Saturday, 28 October 2017

Kampuni zashindania kukuza bangi Denmark

Kampuni zashindania kukuza bangi Denmark


Kampuni nchini Denmark zimeanza kuwasilisha maombi kwa serikali kupata idhini ya kukuza bangi kujiandaa kwa wakati ambao bangi itakuwa halali nchini humo mwaka ujao.

Kampuni 13 tayari zimewasilisha maombi kwa idara ya serikali inayohusika ya Laegemiddelstyrelsen.

Bangi itakuwa halali kutumiwa kama dawa na watu wanaotatizwa na magonjwa yenye uchungu mwingi kama vile saratani na kuganda kwa misuli.

Kuanzia Januari 2018, bangi itakuwa inatolewa kama dawa kwa wagonjwa kwa majaribio ya kipindi cha miaka minne.

Gazeti la Copenhagen Post linasema kuanzia wakati huo, wagonjwa wanaweza kupendekezewa bangi kama dawa na daktari nchini humo.

Lakini bunge bado linajadiliana kuhusu mfumo utakaotumiwa.

Hilo limezifanya kampuni kubwa za kilimo cha mboga na matunda nchini humo kama vile Dansk Gartneri ya Jorgen K. Andersen kutowasilisha maombi kwa sasa.

Bw Andersen ameambia tovuti ya fyens.dk kwamba kampuni yake inatazamia kwamba kutakuwa na mkanganyiko mkubwa katika kutolewa kwa idhini ya kukuza bangi.

Baadhi ya kampuni hata hivyo zinakusudia kukuza sekta ya bangi Denmark na kuuza dawa hiyo maeneo mengine ya nje ambapo bangi ni halali.

Lars Tomassen, mkurugenzi wa Danish Cannabis anasema kwa sasa inaweza kugharimu krone 6,000 ($935; £715) kila mwezi kumtibu mgonjwa wa kawaida kwa kutumia bangi kama dawa

Profesa Jay afungukia ukimya wake

Profesa Jay afungukia ukimya wake

BAADA ya mashabiki wake wengi kutaka kujua kwa nini yupo kimya kwenye anga la muziki, mkongwe Bongo Fleva ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Morogoro, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ameibuka na kuwaeleza kinachomsibu.

Akipiga stori na baada ya kuulizwa sababu za kuwa kimya, Profesa Jay alisema bado anaweka mambo ya kifamilia sawa na yakishakuwa vizuri ndipo atakaporejea tena.

“Kuna mambo mengi ya kifamilia yananiweka bize, najitahidi kuyaweka sawa yakikamilika mashabiki wangu watarajie muziki mzuri kutoka kwangu. Niwaombe tu wawe na subira kwani mambo mazuri hayataki haraka,” alisema Profesa Jay.

Ruby: Siwezi kupotea kwenye mziki kisa kuzaa

Ruby: Siwezi kupotea kwenye mziki kisa kuzaa

MWANADADA kutoka kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ amefunguka kuwa hawezi kupotea kimuziki kisa kuzaa.

Ruby aliiambia Mikito Nusunusu kuwa, anatamani sana kuitwa mama na haofii kuwa atapotea kimuziki kama inavyotokea kwa wasanii wengine kwa sababu amejipanga kikamilifu.

“Natamani sana kuitwa mama kwa kweli na ikitokea muda wowote nitamshukuru Mungu na nitazaa maana sina kipingamizi, siwezi kupotea kimuziki maana mtoto ni moja ya baraka pia,” alisema Ruby.

Mambo 10 yatakayojitokeza leo katika mechi ya Yanga vs Simba

Mambo 10 yatakayojitokeza leo katika mechi ya Yanga vs Simba

YANGA na Simba zinakutana leo Jumamosi kila moja ikiwa imepania kushinda mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Pamoja na yote, watani wanapokutana kunakuwa na burudani nyingi sana ambazo zinatofautisha aliye uwanjani na atakayeangalia katika runinga.

Kwenye Uwanja wa Uhuru, idadi ya mashabiki wanaotakiwa kuingia ni 23,000 tofauti na 60,000 kwenye Uwanja wa Taifa. Pia kumbuka mechi hii ya watani inarejea kwenye uwanja huo baada ya kipindi kirefu.

Kutakuwa na mengi ambayo yatajitokeza ndani na nje ya uwanja, lakini nakupa 10 tu ambayo kwa asilimia 90 utayaona.

Wasio na tiketi:
Watu watajitokeza wengi zaidi kuliko idadi ya wale walio na tiketi na watajazana nje ya uwanja na kusababisha kero kubwa nje ya uwanja.

Bado kuna tabia ya watu kuamini kuwa wanapokwenda uwanjani kuna nafasi ya kuingia angalau kwa njia za mkato. Hivyo hawatakubali kuondoka mapema badala yake wataendelea kujaribu kutafuta njia ya kuingia kadiri itakavyowezekana.

Watu wa dezo:
Kuna mashabiki wa soka ambao wataonekana kwenye Uwanja wa Taifa (labda makala hii iwaponze).

Hao watakuwa wakishuhudia mechi hiyo inayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru bila ya kiingilio kwa kisingizio kuwa ni wafanyakazi wa uwanja huo. Inawezekana wako wataitumia nafasi hiyo kujiingizia kipato.

Hawataona mechi:
Kuna asilimia kubwa ya watakaokwenda uwanjani hawataona mechi hiyo ya watani.

Kwani hawatakuwa na tiketi lakini watakuwa na matumaini ya kujipenyeza ili kuona mechi hiyo. Hii itawafanya wajikute hadi mapumziko hawajaingia na ikiwezekana kipindi cha pili kitawakuta hapo wakishangilia mabao kwa hisia au kuhadithiwa kwa kuwa hawataweza kuingia.

Mzozo jukwaa kuu:
Baada ya zaidi ya miaka 10, mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga imerejea katika Uwanja wa Uhuru. Wako mashabiki hawakuwa wamewahi kuanza kuingia uwanjani timu hizo zikicheza Uwanja wa Uhuru wakati huo Uwanja wa Taifa.

Hao watapata shida kubwa kutokana na aina ya ushangiliaji zinapokutana Yanga na Simba kwenye uwanja huo na hasa jukwaa kuu kwani wanakuwa karibu na mazoezi ya Uwanja wa Taifa yanaweza kuwasumbua na kutakuwa na mizozo mingi sana.

Tafrani ya mgawo:
Kama nilivyoeleza, mechi hiyo imerejea tena Uwanja wa Uhuru na inachezwa kwa mara ya kwanza kukiwa na jukwaa la mzunguko. Kwa wanaokumbuka kabla kulikuwa na jukwaa kuu ambalo lipo hadi sasa, Jukwaa la Kijani maarufu kama Green Stand ambalo lilivunjwa na mzunguko ambalo watu walikuwa wakisimama.

Upande wa Green Stand na mzunguko ndipo palipojengwa jukwaa jipya. Hivyo Simba na Yanga hazijawahi kukutana kukiwa na jukwaa hilo. Hivyo lazima kutakuwa na shida ya kugawana wapi sahihi pa kukaa na hawa wanaishia wapi na lazima askari polisi watalazimika kuingilia kati.

Ajibu ugumu:
Tukirejea uwanjani, mshambuliaji Ibrahim Ajibu wa Yanga atakuwa na wakati mgumu kwa kuwa mashabiki wa Simba watafurahi sana kumuona akiharibu na ikiwezekana kumzomea kila mara na atalazimika kufunga au kutoa pasi ya bao ili kuwanyamazisha.

Hali kadhalika, Emmanuel Okwi naye atakumbana na hali hiyo kutoka kwa mashabiki wa Yanga ambao wasingependa kumuona hata akicheza mechi hiyo.

Makocha:
Makocha wote wawili, Joseph Omog wa Simba na George Lwandamina wa Yanga watakuwa katika wakati mgumu sana na utaona wakiwa na presha muda mwingi hawatatulia katika mabenchi yao.

Kila mmoja anajua kupoteza mchezo wa leo kunaweza kukawa ni njia ya kutokea. Hivyo lazima atakuwa akisimama kila mara kuhakikisha anaweka mambo sawa na kama atazidiwa na kuona anashindwa kufanya hivyo, mara nyingi watawatuma wasaidizi wao ikiwezekana wasikae karibu muda wote wa mechi.

Mfungaji:
Timu yoyote inaweza kushinda kwa kuwa timu hizo zinafanana sana hasa kitakwimu kulingana na mechi zilizocheza.

Uwezekano mkubwa wa wafungaji kutokuwa Okwi wala Ajibu kwa kuwa kila timu itafanya kazi kubwa ya kuwalinda halafu ikajisahau na kutoa nafasi kwa wengine.

Kadi:
Mechi ya leo ina nafasi kubwa ya kadi hasa kama timu itashindwa kufunga au kutimiza inachotaka.

Inawezekana kabisa wachezaji wa Simba wakaanza ‘kupanik’ kama watakufungwa mapema au Yanga wakawa hivyo kama watafungwa halafu wakashindwa kusawazisha katika kipindi wanachotarajia.

Hali hii inaweza kumsababisha mwamuzi kutoa kadi za njano au hata nyekundu kutokana na hali ya kupanik kutokana na presha ambayo wachezaji wanaipata.

Ushirikina:
Hili halina nafasi kubwa lakini kwa mfumo wa uwanja ulivyo tofauti na Uwanja wa Taifa, kuna nafasi kubwa ya mambo ya kishirikina kujitokeza.


Uwanja wa Uhuru uko wazi zaidi na haufichi mambo ambayo yamekuwa yakifanyika hasa kuhusiana na imani chafu za kishirikina. Inawezekana timu hata zikawa tayari kutozwa faini ili kufanya mambo hayo “kujiridhisha”

Kikosi cha simba kitakacho pambana na Yanga leo

Kikosi cha simba kitakacho pambana na Yanga leo


KIKOSI CHA SIMBA:

1. Aishi Manula

2. Erasto Nyoni

3. Mohamed Zimbwe (C)

4. Juuko Murshid

5. Method Mwanjale

6. Jonas Mkude

7. Shiza Kichuya

8. Muzamiru Yassin

9. John Bocco

10. Emmanuel Okwi

11. Haruna Niyonzima

Kikosi kizima cha Yanga kitakachoivaa Simba leo

Kikosi kizima cha Yanga kitakachoivaa Simba leo

KIKOSI CHA YANGA:

1. Youthe Rostand

2. Juma Abdul

3. Gadiel Michael

4. Andrew Vicent

5. Kelvin Yondani

6. Papy Tshitshimbi

7. Pius Buswita

8. Raphael Daud

9. Obrey Chirwa

10. Ibrahim Ajibu

11. Geofrey Mwashiuya

Kichuya awapiga mkwara Yanga, asema ni wepesi

Kichuya awapiga mkwara Yanga, asema ni wepesi

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya Yanga, kwamba wapinzani wao hao ni wepesi na watawafunga leo.

Kichuya amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani bila ya hofu kwani ana uhakika wa ushindi kutokana na maandalizi yao chini ya Kocha Joseph Omog.

Kichuya alisema, katika mechi hiyo kikubwa wao kama wachezaji wamepania kupata ushindi ili waendelee kubaki kileleni katika msimamo ya ligi.

 “Tunajua kabisa mashabiki wa Simba kitu gani wanakitaka katika mechi hii dhidi ya Yanga, hivyo niwatoe hofu kwa kuwaambia kuwa waje kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kutushangilia.

“Watarajie matokeo mazuri ya ushindi na soka safi kutoka kwetu kutokana na maandalizi tuliyoyafanya kambini Zanzibar, sisi wachezaji tunataka pointi tatu ili tubaki kileleni,” alisema Kichuya.

Katika mchezo wa ligi kuu msimu uliopita wa Februari 25, mwaka huu ambao Simba ilishinda mabao 2-1, Kichuya alifunga bao moja kati ya mawili ya timu yake.

SOURCE: CHAMPIONI

Nafasi za kazi leo October 28

Audio | Stanley Enow ft Davido – Caramel | Mp3 Download

Audio | Stanley Enow ft Davido – Caramel | Mp3 Download

Download Here
https://my.notjustok.com/track/download/id/285570/by/0OGjAt9Ig8

Audio | Chris Bee Ft Dullayo – Diva | Mp3 Download

Audio | Chris Bee Ft Dullayo – Diva | Mp3 Download

Video | Baraka Da Prince – Sometimes | Mp4 Download

Audio | Otile Brown Ft. Khaligraph Jones – Nataka | Download

Audio | Otile Brown Ft. Khaligraph Jones – Nataka | Download

Otile Brown Ft. Khaligraph Jones - Nataka

Friday, 27 October 2017

Dawa za kulevya zakamatwa

Dawa za kulevya zakamatwa

Mwanza. Maofisa wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) wakishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama usiku wa kuamkia juzi walikamata zaidi ya kilo 100 za mihadarati aina ya heroin zilizokuwa zikisafirishwa kwenye jahazi kutoka Unguja kwenda Dar es Salaam.

Maofisa hao wa nchini wakishirikiana na vyombo vingine vya kimataifa walilitilia shaka na kuamua kulizuia jahazi hilo lililokuwa na raia kumi wa Iran na Wazanzibari wawili.

Kamishna wa sheria wa DCEA, Edwin Kakolaki amesema baada ya upekuzi wa awali walifanikiwa kukamata paketi 104 za dawa wanazoshuku kuwa ni heroin ambazo watazipeleka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa vipimo.

“Tunaendelea na ukaguzi wa jahazi na sasa tumepeleka mbwa kusaidia kazi hiyo,” alisema Kakolaki.

Hadi jana jioni maofisa wa DCEA walikuwa wakifanya upekuzi kwa kusaidiwa na mbwa wanusaji kuona kama kuna mizigo zaidi.

Habari zaidi zinasema baada ya kuona wamezungukwa, raia hao wa Iran walijaribu kubadili mwelekeo, lakini walizidiwa nguvu na kuanza kutupa baadhi ya mizigo kwenye maji ya Bahari ya Hindi.

Kamishna Mkuu wa DCEA, Rodgers Siyanga amesema kiwango hicho cha dawa kingekuwa kikubwa zaidi isingekuwa kitendo cha watu hao kutupa kiasi kingine baharini.

“Nasema vyombo vya dola viko imara kupambana na usafirishaji wa dawa za kulevya na hatutaacha kuyadhibiti magenge na mitandao yao. Kwa hiyo mtu yeyote anayepanga kuingiza dawa za kulevya ni vema ajiulize mara mbili na aache, tutampata tu,” alisema Siyanga.

Meli iliyotumika katika operesheni hiyo ya usiku wa manane ilitumika pia kulivuta jahazi hilo na kulifikisha Bandari ya Dar es Salaam juzi saa nne usiku.

Ofisa mwingine aliyeshiriki operesheni hiyo alisema baada ya kukamatwa raia hao wa Iran walijitetea kuwa wao ni wavuvi. “Tulipowabana wakadai wanakwenda nchini Somalia kusaka chombo cha wenzao walichodai kutaarifiwa kimeharibika huko.”

Imeelezwa pia kuwa Wazanzibari wawili waliokutwa kwenye meli hiyo walijitetea kuwa wao walitumwa tu kupeleka chakula katika jahazi hilo.

Raisi John Magufuli aliwahi kusema Serikali yake haitakuwa na huruma na watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ambazo zimeharibu nguvu kazi ya Taifa kwa kiasi kikubwa.

Akiamuapisha Siyanga mwezi Aprili, Rais Magufuli alisema, ‘isingekuwa sheria imesema, yeye mwenyewe angekuwa mwenyekiti badala ya waziri mkuu’, huku akimtaka Kamishna Siyanga kufanya kazi bila woga.