Wednesday, 6 December 2017

Mfanyabiashara aliyekamatwa Z’bar bado yupo chini ya ulinzi



Imeelezwa kuwa mfanyabiashara aliyekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na vito vya dhahabu na mamilioni ya fedha ya nchi 15 ataendelea kuwa chini ya ulinzi hadi uchunguzi dhidi yake utakapomilika.

Naibu Mkurungezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Ramadhani Ng’anzi alisema juhudi za ukamilisha uchunguzi dhidi ya tukio hilo zinaendelea.

“Hatuwezi kusema wapi tumefikia hadi pale tutakapokamilisha kazi yetu ya uchunguzi, ila tunaendelea kumshikilikia kwa mujibu wa taratibu zetu,” alisema Ng’anzi.

Kaimu Kamishna wa Polisi Zanzibar, Juma Yussuf Ali alisema mfanyabiashara huyo alikamatwa baada ya kutiliwa shaka wakati akitaka kusafiri nje ya nchi.

Ali alisema kwa mujibu wa taratibu za kipolisi na kiusalama ililazimika kumzuia mfanyabiashara huyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa mali alizotaka kuondoka nazo nje ya nchi.

Msemaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, Makame Abdalla alisema kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo uwanjani hapo ni tukio kubwa la kwanza kutokea.

Shamsa Amfungukia Wema


KUFUATIA kuhama chama kutoka Chadema kwenda CCM kwa mwanadada kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Wema Sepetu, msanii mwenzake, Shamsa Ford ameibuka na kumtahadharisha pamoja na wasanii wote kwa jumla.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Shamsa alisema wao siyo wanasiasa hivyo suala la Wema la kwenda na kurudi kwenye vyama vya siasa inawezekana anapata faida lakini cha muhimu asisahau kazi yake.

“Siwezi kuzungumzia sana suala la Wema kuhama vyama maana ni lake binafsi na huenda lina faida kwake, nawasihi tu wenzangu wasisahau kazi yao ya sanaa iliyowatambulisha kwa jamii,” alisema Shamsa.

TCRA kupitia leseni za vituo vya Luninga



Leseni  za vituo  luninga kupitiwa
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema inafanya mapitio ya leseni za vituo vya luninga ili kufanyia utatuzi kasoro zilizojitokeza wakati wa kuhama kutoka mfumo wa analojia kuelekea digitali.

Aidha, imezitaka kampuni zinazorusha matangazo ya luninga kufuata sheria na kanuni za usajili zinazowataka kurusha bure matangazo ya chaneli za ndani.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba, aliyaeleza hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, alipofanya ziara katika ofisi hizo.

Kilaba alisema kuhama kutoka analojia kwenda digitali ilikuwa ni kazi kubwa ambayo lazima ingeleta changamoto ambazo wanaendelea kuzifanyia kazi.

Alisema kampuni hizo zimekuwa zikikata matangazo ya chaneli za ndani pindi muda wa kifurushi alicholipia mteja kumalizika licha ya mkataba walioingia na TCRA kuelekeza kuwa huduma hizo zitatolewa bure kwa wananchi.

Alisema anatambua kuwapo mvutano kati ya kampuni za urushaji matangazo na watoa huduma wa kituo kuwa nani anapaswa kulipia gharama hizo na ni kiasi gani na kwamba wanalitafutia ufumbuzi suala hilo ili wananchi wapate chaneli hizo bure.

Chaneli zinazotakiwa kupatikana bure ni ITV, TBC, Star TV, Chanel Ten, Clouds TV na TV Tumaini.Naye Naibu Waziri huyo, aliwataka TCRA kusimamia kanuni na sheria hizo ili wananchi wapate huduma hizo bila malipo yoyote.

Aidha, Nditiye, aliitaka TCRA kufunga vibanda vyote vya kusajili laini za simu bila kufuata sheria.Alisema kumekuwapo na idadi ya vibanda na watu wakipita mitaani bila kuwa na vitambulisho na kusajili laini bila kuzingatia kanuni na taratibu za usajili hali ambayo inapelekea baadhi yao kuzitumia kufanya uhalifu.

“Tunataka kila mtu anayetumia laini awe anafahamika. Na taratibu zitumike kama ilivyopangwa kuwa vitambulisho vinavyotakiwa kutumika ni vya kupigia kura au cha uraia. Napendekeza ikiwezekana usajili uwe unafanyika kwenye ofisi za watoa huduma badala ya watu kusajili ovyo mitaani,” alisema. 

Wastara ajitosa Bongo Fleva



STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma baada ya kusikika kwa Wimbo wa Wanawake ambao aliuzindua wakati akienda nchini Sweden, sasa amejipanga kutoa wimbo mwingine unaoitwa Mama na Mtoto ambao nao unaihusu jamii kwa ujumla.

Akibonga na Risasi Vibes, Wastara alisema kuwa ameamua kuimba nyimbo zinazoihusu jamii hasa akina mama na watoto.

“Wimbo wangu wa sasa unaelezea zaidi thamani ya mtoto na akina mama jinsi ya kumlinda mtoto, nimeshatoa ‘single’ yake na video ndiyo namalizia kuifanyia shooting hivyo watu wakae mkao wa kula,” alisema Wastara.

MAGAZETI YA LEO 6/12/2017




Kutokwa Na Majimaji Kwenye Matiti (Galactorrhea)



Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba.Kusimama kwake kama ugonjwa ni pale  yanapotoka wakati mwanamke hana historia ya dalili hizo hapo juu.

Tatizo hili huwapata wanawake wengi na kwa mujibu wa takwimu huathiri asilimia tano hadi 32 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa.Pamoja na kuwapata zaidi wanawake, hali ya kutokwa na majimaji katika matiti pia huweza kuwatokea wanaume watu wazima, vijana walio katika umri wa balehe, wa kike na wa kiume, watoto wachanga wa kike na wa kiume.

Chanzo cha tatizo
Matiti yanaweza kutoa majimaji endapo chuchu zitachezewa au kunyonywa mara kwa mara na kusababisha kuvuruga baadhi ya homoni mwilini.

Homoni zinazohusika zaidi na tatizo hili ni homoni ya ‘prolactine’. Vilevile katika hali hii ya kutokwa na majimaji asilimia 50 ya matatizo chanzo chake bado hakijulikani.

Mama anayenyonyesha homoni zinazochangizwa na kusababisha matiti yatoe maziwa ni ‘Prolactin’, Estrogen’ na Progesterone.

Dawa nyingine zinazoweza kumfanya mtu atokwe na majimaji katika matiti ni dawa kama Methyldopa, madawa ya kulevya na dawa za magonjwa ya akili.

Pamoja na matatizo katika mfumo wa homoni, hali ya kusuguasugua kifua mara kwa mara, hali ya kuwa na hofu  na wasiwasi au shauku f’lani, mfano ya kuhitaji kupata ujauzito husababisha kuamsha homoni za uzalishaji wa maziwa au hayo majimaji.

Vyanzo vingine ni matatizo kichwani kwenye tezi ya ‘pituitary au pituitary adenoma’.
Dawa nyingine zinazoamsha tatizo hili ni kama vile ‘Cimetidine’ ambazo hutibu vidonda vya tumbo.
Pia zipo dawa nyingine za asili ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha zinazoweza kusababisha tatizo hili.

Dalili za tatizo
Mwanamke mwenye tatizo hili la kutokwa na maziwa kwenye matiti wakati si mjamzito na wala hana historia ya kuwa na mimba, huwa hapati ujauzito.

Mwanaume mwenye tatizo hili hupungukiwa na nguvu za kiume, uzalishaji wa mbegu za kiume huwa mdogo.

Kwa ujumla tatizo hili husababisha ugumba.
Kwa vijana na watoto wa kiume au wa kike ni vema uchunguzi wa kina ufanyike.
Maziwa yanaweza kutoka tu yenyewe au kwa kuminyaminya matiti au chuchu.

Uchunguzi
Hufanyika hospitalini kwa madaktari wa masuala ya uzazi. Vipimo vya damu kuangalia homoni, matatizo katika matiti, na ikibidi CT-Scan vitafanyika kuangalia matatizo katika tezi ya Pituitary.
Ushauri Wahi hospitali kwani athari ya tatizo hili ni kupoteza uwezo wa kuzaa.

Epuka kuchezea chuchu ziwe zako mwenyewe au za mpenzi wako au za mtoto kwani unaamsha homoni ambazo katika wakati huo hazitakiwi.

Saratani Ya Shingo Ya Kizazi, Inasababishwa Na Ngono Na Mambo Mengine Ya Fahamu Hapa


 
UTAFITI mpya wa kitabibu umebaini kuwa saratani ya shingo ya kizazi, inasababishwa pamoja na mambo mengine na ngono kama ilivyo kwa ugonjwa wa Ukimwi, madaktari bingwa wa magonjwa ya maradhi hayo wamesema.


wametaja mambo mengine yanayoweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi kuwa ni kujiingiza kwenye mapenzi katika umri mdogo, kuolewa mara nyingi, kuwa na wapenzi wengi, kusafisha sehemu za siri kwa bidhaa zenye kemikali na kuzaa mara nyingi.




Katika kiwango cha kimataifa, wastani wa mwanamke kuzaa bila kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa saratani, ni watoto wanne.

Madaktari hao walisema saratani ya shingo ya kizazi inatokana na aina 40 ya virusi, aina mbili ikiwa ni virusi vinavyosambaa kwa njia ya ngono  “Human papilloma virus (HPV) Squamos cell carcinoma kirusi namba 16 na Adenocarcinoma namba 18, ni kati ya virusi 40 vinavyosababisha saratani ya kizazi na vyenyewe vinachangia tatizo hilo kwa asilimia 70.” Wanasema saratani ya uzazi ndiyo inayoongoza ikilinganishwa na nyingine nchini na asilimia 80 ya wagonjwa, wameambukizwa kwa ngono. “Saratani hiyo husambaa kwa ngono kutoka mwanamke mmoja kwenda kwa mwingine.

Mwanamke mwenye saratani ya kizazi akifanya ngono, mwanamume huchukua virusi na kumwambukiza mwingine atakayefanya naye ngono,” alisema na kuongeza:

“Wagonjwa wengi na wale ambao tayari wana maambukizi, wamekuwa wakikutwa na virusi hawa wa aina mbili ambao wamekuwa wakienezwa zaidi kwa njia ya zinaa. Inawezekana mwanamume akawa ametoa kirusi kwa mwanamke mmoja kwenda kwa mwingine.”

“Hata hivyo, kuna wanaume ambao tayari wameshakuwa na maambukizi ya HPV wanatembea na virusi, hawa tunawaita (high risk sexual male patner) wanaume hawa utakuta kila akioa mke anakufa kwa saratani ya shingo ya uzazi, lakini kamwe virusi hao hawawezi kumwathiri yeye.”

Kuanza ngono mapema nako kunachangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya saratani hiyo, kwani binti anakuwa katika hatari zaidi ya kupata maambukizi mapema na hivyo kuweza kumwathiri mapema zaidi, tofauti na yule aliyeanza baadaye.

“Idadi kubwa ya wanawake wamekutwa na saratani mapema sana, ukilinganisha na umri wao, lakini wengi wao wamekuwa wakikutwa na ugonjwa huu kuanzia umri wa miaka 35 kwenda juu. Hii inamaanisha kuwa walipata maambukizi hayo walipokuwa na miaka 20-25.”

Licha ya hivyo mgonjwa anaweza asitambue tatizo hilo mpaka miaka 10 hadi 15 baadaye ambapo
tatizo linajitokeza hadharani. “Unapopata maambukizi ya HPV inakuchukua muda mpaka kujulikana, kwa kawaida mwanamke anaishi miaka 10 hadi 15 na baadaye anagundulika na tatizo hili, lakini itategemea na kushuka kwa kinga zake.

Kama ikitokea hapo katikati ukajitokeza ugonjwa mwingine kama HIV basi saratani nayo itajitokeza.” Utafiti walioufanywa Septemba 2011 kuhusu tatizo la HIV na saratani ya shingo ya uzazi unaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanawake waliokuwa na maambukizi ya HIV na CD4 ziliposhuka tu, saratani ya kizazi nayo iliibuka, hiyo inamaanisha kuwa tatizo hilo ni kubwa tofauti na linavyodhaniwa. Kwa upande wake virusi vya HPV huambukizwa kwa mwanamke moja hadi mwingine, pale mwanamume anapofanya tendo hilo na mwanamke mwenye maambukizi na kwenda kufanya tendo hilo na mwanamke mwingine. Kinga Madaktari hao wameeleza kinga ya maradhi hayo kuwa ni pamoja na matumizi ya kondomu na uaminifu wa wapenzi katika uhusiano wao.

Ninatoa wito kwa Watanzania na jamii kiujumla kujijengea tabia ya kupima mara kwa mara ili kubaini maambukizi mapema. Ongezeko la watu wanaougua saratani ya shingo ya uzazi imetokana na ongezeko kubwa la watu, ikiwa ni pamoja na tabia ya kuchangia ngono kwa wapenzi.

Alisema chanjo ya saratani ya shingo ya uzazi inayotarajiwa kuanza kutolewa kwa mabinti wa miaka tisa mpaka 12 baadaye, Ni moja ya juhudi ya Serikali katika kupambana na ugonjwa huo.

Kula Blueberry Kunaongeza Uwezo Wa Ubongo



Utafiti mpya umegundua kuwa, kunywa vikombe viwili na nusu vya juisi ya blueberry kwa siku ( mie naziita kunazi za bluu) kunaongeza uwezo wa ubongo wa kufahamu, na kuondoa matatizo ya usahaulifu yanayotokana na utu uzima. Wataalamu wanasema kuwa

kunywa kila siku juisi hiyo kunamzuia mtu uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa kupoteza akili uzeeni au wendawazimu. Blueberry kwa kuwa na kiwango kikubwa cha phytochemical, tunda hilo lina limejaa anti oksidanti na lina uwezo wa kuzuia uvimbe. Vilevile kunazi za

bluu kwa kuwa na mada iitwayo Anthocyanin, huweza kusaidia kuongeza kumbukumbu katika ubongo. Pia tunda hilo husaidia kupunguza kasi ya kitendo cha kupungua kumbukumbu katika ubongo kwa kuondoa gulukosi zinazopatikana kwenye ubongo.

Uchunguzi huo umebaini kwamba, kula blueberry kupitia vidonge maalum vya kusaidia afya au supplements kunaweza kumpatia mtu faida kubwa katika ubongo. Hata hivyo wataalamu hao wameshauri kuwa ni bora tunda hilo liliwe katika hali ya kawaida.

Huko nyuma pia wataaamu walieleza kuwa, Blueberry husaidia kupunguza usongo wa mawazo pamoja na kiwango cha juu cha gulukosi katika damu.
Haya tena wadau…usichelewa kula tunda hili, najua katika nchi zetu za Afrika tunda hili

halipatikana na ndio sababu hata jina lake katika kamusi yetu haliko, lakini usife moyo unaweza kupata tunda hilo madukani na katika supermarkets ambapo huhifadhiwa katika makopo au kama juisi. Kwa wale walioko ughaibuni basi hakuna tabu hiyo na usikose kula tunda hilo tamu wakati wa msimu wake na wakati miwngine wowote.
Daima tuzilinde afya zetu!

Samsung yafanya majaribio ya teknolojia ya 5G



Katika intaneti yenye kasi hivi sasa katika nchi zetu za Afrika ni teknolojia ya 4G na hiki ndio kizazi kinachoonekana kuwa chenye kasi ya intaneti lakini hali ni tofauti kwa Samsung ambao wanafikiria kuhusu kizazi cha 5 cha intaneti.

Tangu mwaka 2015 Samsung imeunganisha nguvu na kampuni nyingine ya mawasiliano ya Japani inayofahamika kama KDDI katika kufanikisha teknolojia ya intaneti ya 5G inatumika kwenye bidhaa/huduma kati ya makampuni hayo mawili.

Samsung kwa kushirikiana na KDDI ilifanya majaribio ya kasi ya intaneti ya 5G kwenye treni ya mwendokasi na kasi ya intaneti hiyo ikiwa ni 1.7Gbps.

Kilichofanyika kwenye majaribio ya intaneti ya 5G.
Kwenye majaribio hayo ambayo yalifanyika kwenye treni iliyokuwa ikisafiri kwa kasi ya zaidi ya Km 100/saa ilihusisha kifaa cha kisasa zaidi cha kuongeza kasi ya intaneti kama ikiwa ndogo (5G router), 5G Virtualised Radio Access Unit (vRAN) na Virtualised core.

Treni hiyo ambayo ilikuwa kwenye kasi huku umbali kati ya vituo viwili ukiwa karibu Km 1.5; ilishuhudiwa katika majaribio hayo video ya kiwango cha 8K kupakuliwa pamoja na video ya kiwango cha 4K iliyokuwa inachukuliwa ndani ya treni kutoka kwenye kamera iliyokuwa eneo la mbele ndani ya treni kuweza kuwekwa (uploaded).

Usalama wa teknolojia hiyo umearifiwa kuwa ni wa kuaminika kwa maana ya uduukuzi (udukuzi wa WI-FI, wizi wa taarifa za abiria, n.k) na kuwa yenye kasi zaidi itakayowafurahisha abiria/watumiaji wa teknolojia hiyo.

Tangu mwaka 2015 Samsung na KDDI wamekuwa wakifanyia majaribio teknojia ya 5G. KDDI wenyewe wanatarajia kuanza kutumia teknolojia ya intaneti ya 5G mwaka 2020.

Matumizi ya teknolojia ya 5G yanatarajia kufungua milango kwa aina mbalimbali za biashara kufikiria kutoa huduma hiyo huku KDDI wakiahidi kuendelea kufanyia majaribio teknolojia hiyo katika sekta mbalimbali.

Tuesday, 5 December 2017

Video | S Kide – Aslay | Mp4 Download

Video | S Kide – Aslay | Mp4 Download
S Kide - Aslay
Video | S Kide – Aslay | Mp4 Download



                              DOWNLOAD NOW

Video | Rudeboy (P – Square) – Fire Fire | Mp4 Download

Video | Rudeboy (P – Square) – Fire Fire | Mp4 Download
Rudeboy (P – Square) – Fire Fire
Video | Rudeboy (P – Square) – Fire Fire | Mp4 Download



                                                  DOWNLOAD NOW

TANGAZA BIASHARA YAKO NA WINOKEMEDIA360




Tangaza Biashara yako nasi ili uweze kufikia malengo uliyo jiwekea katika Biashara yako, WINOKEMEDIA360 inauwezo mkubwa sana wa kuitangaza Biashara yako yoyote ile.

Kama vile
Maduka / Bidhaa
Makampuni na Mashirika
Shule / Vyuo
Viwanja / Mashamba
Nyumba / Apartment
Hotel / Restaurant
Mikutano / Sherehe


Bei zetu ni nafuu sana mawasiliano nasi 0675762540 Au 0688108760 Kwa Namba Ya Whatsapp.

Tanga: Kifaa cha kujifunzia Kingereza chasambazwa


Wadau mbalimbali wa elimu kwa kushirikiana na Serikali wamesambaza vifaa maalum vya kufundishia somo la Kingereza mashuleni ili kusaidia kumaliza changamoto na kuongeza uelewa kwa wanafunzi wa sekondari mkoani tanga.

Kifaa hicho kijulikanacho kwa jina la E.rider kitaanza kutumika rasmi kwa mwaka 2018,huku mtaalamu kutoka shirika la CAMFED ambao ndio wametoa vifaa hivyo anasema kifaa hicho kina uwezo wa kuhifadhi jumla ya vitabu elfu moja na mia nne kwa wakati mmoja.

Kwa upande wa  Mwakilishi wa Afisa Elimu mkoa wa Tanga ametoa wito kwa walimu waliokuwa wakipewa mafunzo ya kutumia kifaa hicho huku kamera ya ITV ikushuhudia mwitiko huo wa waakimu.

 Wadau hao wamefanya  kitendo hicho baada ya kuonekana kuwa lugha ya kingereza imekuwa ni kikwazo kwa wanafunzi wanaofaulu shule za msingi kwenda sekondari hasa mkoani Tanga.