Tanzania\'s leading online News Edition (The National Newspaper). Get access to the most current and latest authoritative news on local issues, politics, events, celebrations, editorial, columnists, features, people and business.
Thursday, 7 December 2017
LIVE: Cha kufahamu kuhusu Tamasha la ''DR SHIKA'' Usiku wa 900 itapendeza
Odinga apewa onyo na Marekani

Raila Odinga
Marekani imemtaka kiongozi wa upinzani nchini kenya Raila Odinga kuacha mpango wake wa kuapishwa kama raisi wan nchi hiyo wiki ijayo.
Odinga aliwasilisha Malalamiko juu ya mapungufu katika uchaguzi mkuu uliopita na kusababisha uchaguzi wa marudio ambapo Uhuru Kenyata alishinda kwa kura nyingi.
Msaidizi wa katibu wa masuala ya Afrika Marekani , Donald Yamamoto ambae ametembelea nchini kenya.
Ametaka majadiliano ya pande zote mbili kati ya upinzani na serikali ilioko madarakani.
Baadhi ya viongozi wa serikali wameonya kuwa tukio hilo la kuapishwa linaweza kuhusishwa na uhaini.
Trump ameutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

Rais Trump amefanya maamuzi ya kihistoria ya kuipindua sera za miaka mingi ya Marekani kwa kuutambua mji wa Yerusalem kuwa ndio mji mkuu wa Israel.
Rais huyo pia ametangaza kuwa Ubalozi wa Marekani utahamishwa kutoka katika eneo la sasa la Tel Aviv kwenda Yerusalem. Amesema kuwa uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za kuleta amani katika eneo hilo la mashariki ya kati.
Trump amesema uamuzi huu haulengi kujiondoa kwa Marekani katika juhudi zake za dhati za kuleta amani ya kudumu bali inataka kutafuta suluhu ya mgogoro wa miaka mingi kati ya Israel na Palestina ambao .Marekani haifungaman na upande wowote na kuingilia mipaka ya Israel na mamlaka zake ,na hatuko tayari kuingilia katika migogoro yao ,hayo ni mambo yao wenyewe.
Huku kwa upande wake Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesikitishwa na maamuzi ya rais Trump na kudai kuwa Marekani imepoteza haki ya kusimamia hatua ya kupatana kwa amani ambayo imekuwa ikitafutwa miongo kadhaa iliyopita.
Huku waziri mkuu wa Israel ,Benjamin Natanyau ameonekana kuunga mkono hatua ya rais Trump kwa kuelezea kuwa ni maamuzi ya kihistoria licha ya kuwa wapalestina wamemkosoa na huku Uingereza na nchi nyingine wanachama wa baraza la usalama wa umoja wa mataifa wameitisha kikao cha dharura ili kujadili maamuzi yaliyofanywa na rais Trump.
Polepole Awapiga Dongo CHADEMA

Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema CHADEMA wamefanya kikao cha dharura kususia uchaguzi wa marudio wa majimbo na kata unaotarajiwa kufanyika January 13 mwakani.
Polepole amewatuhumu CHADEMA kuwa wanatumia mgongo wa kuminywa kwa Demokrasia nchini kususia uchaguzi huo wakati ukweli ni kwamba wamefulia baada ya kutumia vibaya hela ya mfuko wa chama chao.
"Watani wanakutana leo, agenda ni kutoshiriki uchaguzi unaokuja wa marudio kwa kisingizio cha demokrasia lakini ukweli ni matumizi mabaya ya fedha yamefuja mfuko wa chama. Tafuteni visingizio vingine lakini sio demokrasia. Watu wamechoka siasa za matukio. Kikao chema!" Ameandika polepole katika ukurasa wake wa Twitter.

Mtatiro akanusha kuhamia CCM

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amekanusha uvumi unaonea kwenye mitandao ya kijamii kwamba ana mpango wa kukihama chama hicho na kuhamia Chama tawala cha CCM.
Kupitia taarifa yake kwa umma aliyoitoa jana Disemba 6,2017, Mtatiro pia hana mpango wa kugombea jimbo la Kinondoni lililo achwa wazi kufuatia aliyekuwa Mbunge wake kupitia CUF, Maulid Mtulia kujiuzulu na kujiunga na CCM.
“Ndugu zangu, nimeona propaganda nyingi kwenye mitandao juu ya mimi kuhamia CCM au kuwa na mipango ya kuhamia CCM.
"Nataka niwahakikishie watanzania kuwa SIJAPANGA mipango hiyo na sina nia hiyo. Na naomba niwajulishe kuwa mtu akiwa anahamia CCM, hamuwezi kuwa na tetesi, na mimi sina kawaida ya kufanya maamuzi ghafla na kwa kujificha.
"Ningelikuwa na nia ya kuhamia CCM ningewataarifu hapa hadharani, miezi kadhaa kabla ya kufanya hivyo, walau jambo moja ambalo Mungu alinijalia ni kutokuwa mwoga na mnafiki na alinipa uwezo mkubwa wa kufanya jambo naloliamini,” alisema na kuongeza.
“Pili, nimepokea meseji nyingi sana zikiniomba nigombee ubunge jimbo la Kinondoni baada ya Mbunge wa (CUF – Lipumba), Ndugu yetu Maulid Mtulia kuhamia CCM. Nataka niweke msimamo wangu mapema, kwamba sina na sikuwahi kuwa na ndoto za kugombea ubunge wa jimbo la Kinondoni,
Masuala ya kugombea ubunge kwenye majimbo ni masuala mapana, yanahitaji maandalizi, ukaribu wako na wapiga kura na historia yako na jimbo hilo. Kwa kiasi kikubwa hakuna kigezo hata kimoja kati ya hivyo ambacho nimekikaribia, kwa hiyo sitoweza kugombea kama nilivyoona baadhi ya fikra za watu mitandaoni.”
Mtatiro amewahakikisha wanachama wa CUF kwamba anaendelea na majukumu yake ya Kamati ya Uongozi CUF, pamoja na kushirikiana na kila mtanzania kwa njia mbalimbali katika kuijenga nchi.
“Na kupitia michango yangu hiyo naendelea kuijenga Tanzania na hata kuunga mkono juhudi chanya za Rais wetu kuijenga Tanzania huku zile juhudi hasi za Rais huyo huyo hasa kwenye eneo la Demokrasia, Utawala Bora na Uchumi, nikizikemea kila siku.
"Mwisho, wapo wendawazimu wanachekelea, wanafurahia na ama kutamani vyama vya upinzani vife. Ukiona elimu ni ghali, hebu jaribu ujinga,” amesema.
Hata hivyo, Mtatiro amesema anaendelea kuwaheshimu wanaohamia CCM, kwa uhuru, utashi na mapenzi yao au kwa kununuliwa, kutokana kwamba sio wa kwanza wala hawatakuwa wa mwisho kufanya hivyo.
Yanga kutoa pigo Simba

MMOJA WA WACHEZAJI WA TIMU YA SIMBA, JUUKO MURSHEED ANAYEWANIWA NA TIMU YA YANGA
KAMA mazungumzo yanayoendelea kati ya uongozi wa klabu ya Yanga na wachezaji wawili wa klabu ya Simba yatakamilika, Wanajangwani hao kwa mara ya nyingine watakuwa wametoa pigo kwa vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa kama ilivyo kwa Simba na Singida United, ipo kwenye mazungumzo ya siri na kiungo Muzamir Yassin na beki wa kati raia wa Uganda, Juuko Mursheed, ikijaribu kuwashawishi kutua kwenye timu hiyo katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.
Yanga imetuma wajumbe wake wa kamati ya usajili jijini Nairobi inapofanyika michuano ya Kombe la Chalenji, kufanya mazungumzo na nyota hao.
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alimwambia mwandishi wetu kuwa, kwa upande wa Muzamir mazungumzo ya awali yanatoa ishara ya mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar kuweza kutua kwenye kikosi chao hivi karibuni.
"Kuhusu Juuko, bado wapo kwenye mazungumzo, nafikiri baada ya siku chache lolote linaweza likatokea... wachezaji hawa wawili, kimkataba wanaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine kwa sababu mikataba yao imebaki miezi sita kumalizika," alisema Mjumbe huyo.
Aidha, taarifa zilieleza kuwa wachezaji hao wanasakwa vilivyo na Yanga kwa ajili ya kwenda kuchukua nafasi za kiungo Thaba Kamusoko ambaye ni majeruhi pamoja na beki Vincent Bossou aliyeamua kuachana na Yanga.
Muzamir yupo kwenye kikosi cha Kilimanjaro Stars kwenye michuano hiyo ya Chalenji inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), huku Juuko akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda 'The Crane'
Wastaafu wa TRL wamuomba Rais Magufuli kuwasaidia wapate Mafao yao

Morogoro. Baadhi ya wastaafu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) wamemuomba Rais John Magufuli kuingilia kati na kuwasaidia ili waweze kulipwa mafao yao na fedha za kusafirishia mizigo ambazo wanadai kwa zaidi ya miaka mitano sasa.
Wastaafu hao ambao wameungana kudai stahiki zao walistaafu tangu mwaka 2012 hadi Juni, miaka yote wamekuwa wakidai stahiki hizo bila mafanikio.
Wakizungumza na gazeti hili jana, wastaafu hao walisema madai yao makubwa ni fedha za kusafirisha mizigo na familia ili kurejea vijijini kwao.
Katibu wa wastaafu hao, Selungwi Ubwe alisema wapo zaidi ya 100 katika mikoa mbalimbali nchini ambao wameshindwa kurejea makwao kwa kukosa fedha.“Madai yetu ni nauli za kusafirisha familia na mizigo, mafao ya kustaafu, kuna utaratibu wa wastaafu kulipwa tuzo za ustaafu ambazo ni mabati na mifuko 50 ya saruji na fedha taslim kulingana na kiwango chako cha mshahara na muda uliotumikia shirika,” alisema Ubwe.
Naye mstaafu mwingine, Ally Makubi alisema shirika halina budi kuwalipa stahili zao zote kwani walikuwa waadilifu kipindi chote cha utumishi.
“Mfanyakazi anapostaafu hana tegemeo lolote zaidi ya mafao na tuzo ili aweze kuendeleza maisha mengine, hivyo ni vyema Serikali ikaona umuhimu wa kutulipa tena kwa haraka,” alisema Makubi.
Akizungumzia suala hilo, katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu), Christopher Kaziyo alisema kwa sasa wameomba kuwasiliana na mkurugenzi wa Mfuko wa Pensheni (PPF) ili kujua tatizo, kwa kuwa ndio unaopaswa kuwalipa pensheni wastaafu hao. “Suala la mafao sheria zipo wazi kama mwajiriwa akithibitisha makato ya fedha hizo kwenye mshahara wake anastahili kulipwa bila kusumbuliwa,” alisema Kaziyo.
Naye mkurugenzi wa TRL, Masanja Kadogosa alisema hakuna mstaafu yeyote anayedai fedha za kusafirisha mizigo na familia kwani hulipwa baada tu mtumishi anapostaafu.
“Hakuna mtumishi anayetudai fedha za kusafirisha mizigo, kwani fedha hizi hulipwa mwanzo kabisa na kuhusu mafao mifuko ya hifadhi ndio inayopaswa kuwalipa,” alisema Masanja.
Mkurugenzi huyo alisema fedha ambazo wastaafu hao hawajalipwa ni za tuzo ambazo zina utata kidogo, hivyo wapo katika majadiliano ili zilipwe.
Uboreshaji TRL
Kampuni hiyo ilianza uendeshaji wa shughuli zake Oktoba 2007 chini ya umiliki wa mwekezaji kampuni ya Rites ya India ambayo ilikuwa inamiliki hisa 51 na Serikali ya Tanzania hisa 40. Hatua hiyo ilifuatia kuvunjwa kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kukaribisha wawekezaji ambao baadaye walishindwa na kuanzia Julai 22, 2011 hisa zote za kampuni hiyo zinamilikiwa na Serikali.
Kwa sasa Serikali imedhamiria kuboresha wa miundombinu ya treni na kupitia kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (Rahco), tayari imeingia mkataba na kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki kujenga kipande cha pili cha reli ya kisasa ya Standard gauge (SGR) kutoka Morogoro hadi Makutopora yenye umbali kilomita 336 za njia kuu na kilomita 86 za njia za kupishana treni zitakazogharimu Sh4.3 trilioni.
Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Manyara afariki dunia

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Manyara mstaafu, Joel Bendera amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Akizungumza na MCL Digital leo Jumatano Desemba 6,2017 msemaji wa MNH, Aminiel Aligaesha amesema, “Ni kweli Joel Bendera amefariki. Aliletwa leo na gari la wagonjwa saa 6:30 mchana na ilipofika saa 10:24 jioni alifariki.”
Aligaesha amesema Bendera alipokewa hospitalini hapo akitokea Bagamoyo mkoani Pwani.
Kuhusu chanzo cha kifo chake Aligaesha amesema, ‘’Hilo sasa ni suala la familia lakini kwa wakati huu itoshe kusema amefariki.”
Bendera pia amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Mbali ya ukuu wa mkoa, amewahi kuwa mbunge wa Korogwe Mjini na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo katika utawala uliopita wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
Katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais John Magufuli Oktoba 26,2017, Bendera alikuwa miongoni mwa waliostaafu.
Nafasi yake imechukuliwa na Alexander Mnyeti aliyepandishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara akitokea kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Bill Nas apata dili la Mamilion

MWANAMUZIKI ambaye alitamba kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva na ngoma ya Chafu Pozi, Bill Nas baada ya kula dili la Coce Studio Africa pamoja na kufanya matamasha mbalimbali, hivi karibuni amekula dili lingine la mtandao wa simu, ambalo amesema litampigisha hatua kubwa kwenye muziki wake.
Akichonga na ukurasa huu wa burudani, Bill Nas alisema kwamba, dili hilo ni la mkwanja mrefu na hivi karibuni atalifungukia moja kwa moja pale ambapo tangazo alilofanya litaachiwa na wenye nalo.
“Nimepiga dili ambalo nafikiri kwa mashabiki wangu litakuwa ni habari nzuri, sina uhuru wa kulizungumzia tu kwa sababu bado niliofanya nao hawajaliachia, lakini hivi karibuni wataliachia na nitakuwa wazi kusema ni milioni ngapi nimedaka,” alimaliza Bill Nas.
Pam D afunguka kuhusu Ney Wamitego

MWANADADA ambaye anafanya vizuri kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’, amefunguka juu ya skendo ya kujichimbia na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ hotelini wakiwa kwenye ziara ya kimuziki katika mikoa mbalimbali hivi karibuni na kudai hazina ukweli.

Akichonga na Showbiz-Xtra kuhusiana na ishu hiyo, Pam D alisema mara nyingi wakiwa na Nay, kila mmoja anakuwa analala kwenye chumba chake na kilichokuwa kimewapeleka kwenye mikoa hiyo ni kazi na wala si kitu kingine.
“Hayo maneno si ya kweli kabisa bhana, mimi nilikuwa ninalala kwenye chumba changu na Nay kwenye chumba chake kwa hiyo hakuna ukweli wowote ule, sisi ni washkaji tu sijui kwa nini watu wamejiaminisha kwamba sisi ni wapenzi,” alisema Pam D.
Audio | Baraka the Prince – Nipe Nguvu | Mp3 Download
Audio | Baraka the Prince – Nipe Nguvu | Mp3 Download

Audio | Baraka the Prince – Nipe Nguvu | Mp3 Download
DOWNLOAD NOW

Audio | Baraka the Prince – Nipe Nguvu | Mp3 Download
DOWNLOAD NOW
Subscribe to:
Comments (Atom)
 
 
