Wednesday, 13 December 2017

Bifu la Wolper na Husna kwishaaa


Jacqueline Wolper

 MASTAA wawili waliokuwa na bifu kwa sababu ya kuchangia bwana Mkongo ajulikanaye kama Mwami Radjabu, Jacqueline Wolper na Husna Maulid wamemaliza uhasama kati yao na sasa ni full vicheko.

Hali hiyo ilijidhihirisha juzikati kwenye sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Wolper, walipoonekana wakiwa karibu na

kufurahi huku vyanzo vikisema warembo hao walielewana baada ya Husna kumwagana na bwana huyo.

“Si unajua Husna alishamwagana na Mwami ambaye alimvisha mpaka pete ya uchumba lakini hawakufanikiwa kufunga ndoa, kwa hiyo walimaliza tofauti zao,” kilisema chanzo.

Baada ya kuona na kupata habari kutoka kwa chanzo, Za Motomoto News

ilimtafuta Husna ambaye awali alikuwa hapendi kabisa kumsikia Wolper ambaye alikiri kumaliza tofauti zao.

“Tulishamaliza tofauti zetu, sina bifu na Wolper maana aliyekuwa anatugombanisha ni mwanaume na sisi ni wanawake hivyo wanawake tujifunze kuwa wanaume ni watu wa kupita tu,” alisema Husna.


Husna Maulid.

Serikali yatoa taarifa hii kuhusu kufanyika kwa mnada wa madini ya Tanzanite



Baada ya Wema kukutana na Makonda, Steve Nyerere afunguka


 Wema Sepetuakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Siku tatu baada ya muigizaji maarufu wa filamu, Wema Sepetu kumuangukia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mchekeshaji nyota, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ amebwatuka vibaya kuhusiana na ishu hiyo.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa njia ya simu juzi akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea Dodoma, msanii huyo anayedhaniwa kufanikisha kwa kiwango kikubwa kurejea CCM kwa Wema Sepetu, alikiri wawili hao kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani, nyumbani kwa bosi huyo wa mkoa.

“Hakuna uadui wa kudumu katika haya maisha, isitoshe wale wote ni vijana, wamekutana wameombana msamaha na mambo yamebakia kuwa historia. Wanaangalia maisha mengine ya huko mbele kwa sababu safari bado ni ndefu,” alisema mchekeshaji huyo ambaye pia ni mmoja wa viongozi wa kundi linalohamasisha uzalendo kwa watanzania.

Kuhusu kama kuna ahadi yoyote iliyo nyuma ya makubaliano baina ya wawili hao ambao kabla ya kutofautiana wanaripotiwa kuwa marafiki, Steve alisema hakuna kitu chochote zaidi ya wao kuamua kuachana na mambo ya zamani na kufungua ukurasa mpya.

“Hili ni funzo kubwa sana kwa wapambe, hasa wasanii, watu wakikorofishana wawe na akiba ya maneno, kuna watu walikuwa wanatoa maneno ya ovyo kwa mkuu wa mkoa kupitia kwa Wema, sasa leo hawa wamepatana, hivi sura zao wanazipeleka wapi?

“Haya mambo ya maisha, ukiona kuna jambo limewatokea watu, ni vizuri mtu ukawa na kiasi cha maneno, au wengine walikuwa wanamponda Wema kwa kupitia kwa mkubwa, sasa leo hii wanajisikiaje?” alisema.

Alipoulizwa kuhusu kutoonekana kwa mama mzazi wa msanii huyo, Miriam Sepetu nyumbani kwake Sinza Mori, ikidaiwa kuwa huenda amefichwa sehemu kwa malengo maalum, Steve Nyerere alisema kada huyo wa Chadema yupo nyumbani kwake.

“Nani amekuambia mama hayupo? Yupo palepale nyumbani kwake na mambo yanaenda vizuri tu, wala watu hawana haja ya kumtafuta popote,” alisema Steve, akipinga habari za kutokuwepo nyumbani hapo kwa siku kadhaa sasa, ambako kumeripotiwa na magazeti ya Global Publishers.

Uhusiano wa Makonda na Wema uliingia dosari baada ya mkuu huyo wa mkoa kumtaja katika orodha ya kwanza ya watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya, Februari mwaka huu.

Mchekeshaji nyota, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’.



Ukarabati wa nyufa za majengo ya UDSM waanza


Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeanza ukarabati wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yenye ufa.

Taarifa za kuwepo nyufa hizo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii usiku wa Desemba 3,2017 na baadaye ufafanuzi ulitolewa na TBA.

Uchunguzi uliofanywa na MCL Digital umebaini ukarabati umeanza, huku ikielezwa kuwa hauwaathiri wanafunzi wanaotumia mabweni hayo.

“Ukarabati umeanza, mafundi wanafanya kazi nje ya jengo kwa kuondoa plasta ili kuangalia tatizo liko wapi,” kimesema chanzo cha habari kilichozungumza na MCL Digital.

TBA iliyojenga majengo hayo ambayo bado yako katika usimamizi wake imeelezwa pia inaangalia dosari nyingine zilizopo.

Mtendaji Mkuu wa TBA, Mhandisi Elius Mwakalinga Desemba 4,2017 akizungumzia nyufa zilizoko kwenye jengo la Block A alisema hazina madhara na walizitarajia.

Alisema nyufa katika jengo hilo la hosteli ambalo ni kati ya sita yaliyopo Block A zimetokea eneo walilotarajia ambalo kitaalamu linajulikana (expansion joint) hivyo hazina madhara.

Mwakalinga alisema kwa kawaida udongo unaobeba jengo hutitia baada ya muda fulani, hivyo wakati wa ujenzi huacha nafasi kuliwezesha jengo kupumua bila kusababisha nyufa.

Mwakalinga alisema kuna makosa yalifanyika ya kuziba nafasi zilizoachwa (expansion joint) kwa kutumia saruji badala ya mbao au plastiki maalumu hivyo kuonyesha nyufa kwenye jengo hilo.

Kutokana na kusambaa kwa picha kuonyesha nyufa katika majengo hayo, mbunge wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), Kumbusho Dawson alishikiliwa na polisi kitengo cha makosa ya mtandao kwa kuhojiwa na baadaye aliachiwa.


Ushindi wa CCM watenguliwa na Mahakama



Mahakama ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara imetengua ushindi wa CCM wa nafasi ya mwenyekiti wa Kitongoji cha Sola kilichopo Kata ya Mutuka na kuamuru uchaguzi urudiwe.

Mgombea wa CCM alipita bila kupingwa baada ya mgombea wa Chadema kuenguliwa katika mchakato wa uchaguzi.

Hakimu John Shao akitoa hukumu ya kesi namba 1/2017 jana Jumanne Desemba 12,2017ameamuru uchaguzi ufanyike upya kwa nafasi hiyo.

Kesi hiyo ilifunguliwa na mgombea uenyekiti wa kitongoji hicho (Chadema), Vincent Slaa akipinga kuenguliwa na kamati ya rufaa ya uchaguzi ya wilaya hiyo. Aliwakilishwa na wakili Tadey Lister.

Hakimu Shao amesema Mahakama inakubaliana na pingamizi lililowekwa na Slaa kwamba alienguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi bila sababu za msingi, hivyo Sagwale wa CCM akapitishwa bila kupingwa kwa nafasi ya mwenyekiti wa kitongoji.

Amesema Slaa aliondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi uliofanyika Aprili 29,2017 na kamati ya rufaa ya uchaguzi Wilaya ya Babati.

Hakimu Shao ameamuru uchaguzi wa nafasi hiyo urudiwe na upande wa wadaiwa unapaswa kulipa gharama za kuendesha kesi hiyo.

"Kamati ya rufaa ya uchaguzi ya Wilaya ya Babati haikutenda haki ilipoondoa jina la Slaa kwenye uchaguzi, hivyo Mahakama inatengua nafasi ya Sagwale aliyepitishwa bila kupingwa na kuamuru uchaguzi ufanyike upya," alisema hakimu Shao.

Wadaiwa wengine kwenye kesi hiyo ni kamati ya rufaa ya uchaguzi, msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa kata ya Mutuka na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo.

Mbunge wa Babati Mjini (Chadema), Pauline Gekul ametoa shukrani kwa Mahakama kwa kutenda haki kwa kuwa mgombea wa chama hicho aliondolewa kwenye mchakato huo kwa kuonewa.

"Mgombea wa CCM alipitishwa bila kupingwa sasa turudi uwanjani ili nafasi hiyo ipate mwenyewe kwa jasho na kwa halali kupitia kura za wananchi," amesema Gekul.

Aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji hicho, Sagwale alisema wananchi wa eneo hilo wana imani naye kwa kuwa muda mfupi aliowaongoza wamempa ushirikiano wa kutosha.

Pep Gurdiola awaomba radhi Manchester United “kinafiki”



Baada ya mchezo kati ya Manchester United na Man City mwishoni mwa wiki iliyopita, inadaiwa kuliibuka fujo kubwa katika eneo la kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo la uwanja wa Old Traford.

Chanzo cha fujo hiyo kinatajwa kwamba ni kitendo cha Manchester City kushangilia sana na kupiga kelele nyingi, jambo hilo liliwakera baadhi ya watu wa United akiwemo Jose Mourinho na mvutano ulianzia hapo.

Pep Gurdiola ambaye ndiye aliwaongoza vijana wake kuichapa United bao 2 kwa 1 amesema hawakuwa na nia ya kuwakera Manchester United kwani wao walikuwa wakishangilia tu lakini kama wamekereka anawaomba msamaha.

“Lakini na wao kuna michezo ambayo walishinda na wakashangilia sana, sisi tumeshinda Derby na tulipaswa kufurahia hilo na kama limewaudhi tunaomba radhi kwa kila mtu wa United aliyekereka” alisema Pep.

Pep Gurdiola amesisitiza kwamba akama timu ikifanya vizuri uwanjani na ikaibuka na ushindi kinachofuatia ni kwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo ambapo watu wanakwenda kufurahia walichofanya.

Tayari shirikisho la soka nchini Uingereza FA limeiandikia Manchester United barua kuhusiana na tukio hilo ambapo inadaiwa kwamba kulikuwa na vitendo vya urushwaji wa chupa za maji na maziwa kati ya pande hizo mbili.

Hukumu ya Simba na Yanga kujulikana leo



 

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ngazi ya klabu msimu wa 2017/18 Simba na Yanga, watajulikana leo ambapo droo ya kupanga hatua ya awali ya michuano hiyo itafanyika jijini Cairo, Misri.

Yanga ambao ni mabingwa wa Tanzania Bara wanasubiri kuwajua wapinzani wao katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na wakati Simba SC wao wakisubiri kujua wataanza na nani katika Kombe la Shirikisho.

Michuano hiyo huandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Tayari kamati kuu ya utendaji ya shirikisho hilo imeshaanza vikao vya awali tangu Disemba 11 mwaka huu ikijadili maboresho mbalimbali yanayohitajika kufanyika kwenye michuano hiyo.

MKutano huo unaojulikana kama (CAF interclubs competitions think-tank 2017) unatarajia kutoka na uamzi wa juu ya nini kifanyike ili kuboresha michuano hiyo na hii huenda ikaangukia kwenye kubadili muundo wa mashindano hayo.

Tayari klabu zote za Simba na Yanga zimeshawasilisha majina ya usajili wa wachezaji wao kwa ajili ya michuano ya klabu bingwa na Kombe la Shirikisho Afrika. Mabingwa watetezi wa klabu bingwa ni Wydad Casablanca ya Morocco wakati mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho ni TP-Mazembe ya DR Congo.

Dirisha la Helikopta ya Jeshi la Marekani Yaanguka Shuleni Japan



Sehemu ya ndege ye jeshi la Marekani imeanguka kwenye shule katika kisiwa cha Okinawa nchini Japan na kuzua upya misukosuko na watu wa eneo hilo.

Sehemu hiyo ya dirisha ilianguka kwenye uwanja wa shule na kusabisha majeraha madogo kwa mwanafunnzi mmoja.

Katika miaka ya hivi karibuni, ajali kadha na visa vya uhalifu vimesababisha kuwepo upinzani dhidi ya kambi hiyo ya Marekani.

Jeshi la Marekani lilithibitisha kuwa dorisha kutoka moja ya helikopta zake ilianguka kwenye uwanja wa michezo wa shule iliyo nje ya kambi ya yake ya jeshi la wanahewa.

"Tanzania imeshaonekana kuwa ni kichaka cha fedha za kigeni" - JPM

"Tanzania imeshaonekana kuwa ni kichaka cha fedha za kigeni" - JPM

Audio | S Kide – 900 Itapendeza | Mp3 Download

Audio | S Kide – 900 Itapendeza | Mp3 Download

Audio | S Kide – 900 Itapendeza | Mp3 Download

  DOWNLOAD

Alichoandika Zari kwenye Birthday ya Marehemu Ivan

Alichoandika Zari kwenye Birthday ya Marehemu Ivan


Spidi ileile kuileta Treni ya Umeme Tanzania, Prof. Mbarawa kagoma kulala

Spidi ileile kuileta Treni ya Umeme Tanzania, Prof. Mbarawa kagoma kulala


LIVE: "Tanzania imeshaonekana kuwa ni kichaka cha fedha za kigeni"

LIVE: "Tanzania imeshaonekana kuwa ni kichaka cha fedha za kigeni"