugonjwa mwingine, wawili wana matundu makubwa kwenye moyo na mmoja limeanza kupungua.

 “Tunawashauri wazazi na walezi wasisahau kupima afya zao watoto wao watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi yanaanzia utotoni,” alisema.

 Kwa mujibu wa Dk. Majani, mtoto akianza kuugua magonjwa ya moyo, wazazi wengi  wanadhani ni matatizo ya kifua, lakini baada ya kuwafikisha hospitalini na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulika.

Tangu mwaka 2015 hadi sasa, watoto 46 wamefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel na kwamba gharama zimekuwa zikitolewa na taasisi za Israel na Ujerumani kwa makubaliano ya kirafiki na JKCI.

 Watoto 79 walitibiwa kwenye kambi maalumu kuanzia mwaka 2015 hadi 2017 na kwamba huduma hizo ni bure kwa watoto wenye matatizo hayo.

 Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), watu milioni moja wanakadiriwa kuwa na tatizo la moyo.

Wema amfungukia Mke wa Nabii Tito


 Wema Sepetu.

Katika hali isiyotarajiwa, imeelezwa kuwa msanii nyota wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu, amemlipua mke wa ‘Nabii’ Tito baada ya mwanamke huyo kumshawishi kupitia mitandaoni aolewe na nabii huyo.

Chanzo chetu makini kilisema kuwa, msanii huyo amekasirishwa na kitendo cha mke huyo kumshawishi kuolewa na mumewe anayeitwa Onesmo Machija ‘Nabii Tito’ (44).

“Wema Sepetu nakupenda sana hata Nabii Tito anakupenda sana, kwanza mzuri, una shepu nzuri hata katika mambo ya Kiafrika unaongoza kwa uzuri.

“Nabii Tito huyo kwa watu wasiomfahamu wanasema sio nabii lakini kwa mimi ninayemfahamu na kuishi naye naona mambo ya kinabii anayofanya, nakuomba ukubali hata mimi nakupenda sana, kwanza una shepu nzuri.

“Uwe mke mwenzangu, ukubali kuwa mke wa Nabii Tito. Sikia kilio cha mke wa nabii,” amesikika kwenye video mke huyo wa Nabii Tito akimbembeleza Wema.

Naye Nabii Tito kwenye video hiyohiyo amechombeza kwa kubembeleza kwamba Wema akubali kuwa mkewe ili kanisa lao likuwe.

Alipotafutwa Wema na kuulizwa kuhusiana na video hiyo alisema, ameiona na amekasirishwa na kile walichokifanya nabii huyo na mkewe.

“Kiukweli wameniudhi sana kwa kunidhalilisha. Nawasiliana na mwanasheria wangu ili nimburuze mahakamani mwanamke huyo,” alisema Wema.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, mapema wiki hii lilimkamata nabii huyo na kumfanyia mahojiano kutokana na mahubiri ya kidini anayoyafanya na limesema mtu huyo ana matatizo ya akili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Gillesi Muroto amesema Juni 23, 2014, mtu huyo aliwahi kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu ya akili chini ya daktari aliyejulikana kwa jina moja la Dk. William ambapo aliporuhusiwa alitakiwa kurejea hospitalini hapo Julai 9 mwaka huohuo lakini hakurejea.

Kamanda Muroto aliendelea kusema kwamba, baada ya hapo Machija ambaye kanisa lake halijasajiliwa popote, aliibukia mkoani Dodoma katika Kijiji cha Nong’ona kilicho karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) akifanya mahubiri ya kidini yaliyodaiwa kuwa hayakuwa na maadili ya kidini.

“Kwa msingi huo, jeshi la polisi limempeleka Hospitali ya Rufaa ya Milembe iliyoko mkoani Dodoma kwa ajili ya kumpima tena matatizo hayo ya akili na baada ya majibu kutolewa, Dk. Dixon Philipo aliyemshughulikia alithibitisha kwamba bado ana matatizo hayo ya akili,” alisema kamanda Muroto juzi na kusisitiza kuwa wanaendelea kumshikilia kutokana na matendo yake aliyoyafanya ili kufanya uchunguzi zaidi.

Nabii Tito na mkewe pamoja na mfanyakazi wake wa ndani.

MAGAZETI YA LEO 25/1/2018



























Madhara Ya Kufanya Mapenzi Kupita Kiasi



Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.

Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.

Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari, hapa nimeweka chumvi kidogo lakini huo ndio ukweli halisi.

Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.

Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana.

Twende pamoja katika kutazama madhara hayo kwa kina.

1.    Kupoteza hamu ya tendo la ndoa.
Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.

Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.

Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.

2.   Kuujaza mwili tamaa kubwa.
Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa wakati gani?

Watu wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo wale ambao kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake.

Hawa ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani au kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi.

Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate kiu ya penzi.

3.   Kupoteza raha kamili ya tendo.
Raha ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako.

 Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!

4.   Kupoteza nguvu ya mwili.
Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.

Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke. Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.

Sambamba na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.

5.   Kupatwa na magonjwa.
Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi, lakini ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko wakati wa kujamiiana na hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.

Lijue jambo muhimu la kuzingatia katika safari yako ya Mafanikio


Kwa hali yoyote ile ambayo inatokea nje ya wewe haina mchango mkubwa sana wa kuweza kukukwamisha au kukufanya ushindwe kufikia mafanikio yako. Kitu ambacho kitakufanya ushindwe kufanikiwa ni ile hali inayotokea ndani mwako tu.

Hali hiyo inayotokea ndani mwako, ndiyo ina nguvu kubwa sana ya kubadillisha maisha yako na kuwa ya mafanikio kabisa. Hebu jiulize kila unapowaza mafanikio, ndani mwako unajionaje? Unajiona ni kwamba utafanikiwa au utashindwa? Kipi unachokiona ndani mwako?

Haijalishi watu wanasemaje au watasema nini juu yako, hata watu dunia nzima waseme kwamba utafanikiwa, lakini kama ndani yako huoni hivyo ni wazi huwezi kufanikiwa, pia hata dunia nzima iseme kwamba wewe ni wa kushindwa, lakini ikiwa ndani yako unajiona wewe ni mtu wa mafanikio, utafanikiwa.

Kiti kikubwa hapa, jifunze kutokulaumu hali yoyote ile, inayotokea nje katika maisha yako kwamba ndio imekukwamisha. Anayejizuia na kujikwamisha sio mwingine bali ni wewe mwenyewe na hali hasi nyingi ulizozibeba. Kuanzia leo amua kujenga hali bora ndani mwako itakayokupa mafanikio makubwa.

Faida 5 za kuendesha Baiskeli


Najua fika utakuwa umeshangazwa na kichwa ya mada hapo juu, ya kwamba hivi ni kweli kuna faida yeyote ya kuendesha baiskeli kiafya, ukiachana na dhana ya kwamba baiskeli ni chombo cha usafiriambacho hutumika kukufikisha sehemu unayotaka kwenda? Majibu ya swali hilo yapo katika Makala haya kwamba ndiyo zipo faida ambazo utazipata endapo utaendesha baiskeli mara kwa mara.

Miongoni mwa faida hizo ni;
1. Kuendesha baiskeli kunasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa  mafuta  mwilini, kwasababu hupunguza calori  mwilini.

2. Baskeli ni usafiri rahisi unaoweza kujichanga ukanunua na ukaokoa bajeti ya nauli za kilasiku uendapo katika shughuli zako kama si mbali sana na maeneo unayoishi.

3. Hukufanya uwe karibu na watu wanaotembea kwa miguu, kwa mfano ukiwa njiani utasalimiana na watu mbalimbali, tofauti ilivyo gari.

4. Ukitumia baskeli hukupa nafasi ya kuona kupita sehemu ambazo kwa gari usingefika, hivyo hutumia njia fupi.

5. Kuendesha baiskeli husaidia kuimarisha misuli ya mwili hivyo kwa maneno mengine tunaweza tukasema licha ya baiskeli kutumika kama usafiri lakini vilevile ni chombo cha mazoezi, hivyo endesha baiskeli   mara kwa mara ili kuuweka mwili wako sawa.

Vyakula vinavyoondoa mamumivu wakati wa hedhi kwa wanawake

Kila mwanamke hupitia hatua ya kupatwa na hedhi mara moja kwa mwezi, ikiwa ni maumbile ya kawaida waliyoumbwa nayo. Lakini wanawake wengi husumbuliwa na matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati wa siku zao, matatizo hayo hutofautiana kati ya mtu na mtu kutegemeana na afya ya muhusika, wapo baadhi ya wanawake huumwa na kiuno, wengine tumbo n.k

Dlili za matatitizo ya hedhi
Siku chache kabla ya hedhi, baadhi ya wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye hasira. Husumbuliwa na mfadhaiko wa akili, huumwa na kichwa, matiti hujaa maziwa, hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri. Hali hii husababishwa na kukosekana kwa uwiano wa homoni (Homone imbalance) na hali hii huweza kukoma ndani ya saa 24 baada ya kuanza hedhi.

Wengine hupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano wa homoni mwilini, ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani.

Wengine hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa katika siku za hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu, kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na sababu nyingine za kitabibu.

Vifatatavyo ni vyakula vinavyoweza kutibu maumivu wakati wa hedhi

2. Tangawizi
Tangawizi nayo ni dawa nzuri sana ya kutibu matatizo yatokanayo na hedhi, hasa katika tatizo la maumivu makali na kutokupata hedhi. Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na kiweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache, kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo, kwa siku mara mbili kila baada ya mlo.

2. ufuta.
Ufuta (Sesame) nao ni miongoni mwa mbegu za asili unazoweza kula na kutibu matatizo ya hedhi. Saga ufuta na pata unga wake kisha uchanganye na maji ya moto, kunywa mara mbili kwa siku. Kinywaji hiki huondoa maumivu wakati wa hedhi kwa wasichana wadogo.

Ukitumia mara kwa mara kinywaji hiki cha ufuta, hutibu pia tatizo la kupata hedhi kidogo. Pia unaweza kuchangaya maji ya kuoga ya uvuguvugu na mbegu za ufuta zilizopondwa pondwa kiasi cha kiganja kimoja, nayo hutoa nafuu kubwa kwa wanaosumbuliwa na maumivu, hasa ukitumia siku mbili kabla ya siku zako.

3. Papai
Mungu ametuumba na kutupa mazao mengi ambayo yana uwezo wa kutatua matatizo yetu ya kiafya, iwapo tutagundua siri hiyo. Papai bichi nalo linaelezwa na watafiti wetu kuwa lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya utokaji wa hedhi kuwa mwepesi usio na maumivu. Papai huwa na manufaa zaidi kwa wasichana haswa kwa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na kuwa na ‘stress’ au mawazo. Utapata faida hiyo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi (ambalo halijaiva lakini limekomaa)

4. Juisi za mboga za majani.
Kwa kutumia vyakula asilia unaweza kuepukana na maumivu ya mara kwa mara wakati wa siku zako. Katika orodha ndefu ya juisi za mboga zinazotibu kwa uhakika matatizo yote ya hedhi, ni Kotimiri (Parsley), mboga ya majani ambayo upatikanaji wake ni rahisi. Kwa mujibu wa watafiti, Kotimiri ina uwezo wa kurekebisha uwiano wa homoni hivyo kuondoa matatizo kadhaa ya hedhi.

Inaelezwa kuwa uwezo wa Kotimiri kurekebisha matatizo ya hedhi unatokana na kuwa na aina ya kirutubisho kiitwacho ‘Apiol’ ambacho pia kimo miongoni mwa homoni za jinsia ya kike (estrogen). Maumivu na mvurugiko wa siku hurejea katika hali ya kawaida kwa kunywa juisi ya Kotimiri mara kwa mara.

Aidha, juisi hiyo inapochanganywa na juisi ya viazi pori (Beet Root), karoti au matango huwa na nguvu zaidi. Kiwango kinachoshauriwa kuchanganya kiwe na ujazo sawa kwa kila aina ya juisi utakayochanganya. Juisi yenye mchanganyiko huo ni rahisi kutengeneza na ni dawa inayoweza kumsaidia mwanamke wakati wote wa maisha yake bila kuhitaji kutumia dawa zingine kali za kuzuia maumivu (pain killers) ambazo huwa na madhara baadaye.


Wednesday, 24 January 2018