Saturday, 28 October 2017

Wabunge wa namna hii CCM kushughulikiwa

Wabunge wa namna hii CCM kushughulikiwa

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa tayari toka mwaka jana kimeanza mchakato ndani ya chama hicho kuhakikisha kinawashughulikia wabunge na viongozi mbalimbali ndani ya chama na serikali ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa kashfa mbalimbali.

Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi (CCM) Humphrey PolePole amesema kuwa mchakato wa kuwashughulikia viongozi mbalimbali ambao wanatuhuma mbalimbali umeanza na kusema wao watatenda haki kwa kuwapa nafasi ya kujieleza juu ya shtuma hizo au kashfa hizo na baadaye uongozi wa chama utafanya maamuzi juu ya watu hao.

"Serikali hii imejikita kutetea na kusimamia haki na kuhakikisha uadilifu unasimamiwa na hakika haki itasimamiwa na mchakato mzuri wetu wa chama kuhakikisha kwamba mtu ameulizwa, amepewa tuhuma zake na amejitetea lakini sisi tunafanya uamuzi na tumeshakwisha anza kufanya uamuzi toka mwaka jana na mwaka huu katika vikao vinavyokuja na hakika Watanzania wawe na masikio tayari kuweza kujua na tutaendelea kudhihirishia Umma kuwa tunamaanisha kwenye mambo ya maadili" alisema Polepole

Rais Magufuli aliwahi kumuomba Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwa Bungeni wanaweza kuwa utaratibu wao kuwaandikia viongozi wa vyama vya siasa juu ya wabunge mbalimbali ambao wanakuwa wakitajwa tajwa kuhusika kwenye kashfa mbalimbali ili vyama hivyo viweze kufanya maamuzi ya kuwaondoa wabunge hao au viongozi hao katika nyadhifa zao na kuwazuia kugombea tena. ;;

No comments:

Post a Comment