Tuesday, 5 December 2017

Huyu ndiye refa atakayechezesha mechi ya mahasimu wa Manchester Jumapili



REFA Michael Oliver ameteuliwa kuchezesha mchezo wa ujao mahasimu wa Jiji la Manchester.
Uwanja wa Old Trafford unatarajiwa kuhimili vishindo vya mpambano wa mahasimu, Manchester United na Manchester City Jumapili, moja kati ya mechi zinazotarajiwa kuwa na ushindani mkali msimu huu.

Timu hizo mbili kwa sasa zinafuatana juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, huku United wakionekana kama washindani kweli wa City kwenye mbio za ubingwa.

Pointi nane zinazitenganisha kwa sasa timu hizo mbili bvaada ya mechi 15, na City haijaonja ladha ya kipigo msimu wote huu.

Oliver atasaidiwa na washika vibendera Gary Beswick na Simon Bennett, wakati mezani atakuwapo Jon Moss.

Huu si mchezo wa kwanza wa mahasimu hao kwa mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 32, aliyeibukia Ashington, kwani awali alichezesha mechi ya Machi timu hizo zilipokutana.

Oliver ndiye aliyekataa penalti ya Marcus Rashford ambayo mashabiki wa Man United wanaamini ilikuwa ni halali.

Katika mechi zilizotangulia za mahasimu hao, Oliver alimtoa kwa kadi nyekundu beki wa Man United, Chris Smalling timu hizo zilipokutana mwaka 2014.

Mechi ya Jumapili Man United watamkosa kiungo wao, Paul Pogba aliyetolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Arsenal Uwanja wa Emirates baada ya kumchezea vibaya, Hector Bellerin.

United imeamua kutokata rufaa, hivyo itakutana na kikosi cha Pep Guardiola bila mchezaji wake huyo ghali iliyemnunua kwa Pauni milioni 89.

Taasisi ya kupambana na rushwa yabaini ufujaji wa fedha katika mazishi ya Mandela


Leo ni miaka minne imepita tangu kifo cha Hayati Nelson Mandela ambaye alikuwa ni
kiongozi mashuhuri duniani ambaye alifariki tarehe kama ya leo Desemba 5, 2013.

Hata hivyo inadaiwa kuwa mazishi yake yalikumbwa na ufisadi mkubwa ambao unadaiwa kutekelezwa na viongozi wakuu nchini humo.

Mamlaka ya kupambana na rushwa nchini humo imechapisha ripoti yenye kurasa 300, inayoonyesha jinsi gani urasibu mbaya na rushwa viligubika matayarisho ya mazishi ya Nelson Mandela.

Kulingana na ripoti ya Mamlaka ya kupambana na rushwa nchini humo takriban dola millioni 22 ilitumika vibaya wakati wa matayarisho ya mazishi ya Mandela miaka minne ilyopita.

Benki ya Dunia imemhakikishia Rais Magufuli Fedha za Mikopo kwa miradi ya Maendeleo


   Dar es Salaam. Mwakilishi wa Benki ya Dunia (WB) katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa imejipanga kuendelea kutoa mikopo nafuu kwa miradi ya maendeleo hapa nchini ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

Bird alitoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam jana na kubainisha maeneo ya kipaumbele kuwa ni miundombinu hususan barabara na reli, kuongeza uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na elimu kwa kujielekeza katika ubora na kuhakikisha idadi ya wanaoipata inaongezeka. Maeneo mengine ni kuboresha sekta ya afya, upatikanaji wa maji, usimamizi bora wa ardhi, mawasiliano, huduma za fedha jumuishi, vituo vya pamoja vya Serikali na kusaidia familia maskini.

Mwakilishi huyo wa Benki ya Dunia alimpongeza Rais Magufuli kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na benki hiyo.

“Mwaka uliopita Benki ya Dunia imetoa mikopo nafuu yenye thamani ya Dola 1.2 bilioni za Marekani (zaidi ya Sh2.7 trilioni) kwa Tanzania, fedha hizi zimekwenda katika miradi mbalimbali na tunafurahi kuwa miradi hiyo inakwenda vizuri na wananchi wanafurahia,” alisema.

“Kwa sasa tunapanga namna tutakavyotoa mikopo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo katika kipindi kijacho.”

Kwa upande wake, Rais Magufuli aliishukuru benki hiyo kwa ushirikiano wake na Tanzania katika maendeleo na alimhakikishia Bird kuwa Serikali itazisimamia vizuri fedha zote zinazotolewa na benki hiyo ili zilete matokeo yanayotarajiwa.

Rais alisema maeneo ambayo benki hiyo imeyataja kuwa kipaumbele katika fedha zitakazotolewa kuanzia sasa ni muhimu kwa ustawi wa Tanzania.

Alisisitiza kuwa fedha zitakazotolewa kama mkopo zitaelekezwa katika maendeleo na si vinginevyo. “Naishukuru sana Benki ya Dunia kwa kutuunga mkono, nitafurahi kuona mnaendelea kutupatia fedha ambazo zinaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo na kuleta manufaa mapana na endelevu, badala ya kugawa fedha kwa watu na baadaye nchi inakuja kuzilipa kwa kukusanya kodi za wananchi,” alisema.   

Dully Sykes atokwa povu kisa Bombardie



Dully Sykes.

ETI kisa Bombardier! Mkongwe wa Bongo Fleva nchini, Dully Sykse ametoa povu ikiwemo kutangaza vita na wasanii wa kizazi kipya kwa sababu ya kushindwa kumsapoti kwenye wimbo wake mpya.

Dully Sykes ambaye ameachia wimbo mpya wa Bombardier, alisema wasanii wa sasa ambao wengi ni wapya wana roho mbaya na yeye yuko tayari kupambana nao.

“Wasanii wa sasa wana roho mbaya, hawasapotiani kama wasanii wa zamani, ndiyo maana Bombadier yangu hawajanisaidia kuitangaz, hiyo inaonesha muziki ni vita na mimi niko tayari kupambana nao,” alisema Dully.

Godbless Lema, Jerry Muro Wazidisha Utata Safari Ya Mnyika Kuhamia CCM


Licha ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kukaririwa jana kikikanusha fununu zilizozagaa mitandaoni zikielekeza kuwa Mbunge wa Kibamba (Chadema), Mhe. John Mnyika anatazamiwa kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM), bado ishara zimezidi kuonesha kuwa safari ya kinara huyo wa upinzani kuelekea CCM imezidi kuiva.

Tetesi hizo zimegonga vichwa vya mitandao ya kijamii jana jioni  baada ya kada wa CCM, Jerry Muro kutumia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuweka picha ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli na John Mnyika na kuandika maneno kadhaa kama ifuatavyo;

“Wanakuita mvulana, basi nenda kwa Baba ukadeke kidogo kule ulikua unakomazwa tu, #safarimojamatata.”

Wakati wengi wakitafakari maneno ya Jerry Muro, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) naye ametumia mtandao wa kijamii kuandika machache yaliyotafsiriwa kama maneno yanayoongelea sakata la Mnyika kutimkia CCM. 

==>Lema ameandika yafuatayo;






Mwanafunzi Aliyesambaza Picha za Nyufa Hostel za UDSM Atiwa Mbaroni



Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kumbusho Dawson anashikiliwa na polisi akituhumiwa kusambaza picha kuonyesha nyufa kwenye majengo ya hosteli.

Dawson ambaye ni mbunge wa serikali ya wanafunzi (Daruso) alikamatwa jana Jumatatu Desemba 4,2017 mchana.

Makamu wa Rais wa Daruso, Anastazia Anthony amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo jana saa saba mchana.

"Ni kweli Kumbusho alikamatwa jana mchana  na kupelekwa kituo cha polisi cha Chuo Kikuu kwa ajili ya kuhojiwa lakini ilipofika saa tisa alasiri polisi walisema hawana uwezo wa kumuhoji hapa hivyo wakampeleka Oysterbay," amesema Anastazia.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipotafutwa amesema hana taarifa kuhusu tukio hilo. Alisema anasubiri atakapofikishiwa taarifa atazitoa kwa umma.

Bomoabomoa yawaathiri Wafanya Biashara wanafanya shughuli zao chini ya miti



 picha ya mtandao

    Dar es Salaam. Uboreshaji wa miundombinu ya usafiri unazidi mchungu kwa wakazi wa Dodoma, ambako wafanyabiashara wanafanya shughuli zao chini ya miti, na na Dar es Salaam, ambako wanatafakari jinsi ya kuukabili mwezi Januari ulio na mahitaji mengi ya kifedha.

Mjini Dodoma, wafanyabiashara wamebomolewa mabanda yao kupisha ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa, wakati wakazi wa Dar wanatakiwa kupisha upanuzi wa Barabara ya Morogoro.

Ada za watoto kwa ajili ya mwaka 2018, gharama za usafiri, sikukuu na kodi ya pango ndiyo mambo ambayo wakazi hao wa eneo la Ubungo hadi Kimara hawajui watayatekelezaje wakati huu ambao nyumba zao zilizojengwa ndani ya mita 91 kutoka katikati ya barabara, zinatakiwa zibomolewe.

“Hapa nawaza kipato ninachopata, watoto wanatakiwa ada mwezi Januari, wanataka nguo za sikukuu, huko niendako nahitaji kupanga chumba. Kwa hiyo ni majukumu juu ya majukumu,” alisema mkazi wa Kimara Bucha, Anastazia Alfred alipohojiwa na Mwananchi.

Anastazia alisema wapo tayari kuondoka, lakini kinachowaumiza ni hali ngumu waliyonayo hasa kwa kipindi hichi cha mwezi Desemba.

Anastazia, ambaye ni mama wa watoto watatu, alisema watoto wake wanahitaji kulipiwa ada, sare, na nguo za siku kuu lakini hataweza kuyamudu yote kwa kuwa hali ni ngumu.

“Jana tu watoto wameniuliza kuhusu nguo za sikukuu. Nawaonea huruma kwa sababu sikukuu ni siku ya kufurahi lakini mimi nawaza nitakuwa wapi kipindi hicho,” alisema.

“Hapa nawaza tu nipate pesa ya ada ili watoto waende shule mwezi ujao na kama Mungu akijalia nipate hifadhi kwa ndugu ili wakija hapa wabomoe tu. Nipo tayari vitu viharibiwe kwa kuwa sitamuda gharama za kuvihamisha.”

Mkazi mwingine wa Ubungo, Joyce John alisema mwezi huu kuna mambo mengi atashindwa kuyatekeleza kutokana na changamoto ya fedha, akitoa mfano wa gharama za kusafirisha vyombo wakati wa kuhama.

Alisema alikuwa amelenga kutafuta ada kwa ajili ya watoto pamoja na sare za shule, lakini amejikuta akikabiliwa na gharama nyingine ambazo hakuzitarajia.

“Walivyokuja kuweka alama ya ‘X’ nilijua hadi mwezi wa tatu kwa kuwa ni mwezi ambao hauna mambo mengi kwa watoto kama ilivyo mwezi huu wa mwisho wa mwaka,” alisema.

Alisema Serikali ingesogeza mbele ubomoaji ili wakazi waweze kumudu gharama za shule ambazo ndizo zinazowaumiza vichwa wazazi wengi hasa kuanzia kipindi hiki cha Desemba hadi Januari.

Frank Damas, aliyeishi katika eneo hilo kwa miaka sita, alisema anapenda maendeleo lakini haya yana maumivu kwa kile alichodai kuwa baadhi ya wananchi wapo kwenye hali mbaya kifedha.

Alisema kuwa ndani ya hifadhi ya barabara ni kosa, lakini waliuziwa maeneo hayo bila wao kujua kuwa ni hifadhi ya barabara.

“Yani huu ndio mwezi ambao tutaona mengi. Mfano mimi sina watoto, lakini nawaza kwa wale wenye watoto wanaohitaji ada, nguo za sikukuu, bado aende akapange na siku ya kuondoka anahitaji usafiri,” alisema Damas.

Alisema wamepewa notisi muda ambao kila mtu anauona mrefu kutona na matukio mengi kuhitaji pesa.

Dodoma nao walia

Wakati wakazi wa Dar es Salaam wakitafakari hayo, ubomoaji majengo mjini Dodoma unaofanywa na Kampuni ya Miliki ya Mali za Reli (Rahco) wamelazimika kufanya biashara zao chini ya miti na miavuli mikubwa baada ya kukosa maeneo.

Ubomoaji wa maeneo yao ya biashara ulifanyika kwa siku mbili (Jumamosi, Jumapili) na umevikumba vibanda 487 na nyumba 128, kikiwemo kituo cha mafuta, ofisi za mabasi ya Shabiby, ABC na mighahawa mikubwa mitano,

Jana, mawakala wa kampuni za mabasi yanayosafiri kwenda nje ya mkoa walikutwa chini ya miti na wengine katika miamvuli mikubwa wakiwahudumia wateja wao.

Wauzaji wa vyakula nao walionekana wakipika na kuhudumia wateja wao chini ya miti na miavuli.

Jengo kubwa lililojengwa katika viwanja vya mashujaa ambalo hutumika kama jukwaa la viongozi wakati wa shughuli za hadhara, pia limewekewa alama ya kutakiwa kubomolewa.

Katika maeneo ya kituo cha mabasi cha Jamatini ambako kuna wauza mitumba na migahawa mikubwa, wafanyabiashara walikutwa wamejikusanya wakijadiliana ubomoaji na wengine wakibeba vipande vya mbao na mabati vilivyobakia.

Mwenyekiti wa Usafirishaji wa Mkoa wa Dodoma, Laurent Mwashinga alisema hadi sasa hawajapata taarifa yoyote kutoka Manispaa ya Dodoma kuwa wataendeshaje shughuli zao baada ya vibanda vyao kubomolewa.

“Kama unavyotuona inabidi tujibanze katika miti hapa ili tuwahudumie wateja wetu,” alisema.

“Sasa ikija mvua ndio itakuwa shughuli maana hata pakujificha kwa majirani zetu nao wamevunjiwa.”

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa eneo la Jamatini, Neema Ally alisema mgogoro wa kutakiwa kuondoka eneo hilo ulianza Julai mwaka huu na kulikuwa na mabishano kati ya manispaa na Rahco kuhusu nani hasa mmiliki wa eneo na aliyepaswa kulipa kodi.

“Lakini baada ya kutokea kwa mgogoro huo, uongozi wa manispaa ulituhakikishia kuwa eneo hili ni mali yao na kututaka tuendelee kulipa kodi kwao,” alisema.

“Hata hivyo watu waligawanyika wengine walikwenda kuchukua mkataba Rahco ili kuwalipa na wengine walitaka kuendelea na manispaa.”

Hata hivyo, alisema walishindwa kufikia muafaka na hivyo kuacha kulipa kodi hadi Novemba walipokuja kubomolewa na Rahco na kwamba ubomoaji huo umesababishwa na mgogoro.

Lakini ofisa uhusiano wa Rahco, Catherine Moshi alisema ubomoaji haihusiani na mgogoro wa nani alipwe kodi ya pango.

Mazishi ya Mandela yapoteza mamilioni



Miaka minne imepita tangu Nelson Mandela tangu afariki

Mazishi ya aliyekuwa rais wa zamani Afrika kusini ,Nelson Mandela yanadaiwa kukumbwa na ufisadi mkubwa ambao unadaiwa kutekelezwa na viongozi wakuu nchini humo.

Mamlaka ya kupambana na rushwa nchini humo imebaini kuwa takriban dollar millioni 22 ilitumika vibaya wakati wa matayarisho ya mazishi ya Mandela miaka nne ilyopita.

Ripoti hiyo inasema kwamba viongozi hao walivuja pesa na kukiuka taratibu zilizowekwa huku ikisemekana kwamba gharama za bidhaa ziliongezwa maradufu na matumizi mazishi kutajwa kuwa ya juu sana kwa mfano shati za kumbukumbu ya mazishi zilinunuliwa kwa dollar 25 badala ya dollar19 .

Hata hivyo ripoti hiyo imetaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wahalifu waliofanya jambo hilo la kushangaza katika jamii.

Mwandishi wa Mwananchi atoweka



  Dar es Salaam. Mwandishi wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) mkoani Pwani, Azory Gwanda amepotea.

Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa MCL, Francis Nanai ilisema Novemba 30, kampuni ilipokea taarifa za kutoonekana Azory kwa siku tisa.

Kwa mujibu wa mkewe, Anna Pinoni (35), Novemba 21, asubuhi watu wanaokadiriwa kuwa wanne wakiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser nyeupe walifika katikati ya mji wa Kibiti sehemu ambayo Azory hupatikana mara kwa mara na kumchukua.

Katika taarifa hiyo imeelezwa baada ya kumchukua Azory, gari hilo lilielekea shambani kwake saa nne asubuhi na kumkuta mkewe Anna akiwa huko.

Imeelezwa Azory aliyekuwa amekaa kiti cha nyuma alimuita mkewe kutokea upande huo wa gari na kumuuliza alikokuwa ameuweka ufunguo wa nyumba yao.

Taarifa ilisema mkewe alilisogelea gari na kuzungumza naye kutokea dirishani na kumwelekeza alipoficha ufunguo, huku Azory akimwambia amepata safari ya dharura na kama asingerudi siku hiyo Novemba 21, basi angerudi siku inayofuata Novemba 22.

Nanai katika taarifa hiyo, alisema gari hilo liliondoka kwa kurudi kinyumenyume hadi njia panda na kuelekea nyumbani kwa mwandishi huyo.

“Mkewe aliporudi nyumbani aligundua kuna upekuzi ulifanyika kwa sababu alikuta vitu viko shaghalabaghala,” inasema taarifa hiyo.

Tangu siku hiyo, imeelezwa Azory hajaonekana na namba zake tatu za simu za mkononi hazipatikani. Mpaka jana amefikisha siku 14.

Novemba 23, mkewe Anna alitoa taarifa kituo cha polisi Kibiti na kupewa RB namba; Kibiti/RB/1496/2017.

Imeelezwa polisi waliahidi kufanya uchunguzi, lakini mpaka sasa hakuna taarifa zilizotolewa.

Taarifa ilisema kwa mara ya mwisho, Azory aliwasiliana na ofisi za Mwananchi Novemba 20 kwa majukumu ya kikazi.

Nanai alisema MCL inafuatilia suala hilo kwa ukaribu kwa kushirikiana na familia yake na kutoa wito kwa vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa haraka ili kuwezesha kupatikana kwa mwandishi huyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Rufiji, Onesmo Lyanga alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema bado hajapata taarifa za kupotea kwa mwandishi huyo.

“Sina taarifa, ndio kwanza nasikia kutoka kwako kama Gwanda amepotea. Lingekuwa tukio la crime (uhalifu) wasaidizi wangeshaleta taarifa lakini hili la kupotea sijalipaata,” alisema Kamanda Lyanga.

Alisema kama mkewe ameshatoa taarifa polisi amefanya jambo zuri kwa kuwa zitashughulikiwa.   

TANGAZA BIASHARA YAKO NA WINOKEMEDIA360




Tangaza Biashara yako nasi ili uweze kufikia malengo uliyo jiwekea katika Biashara yako, WINOKEMEDIA360 inauwezo mkubwa sana wa kuitangaza Biashara yako yoyote ile.

Kama vile
Maduka / Bidhaa
Makampuni na Mashirika
Shule / Vyuo
Viwanja / Mashamba
Nyumba / Apartment
Hotel / Restaurant
Mikutano / Sherehe


Bei zetu ni nafuu sana mawasiliano nasi 0675762540 Au 0688108760 Kwa Namba Ya Whatsapp.

Madhara ya kujichubua



Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango,

hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao.


 Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata matangazo yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki. Mambo hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge.


Madhara ya kujichubua ni yapi?
Mtu anaeyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito,kutokwa na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro, kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)

Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia ving´arisha ngozi.











Polisi Dodoma kuhusu jamaa aliyetengeneza tukio la kuvamiwa

Polisi Dodoma kuhusu jamaa aliyetengeneza tukio la kuvamiwa


Video | Young Killer Msodoki – Hujanileta | Mp4 Download

Video | Young Killer Msodoki – Hujanileta | Mp4 Download
Young Killer Msodoki – Hujanileta
Video | Young Killer Msodoki – Hujanileta | Mp4 Download




                                                  DOWNLOAD NOW