Thursday, 30 November 2017

Good One yachangia mifuko 200 ya Cement ujenzi ofisi za walimu Dar

Kampuni ya Good One leo wametoa msaada wa mifuko ya cement 200 ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Mkonda za ujenzi wa ofisi na nyumba  za walimu.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja masoko wa kampuni hiyo Thomas Ma amesema kuwa wametoa msaada huo kwa lengo la kufanikisha harakati za mkuu wa mkoa za kutaka walimu wafanye kazi katika mazingira mazuri na yaliyo bora.

Kwa upande wake  makamu mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa ofisi za walimu Dar es salaam ACP Solomon Urio ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa msaada huo.

"Hiki ni kielelezo tosha kwamba mkuu wa Mkoa anafanya kazi nzuri na ipasavyo na ndio maana wananchi wake wanaendelea kumuunga mkono kwa kila hatua, makampuni na watu binafsi wanaendelea kutoa misaada" alisema ACP Solomon.

Kufuatia misaada hiyo ofisi zinaendelea kujengwa sehemu mbalimbali katika wilaya zote tano, hivyo wadau na watu mbalimbali waendelee kuchangia ili kufanikisha ujenzi huo.

Mtanzania Jonesia kuchezesha kombe la Dunia kwa wanawake 2018 nchini Ureno

Mtanzania Jonesia Rukyaa Kabakama ameteuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kuchezesha fainali zijazo za Kombe la Dunia kwa wanawake (Algarve Cup) zitakazofanyika nchini Ureno, mwezi Februari, mwakani.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka TFF, Jonesia, ambaye ni mwanamke, ameteuliwa kupuliza filimbi katika fainali hizo ambazo hukutanisha timu mahiri zilizofanya vema katika michuano ya kila Bara.
Lakini kabla ya kwenda Ureno, Jonesia anatarajiwa kushiriki semina maalumu iliyoandaliwa na FIFA. Semina hiyo itafanyika Doha, Qatar kuanzia Februari 12- 16, mwakani.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limempongeza Mwamuzi Jonesia kwa kuteuliwa na FIFA kuchezesha fainali za Kombe la Dunia na kuhudhuria semina hiyo muhimu kwa maendeleo ya mpira wa miguu.

Waamuzi wengine walioteliwa kutoka Afrika Lidya Abebe wa Ethiopia, Glady Lengwe wa Zambia na Salima Mukansanga wa Rwanda

Audio | Heri Muziki – Watu | Mp3 Download

Audio | Heri Muziki – Watu | Mp3 Download

Audio | Heri Muziki – Watu | Mp3 Download

                                                   DOWNLOAD HERE

SIRIUS EP 01 By DJ arusha 24

SIRIUS EP 01 By DJ arusha 24

BREAKING: Sakata la Mawakala wa CHADEMA, CCM Waliojeruhiwa! Tume Imetoa Tamko

BREAKING: Sakata la Mawakala wa CHADEMA, CCM Waliojeruhiwa! Tume Imetoa Tamko

SANCHOKA

BREAKING NEWS: DKT SHIKA Azungumza na Waandishi wa Habari

BREAKING NEWS: DKT SHIKA Azungumza na Waandishi wa Habari

BREAKING: LHRC wazungumzia ukiukwaji wa haki za binadamu ktk uchaguzi mdogo

BREAKING: LHRC wazungumzia ukiukwaji wa haki za binadamu ktk uchaguzi mdogo

LIVE: Waziri Mwijage anazungumza na waandishi wa habari

LIVE: Waziri Mwijage anazungumza na waandishi wa habari

Wema Sepetu atamani kufa kwa matusi anayotukwana na mashabiki zake

Wema Sepetu atamani kufa kwa matusi anayotukwana na mashabiki zake

Enock Bella WCB awakumzuia Maromboso kufanya shoo na sisi Leaders club

Enock Bella WCB awakumzuia Maromboso kufanya shoo na sisi Leaders club

CLOSE MY EYES 04 CLOSE MY EYES 04- VASCO DJ

CLOSE MY EYES 04 CLOSE MY EYES 04- VASCO DJ

CLOSE MY EYES 03 IMETAFSIRIWA KISWAHILI

CLOSE MY EYES 03 IMETAFSIRIWA KISWAHILI