Sunday, 29 October 2017

Cuba yakanusha kuwashambulia kwa sauti wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani

Cuba yakanusha kuwashambulia kwa sauti wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani


iC uba inasema kuwa hakujakuwa na mashambulizi ya kutumia sauti dhidi ya wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani kwenye mji wake mkuu Havana, ikisema kuwa madai hayo ni kisiasa yenye lengo la kuharibu uhusiCuba inasema kuwa hakujakuwa na mashambulizi ya kutumia sauti dhidi ya wafanyakazi wa ubalozi ano kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Cuba Bruno Rodriguez alipinga madai hayo ya kuwepo mashambulizi ya sauti akiyataja kuwa kuwa uwongo.

Marekani inasema kuwa karibu wafanyakazi wake 20 katika ubalozi wake walikumbwa na matatizo ya kiafya na kuwapunguza wafanyakazi wake kutokana na kisa hicho.

Ripot zinasena kwa hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na mashambulizi ya sauti lakini hata hivo hakuna kile kimethibitishwa.

Marekani haijailaumu Cuba kwa mashambulizi hayo, na serikali ya Cuba imekana mara kwa mara kuwalenga wafanyakazi wa ubalozi. wa Marekania mjini Cuba.

Marekani iliwatimua wanadiplomasia watano wa Cuba, ikisema kuwa Cuba ilishindwa kuwalinda wafanyakazi wake.

Serikali ya Marekani pia ilifuta shughuli za utoaji visa katika ubalozi wake mjini Havanna
Akizungumza mjini Washington wakati wa mkutana na raia wa Cuba wanaoishi nchini Marekani, Bw. Rodriguez alisema kuwa madai hayo yamesababisha kuharibika kwa uhusiano kati ya serikali hizo mbil

Mtibwa Sugar yaweza kurejea Kileleni leo

MTIBWA Sugar inaweza kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo kama itashinda dhidi ya Singida United.

Wakata Miwa hao wa Manungu wanawakaribisha Singida waliopanda Ligi Kuu msimu huu kwenye Uwanja wa Manungu Arena, Morogoro kuanzia Saa 10:00 jioni.

Na baada ya mahasimu wa jadi, Simba na Yanga kumalizana kwa sare ya 1-1 jana Uwanja wa Dar es Salaam na wote kufikisha pointi 18 baada ya mechi nane, wastani wa pointi mbili kwa mcheszo, Mtibwa wanahitaji kushinda kurudi juu.

Kwa sasa, Mtibwa Sugar ya kocha Zuberi Katwila ina pointi 15, baada ya kucheza mechi saba, maana yake ikishinda leo itafikisha pointi 18.

Lakini hilo halitarajiwi kuwa jepesi mbele ya Singida, inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm ambayo ni mshindani kweli.

Kwa ujumla, Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea leo baada ya mechi mbili za Raundi ya nane kuchezwa juzi na jana, nyingie Azam FC wakiifunga Mbeya City 1-0 Ijumaa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mechi nyingine za leo, Maji Maji wanaikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Lipuli FC wanaikaribisha Mbao FC Uwanja wa Samora mjini Iringa, Kagera Sugar wanaikaribish Ndanda FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Njombe Mji FC wanaikaribisha Stand United Uwanja Saba Saba, Njombe na Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine mjini Iringa.

DRC: Watu milioni 3 wamo hatarini ya kufaa nja

Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi ya watu milioni tatu wamo katika hatari ya kufa njaa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kiongozi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia mpango wa chakula Duniani- WFP, ametoa wito wa msaada wa dharura wa kimataifa, ili kumaliza matatizo ya baa la njaa, nchini DR Congo.

David Beasley, ambaye anafanya ziara yake ya kwanza kabisa, katika jimbo linalokumbwa na msukosuko wa mapigano na uasi la Kasai, ameiambia BBC kuwa, zaidi ya watu milioni tatu, wanakabiliwa na baa la njaa.

Anasema kwamba, timu ya wafanyikazi wake, wameshuhudia watoto ambao wanakabiliwa na matatizo ya utapia mlo, huku mamia kwa maelfu yao, wakiwa katika hatari ya kufa, katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo, ikiwa msaada hautawafikia.

Mapigano mabaya yalianza katika jimbo hilo la Kasai mwezi Agosti mwaka 2016, baada ya kiongozi mmoja wa kitamaduni kuuwawa, katika mapigano na wanajeshi wa kulinda amani.

Ghasia mpya imesababisha mauwaji ya watu elfu tatu na kuwafurusha zaidi ya watu milioni moja, wengi wao wakiwa ni watoto kutoka nyumbani kwao.

BBC

Nape Nnauye na Waziri Nchemba walikuwepo jana kushuhudia mechi ya Simba na Yanga

Waziri wa zamani wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakifuatilia mechi ya mahasimu wa jadi, Simba na Yanga.

Jakaya Kikwete amtumia salamu za heri ya kuzaliwa Rais Magufuli

Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amemtumia ujumbe Rais wa sasa wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kuhusu siku yake ya kuzaliwa ambayo ni leo Oktoba 29.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Jakaya Kikwete ameandika ujumbe huo wa kumtakia heri, huku akizidi kumuombea kwa Mungu, ampatie afya na siha njema.

"Nakutakia kila la kheri Mhe Rais Magufuli unaposherehekea siku yako ya kuzaliwa. Nakutakia afya na siha njema na umri mrefu zaidi", ameandika Jakaya Kikwete.

Leo Oktoba 29, Rais Magufuli anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo anatimiza miaka 57, tangu alipozaliwa mwaka 1959 huko wilayani Chato mkoani Geita

Saturday, 28 October 2017

MAGAZETI YA LEO 28/10/2017

MAGAZETI YA LEO 28/10/2017
























Mkuu wa Wilaya apiga marufuku kuajiri mlinzi asiyepata mafunzo ya mgamb

Mkuu wa Wilaya apiga marufuku kuajiri mlinzi asiyepata mafunzo ya mgambo

Mbulu. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Chelestino Mofuga amepiga marufuku raia wa kawaida kuajiriwa kwa kazi ya ulinzi bali shughuli hiyo wapatiwe askari wa jeshi la akiba la mgambo.

Pia, vijana wote wanaohitaji kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ni lazima wapite kwenye mafunzo ya mgambo.

Mofuga aliyasema hayo juzi kwenye uzinduzi wa mafunzo ya mgambo kwa wanafunzi 171.

Alisema atawachukulia hatua watakaoajiri raia wa kawaida kulinda ofisi, maeneo ya biashara, taasisi binafsi na za Serikali badala ya kuwatumia askari mgambo.

Mofuga alisema vijana wote wa Mbulu watakaotaka kujiunga na JKT ni lazima wapitie mafunzo ya mgambo ndipo waombe nafasi hiyo.

“Pamoja na hayo nawapongeza wananchi wa Mbulu kwa kuitikia wito wa vijana kujiunga kwa wingi kwenye mafunzo ya mgambo kwa ajili ya faida yenu,” alisema Mofuga.

Alifafanua kuwa kupitia mafunzo hayo, vijana wengi watanufaika nayo na wataweza kupata ajira mbalimbali tofauti na kabla ya kushiriki mafunzo hayo.

“Pia nachukua nafasi hii kwa kuwahamasisha wananchi wa Mbulu kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha kupata vitambulisho vya Taifa,” alisema Mofuga.

Mmoja ya washiriki 171 wa mafunzo hayo, John Amnaay alimshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa kukataza ajira za ulinzi kutolewa kwa raia wa kawaida.

“Tuna ari ya kushiriki mafunzo ya jeshi la mgambo na tunatoa ahadi ya kuzingatia masomo tutakayopatiwa na walimu wetu,” alisema.

Wafugaji na Wakulima watupiana maneno

Wafugaji na Wakulima watupiana maneno

Tanga. Wafugaji na wakulima wa Kijiji cha Perani wilayani Mkinga wametupiana maneno mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega huku kila mmoja akimtuhumu mwenzake kuwa kinara wa kuvamia eneo kwa shughuli mbalimbali.

Tukio hilo lilitokea jana wakati Ulega alipotembelea kijiji hicho kwa lengo la kukutana na wakazi wa eneo hilo wakiwamo wakulima na wafugaji kwa ajili ya kuzungumza changamoto zinazowakabili.

Wakulima walimweleza Ulega kuwa wamekuwa wakitumia muda mwingi kulinda mashamba yao kutokana na uwapo wa kundi kubwa la ng’ombe wanaopelekwa na wafugaji.

“Mheshimiwa waziri huwezi kufanya chochote kama umepanda mazao shambani kwa jinsi ng’ombe wanavyoshambulia shamba lako. Ni vigumu shamba kufuata ng’ombe sasa nawashangaa wenzetu wanavyosema tunawavamia,” alisema Said Kokoi.

Alisema hali inakuwa ngumu inapotokea mkulima anajaribu kuwaondoa ng’ombe hao shambani kwake kwa kuwa kundi la wafugaji wa jamii ya wamasai linamfuata na kuanza kumshambulia kwa silaha.

“Jambo hili linatuuma mheshimiwa kwa sababu watu wanapotea katika mazingira ya kutatanisha na siku ya kuonekana wanakuwa maiti,” alisema Kokoi.

Hata hivyo, mfugaji Moi Sangaine alimweleza Ulega kuwa wakulima wamekuwa wakorofi kwa kuziba njia ambayo mifugo yao inatakiwa ikanywe maji.

“Wakulima wanaziba njia za mifugo yetu kwenda kunywa maji kutokana na kilimo chao. Ukithubutu kupitisha mifugo ni mgogoro kwa sababu unaharibu mazao yao,” alisema Sangaine.

Hata hivyo, mwenyekiti wa kijiji hicho, Letinga Oyaya alisema eneo hilo lina mpango wa matumizi bora ya ardhi lakini anashangaa ni kwa nini mamlaka husika zinashindwa kusimamia jambo hilo na hivyo kusababisha mgogoro.

“Endapo mpango huu ungekuwa unatekelezwa kikamilifu hatuwezi kufikia hatua hii ya mapigano na kusababisha watu kuishi kwa hofu. Nimeliwasilisha jambo hili mara nyingi katika wilaya lakini hakuna utekelezaji,” alisema Oyaya.

Kutokana na malalamiko hayo, Ulega aliwasihi wafugaji na wakulima kuacha mapigano.

Ulega alisema huu ni wakati wa kuishi kwa amani na utulivu kwa kuwa suala hilo litafikishwa kwenye mamlaka husika kwa ajili ya utatuzi.

Pia, aliwatoa hofu wafugaji kuhusu mchakato wa upigaji chapa wa ng’ombe na kusema Serikali haina nia ya kuchukua mifugo bali utaratibu huo umelenga kutambua mifugo yote nchini.

Watupwa jela miaka 20 kwa kukutwa na meno ya Tembo

Watupwa jela miaka 20 kwa kukutwa na meno ya Tembo

MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma, imewahukumu wakazi wawili wa Dodoma kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali.

Waliohukumiwa ni Jumanne Mlaga na Alfred Nyagawa ambao walikutwa na bunduki moja na meno mawili ya tembo na mifuko yake
kinyume cha sheria ya wanyamapori.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha, alisema imewatia hatiani kutokana na kosa hilo ambalo walilifanya Aprili, 2016.

Alisema katika kesi hiyo upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi sita na vielelezo tisa ambavyo vimewatia hatiani washtakiwa hao.

Pia alisema washtakiwa kutokana na kutiwa hatiani, wamehukumiwa kwenda kutumikia adhabu hiyo na kwamba kama hawajaridhika, wana haki ya kukata rufani.

Alipongeza jitihada za mawakili kusimamia masuala ya ujangili jambo ambalo linachangia kupunguza wahalifu kwa upande wa maliasili na hifadhi zake.

Hakimu alisema mahakama imetoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanajihusisha na
biashara hiyo haramu.

Alisema pamoja na adhabu hiyo, pia mahakama imetaifisha bunduki moja na meno ya tembo waliyokutwa nayo.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, wakili wa washtakiwa hao, Magiri Mbasha, aliiomba mahakama iwapunguzie adhabu kwa sababu washtakiwa wana wazazi wanaowategemea.

Hata hivyo, Hakimu Karayemaha alisema hakuna sababu ya kuwapunguzia adhabu kwa sababu kila Mtanzania ana wazazi na familia ambazo zinawategemea, hivyo adhabu hiyo ni stahiki kwao kwa sababu wamelisababishia taifa hasara kubwa kwa kuwa tembo wengi wanapotea.

Kwa pande wake, Wakili wa Serikali, Salim Msemo, alidai vitendo vya ujangili vimesababisha tembo kupungua kwenye hifadhi mbalimbali kutoka asilimia 60 hadi 40.

Alidai kuwa adhabu hiyo inawastahili na mahakama itoe adhabu ambayo itakuwa fundisho kwa sababu wamekuwa wakitumia wanyamapori kujinufaisha na familia zao badala ya serikali kunafaika.

Taarifa ya watoto 9 kufariki kutokana na kukatika kwa umeme yakanushwa

Taarifa ya watoto 9 kufariki kutokana na kukatika kwa umeme yakanushwa

Mganga Mkuu Mkoa wa Arusha Dkt. Wonanji Timoth amekanusha taarifa za kufariki kwa watoto 9 waliokuwa kwenye Incubator kutokana na katizo la umeme hapo jana hospitali ya Mt. Meru, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote.

Dkt. Timoth amesema kwamba watoto waliofariki walikuwa wanne na sio 9 kama inavyoelezwa kwenye taarifa iliyosambaa mitandaoni, na wamefariki kwa matatizo mengine lakini sio kukatika kwa umeme.

Dkt. Timoth ameendelea kwa kueleza kwamba moja ya sababu iliyofanya watoto hao kufariki ni mama kuchelewa kufika hospitali kujifungua kwa kuwa alijifungulia nyumbani, pamoja na hatari kubwa wanazopata watoto njiti.

Ray: Okwi hawezi kuifunga Yanga

Ray: Okwi hawezi kuifunga Yanga

Vincent Kigosi ‘Ray’.

MSANII wa Bongo Movie’s, Vincent Kigosi ‘Ray’ amewaambia mashabiki wenzake wa Yanga kuwa, wasihofi  mabao ya Emmanuel Okwi wa Simba, kwani huwa anazifunga timu ndogo tu.

Yanga leo Jumamosi inacheza na Simba kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam mechi ya Ligi Kuu Bara raundi ya nane.

Mpaka sasa Okwi ndiye kinara wa mabao akiwa nayo nane.

Ray alisema: “Yanga ipo vizuri kila idara hivyo na ninaamini haitatuangusha kwenye mchezo huu ingawa wapinzani wanapiga kelele za Okwi, watambue kuwa huyo haiwezi Yanga.

“Okwi anaonekana katika mechi ndogo lakini katika mechi kubwa anafunikwa hivyo wasitegemee jipya kutoka kwake.”

TANGAZO: TUNZA GARI YAKO NA KICHOCHEO CHA NANO ( NANO ENERGIZER

TANGAZO: TUNZA GARI YAKO NA KICHOCHEO CHA NANO ( NANO ENERGIZER )

 Tunakitambulisha kichocheo madhubuti cha Nano  kilichothibitishwa ubora wake na shirika la
viwango la kimataifa (ISO 9001:2015). Hii ni teknolojia ya kipekee na ya kimapinduzi kwenye tasnia ya magari na mitambo. kichocheo cha Nano kimetengenezwa na teknolojia ya kisasa duniani ya Nano (Nano technology) kwa ajili ya kuikarabati na kuipa ulinzi injini ya gari yako bila kuifungua. Kichocheo cha Nano huziba mikwaruzo yote ndani ya injini na kuirudisha nguvu ya injini kama ilivyokuwa mpya. Wasiliana nasi kupitia Namba 0715480174.
 Kichocheo cha Nano kinaipa injini ganda au tabaka gumu la ceramic na platinum. Tabaka hili linafanya muunganiko wa kudumu na chuma cha injini (cylinder wall) na kina uwezo madhubuti wa kuhimili uchakavu na michubuko itokanayo na msuguano. Inarudisha uwezo wa kusukuma wa injini (compression ratio) kwa kuweka ganda gumu kwenye ukuta wa cylinder.

FAIDA ZA KICHOCHEO CHA NANO.


  • Hupunguza matumizi ya mafuta kwa 8% - 21%.



  • Huongeza nguvu ya injini hadi kufikia 100%.



  • Hupunguza mlio na makelele ya injini na mtetemo hadi Mara 5 zaidi.



  • Inatoa ulinzi wa injini hadi kufikia 40000 km.



  • Husaidia Kuboresha uhai wa injini na vifaa vingine.



  • Hulinda injini na kuirudisha kwenye ubora wake kama ilivyokuwa mpya.



  • Huongeza msukumo wa injini na kuboresha uunguaji wa mafuta.



  • Hulainisha usukani na gear box.



  • Hupatikana kwa magari ya aina zote, generator, compressor, pikipiki, bajaji na kila aina ya mtambo.



  • Hupunguza utoaji wa moshi kati ya mara 3 hadi 9.



  • Ina garantii ya utendaji kazi kwa 100%.



  • Haiharibiki kwa nanma yoyote ile.



  • Bidhaa bora kabisa iliyothibitishwa kimataifa na kitaifa.



  • Inakupa faida ya kutoifungua injini hivyo kuongeza thamani ya gari hata ukitaka kuiuza.



  • Inakupa faida ya kupata mafuta bure kila unapoweka kwa mara ya 9.


Faida isiyolinganishwa ya ulinzi wa gari lako hadi kufikia km 40000 kwa sh 60000 tu ukilinganisha na gharama za  mafuta na services kwa kipindi hicho.


MATUMIZI


  • Injini inatakiwa iwe imetumika kwa km 3000.



  • Kichocheo cha Nano kinatumika kwa injini za aina yoyote inayotumia oili ya aina yoyote (mineral or synthetic oils).



  • Ili kupata matokeo bora zaidi weka unapofanya service.



  • Ipashe injini yako.



  • Tikisa kichocheo cha Nano kabla ya kuweka kwenye injini.



  • Fungua kifuniko cha injini oili halafu mimina kichocheo cha Nano.



  • Funga kifuniko. Hongera, umefanikiwa.



  • Baada ya kumimina kichocheo cha Nano usibadili oili ya injini mpaka kipindi cha matumizi 

yafuatayo (kilomita 400 kwa pikipiki na bajaji, kilomita 1200 - 1500 kwa magari madogo na kilomita 3000 kwa malori na mabasi).


MAPENDEKEZO.
Kichocheo cha Nano kimefanyiwa majaribio na kukubaliwa na taasisi zifuatazo.

Chuo kikuu cha Taifa cha Kyungpook - Korea.

Chuo Kikuu cha Taifa cha Seoul - Korea.

Taasisi ya Korea ya Mashine na Vifaa.

Chuo Kikuu cha Yeungnam - Korea.

Taasisi ya Korea ya Teknolojia ya magari.

Kituo cha Jeshi la Anga la India.


UTHIBITISHO WA UBORA.

Kichocheo cha Nano kimefanyiwa majaribio maabara, kuthibitishwa, kukubalika na kutunukiwa vyeti vya ubora na taasisi zifuatazo.


Shirika la Ubora la Kimataifa ISO 9001:2015.

Shirika la viwango la Tanzania - TBS.

Mkemia mkuu wa serikali ya Tanzania - GCLA.
Maabara ya kimataifa ya SGS.

Maabara ya kimataifa ya TUV SUD Industrie Service GmbH.


USHUHUDA / MAPENDEKEZO.

Kichocheo cha Nano kimefanyiwa majaribio na makampuni ya kutengeneza magari, kimethibitishwa na kupendekezwa kutumika na makampuni yafuatayo.

MERCEDES BENZ

TOYOTA

GM DAEWOO

VOLVO

HONDA

HYUNDAI

AUDI

kichocheo cha Nano sasa kinapatikana Tanzania na kusambazwa na POWER ENERGY ENGINEERING COMPANY LTD. Tunakaribisha mawakala kutoka wilaya zote za Tanzania. Wasiliana nasi kupitia Namba 0715480174.

Kwa wafanyabiashara: usiikose fursa hii ya kibiashara.

Kwa wamiliki wa vyombo vya moto (Magari, pikipiki, bajaji nk): Tumia Kichocheo cha Nano kwa ulinzi madhubuti wa chombo chako.


ANGALIA VIDEO HII UONE JINSI NANO INAVYOFANYA KAZI..

Wabunge wa namna hii CCM kushughulikiwa

Wabunge wa namna hii CCM kushughulikiwa

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa tayari toka mwaka jana kimeanza mchakato ndani ya chama hicho kuhakikisha kinawashughulikia wabunge na viongozi mbalimbali ndani ya chama na serikali ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa kashfa mbalimbali.

Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi (CCM) Humphrey PolePole amesema kuwa mchakato wa kuwashughulikia viongozi mbalimbali ambao wanatuhuma mbalimbali umeanza na kusema wao watatenda haki kwa kuwapa nafasi ya kujieleza juu ya shtuma hizo au kashfa hizo na baadaye uongozi wa chama utafanya maamuzi juu ya watu hao.

"Serikali hii imejikita kutetea na kusimamia haki na kuhakikisha uadilifu unasimamiwa na hakika haki itasimamiwa na mchakato mzuri wetu wa chama kuhakikisha kwamba mtu ameulizwa, amepewa tuhuma zake na amejitetea lakini sisi tunafanya uamuzi na tumeshakwisha anza kufanya uamuzi toka mwaka jana na mwaka huu katika vikao vinavyokuja na hakika Watanzania wawe na masikio tayari kuweza kujua na tutaendelea kudhihirishia Umma kuwa tunamaanisha kwenye mambo ya maadili" alisema Polepole

Rais Magufuli aliwahi kumuomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwa Bungeni wanaweza kuwa utaratibu wao kuwaandikia viongozi wa vyama vya siasa juu ya wabunge mbalimbali ambao wanakuwa wakitajwa tajwa kuhusika kwenye kashfa mbalimbali ili vyama hivyo viweze kufanya maamuzi ya kuwaondoa wabunge hao au viongozi hao katika nyadhifa zao na kuwazuia kugombea tena. ;;