Tanzania\'s leading online News Edition (The National Newspaper). Get access to the most current and latest authoritative news on local issues, politics, events, celebrations, editorial, columnists, features, people and business.
Wednesday, 22 November 2017
Wizara yataka madai ya wavuvi kuchunguzwa

Mafia. Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Shaibu Anunduma kuunda kamati kuchunguza madai ya wavuvi watatu kupokwa mtumbwi, leseni, simu na kisha kutoswa baharini.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Agosti 2,2017 saa tano asubuhi baada ya kuvua samaki katika Kisiwa cha Mbarakuni kilichopo ndani ya Hifadhi ya Bahari (Marine Park) kinyume cha sheria.
Ulega ameagiza kuundwa kamati baada ya kutokea mvutano kati ya maofisa wa Hifadhi ya Bahari na wananchi wa Kijiji cha Jojo-Mafia wanaojishughulisha na uvuvi wanaolalamika kwamba wananyanyaswa na maofisa hao.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana Jumanne Novemba 21,2017 katika Kijiji cha Jojo, mwenyekiti wa kijiji hicho, Mussa Hassan alisema wavuvi Hamis Athuman, Hamad Faki na Issa Shali walitoswa baharini na waliokolewa na mvuvi wa kijiji kingine saa tisa alasiri ikiwa ni saa nne tangu walipotoswa.
Mwenyekiti huyo amesema wanakijiji wanategemea shughuli za uvuvi katika Kisiwa cha Mbarakuni kuendesha maisha yao lakini wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili.
Kutokana na hali hiyo, Naibu Waziri Ulega amesema ni kosa la jinai kuwatosa baharini wavuvi wanaokiuka sheria za uvuvi.
“Nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria, utaratibu na kanuni. Wavuvi wakikamatwa wanatakiwa kuletwa kwenye kamati ya kijiji na ikishindikana wanapaswa kupelekwa polisi. Mhalifu yeyote anapelekwa polisi,” amesema.
Amesema kamati itakayoundwa kuchunguza tukio hilo inapaswa kuwa huru ili itende haki.
Ulega amesema wanachotaka ni uhusiano mwema kati ya wahifadhi na wananchi na kwamba, maofisa watakaobainika kuwatosa baharini wavuvi hao watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Pia, ameagiza wavuvi kufuata sheria akisema kisiwani hicho na vingine vya Shungimbili na Nyororo vimehifadhiwa kisheria hivyo hawapaswi kufanya shughuli za kibinadamu.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Bahari, Dk Milali Machumu amekanusha wavuvi hao kutoswa baharini.
Amesema kabla ya tukio hilo, wavuvi hao waliwateka maofisa wao na kuwapeleka kijijini.
Waziri ahimiza kilimo cha muhogo

Tanga. Naibu waziri na mkuu wa mkoa katika Serikali ya Awamu ya Nne, Mwantumu Mahiza amejichimbia katika kilimo cha muhogo.
Mahiza aliyekuwa naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi na mkuu wa mikoa ya Tanga, Pwani na Lindi amewahamasisha wananchi kulima zao hilo akisema litawapa utajiri wa haraka.
Kwa sasa Mahiza amejikita kulima muhogo katika Kijiji cha Segera wilayani Handeni mkoani Tanga akisema soko la bidhaa hiyo lipo ndani na nje ya nchi.
Akizungumza wakati wa kongamano la wanawake Mkoa wa Tanga jana Jumanne Novemba 21,2017 amesema wazo la kulima muhogo alilipata akiwa naibu waziri baada ya kuona Rais na waziri mkuu wakijihusisha na kilimo.
“Nilimtembelea Rais kwa wakati ule, Jakaya Kikwete nikakuta muda wake wa mapumziko anautumia shambani na anazalisha mazao mbalimbali, nikaenda kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda pia hali ikawa vivyo hivyo. Nikaona kama Rais na mawaziri wakuu wanalima ni kwa nini mimi nisilime?” amesema Mahiza.
Amesema aliamua kwenda kijijini kwa mumewe kuanzisha kilimo cha mazao mbalimbali na baadaye akajikita kulima muhogo.
“Kwa eka moja kuanzia kuandaa shamba, kupanda na kupalilia unaweza kutumia gharama ya Sh450,000 kama hatua zote unafanyiwa na vibarua. Hadi kukomaa inachukua kati ya miezi minne na tisa kulingana na aina ya mbegu, lakini ukivuna na kuuza unajipatia Sh4 milioni, unataka nini tena?” amehoji Mahiza.
Ametaja aina ya mihogo anayolima na kuuza ndani na nje ya nchi kuwa ni kiroba, mzurikwao, mahiza, kibandamaiti na mpemba ambazo mbali ya kutumika kwa kukaangwa na unga; kuna viwanda vinavyozalisha dawa za binadamu, biskuti, tambi, mikate na vyakula vya mifugo.
Mahiza ameishauri Serikali kuweka programu maalumu ya kuwahamasisha vijana na wanawake kutumia asilimia tano zinazotolewa na halmashauri kupitia makusanyo ya ndani kuzalisha muhogo kwa sababu anafahamu China inahitaji zao hilo kutoka Tanzania na uzalishaji kwa sasa hautoshelezi mahitaji.
Mwenyekiti wa baraza la wanawake Mkoa wa Tanga lililoandaa kongamano hilo, Mariam Shamte ametaka wanawake kwenda shambani kwa Mahiza kujifunza kilimo hicho.
Pia, ameziomba taasisi za fedha kuchangamkia mikopo ya uzalishaji wa muhogo kwa sababu ni zao la muda mfupi.
Nikki wa Pili kujiunga na chama
Msanii Nikki wa Pili ambaye ni miongoni mwa wasanii wasomi nchini, ameitwa kujiunga na chama cha ACT Wazalendo, ili kuongeza nguvu na kukijenga zaidi chama hiko.

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amemuandikia ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter kumuomba kufanya hivyo.
"Njoo ujenge Chama cha kijamaa bana acha mambo yako", ameandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wa Nikki wa pili.
Baada ya tweet ya Zitto Kabwe kumuomba Nikki, Nikki alimjibu kuwa chama cha kijamaa kinajengwa na watu wanyonge, bali yeye kama mtu wa vyombo vya habari sio wa kuaminika kwani hawachelewi kuwauza.
"Chama cha kijamaa hujengwa na vugu vugu la wanyonge wenyewe, ni muwe tu na mkakati wa kuwaunganisha ki ideologia, umoja zao hizo za boda boda, machinga, wakulima, sisi watu wa media hatu kawii kuwauza sokoni kama nyanya", ameandika Nikki wa Pili.
Mpaka sasa haijulikani msanii huyo ni mfuasi wa chama gani kutokana na kuonekana kuwa mwanaharakati wa masuala ya kisiasa na uchumi, na hajawahi kuonekana kwenye jukwaa la chama chochote kufanya kampeni.

Mwakyembe atoa salamu za pole kwa Clouds Media Group

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe atuma salamu za pole kwa kituo cha redio cha Clouds kwa ajali ya moto > Aagiza taasisi zinazohusika kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha tatiz

kauli ya Polepole kuhusu wanaohama chama

Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Humphrey Polepole, amesema chama hicho kwasasa kimeweka misingi ambayo inawabana viongozi wasiotosheka lakini hakina tabia ya kuwasema vibaya wanachama wake wakihama.
Akiongea kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari Ndg. Polepole amesema kuwa Chama chao kinalinda misingi na Itikadi zake ambazo ni kuheshimu utu wa mtu pamoja na kuwatumikia raia hivyo kwa kiongozi ambaye hawezi kufanya hayo lazima atakimbia.
"Mimi kama Katibu wa Itikadi na Uenezi sijawahi kutoa tamko la kumsema vibaya mwanachama anayehama chama chetu kwasababu sio misingi na Itikadi zetu". Pia ameongeza kuwa ni dhambi kubwa kumhukumu mtu anapohama chama kimoja kwenda kingine.
“Hatuna tabia ya kuwasema vibaya wale wanaokihama chama, lakini tumegundua kwamba raia wa kawaida ndio wamekuwa na tabia ya kuwasema kwa sababu wanayaona matendo yao ya kutotosheka”, amesema Polepole.
Aidha Polepole amesisitiza kuwa CCM kwasasa imeweka misingi migumu itakayowabana wasiotosheka na wasio na kiasi ndio maana tumeamua kuweka sheria ya mtu mmoja, cheo kimoja.
Sheria ambayo itawabana wenye kutaka vyeo vingi kwa wakati mmoja.
Ronaldo agoma
Mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amekataa kuzungumza na vyombo vya habari baada ya kufanikiwa kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 6-0 ilioupata timu yake dhidi ya APOEL kwenye Ligi ya Mabingwa.

Ronaldo alipofuatwa na wanahabari baada ya mchezo huo alikataa kuongea hadi pale walipomganda zaidi lakini alisisitiza kuwa hawezi kuongea chochote na hana raha ya kufanya mahojiano na wanahabari.
“Sihitaji kuongea, sihitaji kuhojiwa juu ya lolote, nimechoshwa na nafadhaishwa na namna ambavyo mnabadilisha maneno, leo naweza kuongea jambo moja kisha mkaandika tofauti kabisa na nilichosema”, amesema Ronaldo mbele ya wanahabari waliokuwa wakimzonga kwenye uwanja wa GSP.

Hatua ya Ronaldo kugoma kuongea na wanahabari ni matokeo ya habari zilizoripotiwa hivi karibuni kuwa Ronaldo ana ugomvi na nahdha wake Sergio Ramos baada ya Ronaldo kukaririwa akisema Real Madrid haifanyi vizuri kwenye La Liga kwasababu ina wachezaji wengi ambao si wazoefu baada ya kuwauza Alvaro Morata na James Rodriquez kitu ambacho Ramos alikipinga kwa nguvu.
Baada ya kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 6-0 sasa Ronaldo ameifungia Real Madrid mabao 98 kwenye mechi 96, akimzidi mshindani wake Lionel Messi ambaye ameifungia Barcelona mabao 97 kwenye mechi 119.
Mbowe: Chadema haitetereki kwa kiongozi au mwanachama wake kuondoka
Mbowe: Chadema haitetereki kwa kiongozi au mwanachama wake kuondoka

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema chama hicho hakiwezi kutetereka au kufa kwa kiongozi au mwanachama wake kuondoka.
Amesema kuna mkakati mkubwa unaotumia fedha unaofanywa kuwalaghai viongozi na wanachama wake kukihama chama hicho.
Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa vijana wa chama hicho, Patrobas Katambi kutangaza kujiunga na CCM.
Akizungumza leo Jumatano na Mwananchi, Mbowe ambaye pia ni amesema, "Tuko ‘strong enough’ sio mara ya kwanza watu kuondoka hivyo wanachama wetu wasiogope waendelee kujenga chama na kuendelea na kampeni za udiwani,"
"Huiwezi kututeteresha, kuondoka kwa Katambi si hivi hivi, ushawishi wa fedha umetumika...ingawa ni haki yao ila hao hawaondoki kwa mapenzi yao na hilo halina ubishi,"
"Badala ya nguvu na fedha kuzielekeza kujenga viwanda wao nguvu wamezielekeza kushawishi viongozi wetu, wamewashawishi wengi na Katambi ni miongoni ingawa wengine wamekataa."
Mbowe amesema, "Katambi alikuwa katika majukumu ya chama na aliwaaga wenzake anakwenda kumuguza mama yake mgonjwa hivyo akakatiwa tiketi ya ndege, kumbe alikuwa anakwenda kukamilisha dili ambalo naambiwa limetumia saa 48 kukamilika."
Amesema Chadema ilipofika haiwezi kufa kwani imejijenga na hapo walioondoka lakini mpaka sasa kimeendelea kuwapo.
Mbowe amesema mwitikio wa wananchi katika kampeni za udiwani kwenye kata 43 umeishtua CCM ikiwamo kuhama kwa aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu.

VIWANJA VINAUZWA CHANIKA
VIWANJA VINAUZWA CHANIKA

Viwanja vinauzwa vipo Chanika karubu na Shule ya Didas pia Umeme upo ndani ya Viwanja. kwa mawasiliano zaidi no 0715290325 / 0787290325

Subscribe to:
Comments (Atom)